Usipende kununua magari yaliyotumika Tanzania

Carina ina Kelele kama kifaru cha vita dah [emoji119][emoji23]
 
Upuuzi, sema wanaitaji kuwa makini na sio vinginevyo, nimeagiza magari 7 maishani mwangu, yote nimeuza na niliowauzia wanashukuru mpaka leo.

Nimenunua magari yaliyotumila ma 4 katika maisha yangu na sijajuta,

Cha muhimu:

  • Body zuri.
  • Spare zipo.
Dah kweli niliwahi nunua Noah million nne nikaipiga service ya maana mpaka sahivi ni chuma
 
Hivi unadhani wewe pekee ndo unayajua haya? Hivi unadhani wote wanaonunua used hapa nchini hawajui kuna kuagiza?
 
Hiyo gharama ya ushuru ambayo mtu anaiona kubwa anakuja kufidia kwenye gharama za kurekebisha hiyo gari. Na mimi nilishajiaminisha kuliko kununua gari used kutoka mkononi kwa mtu kwa zaidi ya millioni 15 bora uagize japan.
 
Bei hiyo ni bila kodi na usafirishaji au pamoja usafirishaji na kodi za TRA
Hapo bila
1.Kodi
2.Insurance
3.JAAI
4.Ushuru wa bandari
Kodi (ndio baba lao)
5.Clearance 300k -500k
Gari ya 4M hadi unasajili hapa bongo uwe na 13+M

Msidanganyane kuna gari mwaka 2014 niliitoa babdarini ya ndugu yangu kodi pekee ilikuwa 9.4M
Ushuru 540k
Bei ya kununuliwa UK 7.8M
Hapo sijaweka gharama ya usafirishaji na ukaguzi Inspection fee na bima ya gari ikiwa safarini (baharini)
 
Kuagiza gari nje siyo gharama kama watu wanavyozani


Tatizo lipo kwenye kuisubil hiyo gar ifike, uvumilivu unao!?

Ndiyo maana wengi wanaishia kwenda show room wanabeba na kuondoka


Lakin uliwah kujiuliza unayenunua gar showroom unampa faida kubwa kiasi gan muuzaji!!?

Agiza gari kijana acha uoga
 
Mpwa shituka basi unanitia aibu!!
 
Facts
 
Si kila mtu ana maamuzi yake lakini? Kuna mtu anaona vanguard ya 35 m ni bei ila anachukua used kwa 20m. MIMI siwezi.
Hata kwa 18M mimi nachukua ila iwe na namba za karibu mfano gari ya juu juu yenye usajili DZ utakuta bado ni mpya kabisa.

Tena hasa ambayo inatembelewa mjini tu. Ishu ni kukagua kama kuna faults uzitambue mapema. Na pia anayekuuzia ana mishe gani? Sio unauziwa gari na mtu ambaye hata gari haijui vizuri unanunua tu utapigwa.

Ujinga wa kununua gari eti kisa namba E upigwe kodi almost 15M zaidi wakati gari hio hio unaipata kwa bei chee sifanyi. Bora ununue gari uweke laki 5 ubadilishe ownership tu.
 
Vanguard Namba DZ nzima kabisa hata gearbox haisumbui uipate kwa 15 million? Ukiipata niite nikuchangie milioni 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…