USHUHUDA: Nilivyokutana na ushirikina kazini

USHUHUDA: Nilivyokutana na ushirikina kazini

Tatizo waswahili tuna shida sana! Mzungu akiua Mswahili mgodini hicho ni kifo cha kawaida ila ngoja mtu afie kwenye mgodi wa mswahili!! Tambiko.

Nimefanya nao kazi sana, wanaloga kinyama na hakuna wanachofanya bila kuloga. Ajabu alikuwa hatoi pesa au malipo siku ya Jumanne watu wakachukulia kawaida kumbe majini yake yamemkataza!! Fanya wewe mswahili uone utavyoandamwa na kashfa za uchawi.
wahindi hata umtundike hatoi pesa jumanne au alhamis huo ni mwiko
 
Hiyo ya excavator siwezi kataa. Nilishuhudia kikosi Cha Chita pale C.O alinunua lile mashine la kuvunja mpunga, wazee si wakapiga ndumba bana ili lisifanye kazi? Uliza kilichotokea.
 
Cha kushangaza akija mzungu, mchina au muarabu kuchimba kunakua hakuna vikwazo kama hivyo na wanafanikiwa kuchimba na kupata wanachokihitaji...
Mkuu sio kila anaekamatwa ana makosa wengine huwa wanahifadhiwa tu ili asishambuliwe na wananchi wenye hasira Kali
Baadae huwa wanaachiwa
 
"Na mwingine akaenda akaleta ka kuku kadogo akachimba shimbo pembezon mwa site akakafukia kale kakuku kakiwa kazima. Baada ya hapo wakamwambia Operator awashe machine. Mi naangalia tuu km movie, aisee huezi amini machine ikawa na power kuzidi hata uwezo wake siku zote"[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Chai hii kabisa
 
Mkuu sio kila anaekamatwa ana makosa wengine huwa wanahifadhiwa tu ili asishambuliwe na wananchi wenye hasira Kali
Baadae huwa wanaachiwa
Basi serikali inasababisha ongezeko la wachawi na washirikina
 
Tukiwa huko huko TANGA. Kuna siku serikali ilitaka kutengeneza barabara kipindi kile hakuna fidia Ni umwamba tu. Basi engineer akasema barabara itapita kwenye shamba la mgosingwa mmoja. Mgosingwa akasema hakubaliani na huo uamizi. Serikali ikatumia umwamba ikaleta caterpillar Yale ma D8 ya enzi zile.

D8 likachonga barabara Ila kufika kwenye shamba la mgosingwa D8 likazimika. Washa. Washa na wewe. Cheki kila kitu Kiko vzr lkn D8 haliwaki. Kumbuka D8 huwezi kulivuta Wala kuliondoa mpaka lenyewe liwake. Liko mpaka Leo na barabara ilipita kwingine.

Tukiwa hapo hapo TA Kuna mgeni mkware alitembea na mke wa mtu. Jioni anafika kwake anakuta mb**0 Yale haioni. Kwenda kwa mganga kaambiwa hii mpaka uende kwa mume wa uliyetembea nae maana anayo nyumbani kwake.

Kweli bwana mkware kufika kwa aliyemuibia uroda anaikuta na mayai yote mawili imeanikwa nje kwenye ungo. Aliambiwa ungechelewa ingeweza kuliwa na kunguru ama ingenyauka. Dogo alilipa fidia na kuondoka siku hiyo hiyo
 
Mkuu nani kakudanganya kuwa mzungu halogi?, kwenye watalii wanaopanda Mt. Kilimanjaro takribani 45% wanaenda kufanya hayo mambo. Hii sio blah! blah!.

Kwa mchina unafikiri ujangili kwanini route kubwa ya masoko ni China?, hao jamaa huwaambii kitu kwa wanavyoamini pembe ya ndovu.

Hahah hizi story huwa mnatoa wapi Mkuu. Huna tofauti na hawa jamaa hapa chini. Nadhani hata hii unaamini.

WhatsApp Image 2021-04-23 at 10.22.57 AM.jpeg
 
WAZUNGU WANA UCHAWI WA KUDHURU PIA
tena hauhitaji hata diploma kuufanya kuna moja nilikutana nayo sehemu nikajaribu kilichotokea mpaka sasa najutia
ulijaribu kufanya nn bibiye? toa ushuhuda tafadhali
 
Uchawi upo,uwez thibitisha km ujawai kutwa na misala yake
 
Hakuna kitu kinachosikitisha kama kukatisha uhai wa mnyama hasa asiyeweza kujitetea.Kuku hana kosa lolote anafukiwa akiwa hai.Mnyama kama huyu anastahili kuishi kama nyie mliyemfukia mnavyostahili kuishi
 
Kuna sehemu umenikera sana mkuu,unazika ka kuku kazima kazima kweli.Unaua kiumbe kweli?!Imagine unazikwa wewe mzima mzima ,Dah!
 
Hakuna kitu kinachosikitisha kama kukatisha uhai wa mnyama hasa asiyeweza kujitetea.Kuku hana kosa lolote anafukiwa akiwa hai.Mnyama kama huyu anastahili kuishi kama nyie mliyemfukia mnavyostahili kuishi
Kuku Ni ndege
 
Mambo vipi wakuu,

Kwanza nitajikita kwenye mada kutokana na personal experience ya hapa home Tz. Binafsi nimekulia mazingira ya dini sana , kwa hiyo mambo ya uchawi au ku-practice masuala ya kiganga /jadi sikuwahi.

