Usimuonee huruma Mwanamke

Usimuonee huruma Mwanamke

Biblia inasema wanawake ni dhaifu halafu hapo hapo inasema tuishi nao kwa akili hivi kitu dhaifu unatumia akili kuishi nacho??
Kule eden apart from lile tunda kuna mambo mengine ambayo shetani aliongea na mwanamke ambayo sisi wanaume hatutakaa tuyaelewe kamwe.
Nilichojifunza kule Eden ni uwezo wa hawa bibi zetu kupiga U-turn
 
MWANAMKE :

1) Aliungana na Shetani kumfanya Adam amkosee Mungu muumbaji wake.

2) Alitumiwa na shetani kuchunguza siri ya Samson na mwishowe akamsaliti, Samson akatobolewa macho na kuteswa sana na Wafilisti

3) Aliungana na Shetani kumdharau Ayubu na kumwambia amwache Mungu wake kabisa.

4) Aliambiwa na Mungu asigeuke nyuma, akageuka na kuwa jiwe la chumvi.

NB: Hata leo ugomvi mkubwa wa Mwanaume na Mungu unasababishwa na Mwanamke.

Tuishi nao huku tukiwafahamu walivyo
Ongezea na hii

Luka 8:19-21
Neno: Bibilia Takatifu

Ndugu Wa Kweli​

19 Wakati mmoja mama yake Yesu na ndugu zake walikuja kumwona lakini hawakuweza kumfikia kwa sababu ya msongamano wa watu. 20 Mtu mmoja akamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje wanataka kukuona.”21 Yesu akamjibu, “Mama yangu na ndugu zangu ni wale wote wanaolisikia neno la Mungu na kulitii.”

Yesu alimkataa bimkubwa in broad daylight!!

Watu wengi hapa wamekazia kwenye mke na mademu lakini hata bimkubwa anaweza kukutoa kwenye reli kama wanawake wengine
 
images (28).jpeg

Wanaume walioshindikana na wanawake, mfano wa kuigwa!
 
Mwanamke Ni mtu hatari sana, Mimi ni mfano Hai wa Matendo ya ukatili wa Mwanamke:


Hii naongea kutoka Moyoni mwangu wanao Bisha tabia za wanawake hawazijui.


Sikia hii story ya kweli katika Familia yangu,

Mama mkubwa mke wa Baba yangu walio oana na Baba yangu bonge la Harusi ujanani wali Dumu katika ndoa yao kwa miaka 5tu na wakazaa watoto wa3. Ila ugomvi ulikuwa daily tatizo mwanamke Alikuwa hafanyi majukumu yake ya nyumbani bali alipenda sana starehe na waganga kumchezea mume, Mume akapewa taarifa na majirani akafuatilia aka kuta kweli mkewe na vitu vya ajabu kwenye kabati la nguo na kitandani kwenye mto wa Baba na uvunguni kaweka dawa za mitishamba..


Mume kufuatilia vizuri aka gundua Mwanamke pia alikuwa anaiba hela ndani na kujenge kwao.. Wakaachana ndai ya miaka mi5 ya ndoa.


Mzee akachiwa watoto wa3 wadogo sana, akaishi bila mke kwa miaka4 , wazazi wake wakamshauri Aowe mke mwingine baada ya taarifa za yule mke wake kusambaa kuwa anaishi na mawanaume Mwingine Arusha na nimja mzito, wakati kamuachia watoto tena kwenye Nyumba ya kupanga uja nani akiwa na hali ya kawaida sana kimaisha kwa maana ya kipato cha kawaida.


Mzee kweli akajiongeza aka chukua mke mwingin ambaye ndio mama Yangu, tukazaliwa sisi, baada ya miaka kama 25 kupita tukiwa tusha zaliwa watoto6, Baba alisha pandishwa cheo na kusoma zaidi maisha yakawa makubwa na akawa msaidizi wa mkurugenzi wa Bank kuu ya tanzania na baadaye mkuu wa Azina, akawa kesha wekeza sana kila kona ya jiji la Dar na kwao Mkoani..


Ghafl mauza uza ya ugomvi ndani yakaibuka mzee kawa kama anachanganyikiwa haishi kumpiga mama kila mara yaani akawa kama siyo yeye tena.. Mara afukuze watoto mara hili mara lile, Baadaye Mama yangu akaugua ugonjwa wa ajabu sana akabaki mifupa tupu mm nikiwa ndio nimezaliwa nina mwaka 1 , mzee akawa hajali huduma wala hataki kuangali watoto,


Mama akaja kuchukuliwa apelekwe matibabuni, walizunguka mahospitali yote tanzania na ukumbuke hadi kenya na South africa alipelekwa lakini haponi wala ugonjwa hauonekani, Mwishoe akawa anakaribia kukata roho kabaki mifupa tu waka mrudisha Kijijini kwao asubirie kufa tu. Lakini kule kijijini wazee wa upande wa Mama wakajiongeza wakampeleka kwa mtaalamu wa Jadi aka aguliwa na ukweli ukajulikana alitupiwa jini na mke mkubwa na mambo mengine mengi tu.. bahati nzuri akatibiwa akapona akarudi kwenye hali yake baadaye Wakati anarudishwa nyumbani kwa wazazi wake maana alitokea kwa Matibabu ya jadi.. aka kuta watoto wote wame teletwa na kutelekezwa kwa wazazi wote. . wamekonda nusu ya kufa yule mkubwa kuliko wote aliye kuwa ana mika15 ndio kachangnyikiwa wengine wote wameacha shule na hawataki kabisa kusikia shule wala hawajielewi. Wazee wakoo waka jiongeza kuwapokea na kuwalea.


