Ushuhuda wangu kuhusu RADI (my own testimonial)Nimeshuhudia RADI! Mara mbili, Ni kweli RADI ni kuku kabisa! Tena jogoo anaevutia haswa!

Ushuhuda wangu kuhusu RADI (my own testimonial)Nimeshuhudia RADI! Mara mbili, Ni kweli RADI ni kuku kabisa! Tena jogoo anaevutia haswa!

Hiyo hallucination ndio wawe nayo kijiji kizima.?
Hili nishajibu humu..., Power of Suggestion binadamu akili yake inapenda ku-connect vitu ambavyo havina mpangilio na kuviweka katika mpangilio kulingana na vitu ambavyo wapo familiar navyo...

Wewe toka hapo nje na familia yako angalia mawingu alafu muanze kuambiana kama hamumuoni kuku, sima au mzee mwenye ndevu kwenye mawingu...., utaanza kusikia mmhhh kweeliii na ambaye hajaona eventually ataona...
 
Science inatafsiri uumbaji kwa level za kibinadamu.
Nadhani mkuu haujui Sayansi ni nini...,

the intellectual and practical activity encompassing the systematic study of the structure and behaviour of the physical and natural world through observation and experiment.

Utaona hapo key word ni observation and experiment na ninaongezea na proof (lazima theory iwe proven) kwahio ni mwendo wa proof no more no less.....
Hivyo mpaka hapo baadae sana science itakapo kuwa more advance wanaweza kuja kugundua mambo tofauti kabisa.
Naam watagundua through observation and experiments ili theories / statements ziwe proven without the proof that is not science its something else...
Mfano hapo kale watu waliamini kuwa dunia ni tambarare ila baada ya vumbuzi nyingi tukaja gundua kuwa ni duara. Ingawa bado kuna discussions nyingi tu as to whether dunia ni tambarare au duara.
Naam waliamini (IMANI) and it was not science mpaka ilipokuwa scientifically proven kwahio now its a known fact....
Mambo mengi bado hatujayafahamu.
Naam kuna Unknown knowns na na known unknowns..., mwanasanyi atakuwa wa kwanza kukwambia mpaka kitu kiwe a known fact it takes experimentation and observation...., Hakuna mwanasayansi anayejifanya much know hata anachokitambua leo kama fact ukija na ku-prove otherwise atakuwa wa kwanza kukushukuru and your proof will be known fact...., tofauti na Imani ambapo ukichunguza unaonekana una mapepo, kwenye sayansi tunapenda uchunguze ili uelewa wetu uongezeke...
Science sio ya kuamini sana.
Science ni ya kuamini sana sababu ipo based on experiments, observations and Proof na sio vinginevyo (hivyo vinginevyo ndio sio vya kuamini)..., kama wewe unaona kuna statement sio factual ingia field prove otherwise with concrete proof basi watu tutakusikiliza tu (sio wewe as wewe bali tha facts you present)
 
Naam,

Kumekuweko na speculation nyingi kuhusu RADI. Nyingi zikihusisha radi katika makundi mawili, ambayo ni radi kisayansi,kama umeme asilia na Radi kiimani. Wengi wakiihusisha na ushirikina.

Binafsi ziko katika upande wowote Kati ya hizo pande mbili hapo juu, bali naeleza kile nilichopata kukishuhudia mara mbili kwa macho yangu mawili, utotoni( adolescent age) na ukubwani kidogo nikiwa najitambua.

Nikiwa na yapata miaka kadhaa, tukiwa porini tunachunga ng'ombe tukiwa rika vijana wadogo watatu tuliona jogoo mzuri pembezoni na maeneo tuliyopo, alikuwa anaevutia tulimnyatia na tukamkamata jogoo alikuwa na kila kitu chekundu kuanzia mdomo,manyoya hadi miguu tukamfikisha nyumbani huku manyunyu ya mvua yakiendelea kuongezeka, tukamfungia jogoo jikoni na wengine wakiirudisha mifugo zizini.

Tukiwa tumefurahi na tukiendelea na michezo kwani kitoweo kimepatikana, tukamwambia bibi kuwa tumeokota kuku machungani na tumemfungia yumo jikoni. Bibi kwenda kuangalia! Lahaula! Alianza kupiga kelele za yowe kwa majirani, unajua umbali uliopo baina ya mji na mji. Aliendelea huku analia na kukimbiza huku na kule huku mvua ikiendelea kunyesha.

