Ijumaa Kuu; (ambayo ni sehemu ya Wiki Takatifu kwa Wakristo, hasa Wakatoliki), waumini wengi hufuata utaratibu wa kikanisa kama kufunga na kujinyima, ikiwa ni pamoja na kutokula nyama ya wanyama wa nchi kavu kama vile:
Ng'ombe
Kuku
Mbuzi
Kondoo
Nguruwe
Nyama inayo ruhusiwa siku ya Ijumaa Kuu ni SAMAKI, kwa sababu:
Samaki huishi majini, na kwa mafundisho ya Kanisa Katoliki, hawaangukii kwenye jamii ya “nyama za nchi kavu” zinazopaswa kuepukwa wakati wa kujinyima.
Samaki pia huchukuliwa kama chakula cha kawaida (si cha anasa), kitu ambacho kinaendana na roho ya toba na unyenyekevu wa siku hiyo.
Kwa hiyo, samaki wa aina yoyote—kama sato, sangara, kambale, samaki wote wa maji baridi na samaki wa baharini
—wanaruhusiwa kuliwa Ijumaa Kuu, mradi haivunji nia ya kufunga na kujinyima.
~ Kila lakheri ndugu zangu wakristo katika safari ya kuelekea sherehe za sikukuu ya Pasaka.