Naam,
Kumekuweko na speculation nyingi kuhusu RADI. Nyingi zikihusisha radi katika makundi mawili, ambayo ni radi kisayansi,kama umeme asilia na Radi kiimani. Wengi wakiihusisha na ushirikina.
Binafsi ziko katika upande wowote Kati ya hizo pande mbili hapo juu, bali naeleza kile nilichopata kukishuhudia mara mbili kwa macho yangu mawili, utotoni( adolescent age) na ukubwani kidogo nikiwa najitambua.
Nikiwa na yapata miaka kadhaa, tukiwa porini tunachunga ng'ombe tukiwa rika vijana wadogo watatu tuliona jogoo mzuri pembezoni na maeneo tuliyopo, alikuwa anaevutia tulimnyatia na tukamkamata jogoo alikuwa na kila kitu chekundu kuanzia mdomo,manyoya hadi miguu tukamfikisha nyumbani huku manyunyu ya mvua yakiendelea kuongezeka, tukamfungia jogoo jikoni na wengine wakiirudisha mifugo zizini.
Tukiwa tumefurahi na tukiendelea na michezo kwani kitoweo kimepatikana, tukamwambia bibi kuwa tumeokota kuku machungani na tumemfungia yumo jikoni. Bibi kwenda kuangalia! Lahaula! Alianza kupiga kelele za yowe kwa majirani, unajua umbali uliopo baina ya mji na mji. Aliendelea huku analia na kukimbiza huku na kule huku mvua ikiendelea kunyesha.
Baadhi ya watu waliendelea kujaa, na kutahamaki tukasikia ngurumo kubwa na miale ya radi iliipiga ile nyumba ambayo ndio huko tulipomfungia yule kuku. Wote tuliinama kwa yoga na baada ya mvua kukatika tukagundua kuwa yule kuku hakuwemo tena na alipotea ghafla baada ya Radi ile kutoweka, na haikuleta madhara makubwa sana.
Tukio la pili;-)
Nikiwa likizo last year Std Vii kama ilivyo kawaida nilimtembelea bibi na babu(R.I.P), katika mizunguko yetu ya hapa na pale, tulitenbelea mtoni kuogelea na kupiga stori mbili tatu na washkaji wa kunijibu, maana tulikuwa hatusomi pamoja tena,mimi nilikuwa nikija huku kwa ajili ya likizo tu.
Tukiwa tunaendelea kuogelea kea mbali kidogo niliona tukio kama lile lililotutokea miaka kadhaa nyuma na kufanya tupokee kichapo toka kwa babu, niliona jogoo wa dizaini ile ile! Mwekundu Tii! Akiwa pembeni ya mto akizamisha kichwa makini na kutoa mara kwa mara huku akipigapiga mabawa.
Mapigo ya moyo yalianza kunienda mbio kwa woga hofu! Kwani nilihisi kinachokaribia kutokea na pembeni kulikuwako na vijana wadogo wanachunga.
Kwa hofu tulikuwa tukimuangalia yule jogoo anaevutia sana na wenzangu wote tukiwa tumetoka mtoni tuko pembeni,ghafla ulisikika muungurumo na mitetemo kikubwa+ miale kadhaa ya mianga(Radi) na pale pale ng'ombe watatu walipigwa na Radi pale pale na kufa!.on the spot!.
Haya nimeyashudia mwenyewe kwa macho yangu,nikiwa na akili timamu!
Sayansi inaamini ni umeme wa asilia, lakini napata ukakasi nikiunganisha nilichokishudia kwa macho,na sayansi ya kufundishwa. Ktka radi napata kuuona uhusika wa hivi vitu, MUNGU yupo(imani) maana nimeona kitu kwa macho halisi, na kikapotea.
Maswali ni mengi najiulizaga, yule jogoo kea nini hupotea! Baada ya Radi!? Anaeenda wapi!? Na kea nini sayansi inakataa ukweli kwamba Radi ni kuku!?