Usimshauri ndugu au rafiki asomee uandishi wa habari: ni sekta ambayo inaenda kufa na atateseka sana

Jifunze kuwa content creator, ingia YouTube anza kutengeneza content, utapata matangazo mengi tu.

Ni maajabu unawapa habari Azam TV, badala wewe uwe na online tv yako
 
Hamna kazi ya uandishi ina vilaza wengi sana naweza kuwa smart katika kuendesha kipindi kuliko waliosomea
yap, vishoka wengi. imagine baba levo, mwijaku, masanja, joyce kiria na wengine nao ni waandishi. kwahiyo imekuwa tasnia ya machawa? hivi hawanaga control mechanism?
 
Waandishi wengi ni watu ambao shuleni walikuwa vilaza mno. Wengi wao kidato cha nne walifeli au kupata div IV ya mwisho. Hawakuwa na option zaidi ya kwenda kwenye uandishi. Pia wengi wao walipenda umaarufu zaidi kuliko hela. Media houses kwa sasa hazina uwezo wa kulipa mishahara. Makampuni yanaona ni heri yawekeze kwa Diamond kama mtu binafsi kuliko yaweke hela kwenye Wasafi TV/Fm ya Diamond. Waandishi watumie kujulikana kwao kutafuta kazi nyingine ya kufanya.
 
Shida waandishi waliosomea hawa ajiriwi wanapewa kazi kina dokta kumbuka....

Hiyo sio bongo tu. Hata kenya wanalalamika, nigeria wanalalamika, ghana wanalalamika.

Kwamba media zao siku hizi zinaajiri comedians, actors na tik tokers.. wenye degree za uandishi wa habari wanakosa kazi
 
Elimu yetu hii hii ya kukaririshwa unategemea mtu aibuke na practical experience?
Yes,
tena wanafanya practical jobs vizuri sana, mathalan,
hivi sasa nchi yetu ina mpaka mawaziri wakuu ambao walikua walimu tu, na kuna mawaziri na wakuu wa idara madaktari.

hata huyu muungwana Pascal Mayalla ni muandishi wa habari lakini pia ni mwalimu wa sheria na mfanyabiashara muandishi.

unaweza kusomea na ukafanya practical jobs ya kitu kingine kisichokua taaluma yako...

kwani wao waweze wana nini hata wewe ushindwe una nini gentleman? 🐒
 
Kwahiyo.the great.mzee wa DP World.alikuwa.sahihi
 

Trust, wale wenye akili zao na uelewa, hii mbele yao ni fursa. Wana nafasi adimu ya kujitofautisha, kwa kuandika habari zenye utafiti, balanced, zisizo na uchawa wala vinasaba vyake, na zenye nia ya kuelimisha na kuifahamisha jamii.

Copy and paste journalists wajue hawataweza kupambana na Zembela, Baba Levo au Mzee wa Minyama, ambaop habari zao ziko shallow na zenye mbwembwe nyingi ili kuwaonyesha vijana wanajua wanachofanya. Wale ni wachekeshaji. Vijana wakizeeka wataelewa. Watajuta wakati wamashapigwa.
 
mwajiriwa hupaswi kuwa tajiri ndugu, unapaswa kujikimu pekee yani unyonywe kisha upate ujira mdogo usife njaa
 
Sio Leo Toka kipindi hicho uandishi,utangazaji ni umaskini tu unless uwe na akili nyingi kama Millard ayo otherwise ukisomea journalism umaskini unakumaliza
 
Azam hawezi shindwa Lipa hizo laki 5-3. UKWAJU tu peke yake unaweza Lipa wa andishi wote tz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…