Usijichanganye ukachukua “Simu za mkopo”

Usijichanganye ukachukua “Simu za mkopo”

mkuu wewe ulichukua aina gani? Maana kuna watu nawafahamu waliochukua za mkopo huwa wanapewa MB kama ifuatavyo;
1. samsung A04 - Anapata MB 100 kila akilipa deni la TZS 1000 (tigo)
2. Samsung A04S - anachukua MB 200 kila akilipa mkopo (tigo).
3. Samsung A04e anapata GB 1.5 kila akilipa mkopo wa TZS 8100. Huyu malipo yake anafanya kwa wiki, hizo GB anapewa za kutumia kwa siku 3. Mtandao ni airtel.
A14
 
Kuna anaewajua BLACK! Humu!? ... Ama M-Pesa --Songesha!?

Mara mia! Hizo simu za mkopo!... Maana usipolipia siku 1,2 simu inazimwa deni linabaki pale pale... Ukipata Buku mbili unalipia unaendelea kuwasiliana kama kawaida.

Lakini hawa jamaa wawili niliowataja hapojuu!!!!!
Ni hatari hatari zaidi ya hatari!!!

SONGESHA wao kila baada ya saa24, za kila siku iitwayo siku... Riba!!!

Wananidai 53,000 kwa deni la 20,000 hata mwezi haujaisha! Siwalipi ng'o! Labda nishinde mkeka wa maana!

Vinginevyo wasahau!
 
Wangekopesha iPhone wangewapata wanawake na wanaume walioleft group wengi sana.

Kuhusu malipo ya kila siku, let's say 10,000 baada ya initial deposit ya 500,000 naamini kabisa uzi wa rikiboy ungekuwa unakimbiza kwa stori za kila siku.

Hii ni biashara nzuri sana. Ukizingatia na ufukara wa watz.
 
Siku hizi tunapenda sana kitonga, ni kweli tumesahau kabisa kusave mia mia kwenye kibubu?!
kibubuu?
ooh! You can't be serious! Wanatupiamo na mauzauza humo unaweza weka 500 kila siku ukija vunja kibubu utaambulia 1500 tuu!
 
Kila mtu anapita njia zake ili afikie pale yalipowekwa matamanio yake..... Mwingine ili aweze kupata hiyo simu ni lazima akope na mwingine si lazima kukopa..... Nimeenda dukani nikakuta simu inauzwa 550,000. Nikaambiwa nilipe 250,000/ cash alafu laki 300000 nitailipa taratibu nichague ni muda gani kwa mwaka mmoja, kwa haraka nikachagua miezi 5, hiyo pesa kila mwezi nitarejesha 63,000. Na jumla nitakuwa nimerejesha 315,000. Hivyo simu nitakuwa nimeinunua 565,000 badala ya 550,000/= hapo mimi km mkopaji nina hasara gani? Vijana tumieni akili! Mikopo ipo kusaidia wenye akili na mikopo ipo kwa ajili ya kuumiza wasiokuwa na akili. Km una akili hiyo laki 3 inayokuwa imesalia mikononi mwako unaweza kuwa unazalisha kitu kingine na deni unalivua taratibu alafu umepata simu yaani hitaji la moyo wako.
 
Hawa jamaa sio wazuri sumsung A03 sijui A14 hahaha et kwa siku 2000 kuanzio 50k.

Kwa mwaka inakuja kama laki 7 na elf 70.

No huu ni unyonyaji.
Kwani unapokopa benki unajua unarudisha shilingi ngapi? Yaleyale tu
 
Mikopo ya aina nyingi huwa haiko fair

Sio simu tu
Tatizo la wabongo tunapenda sana mikopo hata bila kufanya uchambuzi wa kina na ili kujiridhisha kama mkopo huu utanifaa au la.

Sasa mtu akisikia tu mkopo huyo ameingia. Linapokuja swala la kurudisha marejeshi ndo anaanza kulalamika. Kwani nini ulikopa? Wengi lengo lao ni kuchukua na kutokomea. Tabia mbaya sana.
 
Bora mikopo ya ujasiriamali, sio hii ya simu huna unachoingiza then ukope daah
Ndo maana ni muhimu kufanya jambo kwa malengo. Wewe kinachokufanga ukope simu janja nini? Je unataka kuitumia kukuongizia kipato au kwa mawasiliano tu ya kawaida? Tusifanye mambo kichwa kichwa
 
Kila mtu anapita njia zake ili afikie pale yalipowekwa matamanio yake..... Mwingine ili aweze kupata hiyo simu ni lazima akope na mwingine si lazima kukopa..... Nimeenda dukani nikakuta simu inauzwa 550,000. Nikaambiwa nilipe 250,000/ cash alafu laki 300000 nitailipa taratibu nichague ni muda gani kwa mwaka mmoja, kwa haraka nikachagua miezi 5, hiyo pesa kila mwezi nitarejesha 63,000. Na jumla nitakuwa nimerejesha 315,000. Hivyo simu nitakuwa nimeinunua 565,000 badala ya 550,000/= hapo mimi km mkopaji nina hasara gani? Vijana tumieni akili! Mikopo ipo kusaidia wenye akili na mikopo ipo kwa ajili ya kuumiza wasiokuwa na akili. Km una akili hiyo laki 3 inayokuwa imesalia mikononi mwako unaweza kuwa unazalisha kitu kingine na deni unalivua taratibu alafu umepata simu yaani hitaji la moyo wako.
Umedanganya bei ya kununua simu kwa mkopo na kwa cash ni vitu viwili tofauti
 
Back
Top Bottom