Usijiroge kununua gari isiyo brand ya Toyota kama unaishi mikoani, maji utayaita Mma !

Usijiroge kununua gari isiyo brand ya Toyota kama unaishi mikoani, maji utayaita Mma !

Sio Mikoani tu hata huko Dar pia wapo watu kama huna hela hawajui lolote lile.

Sitaki kuwaanikia hapa..ila nimejifunza wengi wauza spare,Mafundi waende na wakati na wajifunze.

Kuna Bwana mmoja ,nilimtua specs zote za gari na bado aliniuliza aina ya gari.
Ikabidi nitume na picha ya gari na bado tukabishana sana.
Nikamwacha afanye anavyoweza.Kuja kutuma spares😀😀😀😀😀😀

Bongo ni 50% kwa 50% ukiwa na gari na huna hela ya kueleweka ya matengezo.
 
Nakubaliana na mleta mada 100%..... I will die kwa toyota. Sioni haja ya kwenda na brand ingine. Ukipata hela si una upgrade to toyota... from vits labda premio to Rav 4.. to fortuner to prado to LC300... ya nini kwenda na magari ambayo roho mkononi likipata shida ukiwa safari mpaka uite fundi wa daslama?...wooiiiiiiiii... team toyota to death
Ukishakuwawa mikoani sio Toyota tu, miliki toyota Old, chuma cha kale. Maana ukinunua latest Toyota tatizo lipo pale pale. Magari ya mikoani ni rav 4 first gen, prado first gen, corola polisi n.k
 
wabongo bado waoga sana, mi nimesafiri na mazda axela dar-Mbeya, Mbeya-Songea then Songea-Dar(Via lindi), sijakutana na Axela hata moja, kichwani nikawa nawaza hivi gari ikipata changamoto huku si nimekwisha!
Bpngo bado sana, naonaga IT nyingi zikipita kwenda wenzetu,hasa Honda na mazda kwa upande wa Zambia, kwa rwanda Kia na hyundai wamezielewa sana, kenya mazda na nissan,njoo bongo sasa
 
Fundi wa kwanza wa gari ni wewe mwenyewe (siyo fundi flani) na mchawi wa kwanza wa gari ni wewe mwenyewe(siyo brand ya gari au aina ya gari). Gari zinatoka na maintenance manual na mitandaoni zimejaa tele ila watu hawasomi, wanaishia kulaumu uhaba wa mafundi au gari husika. Unapiga reverse CX5 haijasimama tayari umeshatia Drive gear, kwanini baada ya muda usiue CVT? Hata kwa toyota utaua tuu. Utofauti ni kwamba spear za toyota utazipata kwa urahisi, ila hapo tatizo siyo gari, ni wewe mwenyewe. Unaambiwa ukisha drive long safari uipe muda kidogo ifanye DPF regeneration ila wewe unafika, unapaki na kuzima hapohapo kila mara....unatarajia nini? Huoni hata madereva malorry wenyewe hawazimagi gari muda huohuo baada ya safari? Gari nyingi za kisasa na hasa za diesel zina masharti yake na hazitaki mazoea. Pia uzuri wa gari za kisasa zinakutaarifu tatizo kabla halijawa kubwa hivyo uki potezea ndipo unaishia kulaumu gari flani ni mbaya.
Subaru Forester zilianzaga kudisiwa muaka ya nyuma ila vijana wa Arusha wakakomaa nazo hivyohivyo hadi sasahivi zimekuwa kama toyota. #Drive what you love as long as you can afford it#
Toyota old school hazina maelezo mengi hivi mkuu. Mfano rav 4 za kale zile ukikaa unakuwa upo kama kwenye sufuria kubwa unaweza hata weka maji oil ikipungua na injini ikalalamika kidogo kisha ikazoea.
 
Rav 4Masawe ni GUTA la WANHOO lililochangamka
 
Bpngo bado sana, naonaga IT nyingi zikipita kwenda wenzetu,hasa Honda na mazda kwa upande wa Zambia, kwa rwanda Kia na hyundai wamezielewa sana, kenya mazda na nissan,njoo bongo sasa

Kweli mkuu watu wanauziana uoga sana, ndo anachofanya aliyeleta huu uzi!
 
Nakubaliana na mleta mada 100%..... I will die kwa toyota. Sioni haja ya kwenda na brand ingine. Ukipata hela si una upgrade to toyota... from vits labda premio to Rav 4.. to fortuner to prado to LC300... ya nini kwenda na magari ambayo roho mkononi likipata shida ukiwa safari mpaka uite fundi wa daslama?...wooiiiiiiiii... team toyota to death
Fortuner bei gani naita.ani hiyo gari sana....najua nikiweka mchuchu hapo mbele basi kumvua chupi ni kazi rahisi
 
Fortuner bei gani naita.ani hiyo gari sana....najua nikiweka mchuchu hapo mbele basi kumvua chupi ni kazi rahisi
Hahahhaha. Kwa kweli fortuner ni garu nzuri sana mkuu... i can never complain....ila hizo sababu zako.. hahahah. Hapana kaka. Wewe chukua gari kwa ajili ya mizunguko, sio pisi......

