Nashukuru kwa uvumilivu wenu na napenda kutoa pole kubwa kwa kutoonekana kwangu kwenye Jamii Forum. Sababu zangu zilikuwa nje ya uwezo wangu na pia nilikuwa mbali na mtandao kwa muda.
Ninaamini umuhimu wa kushiriki kwenye simulizi na nipo hapa kurejea na kuendelea nilipoishia kama nilivyowaahidi. Asanteni kwa uelewa wenu na natarajia kuendelea na Sehemu ya nne.
Tukumbushane Matukio ya sehemu ya tatu(3)
Kwa sekunde zilizosalia, nilifanya uamuzi. Nilichukua hatua na kufunga biashara yangu. Niliona jumla ya faida iliyokuwa imeandikwa kwenye simi yangu ilikuwa 40k
(!!!Siku chache nikageuza Jijini Dar Es Salaam, Nikiwa bado na hisia za kufurahia mafanikio yangu, niliendelea na safari yangu ya kura raha jiji la Dar es Salaam. Jiji hili lenye shughuli nyingi lilikuwa ni mahali pazuri pa kufurahia starehe za kisasa na maisha ya jiji. Nilipata fursa ya kufurahia vyakula bora katika migahawa mashuhuri kama samakisamaki, kushiriki katika burudani za muziki wa live, Mlimani City ndo ilikuwa kijiwe changu cha kunywa kahawa.)!!
(!!Sikuishia hapo. Nilifanya ziara za kuvutia katika maeneo maarufu ya jiji kama vile Coco Beach, Mikocheni, na Masaki. Nilijaribu mambo mapya kama vile kusafiri kwa boti hadi visiwa vya Zanzibar na kufurahia jua la bahari la Tanzania.)!!
SASA TWENDE KAZI
SEHEMU YA NNE(4):FURAHA INAGEUKA KUWA HUZUNI
Furaha ya ghafla ya kugundua kwamba nilikuwa nimepata faida kubwa ilinifurahisha. Nilifurahi sana kiasi kwamba nilihisi kama ninapaa angani. Hii ilikuwa ni matokeo ya kazi nyepesi ya kubonyeza kitufe cha Buy na kujikuta nimesahau, ila faida hiyo ilionekana kama zawadi ya ghafla kutoka kwenye soko la forex.
Nilifurahi sana kiasi kwamba nilisahau kuzingatia ukweli wa biashara ya forex: ni hatari na inahitaji uchambuzi thabiti. Kwa kujiona kama mshindi wa bahati nasibu, nilipuuzia kanuni za msingi za biashara. Kufanikiwa kwangu kulionekana kama mchezo wa kubahatisha zaidi kuliko mkakati uliopangwa.
Hata hivyo, michezo ya kubahatisha mara nyingi huwa na matokeo mabaya. Kwa upande mwingine, kuchanganyikiwa na wasiwasi vilianza kuniingia. Nilikuwa na hamu ya kufunga trade na kuchukua faida yangu haraka iwezekanavyo kabla ya soko kubadilika mwelekeo. Hali hii ilinifanya kuhisi kama ninacheza na nyakati.
Kwa sekunde zilizosalia, nilifanya uamuzi. Nilichukua hatua na kufunga biashara yangu. Niliona jumla ya faida iliyokuwa imeandikwa kwenye simu yangu ilikuwa 40k tena kwa mtaji mdogo tu nilioweka na kwa muda mfupi, na hilo ndilo lililozidi kuleta furaha yangu. Lakini kwa moyo ulivyokuwa unapiga kwa kasi, nilivuta pumzi ya kuridhika na kuchukua muda wa kuadhimisha mafanikio yangu.
Hata hivyo, furaha hii ilidumu kwa muda mfupi. Siku chache baadaye, hali ilibadilika ghafla. Soko liligeuka kinyume na matarajio yangu, na nilijikuta nikipoteza sehemu kubwa ya faida yangu. Hii ilinifanya nipatwe na wasiwasi mkubwa na kuanza kutilia shaka uwezo wangu.
Ukosefu wa mpango wa kudhibiti hatari ulinionyesha upande mwingine wa sarafu ya biashara. Niliona jinsi ghafla unavyoweza kuwa na faida kubwa na baadaye kupoteza yote. Hisia za kuchanganyikiwa na kujutia zilinitawala, na nilikosa usingizi kwa siku kadhaa nikijaribu kuelewa kile kilichokwenda kombo.
Mara hii, nilikuwa naona wazi athari za kujituma bila mpango wa kina. Nilikuwa kama mwendawazimu aliyehamasishwa na matokeo ya ghafla na kusahau kwamba katika biashara, uchambuzi wa kina, mpango thabiti, na kudhibiti hatari ni muhimu kuliko kushinda mara moja.
Kwa kukosa utulivu wa akili, nilianza kuona kila fursa kama hatari. Hata maamuzi madogo yaliniogopesha. Hali hii ilinipeleka kwenye mzunguko wa kushindwa tena na tena. Kila siku ilionekana kama kupoteza mapambano, na wakati mwingine, nilianza kujiuliza kama ningeweza kurudi nyuma.
Nikakumbuka jinsi nilivyocheka na kujivunia mafanikio yangu ya awali, na sasa, nilikuwa kwenye hali ya kusononeka na kujuta. Kupoteza ile akaunti yangu ilikuwa kama kupoteza ndoto zangu zote za uhuru wa kifedha na mafanikio. Nilihisi kama mtu aliyepotea nyikani bila mwelekeo, huku giza likinitanda pande zote. Hakika huu ndo wakati ambao sitakaa kusahau kwenye mausha yangu. Japo nimepitia mengi magumu. lakini hili!
Usikose sehemu 5 , inakuja soon. Yaani hapa bandua bandika. Nimalize yamoyoni. Ili watakaujifunza wasiboeke.