Ushuhuda: Hatimaye ametiki

Ushuhuda: Hatimaye ametiki

SHUHUDA: HATIMAYE AMETIKI (based on my true story) 5th epsode
... Binti huyo aliendelea kunikazia nikiongelea swala la mahusiano hata hakunielewa kabisa nilimwambia nimemic zile moment za kipindi kile tukiwa relini, nilimkumbusha lakini alisema hayo yaliishia siku ile na wala nitegemee chochote harafu alipenda kukazia kwenye maongezi neno SIKUPENDI. hivyo kama nategemea chochote ni kama napoteza mda tu.
Kama kawaida yake mda mwingine namkera zaidi harafu nachezea block ila nilijipa moyo kwa kusema Everything is possible, you gonna dream like you have never seen an obstacle yaani niliamini ndoto unaweza zilinda kama haujawahi Kutana na vikwazo. Pia nilisahau msemo usemao kama mtu hakupendi usimulazimishe kupenda.
Ilikua safari ya ndiyo hapana kwake mara ndio mara hapana. Yaani mda mwingine namtafuta hata kwenye simu nyingine ananiuliza wewe nani? Nami namjibu mimi si kasomi mara kasomi gani mbona hata sikufahamu kama mapenzi mapenzi yanavyo tuendesha inanilazimu kujitambulisha majina yote eti naitwa Emmanuel Kasomi ilikuwa moja ya dharau Yaani alinishusha sana lakini mda mwingi tulikuwa tunaongea nae kwa kweli sikuwahi muelewa maana unachat kidogo anakwambia piga. Ukipiga unaongea kidogo mara anasema unamkera.
Siku ziliendelea huku tukisumbuana na mimi niliishi kusumbuana nae tu yaani ndo yalikuwa maisha yetu.
Kulikua na maneno yake aliyo kuwa anapenda kuniambia mara niacha usumbufu, nisimufuatilie, fuata yako nami nifuate yangu. Si hayo tu yaani alinihakikishia kwamba haita tokea hata siku moja mimi kupata nafasi ya kunipenda hata siku moja.
Maisha yaliendelea siku moja ambayo ndo naweza sema ilikuwa siku yangu ya mwisho kusumbuana nae ilikuwa mida ya saa 3usiku.
Nilimtumia sms nikisema uwe na usiku mwema pia nikaongeza na jina kwa kumuita kwa kilugha nikiwa na maana ya mwanamke wangu, lilitumia meno mwanamke wangu kwa kabila langu ili asielewe, alicho nijibu ndio kikafanya nimuwakie na ndio kulifanya nifikie tamati siku hiyo.


To be continued...
 
SHUHUDA: HATIMAYE AMETIKI (based on my true story) 6th epsode
... Nikaamua siku hiyo nisiwe mvivu inatakiwa Nimutolee uvivu yaani niliamua kumtusi kua anavyo jiona na anavyo ishi nilianza kumshushia Nondo.
Kama hizi 👇
"Ujue ukipendwa usjipe kiburi hvyo hata kama mtu humpendi.
Kwani wewe ni mtu wa kwanza kutongozwa yaan kisa hukunipenda ndio ujione kua wewe
ni wewe"
Nilimwambia mambo mengi nikamfundisha jinsi maisha yanavyo enda.
"Usiwe na akili za darasani tu jaribu kua na akili extra zikusaidie maisha".
Alijaribu kujitetea lakini nilizidi kumuwakia
"Yaani ujue unajion sana wewe.
Ni kama sifa kumblock mtu mara kwa mara.
Hivi ungepewa nafasi ya kuwa na mamlaka duniani ingekuwaje.
Yaani unatumia nguvu ya mzungu je ungekua Nayo wewe sasa"
Nilimwambia maneno mengi makali
"Ujue unaweza kua na maisha mazuri leo pia na ndugu wenye maisha mazuri.
Tabia hiyo itakufanya kuwadharau wengine lakini ipo siku unacho jivunia itatoweka"
"Ujue naumia sana unap jiona wewe ni wewe na kupenda kumzarau mtu yaani unamshusha kana kwamba yeye si kitu kwako"
Nilizidi kuporomoka
"Sawa leo unaniona mimi si kitu kwako ila amini ipo siku tabia kama hii utakuta kwa watu wengine.
Hebu jaribu kuishi na watu vizuri"
Maneno mengi sana nilimuwakia.
Yalivyo muingia akajibu tena kwa herufi kubwa
"OKAY, INATOSHA YALISHAISHA NA YALISHAPITA" "OKAY YAISHE"

Moyoni nikasema hapa hapa nikazie hizi zalau zimuishe
Nilimwambia tena maneno mengine
"Sawa ila endelea sina thamani kwak ila ninathaman kwa mtu fulani" akaanza kujibu kwa upole kuwa "Yale yote yaliyotokea nyuma nimeyasahau" na mimi nikasema hapa hapa ameanza kujirudi.
Nikaendelea kumchana na yeye alijibu kwa upole sana "Hayo nlishayapokea" likaendelea kumpa somo akasema ameelewa ila si kama ninavyo taka mimi. Akaanza kueleweka kidogo na mimi kuniomba "sawa isiwe kesi ila ukiendelea na zile tabia zako hatutoelewana hata kidogo" na mimi hapa hapa ndo nipitie kwenye hii mada nikiwa namuelekeza huku natupia kamba mara nikaona tukauli twake tunajirudi "ndo mnavyo danganyaga watoto wa watu,japo watoto wa watu hatunaga akili ila nyie mnachangia pakubwa sana. Kwakuwa watoto wa watu cheap kwaiyo ndo mnaitumia iyo nafasi"
Nikamuelekeza maisha yalivyo nikamwambia jinsi nilivyo mpenda yaani uongo mwingi ili kunogesha maongezi ili ajue anapendwa.
Nilimuelekeza sana mara akaanza kusema "apana ndo naanza kupata picha halisi kumbe ndo mlivyo yaani mnajua kudanganya" na mimi nakazia hapo hapo naona anajileta nikamuelekeza zaidi mara akaanza kuniuliza na mimi "kwamba ndo tuanze kuiga maisha ya watu wengine" nilijitahidi sana kuteka hisia zake siku hiyo. Nikamwambia aniamini mara ohhh "we siwezi kukuamini kwa chochote" nikamsomesha mtoto Mungu si asumani mtoto akatiki akasema "Sawa nimekuelewa basi nisamehe kwa yote yaliyo tokea nyuma tuanze maisha mapya lakini usije niumiza" na mimi moyoni yes nikajua tayari mtoto kaingia King kwahiyo nacheza popote.
Ilikua ni chating kuanzia saa3usiku tulivyo anza kuzodoana hadi inafika muda wa saa nane usiku ilikuwa siku ya kuamkia j'pili.
Hivyo ndo mkeka wangu ulitiki.
Note: Kumbe sometimes si kuwabembeleza ni kuwafokea na kuwabembeleza tena(Yaani kwa lugha nyepesi ni kung'ata na kupuliza).
Hivyo ndio binti Adelina alivyo ingia kwenye mikono ya mtu mzima kasomi kipindi hicho.

Shuhuda: Hatimaye Ametiki
 
Back
Top Bottom