Usimshauri ndugu au rafiki asomee uandishi wa habari: ni sekta ambayo inaenda kufa na atateseka sana

Usimshauri ndugu au rafiki asomee uandishi wa habari: ni sekta ambayo inaenda kufa na atateseka sana

Shida kubwa ya waandishi wa habari wa Tanzania,walio wengi hawajitambui nafasi Yao katika jamii.

Kila mwandishi anakimbilia kutoa habari za yellow stories (michezo,udaku nk),Leo hii kupata investigative stories au investigative journalism ni kipengele kigumu sana.
Pia ujio wa citizen journalism ni Kilio Cha media nyingi hapa nchini.Na iwe wazi kwamba moyo wa media house yoyote ni matangazo bila matangazo ni ngumu sana kuendesha shughuli za uandishi wa habari.
Kama ni kweli Azam media wanalipa kiasi hicho Cha mshahara,basi nachelea kusema tuna safari ndefu ya uhuru wa vyombo vya habari nchini.
investigative journalism italeta mauaji, hamna demokrasia

ndo maana mkia wanarudisha nyuma

sema pia technically hawapo vizuri, production quality ni mbaya mno
 
Traditional/legacy media inakufa; ukiondoa upande wa michezo sioni kama kuna eneo ambalo huu uhalisia unaenda kubadilika
Azam yenyewe iko afloat mostly kwasababu ya tamthilia, ITV wanajiita super brand kwasababu ya taarifa ya habari ambayo kusema kweli kwa hali inavyoendelea unaweza ukalinganisha na chui wa karatasi
na azam wanakabiliwa na kodi za kila aina na wameishawasilisha maelezo yao serikali kama walivyoombavwafanye,ili waweze kupata faida ambayo inaweza kufanya walipe vizuri lakini bado malalamiko yao yanafanyiwa kazi
 
nahisi ina mchango mkubwa kwenye kufanya wananchi wasijue na wachukie mambo ya siasa,

wakati siasa ndo inaamua waishi vipi...
Indifference ya wananchi kwenye mambo ya siasa sio kwa bahati mbaya bali makusudi; hamna watawala wanataka population nzima ya nchi kuwa engaged na mambo hayo (imagine watu milion 60 wote wawe engaged)
 
mada inahusu waandishi kupunjwa maslahi wewe unataka kuleta siasa hapa.
ikiwa hurudhiki na stahiki unatumia ujuzi na maarifa yako kisomi kuchangamkia fursa zingine zenye maslahi mapana na makubwa zaidi, kuliko kua mtumwa ulieng'ang'ana kutumikishwa huku inaendelea kuteseka..

wewe ni zuzu au elimu yako imekusaidia kutumikishwa tu gentleman bila kua na maono nje ya box?

hebu ondoka kwenyehuo utumwa wa mateso na unesoma, lione!! uvivu tu na fear of unknown..

eti maslahi ng'we ng'we ng'we huku umeng'ang'ana kwenye kazi hiyo hiyo🐒
 
Mtu ana degree ya soshiolojia unataka nae akafanye kilimo na ufugaji? Au hiyo mtu unamshaurije?
sio kilimo na ufugaji tu anaweza hata akafanya biashara na hata akawa mwanasosholojia wa hao wafugaji na kilimo.

Sosholojia ni nguzo muhimu sana katika uchumi na maisha na ni chanzo muhimu sana cha sera mbadala ya zilizokwisha wakati.

haiwezekani ukawa mwanasosholojia ukajifungia ndani nyumbani wakati you are belong to communities as their adviser in influencing changes and solutions to some of their issues that affects their daily lives 🐒
 
Uandishi wa habari ni sekta kubwa ila ktk redio na TV haiitajiki elimu ni kipaji cha kuongea tu. Lakini uandishi una fursa nyingi ika wabongo ni vilaza. Imagine sekta ya habari ilivyokubwa halafu muandishi ukose kazi.
 
