Usibishane na anayepinga kuwa Mungu yupo

Lakini mkuu huo mfumo wa energy haukutokea tu from the first place ukaweza kujiendesha kimpangilio kabla ya hapo kulikua na mfulugano mpaka hali ilipokuja kutulia. Evolution ni mfumo wa trials and errors, kila kilichopo ulimwenguni kilianza na chaos kwaiyo haiingii akilini kusema uyo intelligent creator ambaye tunaambiwa ni mjuzi wa yajayo alitumia mfumo wa kubahatisha bahatisha kiasi hiki. Bila shaka mpangilio wa ulimwengu hii ni kazi ya mfumo ambao hauna ufahamu wala mipango yoyote, kila kitu kimetokea tu by-chance
 
Naona Shetan kamwingia na huyu
 
Unaposema mjuzi wa yajayo unamaanisha nini boss?
 
Unaposema mjuzi wa yajayo unamaanisha nini boss?
Namaanisha yule invisible old man aliyepo uko mawinguni anaeabudiwa na waumini wa hizi dini kubwa mbili zilizosambaa sana(ukristo na uislamu). Ujuzi wa yajayo ni moja ya sifa zake
 
Namaanisha yule invisible old man aliyepo uko mawinguni anaeabudiwa na waumini wa hizi dini kubwa mbili zilizosambaa sana(ukristo na uislamu). Ujuzi wa yajayo ni moja ya sifa zake
Ukiufuta ukristo na uislamu kwenye kichwa chako ambao ndo tatizo lako lilipo, MUNGU unamtafsiri vipi?
 
Kiuungwani kitu ambacho hakionekani ni lazima uhoji. Mf. Yesu alizaliwa Betlehemu, uliambiwa tu, je ulihoji? Kama hatukuhoji ujue ndio sababu ya hiyo imani kuenea sehemu kubwa duniani, hasa ulimwengu wa tatu.
 
Naye ndiye Aliyeitandaza ardhi na Akaweka humo majabali na mito. Na katika kila matunda akafanya humo namna mbili (dume na jike). Huufunika usiku juu ya mchana Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wenye kufikiri.

Na katika Ishara Zake ni umbo la mbingu na ardhi, na hitilafu ya lugha zenu na rangi zenu. Kwa yakini katika hayo zimo Ishara kwa wenye elimu.

Na katika Ishara Zake ni kulala kwenu kwa usiku na mchana, na (pia) kutafuta kwenu fadhili Yake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaosikia

Na katika Ishara Zake ni kuwaonyesheni umeme kwa hofu na tumaini, na kuteremsha maji kutoka mawinguni, kwayo Huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Bila shaka katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaofahamu.

Na katika Ishara Zake ni kuwa Amewaumbieni katika jinsi yenu wake ili mpate utulivu kwao, naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaofikiri.

Na katika Ishara Zake ni umbo la mbingu na ardhi, na hitilafu ya lugha zenu na rangi zenu. Kwa yakini katika hayo zimo Ishara kwa wenye elimu.

Na katika Ishara Zake ni kulala kwenu kwa usiku na mchana, na (pia) kutafuta kwenu fadhili Yake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaosikia.

Na katika Ishara Zake ni kuwaonyesheni umeme kwa hofu na tumaini, na kuteremsha maji kutoka mawinguni, kwayo Huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Bila shaka katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaofahamu.
 
Ukiufuta ukristo na uislamu kwenye kichwa chako ambao ndo tatizo lako lilipo, MUNGU unamtafsiri vipi?
Mungu ni wazo la uwepo wa kiumbe mkuu wa kufikirika ambalo lilibuniwa na binadamu ili uyo kiumbe wa kufikirika atumike kama jibu la mambo yote ambayo yapo juu ya uwezo na maarifa ya binadamu.
 
Mungu ni wazo la uwepo wa kiumbe mkuu wa kufikirika ambalo lilibuniwa na binadamu ili uyo kiumbe wa kufikirika atumike kama jibu la mambo yote ambayo yapo juu ya uwezo na maarifa ya binadamu.
Ok boss, Sasa majibu ya maswali yote yako ndani ya uwezo wa binadamu tayari?

Kuhusu kufikirika: Kitu kikiwa ni wazo tafsiri yake ni kwamba hakipo?
 
Ok boss, Sasa majibu ya maswali yote yako ndani ya uwezo wa binadamu tayari?