Baadhi ya watu waliendelea kujaa, na kutahamaki tukasikia ngurumo kubwa na miale ya radi iliipiga ile nyumba ambayo ndio huko tulipomfungia yule kuku. Wote tuliinama kwa yoga na baada ya mvua kukatika tukagundua kuwa yule kuku hakuwemo tena na alipotea ghafla baada ya Radi ile kutoweka, na haikuleta madhara makubwa sana.

Tukio la pili;-)
Nikiwa likizo last year Std Vii kama ilivyo kawaida nilimtembelea bibi na babu(R.I.P), katika mizunguko yetu ya hapa na pale, tulitenbelea mtoni kuogelea na kupiga stori mbili tatu na washkaji wa kunijibu, maana tulikuwa hatusomi pamoja tena,mimi nilikuwa nikija huku kwa ajili ya likizo tu.

Tukiwa tunaendelea kuogelea kea mbali kidogo niliona tukio kama lile lililotutokea miaka kadhaa nyuma na kufanya tupokee kichapo toka kwa babu, niliona jogoo wa dizaini ile ile! Mwekundu Tii! Akiwa pembeni ya mto akizamisha kichwa makini na kutoa mara kwa mara huku akipigapiga mabawa.

Mapigo ya moyo yalianza kunienda mbio kwa woga hofu! Kwani nilihisi kinachokaribia kutokea na pembeni kulikuwako na vijana wadogo wanachunga.

Kwa hofu tulikuwa tukimuangalia yule jogoo anaevutia sana na wenzangu wote tukiwa tumetoka mtoni tuko pembeni,ghafla ulisikika muungurumo na mitetemo kikubwa+ miale kadhaa ya mianga(Radi) na pale pale ng'ombe watatu walipigwa na Radi pale pale na kufa!.on the spot!.

Haya nimeyashudia mwenyewe kwa macho yangu,nikiwa na akili timamu!

Sayansi inaamini ni umeme wa asilia, lakini napata ukakasi nikiunganisha nilichokishudia kwa macho,na sayansi ya kufundishwa. Ktka radi napata kuuona uhusika wa hivi vitu, MUNGU yupo(imani) maana nimeona kitu kwa macho halisi, na kikapotea.

Maswali ni mengi najiulizaga, yule jogoo kea nini hupotea! Baada ya Radi!? Anaeenda wapi!? Na kea nini sayansi inakataa ukweli kwamba Radi ni kuku!?
kea=kwa

wanasayansi (au sayansi kama ulivyoita) hawajawahi/haijawahi kukaa na kujadili kitu kama hicho mkuu.
 
Story za wazee wa mkoa wa njombe ndani ndani huko wanadai radi ni mnyama kama kondoo vile na ana miguu sita pia na msumeno mgongoni, wapo walio wahi kutana nae wote wanasimulia mfanano huo ila mwishoe huishia na mianga mikali na ngurumo zisizo na kifani yaani hii radi tuijuayo. Wana dhana nyingine kwamba radi za namna hii (radi zenye mkono wa mtu) huchochewa na kuvaa nguo rangi nyekundu ila hukingwa kwa kukaa jirani na mnyama kondoo, inasemekana kondoo hupigana na huyo mnyama radi, pia kukaa eneo lenye mianzi (baobab tree) inasemekana radi ikipiga lile eneo lile basi anaweza akanasa kwenye mianzi hiyo kama mnavyojua mti wa mwanzi ulipasuliwa katikati huwa na uwezo mkubwa wa kubana ktkt yake.

Twaweza chukulia tu ni story ila wazee wale walikuwa serious kwa hizo story, ila wao wanàamini hivyo sasa wewe nenda na physics zako utake kufanya majaribio, kuna story moja niwape kwa ufupi, kuna mradi mmoja uliitwa NDDT Ulitekelezwa kuanzia miaka ya 1980's katikati mpka miaka ya 2010 hivi ulikuwa chini ya NORAD, NIDA NA SWEDISH yaan zile nchi za scandinavia waliungana, walipeleka wazungu kujitolewa kama walimu walijenga camps za shule ziliitwa maarufu shule za NDDT, sasa miaka ya 90 mwanzoni kuna mzungu alikuwa na mahusiano mazuri na jirani yake ambaye ni mwenyeji, siku akamuuliza naskia kuna usafiri wa chap chap wa kufumba na kufumbua ni kweli? Yule mzee jina nahifadhi alimjibu hata mimi ni mtaalamu, akamwambia siku moja tujaribu wakakubaliana hivyo, siku imefika alipewa maelekezo yote alitekeleza destination yao ikawa na njombe mjini kiasi cha kama 80 km kutoka hapo kijijini Lupembe, basi bwana aliambiwa fumba macho akafumba baada ya muda fumbua akafumbua, ile kufumbua alikuwa nje ya hotel ya magazeti, enzi hizo ni hotel maarufu sana njombe, basi mzungu yule akaingia hotelini akaagiza soda, akanywa akamwambia mzee mwavi.... Nirudishe process ikarudiwa akawa nje ya nyumba ya yule mzee, mzungu akaaaga akarudi kwake, akatafakari, aka ona bora a park mizigo yake arudi tu ulaya.