Hapa nimemkumbuka jooooooji malatooooo wa ITV

waende wakasome kwa bidii sana, ili wakapate ujuzi na maarifa ya kuja kuibadili fikra na mitazamo ya jamii na maisha kijamii, kiuchumi na kisiasa,

na sio kulalamika kama wewe bila kutumia maarifa na ujuzi wa kitaalamu ulionao baada ya kuhitimu masomo ya chuo, na kutumia fursa bwerere zilizoko nchini kufanya biashara, kilimo, ufugaji n.k🐒
Elimu yetu hii hii ya kukaririshwa unategemea mtu aibuke na practical experience?
 
waandishi wa habari wanapata shida sana, wanaomba omba sana pesa, wanakula sana rushwa ili wasikurushe au wakurushe, inasikitisha sana. nimeshafanya nao kazi miaka kadhaa, na huwa nawaonea huruma. ndio maana wana hasira, wanatangaza kwa kisirani habari hasa zinazodhalilisha watu, ni kwa sababu hawawajali, hawalipwi vizuri na hata hao wanaolipwa mikataba yao ya ajira inatia huruma au haipo kabisa.

however, tuendako, wale ambao Mungu anawatokea wakapata mtaji wa kutafuta habari na kuziuza, kufungua tv mtandaoni na ikawa famous n.k, wanapata sana pesa. mbona ulaya hata hao youtubers tu ambao sio waandishi wa habari wanatengeneza sana pesa? sembuse waandishi wetu wakiamua kujikita kutafuta habari za sekta fulani tu inayogusa jamii, wanaweza kufanya makubwa.
Mrengo ajira ndio unawagharimu.Muandishi akiandaa documentary hata kosa hela. Muandishi aaandae hata documentary za lugha asili hakosi hela. Kazi yao kujazana mjini tu.Wanawake wengi waandishi huitumua TV au redio kutafuta mmme mwbwana na kudanga.
 
Kuna mdau humu ameposti juu ya changamoto zinazowakumba waandishi wa Azam Mikoani eti wameshushiwa ujira kutokea tshs 500,000 mpaka 300,000 kwanza nikagutuka kwamba wanalalamika kwa kulipwa 300,000?!!

Kama Azam waandishi mikoani wanalipwa 300,000 basi ITV hali ikoje? Je, hizi media ndogondogo za dini mambo yakoje? Kusema kweli hamna tasnia inazaa watu wenye "low self esteem" kama journalism maana ili waishi ni lazima walambe miguu ya watu wengi ili maisha yaende; mnaonaga vile vipaza sauti (mic) vinavyojaa katika press conference za kina Haji Manara na Mwijaku? Basi usishangae kila "mwandishi" aliyetokea kapoteza siku nzima ili akapewe tshs 10,000 tu siku iende

Kwa wanawake hali ndio mbaya zaidi katika kutafuta namna ya kujiongezea kipato

Pia soma:DOKEZO - Waandishi wa Habari Azam wanataabika Mikoani, wanahitaji msaada kulipwa stahiki zao
Kwahiyo Mzee wa Azam all purpose flour kashimdwa kutupa maisha mazuri.anaishia kulipa wacheza faul.
 
Hamna kazi ya uandishi ina vilaza wengi sana naweza kuwa smart katika kuendesha kipindi kuliko waliosomea
Aisee. Nilisikiliza mahojiano ya TV online moja na generali ulimwengu.Aisee sio utumbo ule, nadhani generali alimvumilia yule dogo maana aliuliza maswali hata la7 hawezi uliza ujinga ule.
 
Upo sahihi.

Media zinatarajia zijiendeshe kwa matangazo.

Teknolojia iko advanced siku hizi tangazo linaweza kuwafikia watu wengi Tz nzima ukiliweka FB, Insta, X, Reddit. Ukilisponsor hilo tangazo Litamfikia aliye kazini, nyumbani, gesti, shambani wakati kwa traditional media litamfikia akiwa amewasha hiyo redio au TV na siyo muda wote.

So media nyingi zitakufa kwa sababu hakuna ambaye amesolve utata wa kipato kingine kitatoka wapi.
Siku hizi wamebuni kamari kama chanzo cha mapato. Yaani masaa yote ni kamari mwanzo mwisho mpaka inakera kusikiliza radio.
 
Back
Top Bottom