Usimshauri ndugu au rafiki asomee uandishi wa habari: ni sekta ambayo inaenda kufa na atateseka sana

waandishi wa habari wanapata shida sana, wanaomba omba sana pesa, wanakula sana rushwa ili wasikurushe au wakurushe, inasikitisha sana. nimeshafanya nao kazi miaka kadhaa, na huwa nawaonea huruma. ndio maana wana hasira, wanatangaza kwa kisirani habari hasa zinazodhalilisha watu, ni kwa sababu hawawajali, hawalipwi vizuri na hata hao wanaolipwa mikataba yao ya ajira inatia huruma au haipo kabisa.

however, tuendako, wale ambao Mungu anawatokea wakapata mtaji wa kutafuta habari na kuziuza, kufungua tv mtandaoni na ikawa famous n.k, wanapata sana pesa. mbona ulaya hata hao youtubers tu ambao sio waandishi wa habari wanatengeneza sana pesa? sembuse waandishi wetu wakiamua kujikita kutafuta habari za sekta fulani tu inayogusa jamii, wanaweza kufanya makubwa.
 
Zamani nilivyo kuwa mdogo nilifikiri mtu anayefanya kazi ya utangazaji katika radio au TV wanapiga hela kweli, kumbe loooo ,yaani wengi kumbe waandishi wa habari hapa bongo kuyapatia maisha ni pale anapo pata teuzi kutoka serikalini au aombe kazi katika hizi international media ,njee na hapo walio wengi ni apeche alolo.
 
acha kukatisha watu tamaa kwa kufeli kwako kupata na kufanya kazi kwenye fani au ujuzi uliosomea.

kijana awaye yeyote.
Nenda shule, na usome kwa bidii ufaulu vizuri, full stop.🐒
Nyinyi ndio mnapoteza watu kwa mentality za kidwanzi namna hii; nyie ndio mmesababisha mtaani wamejaa watu wana ukurutu wa degree ambazo kupata kazi ni ndoto za alinacha
 
Journalism imeuliwa na kukua kwa internet,

Sio career ambayo tena unahitaji kusomea bali unahitaji kipaji, ig page, youtube channel na laki ya kupata leseni ya TCRA
 
waandishi wa habari wanapata shida sana, wanaomba omba sana pesa, wanakula sana rushwa ili wasikurushe au wakurushe, inasikitisha sana. nimeshafanya nao kazi miaka kadhaa, na huwa nawaonea huruma. ndio maana wana hasira, wanatangaza kwa kisirani habari hasa zinazodhalilisha watu, ni kwa sababu hawawajali, hawalipwi vizuri na hata hao wanaolipwa mikataba yao ya ajira inatia huruma au haipo kabisa.

however, tuendako, wale ambao Mungu anawatokea wakapata mtaji wa kutafuta habari na kuziuza, kufungua tv mtandaoni na ikawa famous n.k, wanapata sana pesa. mbona ulaya hata hao youtubers tu ambao sio waandishi wa habari wanatengeneza sana pesa? sembuse waandishi wetu wakiamua kujikita kutafuta habari za sekta fulani tu inayogusa jamii, wanaweza kufanya makubwa.

Media ecosystem Tanzania iko tofauti kidogo ; vichwa vya watanzania ni nusura ya Mazezeta maana mwandishi akisema afocus kwenye taarifa za uchumi au mada nyingine ya maana lazima aangukie pua; watu wanataka udaku , mpira na ngono
 
I agree, but niamini, style ya mtu kufanya jambo will always put him/her to the top! Of course siwezi shauri mtu kufanya jambo lolote, ila mtu Akiwa na passion anaweza sogea
 
Yellow journalism ni janga la taifa
Hard stories au hard news zipo kibao mtaani zenye kugusa maisha ya watu,shida kubwa ipo kwa waandishi na wamiliki wa media house,ambao ni mwiba kwa waandishi hasa kwenye kuzingatia ethics.

Pale SAUT wanao jiunga na kitovu cha journalism na mass communication ni wengi sana lakini mwaka wa tatu,wengi hukimbilia PR,hivyo kufanya wahitimu kamili wa uandishi wa habari hawafiki hata 30.
 
Nyinyi ndio mnapoteza watu kwa mentality za kidwanzi namna hii; nyie ndio mmesababisha mtaani wamejaa watu wana ukurutu wa degree ambazo kupata kazi ni ndoto za alinacha
waende wakasome kwa bidii sana, ili wakapate ujuzi na maarifa ya kuja kuibadili fikra na mitazamo ya jamii na maisha kijamii, kiuchumi na kisiasa,

na sio kulalamika kama wewe bila kutumia maarifa na ujuzi wa kitaalamu ulionao baada ya kuhitimu masomo ya chuo, na kutumia fursa bwerere zilizoko nchini kufanya biashara, kilimo, ufugaji n.k🐒
 
Mtu ana degree ya soshiolojia unataka nae akafanye kilimo na ufugaji? Au hiyo mtu unamshaurije?
 
Mimi mwenyewe zao la SAUT, nimesoma na hao watu kozi kazaa (niko PR), nikiwaza lile nyomi la journalism na mass communication najiuliza sahizi wanafanya nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…