Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 9,548
- 28,817
- Thread starter
- #81
Wakati ndio huu jiraniKweli Goba inakua kwa kasi sana. Mabwepande twende lini sasa jirani yangu?
Wakati ndio huu jiraniKweli Goba inakua kwa kasi sana. Mabwepande twende lini sasa jirani yangu?
Ardhi ni mali. Ardhi haiongezeki, watu ndio wanaongezeka. Sasa hivi hata ukinambia kuna eneo mlimani unauza, nakuja kununua.
Mwaka majuzi ile kama Kuna story zilizuka sijui Goba kaonekana chui kama ulisikia iliishiaje au ilikua chai?
Dogo nipe heshima yangu, wakati fulani mnaona tunacheka nanyi mnaona GenZ wenzenu sioDuh 🙄 Nje ya mada, kipindi wewe unawaza kununua kiwanja wengine tulikuwa tunafuta kamasi bado .
Humu huwa nadhani najibishana na GenZ.
Kumbe ujinga ulikuwa nao Toka kitambo 🤣 🤣 🤣2003 Nilipelekwa kibaha kuoneshwa ardhi pale picha ya ndege. Nikafika eneo husika ni robo kilometer kufika lami
Ile ardhi ilikuwa ekari moja na nusu kasoro.. Yule mzee alitaka 1M tena kwa instalments
Kwenye draw ya gari nilikuwa na na kama 1.2 haina kazi. Yule mzee akanisihi sana nisipaache pale mahali na kama nina laki 2 nimpe kwanza
Kuna kasauti kakaniambia moyoni achana naye huyo anakupanga kwani utakuja kuishi lini huku kwa ujinga wa ujana nikakasikiliza kale kasauti
Nikamwambia mzee Leo sina hela ila nakupa hii 20,000 ya usumbufu.. Akaipokea kisha akasema asante lakini ukiweza ongeza 80,000 itimie laki nikuwekee hii ardhi utanukumbuka. Nikagoma
Tukaondoka na mtu niliyekuja naye kufika Kibaha container bar tukapiga ugali samaki wa nguvu
Tukaondoka mpaka Mbezi kufika pale tukaanza kupiga maji.. Tukaondoka kwenye saa 9 mchana
Kufika saa 11 jioni tuko Mama land bar External .. Bata likaendelea
Saa tatu usiku tukanyanyua kuelekea Moshi Bar Goms! Hiyo haikuwa na come back
Siku iliyofuata kuangalia balance nina kama laki7 na ushee
Mwaka 2016 nikapata kazi Kibaha na kuamua sasa kujiwekeza baada ya ujinga kunitoka, nikasema niende kwa yule mzee
Kufika pale nikakuta palishauzwa na kukatwa viwanja vya 20 kwa 20
Kilikuwa kimebaki kimoja tu bondeni na bei ilikuwa million 3 haipungui hata mia😂
Yaani mil.10 ninunue plot ya kujenga wakati napata ekari 30 eneo ambalo ni chini ya km 7 kutoka lami?Bro umeongea Ukwel mtupu.
Shida vijana ambao wanatakiwa kuwekeza (20's - 30's) bado wako Sinza , kinondoni kijitonyama na hawawez kujua haya.
Wanawaza Mamillion meng. Na kuyapata ndio mtihani.
Maeneo kama Mabwepande, mbopo, msumi, makabe, Kibamba na kule kibwegere . Ukiwa na 6 Mill unapata kiwanja kikubwa wastan wa 20*20.
Kwahiyo Ukiwa na 10+ Mill unapata kaeneo kakubwa tu kutosha kujenga nyumba.
Kijana wakat unasubiria Mill 100 za kununua kiwanja prime areas. Hebu anza na kuwekeza na kiwanja sehem za mbali.
You never know. Unaweza usipate hizo hela ukazeekea nyumba za kupanga.
Unaponunua maeneo Vijijini strictly iwe ni Kwa Ajili ya kuyafanyia uzalishaji mwenyewe au Kwa kukodisha.Tatizo siyo kila maeneo yana panda thamani mkuu ,hicho watu hawataki kuambiwa..kumbuka tanzania kuna mapori mengi mnoo na kwa mtazamo huo kwamba kila eneo linapanda thamani,mababu zetu kule vijijini wasinge kufa masikiini.
Hivo kuna factors muhimu za kuzingatia unapo nunua hayo maeneo,siyo unakupuka tu unaenda kununua eneo mpwapwa vijijin kisa eti yanapanda bei..utakuja ulie
Seems like Sumbawanga mjini 😂😂😂Pole sana Mkuu, umefahamu kuhusu ardhi kwa kuchelewa sana. Nikupe hongera kwa kujifunza kwako. Binafsi nilijufunza kuhusu ardhi mapema sana, nikiwa yanki tuu. Nakupa kisa..
