Acha uongo mkuu.
Hii tabia ya kumwita shetani mwongo wakat ninyi ndo waongo ni unafiki wa hali ya juu.
Mosi, Shetani hakumdanganya Eva ila shetani alimwambia Eva ukweli ambao Mungu hakutaka waujue.
Shetani alimwambia Eva kuwa wakila matunda ya mti huo watafumbuliwa macho na watakuwa kama Mungu kwa kujua mema na mabaya. Baada ya Eva na Adam kula matunda kweli walifumbuliwa macho yao na wakatambua kuwa wako uchi na wakajificha Mungu asiwaone(mwa 3:1-11)
Pili, Shetani alimwambia Eva wakila matunda waliyokatazwa hawatakufa. Na hii haikuwa uongo ilikuwa ni kweli mana hata Mungu mwenyewe anakili hapa (mwa 3:22-24). Baada ya Mungu kujua Adam na Eva wamekuwa kama yeye kwa kujua mema na mabaya akaamua kuwafukuza katika bustani ya Eden ili wasije kuchukua matunda ya mti wa uzima wakala ili wakaishi milele. Kwa hiyo wangefanikiwa kula hilo tunda basi wasingekufa.
Naomba niishie hapa maana mpaka hapa sijaona uongo wa shetani isipokuwa wewe na Eva ndo waongo kwa kutaka kugeuza ukweli kuwa uongo.