GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Hivi ni kweli watu wanaopinga uwepo wa Mungu wanaamini hivyo kwa mioyo yao? Sidhani!
Kama wapo, ni wachache miongoni mwa wengi wanaodai hivyo. Na kama kweli mtu hafahamu kuhusu uwepo wa Mungu na UWEZO Wake, ni sahihi kumwelewesha, lakini kama anapinga kwa lengo la kupinga ni kupoteza muda kujaribu kumweleza.
Nina mashaka kuwa huenda wanaodai Mungu hayupo, hawafanyi hivyo kwa sababu hawajui, bali wameamua kuwa wapinzani wa Mungu. Kwa lugha nyingine, wameamua kwa hiyari yao kumsaidia Shetani kuwapotosha watu wa Mungu.
Na kama mtu kachagua kuwa upande wa Shetani, ni busara kujihadhari unapoamua kumjibu. Labda, anatafuta ama kukukwaza tu au kuidhoofisha imani yako. Usimpe hiyo nafasi.
Shetani hajabadilisha mbinu. Si mbunifu. Mbinu zile zile alizozitumia zamani kuwaangusha watu wa Mungu ndizo anazozitumia hata sasa.
Unakumbuka alivyomdanganya Eva? Alijua fika kuwa Adam na mkewe waliumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, lakini bado aliwaambia wakikaidi Maagizo ya Mungu, watafanana na Mungu.
Watafananeje na Mungu na huku walikuwa wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu? Tayari walikuwa wanafanana na Mungu! Shetani alichotaka ni kuwafanya wamkosee Mungu kwa kukaidi Agizo Lake kwao.
Alimwambiaje Yesu? Alifahamu kwa usahihi kabisa kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, lakini bado alijaribu kumtia mashaka kwa namna ile ile aliyowaangusha Adam na Eva. Alimwambia, "Ikiwa Wewe ni Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate"
Hizo kauli zilizotumiwa na Shetani kuwaangusha Adam na Eva dhambini na aliyojaribu kumlaghai nayo Yesu zinatofautianaje na za watu wanaotaka wathibitishiwe kuwa Mungu Yupo?
Shetani alilenga kumfanya mwanadamu wa kwanza asimwamini Mungu, akafanikiwa. Ndicho alichokusudia pia kwa Yesu, lakini akaangikia pua.
Ni bora unapoona watu kama hao wameibua maswali yenye lengo la kukejeli au kubishana, ukakaa kimya, au ikibidi kuwajibu, ukafanya hivyo kwa tahadhari. Labda tu kama itabainika kuwa lengo lao ni kutaka kujua na si vinginevyo. Kinyume na hapo, ni kupoteza muda kubishana nao.
Akikukejeli, usimrudishie. Ukimrudishia kejeli ni sherehe kwa Shetani. Ndicho anachotafuta. Anataka umkasirishe Mungu.
Akikutukana, kaa kimya. Shetani angetamani na wewe ungetukana, tena kwa tusi kubwa kuliko la aliyekutukana.
Chunga usemi wako. Ukiona utakachokisema hakitakuwa na msaada, ni bora ukae kimya. Au umjibu kwa kumkumbusha kuwa Mungu anampenda. Akijibu kwa jazba, endelea kumwambia, "MUNGU ANAKUPENDA", halafu utaona kama ataendelea na kejeli zake au la.
Narudia tena! Wengi wa wanaopinga juu ya uwepo wa Mungu huenda wanafanya hivyo kwa lengo la kupotosha wenye imani haba, na si kwamba hawajui kuwa Mungu Yupo.
Shauku ya Shetani ni kuona kuwa watu wengi wanaamini Shetani hayupo. Anajua akifanikiwa kuwaaminisha kuwa hayupo, ataweza kuwaaminisha pia kuwa Mungu hayupo. Akishindwa kuwaaminisha hivyo, atatafuta mbinu ya kuwafanya watu waamini kuwa ana nguvu sana.
Shetani ni muongo na baba wa uongo. Maisha yake ni uongo. Usiiingie kwenye mtego wake.
Mungu Yupo, tena Yu Hai. Na Shetani naye pia yupo, na anajua kuwa mwisho wake ni mbaya tu, hana namna ya kuukwepa.
Lakini Mungu ni Mzuri na ni Mkuu sana, hana mpinzani.
Ni hayo tu.