Usikubali kusaini nyaraka hii unapopekuliwa na Polisi

Mtabishana wao watasema sahihi ni yako na wewe utasema sahihi sio yako, hapo itafunguliwa kesi ndogo na ile ya msingi itaachwa, kwenye kesi ndogo wataitwa waataalamu wa maandishi ikibainika ulidanganya utapewa adhabu ndipo inaanza kusikilizwa kesi ya msingi tena

Inakuwa hasara kwako maana kesi ndogo nayo haiishi haraka inachukua muda, plus adhabu ya kuidanganya mahakama unapewa adhabu ambayo hata ukishinda utatumikia adhabu ya kesi ndogo sasa kwanini usiokoe muda kwa kwenda straight aidha ushindwe utumikie adhabu moja au ushinde kabisa

Unafikiri mambo ni mepesi hivyo?
 
Asante sana
 
 
Kumbe yule Prof.wa Arusha angegomea kusaini yale meno ya Tembo yaliyokutwa kwenye mizinga ya nyuki shambani mwake
 
Kazi ya wakili ni kukataa kosa hata kama umetenda kweli
 
Mkuu ukisoma vizuri ninaona amesema kama ulivyoandika wewe...'iwapo hukukutwa nacho'... hata kama ni kidogo mfano wa pipi au sindano.
 
Kisheria kabla ya upekuzi lazima awepo mtu mwingine ambae mtuhumiwa atamchagua
Inaruhusiwa pia kumsachi polisi ingawa wanaweza kuwa wanatafuta tv
Polisi watapekua mbele ya mtuhumiwa na shahidi wako,chochote kitakachopatikana ni lazima kisainiwe na mtuhumiwa na shahidi
Kukataa kusaini ni Obstruction of justice
 
Kazi ya wakili ni kukataa kosa hata kama umetenda kweli
Hata akikataa kuna hatua za kumtia hatiani mteja kwahiyo wasoma uzi wasiamini sana hiyo mbinu kama itawatoa kirahisi
 
Mkuu ukisoma vizuri ninaona amesema kama ulivyoandika wewe...'iwapo hukukutwa nacho'... hata kama ni kidogo mfano wa pipi au sindano.
Kama ndivyo yuko sahihi, ila michango iliyofuata ndio ilinitia mashaka kama wadau wameelewa
 
Huwi kwenye anga zao unakuwa kwenye anga zako

Upekuzi hufanyika nyumbani kwako, ofisini kwako nk kwahiyo huwezi kubisha kusaini nyaraka zilizokutwa ofisini kwako wakati hakuna namna ya mtu mwingine kuziingiza

Hapo utakuwa umejitakia kipigo
Mtanzania ukimkumbusha ''kipigo cha polisi'' anaona ni haki yake akipate!
 
Huyu ni Wakili kweli? Nina mashaka na uwakili wake!! Upekuzi umefanyika kwa kufuata taratibu na sheria halafu mtu akatae kusaini.
Kama upekuzi umefanyika kwa kufuata taratibu, una saign kwa kuwa ni kweli vilivyokutwa unahusika navyo!
 
Je! Ni sahihi Kisheria Kabla Askari hajaanza kuendesha upekuzi Basi Apekuliwe kwanza? Na nani anaruhusiwa Kisheria kumpekua Askari Ili kujiridhisha kwanza kama hajaja na kitu kwa mtuhumiwa?
 

Kuna walakini mkubwa ktk andiko lako. Iwapo ungekuwa mwalimu, nina imani wanafunzi wako wote wangefeli!
Yaani umekutwa na pembe za ndovu, kisha ukatae kusaini fomu kwa vile hiyo fomu itakuwa na ushahidi dhidi yako?
In the first consideration point, kwanini ukutwe na pembe za ndovu?
Kama ni suala la kulazimishwa kusaini fomu wakati hujakutwa na pembe hizo hilo ndilo suala la kuongelea, nini kifanyike.

Naona vilaza wenzako 61 wamekupa like. Wonders!

Sent from my TECNO BC1 using JamiiForums mobile app
 
Mtiririko wa michango ya wadau inaonyesha ni jinsi waTanzania tuna shida kwenye kusoma maandishi.....hatusomi maandishi bali tunasoma maandishi ili tupate cha kujibu kwa kutafuta makosa ya mwandishi......tunasoma habari huku tayari tuna matarajio ya namna tunataka habari iwe........

Huu ni ugonjwa mbaya unaotuweka mbali waTanzania na maarifa mengi kwenye zama hizi za sayansi na teknolojia......

TUBADILIKENI WATANZANIA....

NB;
UBARIKIWE MLETA MADA KWA ELIMU NZURI......
 
Huyu ni Wakili kweli? Nina mashaka na uwakili wake!! Upekuzi umefanyika kwa kufuata taratibu na sheria halafu mtu akatae kusaini.
Hivi una habari polisi wana kawaida ya ku-plant evidence?! Au sometimes mtu mwenye visasi na wewe anaweza ku-plant evidence halafu akakuripoti polisi!!

Anachosema ni kwamba, with your knowledge una uhakika kabisa kwamba, kwa mfano ndani kwako hakuna heroin, lakini ghafla wanakuonesha paketo ya heroin !

Hapo ndo unaambiwa goma kusaini kwa sababu ukishasaini, inakuwa umeshakubali kwamba hiyo bhangi ni wewe ndie uliweka!
Hakusema hivyo kwa sababu, hali hiyo inatokea katika mazingira ya kupandikiziwa evidence!! Kwa mfano, polisi anakuta kabisa pistol ikiwa chini ya godoro huku wewe ukiwa hujui imefikaje fikaje hapo... kumbe kuna mtu kakuchezea mchezo! Kwahiyo sio kwamba hujakutwa na hicho kitu, bali unakutwa nacho kabisa lakini hujui kimefikaje fikaje hapo!
 
Nadhani jamaa ameshindwa tu kufafanua! Guys, unaweza kukutwa na pembe za ndovu lakini zimewekwa na mtu mwingine kabisa ili labda kukukomesha na mambo mengine kama hayo! Anachomaanisha hapo ni katika mazingira ya planted evidence!

Mwenyewe unajua nyumba ipo salama kumbe wabaya wako wameficha drugs darini na kisha wanaitaarifu polisi kwamba nyumba fulani kuna drug dealer! Wakati mwenyewe unajiamini, unakuta polisi wanaibuka na kete za heroin! Lakini wakati mwingine, ni hao hao polisi wanaweza kutumika ku-plant evidence... hicho ndicho anachosema!!
 
Je kama nikipewa mkung'uto wa nguvu na kusaini, nikifika mahakama siwezi kugeuka na kusema nililazimishwa ? Naaza hivi ! Ndugu hakimu nashukuru kufikishwa katika chombo hiki cha kutoa haki, "Nililazimishwa, sasa nakanusha kilichoandikwa, si kweli" hapo imekaaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…