Usikubali kusaini nyaraka hii unapopekuliwa na Polisi

Mkuu, kama cheti hicho kinaweza kuwa admissible na kuwa na mashiko bila hata ya saini ya mtuhumiwa kuna umuhimu gani wa kumlazimisha asaini?? Maana unasema kabisa watu huwa hawasaini kwa kupenda bali kwa lazima.

Na unaona ni sawa kwa mtuhumiwa kuzabwa vibao sababu amekutwa redhanded ilhali yeye hakubali kuwa amekutwa redhanded? Unaona ni sawa kwa sababu tu hakutakuwa na ushahidi wa kuonesha kuwa alipigwa? Hao independent witness wanakuwa wapo kwa ajili ya kushuhudia kila kinachotokea au wapo kwa ajili ya kuhakikisha mtuhumiwa anasaini?

Sio vyema kabisa kufurahia matumizi ya nguvu kwenye upekuzi au ukamataji. Hapa bado tunahitaji sana maaskari wetu wapewe body cams ili kuepusha mambo kama haya. Kesi inajengwa kwa ushahidi imara na sio wa kulazimishana
 
Wataalamu wa mwandiko watafanya nini kugundua ni mimi nimeandika?..ikiwa nimebadilisha uumbaji wa herufi na nimebadilisha sign?..mfano mwandiko ulioandika kwa mkono wa kushoto ambao siutumii kuandika.
 
Wakili Yakubu ameeleza hivi;

Aidha, ni muhimu kujua kuwa ikiwa unapinga kuhusu kile kinachochukuliwa kuwa hukukutwa nacho ama hakikukutwa kwako basi usikubali kusaini fomu hiyo.

Hii ni kwasababu kukubali kwako kusaini fomu hiyo tafsiri yake kisherria ni kuwa umekubali kuwa umekutwa na hicho kitu.

Na endapo utafikishwa mahakamani basi fomu hiyo itawasilishwa kama ushahidi na kwasababu ulisaini basi ulikubali kuwa ulikutwa na kitu hicho.

Vinginevyo uwe unakubali kuwa ni kweli hicho kitu umekutwa nacho, basi hapo waweza kusaini. Lakini kama hukubali basi usisaini.
 
Huyu ni Wakili kweli? Nina mashaka na uwakili wake!! Upekuzi umefanyika kwa kufuata taratibu na sheria halafu mtu akatae kusaini.
Hata mimi imenishangaza hasa ukizingatia mfano alioutoa wa Wachina kukutwa kwenye gari na nyara za serikali!
 
Wataalamu wa mwandiko watafanya nini kugundua ni mimi nimeandika?..ikiwa nimebadilisha uumbaji wa herufi na nimebadilisha sign?..mfano mwandiko ulioandika kwa mkono wa kushoto ambao siutumii kuandika.
Utaandikaje wakati huo mkono hautumii? Labda uanze kufanya mazoezi leo hii.
 
Huyu ni Wakili kweli? Nina mashaka na uwakili wake!! Upekuzi umefanyika kwa kufuata taratibu na sheria halafu mtu akatae kusaini.
Umesoma na kuelewa?
Amesema Kama unauhakika umekutwa nacho sawa, lakini hujakutwa na kitu usisaini.

Kufuatwa kwa taratibu za upekuzi hakufanyi ukutwe na kinachohisiwa.
Be serious
 
Unaweza kusaini ktk listi unayoiona.... Bila tatizo.... Alafu jamaa wakaongeza pembe ya ndovu katika listi wakati wewe haupo... Mchakato ukaanzia hapa....

Inatia shaka....
 
Soma kwa uangalifu na umakini utaona hayo uyasemayo yamo
 
Reactions: T11
hapa tunaongelea admissibility of a certificate of seizure which the accused did not sign for whatever reason. kama kuna independent witness plus the searching officers, ni admissible. utazunguruka koote lakini utarudi tu kwenye point hii. msidanganye watu.
 
hapa kuna vitu viwili, iwe ni risiti au certificate of seizure,kama kuna ushahidi kwamba ulitakiwa kusaini ukagoma, na wapo mashahidi waliosaini kwenye certificate na wakaongea hivyo mahakamani, hiyo risiti itakubana tu hata ufanyeje. labda PP awe boya.
kama
 
Alichosema wakili ni kuwa usisaini kama hukubali kukutwa na hivyo vitu au hukubali kuwa ni vyako. Wewe ulichojibu ni kuwa hata bila kusaini bado cheti kina maana, lakini wakati huohuo ukalazimisha mtu asaini kwa sababu hata asiposaini bado haitamsaidia.

Sasa kama hata asiposaini haimsaidii, kwa nini alazimishwe kusaini?? Sio kwamba saini yake itarahisisha kazi kwa upande wa huyo PP kuliko ambavyo asiposaini. Hakuna kinachodangwanywa hapa, kutosaini kunamsaidia mtuhumiwa kuliko ambavyo angesaini, ndicho anachosema wakili
 
Tatizo virungu aisee, acha kabisa, ukipigwa kimoja cha ugoko unaasaini tu lasivyo utapewa kilema cha kudumu
 
Nashukuru mkuu lakini heading yake haijakaa kimkakati.
 
Wataalamu wa mwandiko watafanya nini kugundua ni mimi nimeandika?..ikiwa nimebadilisha uumbaji wa herufi na nimebadilisha sign?..mfano mwandiko ulioandika kwa mkono wa kushoto ambao siutumii kuandika.
Unafikiri unachofikiri watu hawakufikiri?
 
Kuna mashahidi kadhaa wanakuwepo wanaotakiwa kujiridhisha kinachofanyika kina uhalali labda nao hao washawishiwe kukuruka
 
Unatakiwa kuwa makini sasa wewe mwenye nyumba na inashauriwa hata kuingia ndani utangulie wewe, hata chumbani tangulia wewe wengine wafuate hiyo bastola wataweka saa ngapi?

Polisi hawawezi kuhadaa ujumbe mzima wa watu zaidi ya watano wakugeuke utakuwa ulichokwa tu na mtaa wako
 
Unawajua Polisi wa Tz? Hujakaa sawa una mbata moja inakukalisha chini, ile unataka kujua ni yupi kakupiga unapigwa katafunua moja halafu unapewa pen usaini.
Hapo utajipima mwenyewe.


Labda wanawafanyia hayo wajinga wajinga wasojielewa!

Lakini nawashauri polisi hata wajinga wasiwatende kwa hiyana bali kwa haki na kanuni .
Msitumie ujinga wa mtu kama fimbo ya kumchapa nayo.

Zingatieni miiko yenu ya kazi.

Polisi haruhusuwi kumpiga au kumdhuru mtu kwa namna yoyote ile isipokuwa pale tu inapobidi kwa kujihami au kujilinda.

Anaweza ku apply minimum force pale mtuhumiwa anapokataa kutii amri bila kumdhuru au kumsababishia maumivu.

Hiyo ni kwa mujibu wa mkataba wa Haki za Binadamu ambao nchi yetu imeridhia na kuingia mikataba ya kimataifa kama mwanachama wa jumuia ya Madola.

WaTZ mnapaswa kujua hayo.

Polisi ni watu tu kama nyie wanalipwa kodi zetu watutumikie kwa kutulinda sisi na mali zetu.

Msiwaogope!

Kuwa Polisi ni mgawanyo wa majukumu na tunategemeana.

Kila binadamu anastahili heshima na Utu bila kujali chochote.
 

Je wakitaka Dole Gumba ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…