Kuna kizazi kitafika wazo la uwepo wa Mungu litapotea story za yehova, allah n.k zitabaki makumbusho na library tu
Boss, Vizazi vimekuwa vikipita na vitaendelea kupita, sayari ya Dunia kama tuijuavyo huenda ikapita, Kila wakati nyota zinakufa na kuzaliwa upya, hatuna uelewa hata wa tafsiri halisi ya muda,
Nilikuwa natazama makala ya how universe work wanasayansi wakawa wanazungumza kuhusu uelewa wa binadamu linapokuja suala la black holes, mwanasayansi mmoja akasema anaamini black hole ni portal ya time travel na siku mtu akigonga mlango wako akasema yeye ni mjukuu wako wa miaka ya mbele usibamize mlango, huenda binadamu kaweza kusafiri ndani ya black holes. Kama nadharia yake ni sahihi na ikifikia hatua hiyo muda kama tuujuavyo utakuwa na tafsiri tofauti kabisa na haitajalisha una umri gani maana unaweza kusafiri na kukutana na wewe ukiwa mdogo.
Sasa usihitimishe mambo usiyo na uelewa nayo, hitimisha yale uliyo na uelewa nayo.
YEHOVA, ALLAH N.K ni majina ya lafudhi uijuayo wewe, ikipita haimaanishi kuwa wazo la MUNGU limepita, kabla ya lugha unayoifahamu palikuwepo na lugha na MUNGU alitamkwa kwa lafudhi tofauti. Huna hakika iwapo kabla ya vizazi unavyovisoma katika historia hapakuwepo na vizazi ambavyo vilikuwa more advance kuliko sasa na hatma yao ilikuaje na still wazo la uwepo wa MUNGU lipo hivyo usihitimishe kuhusu wakati ujao, miaka mingi mbele ambapo hujui nini kitaipata dunia na iwapo binadamu ataendelea kuwa kiumbe chenye akili kuliko wengine au patatokea kiumbe kipya. USIHITIMISHE USIYO NA UELEWA NAYO BOSS.
Suala sio kukubalika suala ni limekubalika katika namna ipi. Kama suala limekubalika zama za ujinga hata kama ni uongo basi liendelee kukubalika tu? Hapana.
Boss Uongo unaupima vipi? Nilikuuliza iwapo nimeota nakimbizwa na ngiri nikashtuka na jasho linantoka, nikishindwa kuthibitisha kuwa palikuwa na ngiri aliyenikimbiza inamaanisha kuwa mimi ni muongo ilihali nilimuona ngiri na nikakimbia? Katika wakati ule ambapo nakimbia, wakati wa ndoto, nipo katika uongo kwasababu nipo katika ulimwengu wa fikra? Uhalisia wa ulimwengu wa fikra ni upi? Usiseme haupo sababu upo na unaathiri maisha ya binadamu ya kila siku.
Wazo la uwepo wa Mungu limeendelea kuwepo kwa sababu watu tulikalilishwa tangu utotoni lakini sio kwa sababu ya usahihi wake.
Mkuu Wazo la uwepo wa MUNGU halikuanza wakati wa utoto wako. Hata ukristo na uislamu tu una historia ndefu kuliko babu zako wengi sana. Wazo la uwepo na MUNGU ni historia ya uwepo wa binadamu duniani na huenda vipo sambamba au huenda binadamu wa kwanza kuamini kuhusu wazo la MUNGU naye alirithi huko alipotoka kwenye evolution iwapo tutarely on science badala ya maandiko ya kiimani.
Wewe kwa akili ulizonazo sasa hivi ingetokea ndio umesoma biblia kwa mara ya kwanza alafu ukutane na story za nyoka anaeongea bila shaka ungejua huo ni uongo tu.
Tatizo lako ni biblia na mafundisho ya ukristo au wazo la uwepo wa MUNGU? Huenda hata nyoka aliyetamkwa siyo nyoka unayemfahamu. Kama unataka kuuchunguza ukristo au uislamu uchunguze, uelewe kisha hitimisha ila usichukulie mambo juu juu na kuhitimisha. Biblia imetafsiriwa kutoka vizazi vya kale na huwezi thibitisha usahihi wa tafsiri, wanasema unamhitaji roho mtakatifu kuielewa biblia. Huyo roho unaye? Wanaposema roho mtakatifu unaelewa? Au unataka kurekebisha mashine ambayo hujui inavyofanya kazi na ina manual iliyoandikwa kwa lugha usiyoifahamu?
Ndugu yangu tukisema tuamini bila uthibitisho tutatoa nafasi ya kuleta madai yoyote ya kufikirika.
Ulimwengu wa fikra usihitimishe kuwa haupo, pengine wapo wanaouishi katika uhalisia wako uliouzoea. Ndugu yangu hii dunia ina mengi tusiyoyafahamu, tusihitimishe tu kila kitu kiwepesi. Hata sayansi haifanyi maitimisho kirahisi rahisi.
Ulivyotoa mfano wa muundo wa energy kuwa katika mpangilio ambao ni supportive kwa maisha binadamu iyo ni sayansi pia. Kama umetoa maelezo ya kisayansi kuonesha uwepo wa Mungu kwanini ukatae maelezo ya kisayansi kupinga uwepo wake?
Sayansi haijawahi hitimisha kuwa hakuna MUNGU. Unless uanze kumpa sifa fulani fulani kisha reasoning na logic ziingizwe hesabu zikate kuwa mungu wa sifa hizo yupo. Otherwise sayansi imekuwa ikisema hakuna ushahidi wa uwepo wa MUNGU siyo hakuna MUNGU. Hii itaendelea kuwa hivi vizazi na vizazi.
Nimebase kwenye ukristo na uislamu kwa sababu ndizo dini ambazo wewe umefanya rejea ya mada yako.
Mimi sijaanzisha mada, nimetoa hoja kwenye mada.
Ukristo na Uislamu ni dini kama dini nyingine. Ni matokeo ya kutafsiri wazo la uwepo wa MUNGU. Chukulia dini kama vazi inayositiri utupu. Mavazi ni mengi na ya aina nyingi na kila mtu huyakosoa na kuyasifia kutokana na tafsiri yake ya uzuri na ubaya wa vazi ilihali lengo ni kusitiri tu.
Ndivyo dini zilivyo. Lengo ni kumtafsiri MUNGU ambaye huwezi kumuwakilisha katika ukubwa wa wazo lake, lazima umvike vazi la dini.
Hata wewe ukitaka kuanzisha dini kuna namna utamtafsiri MUNGU na namna utakavyomwabudu. Sasa Hoja hapa ni uwepo wa MUNGU siyo uwepo wa dini kama vazi la kumtafsiri MUNGU.
Tumekubaliana kuwa MUNGU ni wazo linaloishi ili kuyapa uhalali yale yaliyo nje ya uwezo wa binadamu.
Tukakubaliana kwamba ni wazo lisilo na mwisho as long as linaishi sababu siku zote binadamu kuna jambo litakuwa nje ya uwezo wake na hatakuwa na majibu na kwa wakati huo wazo la MUNGU litamjia wakati akitafuta majibu.
Basi uelewe kwamba wazo la MUNGU ni pana sana, halielezeki bila kulivalisha vazi la dini, katika kulivika vazi la dini ndipo sifa za MUNGU kutegmeana na dini huzaliwa na ndipo wakosoaji kama wewe hutokea, Otherwise huna hoja inayojisimamia ya kulipinga wazo la uwepo wa MUNGU nje ya dini.