Kama wewe ni mzaliwa wa Dar es salaam au sio mkazi wa nyanda za juu kusini utaona hizi ni story tu, pole sana!
Aisee hiyo story ya Radi naa kondoo umeongea kama umeicopy kutoka kichwa mwangu, Story za wabena na wahehe hizo.
 
Naweza kukubaliana nawewe ila. kwaupande wangu radi inaskia nakuonekana .nikiwa mdogo mvua ilipo kuwa ina nyesha nilikuwa na mtindo wakutoka nje yanyumba kuchezea mvua nakupiga kelele. au2mbinja, hapo radi itapiga kwanguvu nikitazama juu naona lama lindege .linapita basi nafurahi nakaa kidogo napiga tena linapita..sikumoja nilivaa nguo nyekundu.nimetoka dukan mvua kinanyesha nlikuwa nakimbia njia ina migomba. Namit hamad ilipiga radi ilinipita sentimita chache sana pona yangu niile kukimbia ilikosa target. Yapili nimwaka huu kwenye mwenz wa3 4. .hiinilishudia mwenyw mbezi juu tulikuwa tumeket tuna kula vitu kunakamvua mvua kunamti tuu mkubwa ghafla radi hyo hapo inazunguka juyamti kama umeme.kulikuwa na masai akachomoka akashika majani makavu akapiga magoti akaanza kuongea ewe radi sisi atuna ubaya tunakunywa tu naomba uondoke .namaneno siyakumbuk ghafla radi hyo ikaenda kuangukia mbali kidogo tukaona moshi tu ..hapo sisi tumelala chini badae tunamuliza masai anasema nikawaida tu ashazoea huko kwao
1.radi ilikosa target

2.radi ilikuwa inazunguka TU juu ya mti,Mara mmasai akaanza KUOMBA ,baadaye tukasikia radi imepiga sehemu NYINGINE

3.sawa MKUU,Sina Cha KUSEMA
 
Hio Radi ilikuwa mwendo / kasi gani ? Slow Motion ?

Sababu kinachoonekana ni waves ambazo ni light na Sauti (Sound) sasa kasi ya hivyo vitu mkuu kweli unapata muda wa kupiga magoti na kupiga nayo story...

Au labda haikuwa moja zilikuwa na washikaji zao ili aliyoipigia magoti sio ile iliyopiga pengine....
Nimejiuliza Sana,nimekosa MAJIBU
 
🤣🤣 mimi pia kwa masimulizi ya watu waliopata kuona wanasema huonekana kuku mwekundu kabla ya radi kupiga.
Wengi hawaamini, ni ngumu kuwafanya waamini. Ila ni kuku! Na tulimshika kwa mikono yetu na kumfungia jikoni ndiyo yakakatokea hayo niliyoeleza
 
ilo jogoo umeweka ww. vitu vingi unavyo viona kwa macho yak ya nyama sio vilivyo
Hadi kufikia hatua ya kumkamata kwa mikono na kwenda nae hadi nyumbani Bado huamini tu!? Ama kweli watu mmeumbwa na vichwa ngumu kuamini
 
Sijaona picha ya jogoo
Naam,

Kumekuweko na speculation nyingi kuhusu RADI. Nyingi zikihusisha radi katika makundi mawili, ambayo ni radi kisayansi,kama umeme asilia na Radi kiimani. Wengi wakiihusisha na ushirikina.

Binafsi ziko katika upande wowote Kati ya hizo pande mbili hapo juu, bali naeleza kile nilichopata kukishuhudia mara mbili kwa macho yangu mawili, utotoni( adolescent age) na ukubwani kidogo nikiwa najitambua.