Kuhusu kufikirika: Kitu kikiwa ni wazo tafsiri yake ni kwamba hakipo?
Hapana bado binadamu hana majibu yote kuhusu ulimwengu kutokana na ugeni wake mfano leo hii hatujui ulimwengu ulitokea wapi ndio maana tunampachika Mungu hapo tukija kujua chanzo cha ulimwengu litaibuka swali jingine hicho chanzo cha ulimwengu chanzo chake ni nini? tutampachika tena Mungu hapo. Unaona hapo kila tunaporudi kwenye backward chain lazima tutafika point ambayo maarifa ya binadamu yamefika mwisho na hapo ndipo anapachikwa Mungu. Pale ambapo maarifa yetu yamefika mwisho ni vya tukakubali hapa hatujui, binafsi naona ni bora kubaki na swali ambalo currently halina jibu kuliko kubeba tu jibu lolote hata kama halina uthibitisho wala mtililiko wa kimantiki ilimradi tu swali husika lisiwe unfilled.

Hili wazo likubalike lazima liwe na supported evidence. Ni uthibitisho unatangulia ndipo wazo linakubalika. Kinyume na hapo wazo husika linabaki kuwa story ya kutungwa tu. Ukisema chanzo cha binadamu ni udongo ulikusanywa ukapuliziwa pumzi ndio akatokea binadamu lazima ueleze in machenism iyo inawezekana vipi ndio wakuamini sio kuwataka watu waamini tu mawazo yako kwa kuwatishia wasipoamini utawatupa kwenye tanuli la moto.
 
Reactions: Tsh
Ok boss, Sasa majibu ya maswali yote yako ndani ya uwezo wa binadamu tayari?

Kuhusu kufikirika: Kitu kikiwa ni wazo tafsiri yake ni kwamba hakipo?
Hapana bado binadamu hana majibu yote kuhusu ulimwengu kutokana na ugeni wake mfano leo hii hatujui ulimwengu ulitokea wapi ndio maana tunampachika Mungu hapo tukija kujua chanzo cha ulimwengu litaibuka swali jingine hicho chanzo cha ulimwengu chanzo chake ni nini? tutampachika tena Mungu hapo. Unaona hapo kila tunaporudi kwenye backward chain lazima tutafika point ambayo maarifa ya binadamu yamefika mwisho na hapo ndipo anapachikwa Mungu. Pale ambapo maarifa yetu yamefika mwisho ni vyema tukakubali hapa hatujui, binafsi naona ni bora kubaki na swali ambalo currently halina jibu kuliko kubeba tu jibu lolote hata kama halina uthibitisho wala mtililiko wa kimantiki ilimradi tu swali husika lisiwe unfilled.

Hili wazo likubalike lazima liwe na supported evidence. Ni uthibitisho unatangulia ndipo wazo linakubalika. Kinyume na hapo wazo husika linabaki kuwa story ya kutungwa tu. Ukisema chanzo cha binadamu ni udongo ulikusanywa ukapuliziwa pumzi ndio akatokea binadamu lazima ueleze in machenism iyo inawezekana vipi ndio wakuamini sio kuwataka watu waamini tu mawazo yako kwa kuwatishia wasipoamini watatupwa kwenye tanuli la moto.
 
Kwa mfumo huu ni kwamba Wazo la uwepo wa MUNGU ni la milele.
Wazo la uwepo wa MUNGU lipo sababu limekubalika katika jamii ya mwanadamu. Binadamu amechagua kuamini uwepo wa MUNGU ndo maana wazo hili limeendelea kudumu vizazi na vizazi.
Hili wazo likubalike lazima liwe na supported evidence.
Hii ni science. Kuna maisha nje ya sayansi. Na katika maisha, si lazima kuwe na uthibitisho ndipo wazo likubalike. Ubongo wa binadamu unaweza kuamini mambo ambayo kuyathibitisha haiwezekani.

Mfano: mtu aliyeshtuka toka ndotoni jasho likimtoka na kukusimulia kuwa alikuwa anakimbizwa na fisi atathibitisha vipi? Hawezi ila yeye alimuona fisi na alikimbia.
Ni uthibitisho unatangulia ndipo wazo linakubalika.
Hii ni sayansi. Kuna maisha nje ya sayansi.
Kinyume na hapo wazo husika linabaki kuwa story ya kutungwa tu.
Kutungwa tafsiri yake ni kutokuwepo? Maana kutungwa hata gari lilitungwa kwanza ndipo likaletwa. Je lilipokuwepo akilini mwa binadamu halikuwa halisi?
Hapa umeingia kwenye ukristo na uislamu.
Dunia ina imani nyingi sana, kuna imani siku ya mwisho hakuna moto bali watenda wema watalipwa wema kwa kupewa utajiri na watenda mabaya watalipwa mabaya kwa kupewa umasikini na kuwa watumishi wa watenda wema milele na milele. Kama ukristo na uislamu unaona haupo sahihi unaweza kufikiri usahihi wako na ukauamini.
 