Lakini kwa uzoefu na namna nilivyoona katika kutembea mikoa ya hapa Tanzania, hasa huko vijijini watu wamelazimika kutofanya Maendeleo, kuyahama makazi yao kwa kuogopa kulogwa. Unakuta eti Kijijini mtu alikuwa hawezi kujenga nyumba nzuri na kuezeka bati, ukifanya hiyo kitu unaanza kuandamwa na mambo mengine kama hayo.

Personal Experience.

Nilipoamua ku-resign kazi na kuanza mishe zangu binafsi, niliingia kwenye kazi za mining na huku ndio nilikutana na hayo mambo.

Tulienda kuanzisha mining site Handeni- Tanga. Aisee, nilikuwa nausikia tu ushirikina sasa kule ndio nilienda kuona. Yaani mtu analoga machine (Excavator) inakuwa haifanyi chochote, tunaita mafundi wa kila aina wanachokonoa wee ila waapi, na machine bado mpya.

Baadae one of the labors niliokuwa nao pale site akaniita na wenzake pembeni, wakaniambia ndugu yetu, hapa kutakuwa na kitu kimefanyika, wakanitaka twende na mganga ili tuka unlock. Mimi nikawa siamini kama mashine inaweza logwa na sikuwa na imani na zile mambo kbs.

Basi nikawauliza kama wanaweza kwenda wenyewe wafanye kwa niaba wakasema poa niwape elfu 20 wanunue kuku, basi mshikaji akanambia tuwape. Mini nikawapa wakaondoka bwana, hapo tumehangaika na fundi wiring na hydrologic system wote wanasema hawaona tatizo, ila machine haina kabisa nguvu ya kuchimba.

Wale wadau walirudi time za jioni around 5pm, na maji yenye dawa kwenye chupa pamoja na vimiti viwili. Wakasema Operator wa machine aweke mfukoni kimti kimoja na kingine aweke chini ya seat yake, na yale maji ya dawa imwagiwe machine na kuzunguka eneo la mgodi. Operator akasema fresh ,yeye alikuwa anaamini sana, wale jamaa wakamwaga maji kwny machine nakuzunguka pale site, na mwingine akaenda akaleta ka kuku kadogo akachimba shimbo pembezon mwa site akakafukia kale kakuku kakiwa kazima.

Baada ya hapo wakamwambia Operator awashe machine . Mi naangalia tuu km movie, aisee huezi amin machine ikawa na power kuzidi hata uwezo wake siku zote. Nikashangaa sana , jamaa wale wenyeji wanacheka wananiambia "karibu Tanga mgosi".

Hii ni kwa ufupi tu, nina mengi sana nime experience sehemu mbali mbali hasa katika kazi ya mining, maana mnaenda kuanzisha kazi sehem porini kumbe palikua ni mahali pa matambiko, basi vituko ni vingi nikijaaliwa muda nitakua naandika matukio mengine . Watu wana uwezo wakupoteza madini aridhini, yaani unachimba wee nakuunguza hela ila huoni kitu, wakati mwanzo mambo yalikua fresh kbs. Lakini mwisho wa siku nina Imani na Mungu , hatutakiwi kuweka Imani kwa waganga kwasababu nao ni binadam, uchawi upo na Mungu yupo.

Serikali haiamini katika uchawi, ni sawa kbs lakini ukweli ni kwamba uchawi umelostisha sana watu, pengine watu wangekuwa na maendeleo sehemu mbali mbali isingekuwa haya mambo. Siku hizi kidogo yanapungua ,nadhani muingiliano wa wageni na wenyeji sehemu mbalimbali unafanya watu ku-focus kwenye maendeleo. I'm not sure kama tumeshawah kuwa na sheria inayokemea haya mambo kwa kuwa ni invisible world.

Naomba niishie hapo kwa leo, najua wengi wetu tuna experience tofauti tofauti, kuwa huru ku share nasi tujifunze kitu.
BS!

Kuna mawili... ama hii stori yako ni fiction au huyo "operator" wako kakuchezea shere tu kutaka nawe uanze kauamini hayo mambo ya kijinga.

Ushirikina upo kama dini - wapo wanaoamini na wasioamini - lakini hauna athari yoyote kwa mwanadamu let alone lifeless objects like machines!
 
Kwa kuwa UCHAWI na JADI ni elimu inayorithishwa basi ITAENDELEA KUWEPO.

Waswahili wanasema "shiriki ushirikishwe".
N ni imani kama zilivyo imani zingine. Wapo, watakuwepo na wataendelea kuwepo. Mchawi mmoja anaweza rithisha mpka watoto/wajukuu 20. Kibaya ni kuwa, kwenye kila watu watano, kati ya wawili mpaka watatu wanaweza kuwa wachawi. Kibaya zaidi huwezi kuwajua kwa hali zao, kuna masikini na matajiri, warembo na wabaya, vijana kwa wazee, Wachamungu na wasio wachamungu.

Uchawi ni nouma mazeee
 
Mikoa ya tanga, Lindi, pwani hii imefungwa kichawi ni ngumu Sana kuwa na maendeleo hadi zindiko liondolewe upo uchawi wa kuuroga mkoa mzima usiwe na maendeleo.Afrika ya weusi yote ni kama imerogwa thus hakuna maendeleo
kama vile nakuamini amini hivi. Ni mikoa maskini haswa. Wana Laana hao jamaaa
 
Back
Top Bottom