Nataka kukupa siri ya kujua ukweli,usije ukajibu kitu usichokijua ila tumia mda wako wa kutafuta ukweli wa kitu hichohicho usichokijuaWanaoabudu Mungu wa kiarabu aliye katika jiwe jeusi liitwalo Kaaba
Kalibu sana ndugu yangu nimependa hoja yako, hivi unaweza ukaupanda muhindi au ukamfuga ng'ombe ukawa unamuheshimu? Nazumgumzia hivyo vitu vyenye uhai,Bro maandamano .
Uzi wako umeandika hauna hata aya na ngumu sana kuusoma.
Anyway. Hoja ni maisha yako unayoishi baada ya Kuacha Ukristo.
Ila umekurupuka.
Padri kukufundisha Na kukufungisha ndoa ni kwa kuwa wanapewa Elimu kuhusu hayo mambo na wanakuwa wameona , wameshuhudia ndoa nying na wanauzoefu wa namna watu wa ndoa wanavyoishi.
Kwahiyo sababu hii ndio ukaona bora uende Uislam kwa sababu role model wako ni mwenye ndoa 11+ kama Chizi Maarifa .
Sanamu na msalaba zilizoko kanisan haziabudiwi. Ni heshima tu inatolewa. Na ni ishara.
Ka
Kalibu sana ndugu yangu nimependa hoja yako, hivi unaweza ukaupanda muhindi au ukamfuga ng'ombe ukawa unamuheshimu? Nazumgumzia hivyo vitu vyenye uhai,
Sasa inawezekana vipi ukanipa tenda ya kukuchongea sanamu kutokana na ujuzi wangu tena nikawa nalichonga huku nakula bangi langu pembeni halafu nikakuta unaliheshimu hilo sanamu, inaingia akilini kweli?
Mnauhakika gani kama za wahusika maana kipindi wako hai hakukuwepo na teknolojia ya picha?Je ukichonga sanamu bila kuvuta bangi . Nitaliheshimu?.
Hoja sio nani anachonga au anachongaje. Hoja ni heshima.
Msalaba na Zile sanamu ni alama za ibada na sio kuziabudu.
Tuanzie Hapa. Kuna ile ishara ya nyoka wa shaba kipind cha Mussa.
Yahweh aliruhusu ile alama ili aone utiifu na imani kwa wana wa Israel.
Ila sio kwamba wana wa Israel waiabudu.
Je kuna tofaut gan na ishara ya sanamu za bikira Mariam na Yesu za sasahivi?.
SafiNilizaliwa katika imani ya kikristo katika dhehebu la kikatoliki nilibatizwa nikiwa najitambua baada ya kufanya mafundisho,lakini kila kitu tulikuwa tunakalilishwa na siku ya mtihani alikuja Askofu anakuulizwa swali unamjibu,
Nikapata na sakrament ya kitubio na kipaimara yaani naruhusiwa kuungama dhambi zangu kwa padri na kula ule mkate nilijisikia furaha sana
Baadaye nikapate mafundisho ya ndoa kutoka kwa pandre ambaye hajui nini maana ya ndoa ninachokumbuka alisisitiza uvumilivu na kifo ndiyo kitakacho tutenganisha nikafunga ndoa na maisha yakawa yanaendelea
Lakini nilipoingia kwenye Uisilamu niliona kila kitu kipya kwanza kusujudu kuna sheria zake kuna viuonga ambavyo inabidi viguse chini siyo unasujudu tu,kumbuka Musa,Yesu,Mitume na Manabii wote walisujudu hakuna aliyepiga ishara ya msalaba,inamaana Mungu alimfundisha mwanadamu jinsi ya kusujudi bali kufanya ishara ya Msalaba aliyeanzisha ni mwanadamu
Hata kutawadha Mungu ndiye aliyemfundisha Mwanadamu kama hujui huwezi na itakuchukua mda ili kujua, Uisilamu ni Usafi mtu unaswali ukiwa msafi wa mwili na mavazi, huna mikojo wala mavi hata kama kuna watu wanasema Mungu anaangalia roho
Na katika Uisilamu anayeogopwa ni Mungu Allah tena mmoja hana mshirika na kila mnachoomba mnamuomba yeye kwani yeye ndiye aliyeumba kila kitu unachokiona pamoja na binadamu na majini,unapokwenda kuswali sala tano unaenda kama wewe siyo kwa ajili ya nabii au mtume, hapana ni kwa ajili ya Mungu aliyekuumba,na kinapokuja kipindi cha mfungo wa Ramadhani mwezi wa toba unaona kabisa watu wanafanya toba ya kweli na kuacha maasi,maana yake watu wana imani na Mungu wao kama anawasamehe na hawataki kupoteza hiyo fursa
Upande wa ndoa mnaoana kwa wema na mtaachana kwa wema kila mtu anajua ndoa ni safari ndefu siyo rahisi eti mkavumiliane siyo kitu rahisi ndiyo maana watu wanaishi na visasi ndani ya ndoa maana kuna mambo hayasameheki,kuoa mke zaidi ya mmoja kiubinadamu ni kweli kabisa sababu wanawake wako wengi kila mtu akisema aowe mwanamke mmoja tu halafu asichepuke unategemea hao walioko inje wataishije?