ukitaka ya kuanzia 2018 mpaka 2020 ivi unaweza pata kwa 80 - 100m, ikisogea ya 2021 - 22 maybe itafika 120m, 2023 onwards zilipata facelift latest zinaenda mpaka 150 - 180m, hizo ni bei za kuimport kutoka S.A.. ukitaka brand new zero kms pale toyota karimjee kwa sasa ni around 240m
 
Umeelewa maana ya resale value???... namaamisha kuiuza after kukaa nayo hapa bongo kwa miaka kadhaa.. not straight after importation....
twende mbele turudi nyuma kumaintain fortuner ni rahisi zaidi kulinganisha na ford ranger kwasababu ya uwingi wa mafundi wanaozielewa toyota.. spare parts huko nje might be the same price sikatai, but locally kwasababu za toyota ni fast moving business people lazma wataweka faida kidogo kuliganisha na za ford, huo ndo ukweli mchungu....TOYOTA ITABAKI KUWA TOYOTA
Mkuu kwenye magari ungeachana nako tu fortuner ipi ni gharama ndogo kutengeneza na ford ranger ipi unazungumzia ondoa mawazo ya kimasikini hayo unafikiri kuuza baada ya kutumia ili iweje si ufungue yard basi ununue na kuuza nenda Lusaka hapo uone watu wanavyosukuma gari za ukweli kwa sababu hawawezi kuuza baada ya kutumia mtu gari inatengenezwa na mashine siku hizi tumerahisishiwa mkuu hata uwe na jina gani ikiingia kwenye mashine kama ipo itatengenezwa unazungumzia Dar Songea wakati Gari zinatoka SA mpaka Arusha zinapita mapori mangapi na leo zipo Dar..
 
Jamani eeeh Mimi nasema hivi gari zote Ni nzuri wapendwa changamoto zetu wabongo tunanunua gari zimechoka Sana gari Ina zaidi ya kilomita laki moja na arobaini na bado hufanyi service ya maana kwa Nini lisikusumbue ? Wewe gari za ulaya na misensa yote hiyo bado unataka upite kwenye madimbwi ya maji , gari ya ulaya unataka uende nayo kwenye barabara hata mkokoteni wa ng'ombe unapata shida kupita ? Kwanza tununue magari kwa kuyafahamu na kuyajua vizuri linahitaji matunzo gani na halipaswi kuendeshwa barabara zipi hapo utakaa Sana na gari
 
Hahahhaha. Kwa kweli fortuner ni garu nzuri sana mkuu... i can never complain....ila hizo sababu zako.. hahahah. Hapana kaka. Wewe chukua gari kwa ajili ya mizunguko, sio pisi......

ukitaka ya kuanzia 2018 mpaka 2020 ivi unaweza pata kwa 80 - 100m, ikisogea ya 2021 - 22 maybe itafika 120m, 2023 onwards zilipata facelift latest zinaenda mpaka 150 - 180m, hizo ni bei za kuimport kutoka S.A.. ukitaka brand new zero kms pale toyota karimjee kwa sasa ni around 240m
Ah wewe usidanganyime magari mazuri tuna unua ile tule watoto wazuri. Anyways kwa bei hizo wavha tuu niendelee na haka ka crown kangu kanatosha kuwala mwaj ndala ndefu
 
Toyota old school hazina maelezo mengi hivi mkuu. Mfano rav 4 za kale zile ukikaa unakuwa upo kama kwenye sufuria kubwa unaweza hata weka maji oil ikipungua na injini ikalalamika kidogo kisha ikazoea.
Upo sahihi
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Jamani eeeh Mimi nasema hivi gari zote Ni nzuri wapendwa changamoto zetu wabongo tunanunua gari zimechoka Sana gari Ina zaidi ya kilomita laki moja na arobaini na bado hufanyi service ya maana kwa Nini lisikusumbue ? Wewe gari za ulaya na misensa yote hiyo bado unataka upite kwenye madimbwi ya maji , gari ya ulaya unataka uende nayo kwenye barabara hata mkokoteni wa ng'ombe unapata shida kupita ? Kwanza tununue magari kwa kuyafahamu na kuyajua vizuri linahitaji matunzo gani na halipaswi kuendeshwa barabara zipi hapo utakaa Sana na gari
Ndio maana mkuu kuna mchangiaji kasema bora mtu umiliki gari Za kizamani kama zile landrover, rav 4,premio,pajero, escudo haswa haswa kwa safari hizi Za off-road ni, sasa unakuta mtu ana Mazda anataka aende nayo kigoma😂na arudi dsm bila shida
 
Thinking ya kimasikini kabisa, na unaona safi kabisa watu wa mikoani wasipate kuenjoy European cars, mafundi na spares inatakiwa zije nyuma ya gari yaani gari ziingie kwanza kisha vingine vifuate, ndivyo maendeleo yalivyo.
 
Ndio maana mkuu kuna mchangiaji kasema bora mtu umiliki gari Za kizamani kama zile landrover, rav 4,premio,pajero, escudo haswa haswa kwa safari hizi Za off-road ni, sasa unakuta mtu ana Mazda anataka aende nayo kigoma😂na arudi dsm bila shida
Nilisafiri naVW Toureg, kufika Singida tyres zikawa zimevimba. nilipata shida kubwa kupata tyres za kununua ili kubadili iliyo mbovu.
 
Back
Top Bottom