Mama alipo fuatilia aka ambiwa alivyo ondoka tu kwenda matibabuni, Week ile ile Mke mkubwa aliyekuwa ame achana na baba kwa miaka 25 alirudi na kugina ndani kwenye nyumba aliyejenga Mama yetu na Baba, na wakati huo Mzee hajitambui tena kawa kama mjinga wala hakumbuki watoto ana itwa ustawi wa jamii anaulizwa matumizi ya watoto ana sema mbona yeye hana watoto zaidi ya watatu aliyo nao nyumbani,?? watu wakadhani ni utani, kuja kumbana sana wakaagundua kweli hana kumbukumbu .. ila kesi ikaenda mahakamani ika amuliwa ahudumie watoto na aangaliwe kama akili ziko sawa. baadaye Ikaisha kienyeji Majaji wakapewa hongo na yule mke kubwa maana sasa yeye ndio alishikilia account zote za baba na mzee alifukuzwa kazi maana alikuwa haeleweki tena..


Baada ya Muda Baba kaja kufa kiajabu ajabu tu.. tuka mzika, mama mkubwa kaendelea kuishi ndani na wanawe, Ukoo ukasema kuwa kila kitu kwenye nyumba aliyokimbilia kuishi Mke mkubwa nicha watoto wa mke mdogo kwa kuwa Marehemu alisha Andika na kuwambia Wazazi wake kuwa Nyumba ya ujanani aliyo jenga kabla ya mama yangu kuishi naye na kuzaa naye ni ya watoto wake watatu aliye zaa n mke wake wandoa, ila hii mpya aliyojenga akiwa na mke mdogo yaan maa yang ni ya watoto 6 aliyo zaa na mama yangu.. Una ambiwa kile kikao cha ukoo kilivurugika kwa ugomvi mke mkubwa akawa moto na yule aliye kuwa kiongozi wa ukoo alikufa ndani ya week iliyofuata, Kukawa na viongozi wengine wanao chaguliwa Kushika nafasi ya Ukoo ila wakigusia haki za watoto wa mama yangu tu wanakufa, mpaka sasa Ninavyo ongea Baba wakubwa wa5 wote wamekufa kimaajabu. . na haki yetu hatuja ipata .. ndugu zangu karibia wote ni vichaa . nime baki mm tu ndio angalao nina jitambua..ingawa vita ya maisha yangu ni kubwa kama siyo kujificha katika maombi wangesha ni maliza..


Lakin kikubwa kinacho ni shangaza ni kuwa Baba anaonekana kule kijijin watu kazaa wana muona akiwa mchafu na manywele ila waki msogelea anapotea, mwanzoni tulidhani ni utani tukasema labda watu wanongea tu kwa kuwa yaliyotokea kweye familia yangu yameumiza watu wengi hadi majirani wa kule kijiji hivyo wanazusha tu kwa hasira walizo nazo juu ya mateso wanayo yaona kwa ndugu zangu.. Lakin sasa Hivi ni navyo ongea juzi tu mwezi wa kumi na moja mwaka huu uliyoisha. Kaka yangu mkubwa akiwa ndani kwake Katokewa na baba, kaamka zake aka kojoe ghafla akamuona mzee kakaa kwenye kochi ila haongei kitu alipo piga kelele mzee kapotea.


Je! KATIKA HALI KAMA HII MWANAMKE ANAYE ZUNGUMZIWA NA. HERIET HAPA ANATOFAUTI GANI NA HUYU MKE KUBWA WA BABA??


Jamani Uchawi Upo.. Ila naku hakikishia siku nikiingia kwenye Uchawi.. Nita angamizaa kizazi cha huyu Mwanamke mpaka kitukuu cha mwisho.. Naupima tu Uvumilivu wangu katika maombi.. Mungu aniongoze maana naijua nafsi yangu ilivyochoka na siku nikihamia kwa Shetani nitakuwa Shetani Halisi wala sita Igiza kabisa.
Pole sana mkuu kwa yote hayo yalio watokeeni.
Najaribu kufikiria mwisho wa huyo mama na kizazi chake sijui itakuwaje aisee??
Mimi nikuombe hio paragrafu ya mwisho usiishi ndugu yangu mpendwa, siku zote usilipe ubaya kwa ubaya, ubaya unajilipa wenyewe, iache asili ifanye kazi yake kuwalipieni ndugu yangu poleni mno.
 
