G-Funk
JF-Expert Member
- Feb 10, 2022
- 2,398
- 5,554
Asilimia sio ishu, mtu gari si unakagua. Shida yetu tunapenda kitonga mtu hela hana anafosi kununua gari flani.Hii nakupa tu ushauri ww unayetaka kumiliki gari lako na lisikupe mawazo ya kuonana na mafundi Kila siku.
Asilimia 85 ya magari used Tanzania mmliki huuza kwa Sababu gari linamsumbua, asilimia.
Asilimia 10 tu huuza gari kwa Sababu ya changamoto za kimaisha.
Asilimia 5 tu ndiyo huuza gari Ili wanunue gari lingine.
Mbaya zaidi mbongo kusema ukwel ni dhambi kubwa kwake atakwambia hii gari ni kuwasha na kuondoka kumbe yeye anajua shida Iko wap hakwambii.
Ukifika huko unashangaa gar inamatatizo kibao
Nashauri ingiza gar Toka nje kidogo zinakuwa nzima japo ni used, usiogope ushuru kwa Sasa unalipika siyo kuhangaika na gari lililomshinda mwenzako.
Madalali watakuja hapa kupinga huu utafiti wangu lakin mm Big thinker nimetimiza jukum langu usije sema sikukwambia
Gari zinajulikana vimeo na gari kweli, gari nyingi za namba mpya unakuta bado nzima tu provided ziko kwa watunzaji.
Unakuta mtu anataka Crown Athlete ila ana million 7. Gari hio ili uipate yenye viwango unaipata kwa 13.5M ila mtu anang'ang'ana mwishowe unauziwa gari namba DE huko gari imesajiliwa 2015 bongo miaka 7 nyuma mtu aliingiza mjini kashaifuja na kuiuza imeuzwa zaidi ya mara moja wewe unakuja kuveshwa gari imechoka ina poor economy ya wese ila alimradi una wenge na 👑 Athlete.