Usibishane na anayepinga kuwa Mungu yupo

Usibishane na anayepinga kuwa Mungu yupo

Kitu kilichopo kinathibitishika kuwa kipo.

Kila siku unaambiwa kuthibitisha hilo unashindwa.

Na unadhindwa kwasababu Mungu huyo hayupo.

Mazoea na urithi wa mapokeo kutoka zama za giza na ujinga ndo umetufikisha hapa.

Your psychology is totally corrupted
Huo ndio ukweli

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Je Nishati yenyewe iliwezaje kuwepo kutoka kwa kutokuwepo kwa kitu?

Yani kabla ya uwepo wa nishati, Nini kilikuwepo kabla?
Swali lako linakuwa gumu kwangu kwa sababu mimi ni sehemu ya nishati yani ni sawa mtoto tumboni mwa mama yake ahoji uwepo wa mama yake, siku akizaliwa atapata jibu vivyo hivyo nami sku nikitoka kwenye umbile hili nikarudi kuwa nishati nitajua chanzo changu bila shaka .
 
Unachosugest ni kuwa kuna uwezekano kuwa nguvu hii haikuwa imegawanyika hapo kabla na ndio matokeo ya uwepo wa mfumo uliopo?
Mfano maji ni maji ila ili yawe na utofauti lazima yatoke kwenye badiliko moja kwendajingine ili yaweze kupata majina tofauti mfano mvuke na barafu ila haiwezi kubadili asili kuwa ni maji .
 
Sasa mkuu,

Energy yenyewe Kisayansi wanadai kwamba [emoji116]

"Energy cannot be created or destroyed but it can be transformed from one form to another"

Sasa "Energy" iliwezaje ku Exist kutoka kwa kutokuwepo kitu?
"Kutokuwepo kitu" Mkuu unajua There is no such thing as nothingness, everthing is something. Yaani hakuna kitu kinaitwa nothing, "kutokuwepo kitu"(Nothingness), ni concept tu ya kutafsiri uhalisia wa vilivyopo. Ni kama herufi 0. Ipo pale ili kurahisisha tafsiri ya uhalisia wa 1,2,3 n.k

Sasa Kama energy haiwezi kutengenezwa wala kuharibiwa tafsiri yake ni nn? Inamaana Energy ni kila kitu ikiwemo hichi tunachokiita "kutokuwepo kitu" na yote tuyaonayo ni matokeo yake.

Kiswahili ni kigumu japo ndo lugha yetu kuu na ya kwanza ila ninachomaanisha ukiondoa kila kitu inabaki energy na yenyewe ipo tu haijatengenezwa wala haiharibiki. Angalau hili ndilo tujualo binadamu mpaka sasa.
 
Yani hili swali lake linajiviringa kama swala ya kuku na yai nani wa kwanza.
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Swali lako linakuwa gumu kwangu kwa sababu mimi ni sehemu ya nishati yani ni sawa mtoto tumboni mwa mama yake ahoji uwepo wa mama yake, siku akizaliwa atapata jibu vivyo hivyo nami sku nikitoka kwenye umbile hili nikarudi kuwa nishati nitajua chanzo changu bila shaka .
Inategemeana na mifumo ya utambuzi.

Assume umetoka katika huu mfumo, je mfumo mpya utakaokuwa nao utakuwa na mfumo wa utambuzi?

Au kabla ya kuwa na mfumo huu wa ubinadamu ulio nao ulikuwa na mfumo wa utambuzi? Ukumbuke kwa mfumo huu tulionao, ubongo ndo unawezesha sisi kuwa na utambuzi.

Hii concept kwa sisi tunaoamini ndo inanifanya nifikiri kuhusu imani ya siku ya hukumu kwa waliokwisha kufa, Je huu utambuzi tulionao hizi bongo zetu ndo perment memory storage au kuna server somewhere na bongo zetu ni receiver tu kama unavyoplay nyimbo zilizopo kwenye simu kwa kutumia redio ya gari? Sijajua bado.