 
Kuna kizazi kitafika wazo la uwepo wa Mungu litapotea story za yehova, allah n.k zitabaki makumbusho na library tu

Suala sio kukubalika suala ni limekubalika katika namna ipi. Kama suala limekubalika zama za ujinga hata kama ni uongo basi liendelee kukubalika tu? Hapana. Wazo la uwepo wa Mungu limeendelea kuwepo kwa sababu watu tulikalilishwa tangu utotoni lakini sio kwa sababu ya usahihi wake. Wewe kwa akili ulizonazo sasa hivi ingetokea ndio umesoma biblia kwa mara ya kwanza alafu ukutane na story za nyoka anaeongea bila shaka ungejua huo ni uongo tu.

Ndugu yangu tukisema tuamini bila uthibitisho tutatoa nafasi ya kuleta madai yoyote ya kufikirika.

Ulivyotoa mfano wa muundo wa energy kuwa katika mpangilio ambao ni supportive kwa maisha binadamu iyo ni sayansi pia. Kama umetoa maelezo ya kisayansi kuonesha uwepo wa Mungu kwanini ukatae maelezo ya kisayansi kupinga uwepo wake?

Nimebase kwenye ukristo na uislamu kwa sababu ndizo dini ambazo wewe umefanya rejea ya mada yako.
 
Kuna kizazi kitafika wazo la uwepo wa Mungu litapotea story za yehova, allah n.k zitabaki makumbusho na library tu
Boss, Vizazi vimekuwa vikipita na vitaendelea kupita, sayari ya Dunia kama tuijuavyo huenda ikapita, Kila wakati nyota zinakufa na kuzaliwa upya, hatuna uelewa hata wa tafsiri halisi ya muda,

Nilikuwa natazama makala ya how universe work wanasayansi wakawa wanazungumza kuhusu uelewa wa binadamu linapokuja suala la black holes, mwanasayansi mmoja akasema anaamini black hole ni portal ya time travel na siku mtu akigonga mlango wako akasema yeye ni mjukuu wako wa miaka ya mbele usibamize mlango, huenda binadamu kaweza kusafiri ndani ya black holes. Kama nadharia yake ni sahihi na ikifikia hatua hiyo muda kama tuujuavyo utakuwa na tafsiri tofauti kabisa na haitajalisha una umri gani maana unaweza kusafiri na kukutana na wewe ukiwa mdogo.

Sasa usihitimishe mambo usiyo na uelewa nayo, hitimisha yale uliyo na uelewa nayo.