Nikiwa na yapata miaka kadhaa, tukiwa porini tunachunga ng'ombe tukiwa rika vijana wadogo watatu tuliona jogoo mzuri pembezoni na maeneo tuliyopo, alikuwa anaevutia tulimnyatia na tukamkamata jogoo alikuwa na kila kitu chekundu kuanzia mdomo,manyoya hadi miguu tukamfikisha nyumbani huku manyunyu ya mvua yakiendelea kuongezeka, tukamfungia jogoo jikoni na wengine wakiirudisha mifugo zizini.

Tukiwa tumefurahi na tukiendelea na michezo kwani kitoweo kimepatikana, tukamwambia bibi kuwa tumeokota kuku machungani na tumemfungia yumo jikoni. Bibi kwenda kuangalia! Lahaula! Alianza kupiga kelele za yowe kwa majirani, unajua umbali uliopo baina ya mji na mji. Aliendelea huku analia na kukimbiza huku na kule huku mvua ikiendelea kunyesha.

Baadhi ya watu waliendelea kujaa, na kutahamaki tukasikia ngurumo kubwa na miale ya radi iliipiga ile nyumba ambayo ndio huko tulipomfungia yule kuku. Wote tuliinama kwa yoga na baada ya mvua kukatika tukagundua kuwa yule kuku hakuwemo tena na alipotea ghafla baada ya Radi ile kutoweka, na haikuleta madhara makubwa sana.

Tukio la pili;-)
Nikiwa likizo last year Std Vii kama ilivyo kawaida nilimtembelea bibi na babu(R.I.P), katika mizunguko yetu ya hapa na pale, tulitenbelea mtoni kuogelea na kupiga stori mbili tatu na washkaji wa kunijibu, maana tulikuwa hatusomi pamoja tena,mimi nilikuwa nikija huku kwa ajili ya likizo tu.

Tukiwa tunaendelea kuogelea kea mbali kidogo niliona tukio kama lile lililotutokea miaka kadhaa nyuma na kufanya tupokee kichapo toka kwa babu, niliona jogoo wa dizaini ile ile! Mwekundu Tii! Akiwa pembeni ya mto akizamisha kichwa makini na kutoa mara kwa mara huku akipigapiga mabawa.

Mapigo ya moyo yalianza kunienda mbio kwa woga hofu! Kwani nilihisi kinachokaribia kutokea na pembeni kulikuwako na vijana wadogo wanachunga.

Kwa hofu tulikuwa tukimuangalia yule jogoo anaevutia sana na wenzangu wote tukiwa tumetoka mtoni tuko pembeni,ghafla ulisikika muungurumo na mitetemo kikubwa+ miale kadhaa ya mianga(Radi) na pale pale ng'ombe watatu walipigwa na Radi pale pale na kufa!.on the spot!.

Haya nimeyashudia mwenyewe kwa macho yangu,nikiwa na akili timamu!

Sayansi inaamini ni umeme wa asilia, lakini napata ukakasi nikiunganisha nilichokishudia kwa macho,na sayansi ya kufundishwa. Ktka radi napata kuuona uhusika wa hivi vitu, MUNGU yupo(imani) maana nimeona kitu kwa macho halisi, na kikapotea.

Maswali ni mengi najiulizaga, yule jogoo kea nini hupotea! Baada ya Radi!? Anaeenda wapi!? Na kea nini sayansi inakataa ukweli kwamba Radi ni kuku!?
 
1.radi ilikosa target

2.radi ilikuwa inazunguka TU juu ya mti,Mara mmasai akaanza KUOMBA ,baadaye tukasikia radi imepiga sehemu NYINGINE

3.sawa MKUU,Sina Cha KUSEMA
Sjajua mm sio mtaalam...ila nilishuhudia
Labda ilikuwa namaongezi na masai
 
Mambo ya radi mtafute mtu mmoja anaitwa Pedeshee Mkombe ye ndo alikuwa mtaalamu wa kutengeneza radi sumbawanga
 
Sasa wewe unang'ang'ania mawingu basi na wewe toka nje na familia yako uwaambie oneni jogoo huyu hapa uone kama wataona hizo formation za mawinguni zipo tu hata maipoonyeshana akili zetu zinafananisha na vitu tulivyowahi kuviona au tunavyovijua!
 
Back
Top Bottom