Usikubali kusaini nyaraka hii unapopekuliwa na Polisi

Huyu ni Wakili kweli? Nina mashaka na uwakili wake!! Upekuzi umefanyika kwa kufuata taratibu na sheria halafu mtu akatae kusaini.

Kuna namna huwa wanakuja na kitu, wanakuwekea kisha wanakutaka usign kisha waondoke nacho. Sasa kama ni madawa na unahakika hukuwa nayo basi unatakiwa kukataa.
 
Kuna Mijitu migumu kweli kuelewa,Mshaambiwa kama haujakutwa na hicho kitu basi usisign na kama umekutwa nacho basi ndiyo chako hicho.Mimi hata uniwekee Ngada kama siyo yangu bora uniuwe hapo hapo Magetoni kwangu sema sisaini hata aje Rpc.
 
Kuna Mijitu migumu kweli kuelewa,Mshaambiwa kama haujakutwa na hicho kitu basi usisign na kama umekutwa nacho basi ndiyo chako hicho.Mimi hata uniwekee Ngada kama siyo yangu bora uniuwe hapo hapo Magetoni kwangu sema sisaini hata aje Rpc.

Kabisa unawaambia ngoja umwite mwanasheria wako mfanyie forensic kuweza kujua kama kuna finger print zainazihusiana na wewe.....Hakuna kusaini kitu ambacho haijakutwa nacho.
 
apo mwisho sijaelewa hii sheria ni ya china au TZ?
 
Jamaa we ni tapeli ulituacha kwenye mataa na petition tukasaini leo ndo unaonekana kiufupi hufai hata kama unasema ukweli
 
Kuna namna huwa wanakuja na kitu, wanakuwekea kisha wanakutaka usign kisha waondoke nacho. Sasa kama ni madawa na unahakika hukuwa nayo basi unatakiwa kukataa.
Mkuu nakubaliana nawe

Wanajamvi hebu tupunguze haraka tuwe makini tunapo soma maandiko. Mleta mada hajashauri kuwa usisaini hiyo karatasi kama umekutwa na kitu ambacho ni cha kwako,kasema kama polisi wamekuta kitu ambacho si chako usisaini. Haki hailetwi kama pilau la hitima haki hupiganiwa. Tupiganie haki zetu si kuogopa kuwaambia ukweli polisi kwa kuogopa kupigwa.
 
Mbona kaongea hapo mwisho yaani mistari ishirini tuu hujaelewa kitu sasa iwe kitabu itakuaje...
 
Wakili MSOMI,nashukuru kwa ufafanuzi wako hapo hiyo form unaletewa katika mazingira gani?Hati uwe na uwezo wa kutosaini!?
Bongo wengi wamebambikiwa kesi alichoongea jamaa yupo sahihi ili watu wajue na wapate Elimu tena katoa na kesi hapo...juzi tuu hapa tumesikia kauli ya kesi zisizo na ushahidi zifutwe au watu wasishtakiwe hapo kuna picha gani...
 
Huyu ni Wakili kweli? Nina mashaka na uwakili wake!! Upekuzi umefanyika kwa kufuata taratibu na sheria halafu mtu akatae kusaini.
Wewe ndo hujaelewa,mara ngapi police wanabambikizia watu kesi?Mfano;unaweza letewa bangi,bunduki,nyara,nk nyumbani kwako kabla ya upekuzi bila wewe kujua aidha kwa kutumia marafiki zako,jirani zako ambao wanajua madhaifu ktk kuacha milango wazi au vyovyote vile.Na baada ya kuchomekewa vitu hivyo police wanakuja nyuma kufanya upekuzi feki kwa kufata taratibu zote za kujipekuwa na kupekuliwa kabla ya kuingia kwako mbele ya waangalizi km balozi,mwenyekiti,jirani au vyovyote vile.
Wewe binafsi unajua hujawahi kuwa mharifu wa nyara,madawa ya kulevya,silaha haramu,nk.Utakubalije kusaini hati hiyo hata kwa virungu?
Nadhani nami ndio uelewa niliomuelewa mtoa mada aidha tuelimishane zaidi rafiki.
 
Dear,umesahau sahihi ya kidole gumba watakubania hapa
 
Kwenye iyo fomu si pia vinaorodheshwa na vitu ambavyo vimekutwa kwenye iyo office au nyumba, na pia kunakuwa na sehemu ya kusaini mjumbe au balozi,,, au iyo ni tofauti na search warrant!?
Search warrant= hati ya kufanya upekuzi. Hiki ndicho kibali kinachowapa nguvu ya kufanya upekuzi. Ingawa askari anaweza fanya upekuzi bila hata ya kuwa na hati ya upekuzi akihisi kwenye gari yako kuna madawa ya kulevya etc ila ni lazima shahidi huru awepo.

Certificate of seizure na search warrant ni nyaraka mbili tofauti ila hutumika katika tukio moja la upekuzi.

Certificate of seizure hutolewa baada ya kufanya upekuzi ndani ya nyumba na ofisi. Upekuzi unapofanyika lazima awepo shahidi huru(independent witnes) mara nyingi ni wajumbe wa mtaa au mtaa chairman.

Certificate of seizure huorodhesha mali zote ambazo zimekutwa katika ofisi yako au kwenye gari.

Certificate of seizure lazima isainiwe na mwenye ofisi, gari, au mtu yeyote ambaye amefanyiwa upekuzi, askari polisi na shahidi huru. Baada ya hapo polisi lazima akupe risiti ya upekuzi kwa mujibu wa sheria. Lengo la kusaini ni kwamba unakubali kwamba umefanyiwa upekuzi kwa mujibu wa sheria na umekutwa na hizo mali au nyaraka.

Ukiona upekuzi unafanyika bila shahidi huru ujue huo ni illegal search.
 
Angesema pia polisi kukagua gari langu anatakiwa awe na nini? Au kama kuna utaratibu wowote anatakiwa kuufuata
 
Nikukumbushe wakili wakati mwingine hiyo form mtuhumiwa husainishwa baada ya kipigo kikali ( labda kama huwajui polisi)
issue kubwa hapa labda kama mtuhumiwa amesainishwa baada ya kipigo kikali anaichomoaje mahakamani...!
obvious he/she was not a free agent ....
ungeiweka pande mbili ili wadau waelewe kinaganaga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…