Hatahivyo, huwa tuna mipaka ya kuhoji haya mambo kiimani na hili hunifanya nitafiti nje ya imani.
 
Yani hili swali lake linajiviringa kama swala ya kuku na yai nani wa kwanza.
Hahaha, Well nasikia sikia kuwa alianza kuku sababu ya protein inayopatikana kwenye kasha la yai haipatikani popote zaidi ya kwa kuku.
 
Inategemeana na mifumo ya utambuzi.

Assume umetoka katika huu mfumo, je mfumo mpya utakaokuwa nao utakuwa na mfumo wa utambuzi?

Au kabla ya kuwa na mfumo huu wa ubinadamu ulio nao ulikuwa na mfumo wa utambuzi? Ukumbuke kwa mfumo huu tulionao, ubongo ndo unawezesha sisi kuwa na utambuzi.

Hii concept kwa sisi tunaoamini ndo inanifanya nifikiri kuhusu imani ya siku ya hukumu kwa waliokwisha kufa, Je huu utambuzi tulionao hizi bongo zetu ndo perment memory storage au kuna server somewhere na bongo zetu ni receiver tu kama unavyoplay nyimbo zilizopo kwenye simu kwa kutumia redio ya gari? Sijajua bado.

Hatahivyo, huwa tuna mipaka ya kuhoji haya mambo kiimani na hili hunifanya nitafiti nje ya imani.
Mfumo huu wa utambuzi tulio nao upo kifizikia zaidi ,ili tuweze kuishi kwenye hii dimension , mfano ili maji yaweze kuwa barafu lazima yakae pamoja kwa mgandamizo wa aina yake , ili tu yaweze kuwa kwenye hiyo dimension , ila ikifika mda wa kubadilika kwenye dimension nyingne yana change hata mfumo wake, au mbegu ili iweze kubadilika kuwa mmea lazima ioze kabsa alafu ipande tena kama mmea.

Apo kwenye matendo mema na mabaya inatumika zaidi low of attraction , kile unachopanda ndicho utakachokivuna.

Ukipenda watu, watu watakupenda , ukiheshimu utaheshimiwa hizo ni principles tu za hii dimension .

Hii dhana ya kuchomwa moto ipo sahihi kuwekwa kwa sababu watu wengi waliishi kwenye matrix ,nakupoteza ule uwezo wa kujitambua , mfano kuna mwanafunzi anasoma ili awe na maisha mazuri na kuna mwingne anasoma ili asichapwe , anaejitambua ni yupi apo ? Ukiondoa fimbo kwa huyo mmoja hatasoma kamwe, ila huyo mwingne wala hana shida .
 
Hahaha, Well nasikia sikia kuwa alianza kuku sababu ya protein inayopatikana kwenye kasha la yai haipatikani popote zaidi ya kwa kuku.
Na yeye kuku alianzia wap?
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Zaidi ya asilimia 99% huwa ni mawakala wa shetani. Usione hivyo muda wanapokuwa wanapinga, nao wanakuwa wako kwenye mavuno kama ambavyo wewe huwa unafanya mikutano ya injili ili kuokoa roho za watu
Binafsi nafikiri, katika hao wanaopinga, kuna makundi matatu hivi:
1. La wasiojua lolote kuhusu Mungu, kwa hiyo ni rahisi kuwadanganya.

2. Wanaopinga lakini hawamaanishi wanachosema, wanataka tu kubisha kwa lengo la kujifurahisha au kutoa changamoto.

3. Wanaojua Mungu Yupo, lakini wameamua kupotosha.
Wanapopinga wanakuwa wapo kazini. Anapofanikiwa kumpotosha mtu, huenda kuna ujira anaoupata kutoka kwa aliyemtuma kupotosha watu wa Mungu.
 
Hivi ni kweli watu wanaopinga uwepo wa Mungu wanaamini hivyo kwa mioyo yao? Sidhani!

Kama wapo, ni wachache miongoni mwa wengi wanaodai hivyo. Na kama kweli mtu hafahamu kuhusu uwepo wa Mungu na UWEZO Wake, ni sahihi kumwelewesha, lakini kama anapinga kwa lengo la kupinga ni kupoteza muda kujaribu kumweleza.