Baada ya kumaliza form six 2008, nasubiri kwenda chuo, nilipiga dili moja ya mbao na wachina. Muda wa kwenda chuo ukafika, nikiwa na hela mkononi. Zile hela Baba yangu akanambia nunua viwanja, maana unakwenda chuo hizo hela utakula zitaisha tuu. sikutaka maana niliona nitazika hela tuu, lakini pia sikutaka mkwaza mshua, lengo langu lilikuwa ni kuvuta ka corona old model nikavimbe nako chuo. Huku nikila 100% ya Bumu la serikali. 😁
Nikanunua viwanja kumi, vinafuatana kwa laki sita kila kimoja, pamoja na hati laki nane, nililipa 8M halmashauri X. Nikapewa zile hati, nikamwachia mshua anitunzie hati. 2010 ukatokea mradi wa maji, Muhindi (Mkandarasi) akawa anatafuta eneo la kuweka yard (Karakana) ya muda, maana alipewa kazi ya kutandika mfumo wa maji mjini mzima. Mradi ulikuwa unafadhiliwa na Benki ya Dunia, JK raisi enzi hizo.
Akapapenda pale kwangu maana palikuwa ni karibu na wanakotegea maji, akanilipa 19M kuweka yard tuu. Akajenga na maofisi ya mabati na mbao pale pale kwangu, na vyoo vya muda yaani kiufupi akapaendeleza japo hakuweka miundombinu ya kudumu. Alikuwa anajenga ofisi za mbao na karakana za mabati.
Viwanja ulikuwa ni mradi wa serikali, serikali imekata viwanja inaviuza kutanua mji. Yaani serikali ilikuwa inabembeleza watu kununua viwanja vile, maana palikuwa pori, kula mtu anasema aah nikakae na nyani kule porini. 😁
Mradi ulipoisha Muhindi, aliniachia manyumba yale ya mbao, mabati kibao na mavyuma chakavu kama yote. Niliuza mavyuma yale, makorokoro kibao. Screpa kibao nilipima aisee, mafundi mchundo wa majiko, kuchomelea walikuwa wanashinda pale kusafisha yard. Nikapata mtaji wa kuvimbia mjini mpaka leo.
Mpaka leo panafahamika kama Majengo kwa Wahindi. Sasa hivi hakuna viwanja kuna manyumba ni mji mpya. Ila mimi bado napangisha yard. 😁
Ukitaka kiwanja mitaa ile, kwa wale ambao hawajajenga basi mnaanzia 8M kwenda juu, hapo ana shida zake muuzaji. 😋
Ardhi ni mali. Ardhi haiongezeki, watu ndio wanaongezeka. Sasa hivi hata ukinambia kuna eneo mlimani unauza, nakuja kununua.
FactSehemu siyo mpaka uishi speed ndogo ya kufikili jenga pangisha
Wapo kibao tu, ndio haohao wlitoka mijin wakauz wakanunua mapori huko mabwepande sijui viwege Bunju, madale na ndio haohai wanauza uza mpaka leo. Ukiona mtu kanunua bunju ndan ya miaka hii 10 ujue kauziwa na haohaoSijui sana ila kwa uzoefu wangu wilaya ya Kinondoni kuwakuta Wazaramo ni hadimu sana.
Lakini pia ni watu rahisi sana kuuza maeneo yao tena kwa bei ndogo huwa wanahamishwa
Kumbe ujinga ulikuwa nao Toka kitambo 🤣 🤣 🤣
Kazi ya mama kubadili goba
View: https://www.instagram.com/reel/DU8KSMcDN7X/?igsh=MXFudXY0eXFrMm8zZA==
On serious note nalihitaji hilo eneoYaani mil.10 ninunue plot ya kujenga wakati napata ekari 30 eneo ambalo ni chini ya km 7 kutoka lami?
Haha sawa lakini mimi sio GenZ.Dogo nipe heshima yangu, wakati fulani mnaona tunacheka nanyi mnaona GenZ wenzenu sio
Unajua ni vile tu sisi wa kizazi cha millenials ni watu moja poa sana, huwa tunajua kuishi na GenZ mnatuita mabroo.
Shida ni Generation X wameshindwa kuwaelewa
Seems like Sumbawanga mjini 😂😂😂
Nimenunua Madale miaka hiyo sijaona Wazaramo, kama wapo maeneo hayo kwa uchache sana Temeke ndio najua ina Wazaramo kwa wingi. Hata kama wapo huwa sio watu wa kujichanganya na jamii zilizistaarabika piaWapo kibao tu, ndio haohao wlitoka mijin wakauz wakanunua mapori huko mabwepande sijui viwege Bunju, madale na ndio haohai wanauza uza mpaka leo. Ukiona mtu kanunua bunju ndan ya miaka hii 10 ujue kauziwa na haohao
Hahaa haya usije kusema millenialHaha sawa lakini mimi sio GenZ.
Umesema vyemaVijana msifanye makosa tuliyofanya kaka zenu. Kama uwezo upo wekeza kwenye viwanja/majengo. Ujana maji ya moto