YEHOVA, ALLAH N.K ni majina ya lafudhi uijuayo wewe, ikipita haimaanishi kuwa wazo la MUNGU limepita, kabla ya lugha unayoifahamu palikuwepo na lugha na MUNGU alitamkwa kwa lafudhi tofauti. Huna hakika iwapo kabla ya vizazi unavyovisoma katika historia hapakuwepo na vizazi ambavyo vilikuwa more advance kuliko sasa na hatma yao ilikuaje na still wazo la uwepo wa MUNGU lipo hivyo usihitimishe kuhusu wakati ujao, miaka mingi mbele ambapo hujui nini kitaipata dunia na iwapo binadamu ataendelea kuwa kiumbe chenye akili kuliko wengine au patatokea kiumbe kipya. USIHITIMISHE USIYO NA UELEWA NAYO BOSS.
Suala sio kukubalika suala ni limekubalika katika namna ipi. Kama suala limekubalika zama za ujinga hata kama ni uongo basi liendelee kukubalika tu? Hapana.
Boss Uongo unaupima vipi? Nilikuuliza iwapo nimeota nakimbizwa na ngiri nikashtuka na jasho linantoka, nikishindwa kuthibitisha kuwa palikuwa na ngiri aliyenikimbiza inamaanisha kuwa mimi ni muongo ilihali nilimuona ngiri na nikakimbia? Katika wakati ule ambapo nakimbia, wakati wa ndoto, nipo katika uongo kwasababu nipo katika ulimwengu wa fikra? Uhalisia wa ulimwengu wa fikra ni upi? Usiseme haupo sababu upo na unaathiri maisha ya binadamu ya kila siku.
Wazo la uwepo wa Mungu limeendelea kuwepo kwa sababu watu tulikalilishwa tangu utotoni lakini sio kwa sababu ya usahihi wake.
Mkuu Wazo la uwepo wa MUNGU halikuanza wakati wa utoto wako. Hata ukristo na uislamu tu una historia ndefu kuliko babu zako wengi sana. Wazo la uwepo na MUNGU ni historia ya uwepo wa binadamu duniani na huenda vipo sambamba au huenda binadamu wa kwanza kuamini kuhusu wazo la MUNGU naye alirithi huko alipotoka kwenye evolution iwapo tutarely on science badala ya maandiko ya kiimani.
Wewe kwa akili ulizonazo sasa hivi ingetokea ndio umesoma biblia kwa mara ya kwanza alafu ukutane na story za nyoka anaeongea bila shaka ungejua huo ni uongo tu.
Tatizo lako ni biblia na mafundisho ya ukristo au wazo la uwepo wa MUNGU? Huenda hata nyoka aliyetamkwa siyo nyoka unayemfahamu. Kama unataka kuuchunguza ukristo au uislamu uchunguze, uelewe kisha hitimisha ila usichukulie mambo juu juu na kuhitimisha. Biblia imetafsiriwa kutoka vizazi vya kale na huwezi thibitisha usahihi wa tafsiri, wanasema unamhitaji roho mtakatifu kuielewa biblia. Huyo roho unaye? Wanaposema roho mtakatifu unaelewa? Au unataka kurekebisha mashine ambayo hujui inavyofanya kazi na ina manual iliyoandikwa kwa lugha usiyoifahamu?
Ndugu yangu tukisema tuamini bila uthibitisho tutatoa nafasi ya kuleta madai yoyote ya kufikirika.
Ulimwengu wa fikra usihitimishe kuwa haupo, pengine wapo wanaouishi katika uhalisia wako uliouzoea. Ndugu yangu hii dunia ina mengi tusiyoyafahamu, tusihitimishe tu kila kitu kiwepesi. Hata sayansi haifanyi maitimisho kirahisi rahisi.
Ulivyotoa mfano wa muundo wa energy kuwa katika mpangilio ambao ni supportive kwa maisha binadamu iyo ni sayansi pia. Kama umetoa maelezo ya kisayansi kuonesha uwepo wa Mungu kwanini ukatae maelezo ya kisayansi kupinga uwepo wake?
Sayansi haijawahi hitimisha kuwa hakuna MUNGU. Unless uanze kumpa sifa fulani fulani kisha reasoning na logic ziingizwe hesabu zikate kuwa mungu wa sifa hizo yupo. Otherwise sayansi imekuwa ikisema hakuna ushahidi wa uwepo wa MUNGU siyo hakuna MUNGU. Hii itaendelea kuwa hivi vizazi na vizazi.
Nimebase kwenye ukristo na uislamu kwa sababu ndizo dini ambazo wewe umefanya rejea ya mada yako.
Mimi sijaanzisha mada, nimetoa hoja kwenye mada.

Ukristo na Uislamu ni dini kama dini nyingine. Ni matokeo ya kutafsiri wazo la uwepo wa MUNGU. Chukulia dini kama vazi inayositiri utupu. Mavazi ni mengi na ya aina nyingi na kila mtu huyakosoa na kuyasifia kutokana na tafsiri yake ya uzuri na ubaya wa vazi ilihali lengo ni kusitiri tu.

Ndivyo dini zilivyo. Lengo ni kumtafsiri MUNGU ambaye huwezi kumuwakilisha katika ukubwa wa wazo lake, lazima umvike vazi la dini.

Hata wewe ukitaka kuanzisha dini kuna namna utamtafsiri MUNGU na namna utakavyomwabudu. Sasa Hoja hapa ni uwepo wa MUNGU siyo uwepo wa dini kama vazi la kumtafsiri MUNGU.

Tumekubaliana kuwa MUNGU ni wazo linaloishi ili kuyapa uhalali yale yaliyo nje ya uwezo wa binadamu.

Tukakubaliana kwamba ni wazo lisilo na mwisho as long as linaishi sababu siku zote binadamu kuna jambo litakuwa nje ya uwezo wake na hatakuwa na majibu na kwa wakati huo wazo la MUNGU litamjia wakati akitafuta majibu.

Basi uelewe kwamba wazo la MUNGU ni pana sana, halielezeki bila kulivalisha vazi la dini, katika kulivika vazi la dini ndipo sifa za MUNGU kutegmeana na dini huzaliwa na ndipo wakosoaji kama wewe hutokea, Otherwise huna hoja inayojisimamia ya kulipinga wazo la uwepo wa MUNGU nje ya dini.
 
Haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…