Nina mashaka kuwa huenda wanaodai Mungu hayupo, hawafanyi hivyo kwa sababu hawajui, bali wameamua kuwa wapinzani wa Mungu. Kwa lugha nyingine, wameamua kwa hiyari yao kumsaidia Shetani kuwapotosha watu wa Mungu.

Na kama mtu kachagua kuwa upande wa Shetani, ni busara kujihadhari unapoamua kumjibu. Labda, anatafuta ama kukukwaza tu au kuidhoofisha imani yako. Usimpe hiyo nafasi.

Shetani hajabadilisha mbinu. Si mbunifu. Mbinu zile zile alizozitumia zamani kuwaangusha watu wa Mungu ndizo anazozitumia hata sasa.

Unakumbuka alivyomdanganya Eva? Alijua fika kuwa Adam na mkewe waliumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, lakini bado aliwaambia wakikaidi Maagizo ya Mungu, watafanana na Mungu.

Watafananeje na Mungu na huku walikuwa wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu? Tayari walikuwa wanafanana na Mungu! Shetani alichotaka ni kuwafanya wamkosee Mungu kwa kukaidi Agizo Lake kwao.

Alimwambiaje Yesu? Alifahamu kwa usahihi kabisa kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, lakini bado alijaribu kumtia mashaka kwa namna ile ile aliyowaangusha Adam na Eva. Alimwambia, "Ikiwa Wewe ni Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate"

Hizo kauli zilizotumiwa na Shetani kuwaangusha Adam na Eva dhambini na aliyojaribu kumlaghai nayo Yesu zinatofautianaje na za watu wanaotaka wathibitishiwe kuwa Mungu Yupo?

Shetani alilenga kumfanya mwanadamu wa kwanza asimwamini Mungu, akafanikiwa. Ndicho alichokusudia pia kwa Yesu, lakini akaangikia pua.

Ni bora unapoona watu kama hao wameibua maswali yenye lengo la kukejeli au kubishana, ukakaa kimya, au ikibidi kuwajibu, ukafanya hivyo kwa tahadhari. Labda tu kama itabainika kuwa lengo lao ni kutaka kujua na si vinginevyo. Kinyume na hapo, ni kupoteza muda kubishana nao.

Akikukejeli, usimrudishie. Ukimrudishia kejeli ni sherehe kwa Shetani. Ndicho anachotafuta. Anataka umkasirishe Mungu.

Akikutukana, kaa kimya. Shetani angetamani na wewe ungetukana, tena kwa tusi kubwa kuliko la aliyekutukana.

Chunga usemi wako. Ukiona utakachokisema hakitakuwa na msaada, ni bora ukae kimya. Au umjibu kwa kumkumbusha kuwa Mungu anampenda. Akijibu kwa jazba, endelea kumwambia, "MUNGU ANAKUPENDA", halafu utaona kama ataendelea na kejeli zake au la.

Narudia tena! Wengi wa wanaopinga juu ya uwepo wa Mungu huenda wanafanya hivyo kwa lengo la kupotosha wenye imani haba, na si kwamba hawajui kuwa Mungu Yupo.

Shauku ya Shetani ni kuona kuwa watu wengi wanaamini Shetani hayupo. Anajua akifanikiwa kuwaaminisha kuwa hayupo, ataweza kuwaaminisha pia kuwa Mungu hayupo. Akishindwa kuwaaminisha hivyo, atatafuta mbinu ya kuwafanya watu waamini kuwa ana nguvu sana.

Shetani ni muongo na baba wa uongo. Maisha yake ni uongo. Usiiingie kwenye mtego wake.

Mungu Yupo, tena Yu Hai. Na Shetani naye pia yupo, na anajua kuwa mwisho wake ni mbaya tu, hana namna ya kuukwepa.

Lakini Mungu ni Mzuri na ni Mkuu sana, hana mpinzani.