Nina shemeji yangu anaishi nchi mojawapo inayopakana na Tz, yuko kwenye mchakato wa kutafuta mke wa kuoa.
Kwa vile huwa anakuja Tz mara kwa mara basi akakutana na binti mrembo mwenye mtoto mmoja. Binti akamuelezea shemeji jinsi alivyozalishwa na kutelekezwa. Shemeji akamuonea huruma akamwambia amuoe binti akamjibu kwa sasa ndoa bado bado wawe kwanza wachumba.
Shemeji akakubali , akawa anamhudumia yule binti ikiwemo kumpangia nyumba, kumfungulia biashara pamoja na mtoto wake kulipiwa ada shule ya binafsi.

Shemeji akamnunulia binti mrembo simu ya gharama akaweka na upelelezi wake..yaaah yaaah binti kumbe hajatulia shemeji akapata maovu yote ya binti ikiwemo ya binti akiwa kwa mganga akitoa mimba ya lijamaa lingine.

Shemeji akakata mawasiliano binti akaanza kusisitiza yuko tayari kuolewa, shemeji akaweka ushahidi wa maovu yake , ikawa mahusiano yameishia hapo huku binti akijuta.

Usimuonee hurumaaa!!
Inatisha
 
Kwa kweli. Kuna mwanamke alikua na shida ya ada mtoto wake kafukuzwa shule. Kaja kwangu machozi yanamtoka. Nikamkopesha 1M toka mwezi March. Mpaka leo mwaka unaisha ananipiga tu kalenda. Daaaa wanawake
Hakuna wanaume wanaokopa na hawalipi?
 
USIMUONEE HURUMA MWANAMKE.

Kwa Mkono wa Robert Heriel.

Wangestahili huruma lakini si sasa.
Wangestahili kupendwa lakini si Zama hizi.
Wangestahili kujaliwa na kuheshimiwa lakini hiyo ingefaa Zama zile sio Zama hizi.

Hata zamani walipokuwa wanasifa za wanawake hawakuonewa huruma sembuse sasa ambapo wamepoteza sifa ya uanamke Kwa 90%. Sasa hivi ndio hawapaswi kuonewa huruma hata kidogo.

Ni Mama zetu, shangazi zetu, wake zetu, dada na Bibi zetu lakini kamwe usimuonee mwanamke huruma hasa katika Zama hizi. Ni kitanzi na kaburi lako mwenyewe.

Siwafundishi roho mbaya Kwa maana sio asili yetu wanaume. Sisi ni watu wema tangu kale mpaka pale huruma mbaya ilipotuingia na hapo ndipo ubaya ukatuingia.

Jitahidi kuwa mbinafsi Kwa kadiri utakavyoweza ili kujifurahisha wewe mwenyewe kuliko kuhangaika kumfurahisha mwanamke. Haitakusaidia popote pale zaidi ya kujiumiza na kuonekana kazi bure.

Usimuonee huruma Mwanamke hata Kama macho yako na akili yako vinaona anastahili kuonewa huruma.

Pengine Mama Yako tuu angalau huyo waweza mkumbuka kidogo lakini waliobaki cheza nao Kwa akili nyingi huruma sifuri.

Huruma yako iwe na maslahi mapana. Apate kumi upate Mia. Apate Mia upate elfu. Usitumie moyo wako, tumia akili.

Usiwe na huruma Kwa maana wanawake hupenda kuonewa huruma Kwa wale watu wasiowapenda, huziweka nyuso zao za huruma ili kukulaghai na kuziteka hisia zako, usiwaangalie usoni wala usisikie sauti zao pindi Wazungumzapo.

Walakini usimsahau mke WA ujana wako ukamtendee wema ikiwa ulimchukua akiwa means mwali bikra Safi. Huyo na Mama yako walau unaweza wapa huruma yako kidogo hata Kama wangekutenda makosa kadha wa kadha.

Lakini kama hawana sifa hizo kamwe huruma yako isiwe karibu na Mwanamke.

Pia usitake huruma zozote kutoka Kwa yeyote, tena akiwa mwanamke ndio usizitafute huruma zake.

Sina la ziada. Mwaka mpya mwema

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Makanya, Kilimanjaro
Doh!!cna la kuchangia kwenye ili kwakuwa nimechelewa.
"Ucmuonee huruma mwanamke'Ni maneno niliyokuwa nayackia kila cku ila ckuyajua kabisa umuhim wake.
Ila sasa nimeyajua.Nami naludia kusema tena ucmuonee huruma mwanamke.
 
Doh!!cna la kuchangia kwenye ili kwakuwa nimechelewa.
"Ucmuonee huruma mwanamke'Ni maneno niliyokuwa nayackia kila cku ila ckuyajua kabisa umuhim wake.
Ila sasa nimeyajua.Nami naludia kusema tena ucmuonee huruma mwanamke.
Nje ya Mada ....Jifunze kuandika vyema mkuu...
 
Hakika hilo ndio linaloweza mtesa mwanamke na si jingine, na akifanikiwa kuzowea mazingira ya mateso basi kila mwanaume atakae kuwa nae au kuishi nae lazima alizwe na kujuta maishani mwake
 
Back
Top Bottom