Usiache kununua ardhi. Niliyojifunza Goba sikufanya makosa Madale

Mzee Alikuwaga na eka kama 8 hiyo 1990s goba sema longtime alizinywa
lilikuwa kama shamba
Nakumbuka na swahiba wake Paul bomani alikuwa na eneo kubwa sana huko + mifugo na bwawa la samaki sijui kama bado wanalo

Ova
 
Mabwepande 2026? Umeshachelewa
 
Kibamba ni wapi unapata eneo la 20*20 kwa milioni sita mkuu.. Juzi nimetoka kuweka kambi hapo luguruni kusaka ardhi kibamba ya ukubwa huo kwa 10M lakini sijatoboa mpaka likizo imeisha nimerudi Arusha


Kule mbezi kwembe pia nilizunguka huku na huko nikaambiwa nikaongeze hela na wala hawaongei mara mbili
 

Luguruni bei imechangamka kidogo.
Ungefika Kibamba CCM. - alaf upande ule wa Kulia ukiwa unatokea mjini. (Kushoto ukiwa unatokea Kibaha).
Mwendo wa 4Km. Na kuna Lami. Panaitwa Kibwegere.
Unapata 20×20 kwa Mill 6 au 7.

Mwaka jana kuna shemej angu nilimuunganishia. Maana kuna jamaa angu kajenga kule na alisikia kuna kiwanja karibu na kwake kinauzwa. Na kwakuwa shemej angu alikuwa anahitaj. nikaunganisha.
Hakuna cha udalali wala nini.
Na kiwanja kikanunuliwa.
 
Misugusugu Nina yo viwanja 20 kwa 20 3M tuu
 

Alaf ngoja nikusanue kitu.

Ukiwa unahitaj kiwanja nenda front mwenyewe. Anzia kwa vijiwe vya boda boda. Jitambulishe. Jifanye kama unayo taarifa tayar kuwa kuna kiwanja kinauzwa ila umepoteza namba ya mtu aliyekuelekeza.
Je hawajasikia kiwanja kinauzwa flan, (hapo ushapita na boda na kukagua eneo gan unataka na lina mark gan maarufu, mfano ccm, garage, sheli, kona kali nk).

then sikiliza majibu ya boda.
Nenda vijiwe hata vitatu vinne.
Pia ukipata info.
Nenda kaa bar flan agiza kinywaj alaf soma mchezo.
Utaona tu mtu anayefanania kama mwenyeji. (Angalia watu wale wa makamu makamu) mfate muombe kuongea na anzia kumdodosa bei na maeneo ya kununua.

Na ukielekezwa sehem . Bas Due deligence muhimu.
Matapeli weng ila ukiwa na utulivu utafanikiwa.

Madalali wanapandisha sana bei ya viwanja.
 
Asante sana
 
Hiyo 2016 kipande vha 20 kwa 20 kilikua milion 3 leo si itakua imefika 5M

Kama ungechukua hilo eneo kwa 1M pengine leo ungeuza kwa pesa nyingi
 
Vijana huu ushauri ufanyieni kazi! Una tu milioni twako kadhaa nunua ardhi hata kama ni shamba! Utakuja kumshukuru huyu mwamba. Mimi najuta huko nitokako laiti ningemsikiliza wife sasa hivi ningekuwa mfalme! Pale mjini viwanja walikuwa wanauza laki 3 mpaka 5 vya 50 x 20. Hela ilikuwapo lakini namgombeza vyote hivyo vya nini! Sasa hivi bila 5m - 7m hupati!
 
Ni wapi huko mbona imepanda thaman haraka hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…