Niseme Uisilamu ni Dini iliyokamilika ingawa si mjuzi wa mambo mengi lakini kwa hayo najiona niko sehemu sahihi na salama
Hii ni version gani ya uislam?Uzuri mimi kinywa changu kisafi nimefundishwa kumuheshimu kila mtu na viumbe vya Mwenyezi Mungu hata nguruwe na Mbwa kwangu ni haramu siyo kwamba nikiwaona nianze kuwapiga hapana kama ninachakula nitawapa
Tangu lini Mungu akawa na jinsia🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣Kwahiyo unakubali kuwa mwanamume aitwaye YESU:
kaka huku hupawezi kaka, huku umevamia kaka.Wewe tuludi kule kwenye siasa na mambo ya nchi...Huku utaondoka kapa.Unprecedented level of foolishness, matapeli wa zamani kutokea Mashariki ya Kati waliwakamata na wanaendelea kuwakamata majuha wengi sana. Mmebaki kushindana na kubishana kwenye vitu visivyo na kichwa wala miguu, babu zetu wali-enjoy imani zao kabla ya ujio wa wahuni kutoka mbali huko.
Ndoa ya jinsia moja,wapi imeruhusiwa hiyo ndoa ya jinsia moja?Kama Mungu ameruhusu hakuna tatizo,tatizo ni pale kufanya vitu ambavyo Mungu hajarusu kama ndoa ya jinsia moja
Kalibu kwenye Uisilamu
Sasa mbona hamna ulichokimbia, vp lile jiwe pale macakile kitendo cha kubusu misalaba siku ya ijumaa vitu ambavyo haviongea tena vimeletwa pale kwa msaada wetu wenyewe halafu tunaviinamia mfano sanamu ya Yesu na bikira Maria nikaona hapa sipo penyewe inabidi nianze kumtafuta Mungu wa kweli ndiyo nikaanza kuufwatilia Uisilamu
Sasa unaniuliza mimi tena Muisilamu,hujui kama kuna Viongozi wa dini kutokana na tamaduni zao yaani wazungu wameruhusu ndoa ya jinsia mojaNdoa ya jinsia moja,wapi imeruhusiwa hiyo ndoa ya jinsia moja?
Nimekwambia mbwa na nguruwe kwangu ni haramu,lakini siyo kwamba nikiwaona nianze kuwadhuru,hapana wale ni viumbe wa Mwenyezi Mungu,inawezekana kwangu kukawa na makombo ya chakula niko radhi kuwapa kuliko kuvitupaHii ni version gani ya uislam?
Kwamba muislam wewe nguruwe siyo adui yako tena unaweza ukamlisha ale anenepe afurahi,mkiandika vitu vya uwongo muwe mnaangalia kama vinaleta maana humu wote sisi watu wazima siyo watoto
Hivi Ukristo na Uisilamu upi unasababisha umalaya?unaamini wale mapandri hawafanyagi kitu,au unakijua kipimo cha kuwa pandri wanapimaga nini?Yan zunguka yako yote lengo lako kuu ni kutetea umalaya amna lolote jipya