Ni hayo tu.
Hata wewe mwenyewe unakwenda tofauti na kanuni ya Mungu,huna tofauti na anayesema Mungu hayupo
 
Binafsi nafikiri, katika hao wanaopinga, kuna makundi matatu hivi:
1. La wasiojua lolote kuhusu Mungu, kwa hiyo ni rahisi kuwadanganya.

2. Wanaopinga lakini hawamaanishi wanachosema, wanataka tu kubisha kwa lengo la kujifurahisha au kutoa changamoto.

3. Wanaojua Mungu Yupo, lakini wameamua kupotosha.
Wanapopinga wanakuwa wapo kazini. Anapofanikiwa kumpotosha mtu, huenda kuna ujira anaoupata kutoka kwa aliyemtuma kupotosha watu wa Mungu.
Unavyosema Mungu yupo tayari umeonyesha mapungufu makubwa kwa Mungu kwamba yupo sehemu fulani tu kama kiumbe , anatawala tokea huko , mambo yanayoendelea yeye hausiki nayo anahusika na mazuri tu mabaya no, maana yake sio muweza wa yote.

Moja kwa moja umeshampa personality , ila kama yupo kila mahali na ni roho ,ata kwako yupo na kinachoendelea apa duniani na yeye ni mhusika .

Kuna namna tumerithi tu vitu bila kujua walio tangulia walifikiri vipi kuamini hivyo vitu.
 
Sema Huwezi kujenga hoja na kujibu hoja na maswali ya Atheist, wanao amini Mungu hayupo.

Usiseme kwamba waamini Mungu hayupo(Atheists) hawajui lolote kuhusu Mungu,

Wakati mkiulizwa maswali yanayo husu uwepo wa huyo Mungu hamuwezi kuyajibu mnabaki na vitisho vyenu vya kidini vya Jehanamu na moto wa milele.

Sasa naku uliza hivi, Mungu mwenye kujua yote na mkuu wa vyote ,Alishindwaje kuwa na "Direct access" kwa viumbe vyote kumtambua yeye yupo kwa wakati mmoja pasipo kuwepo utata wa kiimani na kidini?
 
Mungu ANAKUPENDA.
 
Unavyosema Mungu yupo tayari umeonyesha mapungufu makubwa kwa Mungu kwamba yupo sehemu fulani tu kama kiumbe , anatawala tokea huko , mambo yanayoendelea yeye hausiki nayo anahusika na mazuri tu mabaya no, maana yake sio muweza wa yote.

Moja kwa moja umeshampa personality , ila kama yupo kila mahali na ni roho ,ata kwako yupo na kinachoendelea apa duniani na yeye ni mhusika .

Kuna namna tumerithi tu vitu bila kujua walio tangulia walifikiri vipi kuamini hivyo vitu.
Hawa wafia dini hawana hoja za kuwajibu Atheists

Wana ishia kuzunguka zunguka na kukutishia hofu zao za kidini za Jehanamu na moto wa milele pasipo kutoa majibu.
 
Lakini Mungu ANAKUPENDA!
Mkuu, Mie sina shida na uwepo, kiukweli ningekuwa na furaha kama kweli Mungu angekuwepo kama anavyoelezwa kwa sifa zile, kwani hata kusingekuwa na mateso, vifo, njaa wala chochote kibaya.

Ningefurahia upendo huo.

Lakini kusema tu kuwa Mungu huyo anayedaiwa kuwepo (ili hali hayupo) eti ananipenda halafu kaumba ulimwengu huu wenye mabaya kuwezekana, hyo ni contradiction tayari.
Na contradiction hii inanivuta kuhitimisha kuwa huyo Mungu wa design hiyo hawezekani kuwepo.

Kwahyo dhana ya Mungu huyu ni hadithi tu, wala haina ukweli wowote ule.

Hakuna kitu kinaitwa Mungu, Mungu ni dhana tu ya kutungwa.

Hata kwenye somo la kiswahili, nlisoma kwenye nomino za dhahania, moja wapo ya mifano iliyotolewa nakumbuka miwili, ambayo ni njaa na Mungu.
 
Back
Top Bottom