maandamano
JF-Expert Member
- Nov 12, 2025
- 726
- 1,548
Nilizaliwa katika imani ya kikristo katika dhehebu la kikatoliki nilibatizwa nikiwa najitambua baada ya kufanya mafundisho,lakini kila kitu tulikuwa tunakalilishwa na siku ya mtihani alikuja Askofu anakuulizwa swali unamjibu,
Nikapata na sakrament ya kitubio na kipaimara yaani naruhusiwa kuungama dhambi zangu kwa padri na kula ule mkate nilijisikia furaha sana
Baadaye nikapate mafundisho ya ndoa kutoka kwa pandre ambaye hajui nini maana ya ndoa ninachokumbuka alisisitiza uvumilivu na kifo ndiyo kitakacho tutenganisha nikafunga ndoa na maisha yakawa yanaendelea
Lakini nilipoingia kwenye Uisilamu niliona kila kitu kipya kwanza kusujudu kuna sheria zake kuna viuonga ambavyo inabidi viguse chini siyo unasujudu tu,kumbuka Musa,Yesu,Mitume na Manabii wote walisujudu hakuna aliyepiga ishara ya msalaba,inamaana Mungu alimfundisha mwanadamu jinsi ya kusujudi bali kufanya ishara ya Msalaba aliyeanzisha ni mwanadamu
Hata kutawadha Mungu ndiye aliyemfundisha Mwanadamu kama hujui huwezi na itakuchukua mda ili kujua, Uisilamu ni Usafi mtu unaswali ukiwa msafi wa mwili na mavazi, huna mikojo wala mavi hata kama kuna watu wanasema Mungu anaangalia roho
Na katika Uisilamu anayeogopwa ni Mungu Allah tena mmoja hana mshirika na kila mnachoomba mnamuomba yeye kwani yeye ndiye aliyeumba kila kitu unachokiona pamoja na binadamu na majini,unapokwenda kuswali sala tano unaenda kama wewe siyo kwa ajili ya nabii au mtume, hapana ni kwa ajili ya Mungu aliyekuumba,na kinapokuja kipindi cha mfungo wa Ramadhani mwezi wa toba unaona kabisa watu wanafanya toba ya kweli na kuacha maasi,maana yake watu wana imani na Mungu wao kama anawasamehe na hawataki kupoteza hiyo fursa
Upande wa ndoa mnaoana kwa wema na mtaachana kwa wema kila mtu anajua ndoa ni safari ndefu siyo rahisi eti mkavumiliane siyo kitu rahisi ndiyo maana watu wanaishi na visasi ndani ya ndoa maana kuna mambo hayasameheki,kuoa mke zaidi ya mmoja kiubinadamu ni kweli kabisa sababu wanawake wako wengi kila mtu akisema aowe mwanamke mmoja tu halafu asichepuke unategemea hao walioko inje wataishije?
Niseme Uisilamu ni Dini iliyokamilika ingawa si mjuzi wa mambo mengi lakini kwa hayo najiona niko sehemu sahihi na salama