Usipotoshwe na watu wasioelewa maana na utaratibu wa kuwa na raia pacha. Angalia hapa maelezo ya uraia pacha na niulize swali lolote nitakujibu

Usipotoshwe na watu wasioelewa maana na utaratibu wa kuwa na raia pacha. Angalia hapa maelezo ya uraia pacha na niulize swali lolote nitakujibu

Hapo ndipo unapokosea. Tunaposema uraia pacha sio kwa Watanzania pekee, bali ni kwa Watanzania kuwa na uraia pacha na nchi nyingine na wasio raia wa Tanzania kuwa na uraia pacha na Tanzania. Haiwezi ikaa suala la upande mmoja kama unavyosema
Mimi najikita kuongelea uraia pacha wa upande wa mtanzania wa country of origin Tanzania kuwa hauna faida yeyote lakini pia uraia pacha wa mtu wa taifa lingine mfano mchina, mhindi na mwarabu una faida gani kubwa wakati kazi yao kubwa inakuwa ku import tu bidhaa toka Nchi zao kuja kuuza kwetu? Na ku drain pesa zetu za kigeni tu? Inasaidia Nini? Hata hao wa Nchi zingine haisaidii
 
Na swalijingine

Tanzania ikiruhusu uraia pacha, ni kwa ajili ya Watanzania pekee?

Hapana. Unaporuhusu uraia pacha inakuwa ni kwa ajili ya Watanzania wanaotaka kuchukua uraia wa nchi nyingine, na watu wa nchi nyingine wanaotaka kuchukua uraia wa Tanzania. Ni lazima Tanzania na nchi hiyo nyingine zote ziwe zinaruhusu uraia pacha.
 
Mimi najikita kuongelea uraia pacha wa upande wa mtanzania wa country of origin Tanzania kuwa hauna faida yeyote lakini pia uraia pacha wa mtu wa Yaifa lingine mfano mchina, mhindi na mwarabu una faida gani kubwa wakati kazi yao kubwa inakuwa ku import tu bidhaa toka Nchi zao kuja kuuza kwetu? Na ku drain pesa zetu za kigeni tu? Inasaidia Nini? Hata hao wa Nchi zingine haisaidii
Mkuu Yehodaya, nadhani kuna point hapa unagusia, kwamba Watanzania wakiruhusiwa kuwa na uraia pacha kutakuwa na negative effect kwamba watatoa capital Tanzania kwenda nchi nyingine?

Inawezekana, lakini sidhani kama effect itakuwa kubwa kiasi hicho. Watanzania watakaoingiza capital nchini ni wengi kuliko watakaotoa capital nchini.

Na upande wa pili ni wale watakaopewa uraia wa Tanzania kuingiza capital nchini. Lazima haya mambo yaende pamoja kwa kuwa hatuwezi kuwa na uraia pacha unaoruhusu raia wa nchi nyingine kuwa na uraia pacha na Tanzania lakini raia wa Tanzania wasiwe na uraia pacha na nchi nyingine
 
Kwa miaka kibao uzoefu uko wazi watanzania walioko nje hawasaidii viwanda vya Tanzania kuuza bidhaa za Tanzania kwenye nchi zao Kama wahindi na waarabu .kikubwa Ni kuangalia faida ya diaspora kwenye uchumi mkubwa wa movement of goods kwenda soko kule aliko sio vihela vidovidogo vya remmittance vya pesa za rambi rambi na michango ya harusi

Wahindi na waarabu tunao miaka nenda Rudi lakini wanachofanya Ni kutuletea tu bidhaa zao .Sisi soko lao la bidhaa zao tu kwa asilimia kubwa.miaka nenda Rudi.Mchina kaja ndio kabisa katufanya gulio la bidhaa zake.Ukimpa uraia pacha ana kipi kikubwa kwa Nchi.? Ni Ku drain tu our forex kununua bidhaa kutoka his country of origin at our forex expense Wahindi,waarabu,wachina etc hutoa uraia pacha wakijua what will happen kwa viwanda vyao na bidhaa zao.
 
Kwa ninavyowaona wageni wakipata uraia wa Tanzania hamna maajabu watafanya. Yani Mhindi umpe uraia wa Tanzania akiwa katoka India unadhani atafanya nini, ataleta mapikipiki yao auze achukue hela arudishe kwao India. Ukimleta Mfaransa hivo hivo atafanya. Hawa wataondoa nafasi za wabongo wanao-import bidhaa za nje, watakuwa export houses za makampuni ya kwao

Wabongo walioko nje ni wachache na wana hela kidogo tu za kupandia ndege. Ukiwaambia watoe mitaji walete uku haiwezi fidia hela inayochotwa kwenye mzunguko wetu kwenda nje. Kwa mtazamo wa kiuchumi

Umeeleza mengi ambayo sikuyafahamu. Asante
 
Ikiwa Watanzania wazawa tu tena mpaka wamepewa hatamu serikalini, Wanauza Taifa kwa vipande vya fedha, Itakuwaje kwa mzaliwa wa UK aliyepewa haki yavkuitumikia Tz sambamba na UK yake moyoni?

Sisi nje waliopo nje wengi wamejiendea wenyewe, lakini wageni wengi toka nje WAMETUMWA(hata tudhaniao kuwa ni watalii) Wanakuja with missions, sisi tunawaza njaa zetu binafsi.

Tujenge uwezo kwanza, Uwezo was Kutuma watu nje, sio Uhuru wa kila ajisikiaye kwenda sense tu.
 
Nimekuwa nikisoma maoni na hoja za watu kuhusu Tanzania kuruhusu uraia pacha, na nimeshangaa sana na kugundua watu wengi sana wanaotoa maoni kuhusu uraia pacha hawaelewi kabisa inakuwaje mtu anakuwa na uraia pacha. Na hili nimeona hata toka kwa wanasiasa wanaopinga uraia pacha, na kuona kwamba wengi hawaelewi kabisa hili suala na wanaliongelea bila kuwa na ufahamu nalo.

Sasa nimeona ni vema kuwa na thread ambayo itasaidia kuelimisha watu juu ya suala hili. Na nitaanza na maswali ya msingi juu ya uraia pacha, na kujibu mengine yatakayofuta.

1. Tanzania ikiruhusu uraia pacha, ni kwa ajili ya Watanzania pekee?
Hapana. Unaporuhusu uraia pacha inakuwa ni kwa ajili ya Watanzania wanaotaka kuchukua uraia wa nchi nyingine, na watu wa nchi nyingine wanaotaka kuchukua uraia wa Tanzania. Ni lazima Tanzania na nchi hiyo nyingine zote ziwe zinaruhusu uraia pacha. Masharti na vigezo huzingatiwa.

2. Inakuwaje hadi mtu anakuwa na uraia pacha?
Inategemea masharti ya kila nchi. Kimsingi, huombi kuwa raia pacha, bali unaomba uraia wa nchi ya pili, na kama ukikubaliwa ndio unakuwa raia pacha, kwa kuwa sasa utakuwa na uraia wa nchi zaidi ya moja.

Jambo la msingi ni kwamba sio rahisi mtu kupata uraia pacha. Mara nyingi, mtu anapewa uraia pacha ikiwa ameishi kihalali mfululizo katika nchi ya pili kwa muda usiopungua miaka mitano. Na nchi nyingine zitataka upitie kwanza hatua ya kuwa mkazi wa kudumu (permanent resident) kabla ya kuomba uraia na kuwa traia pacha. Kwa hiyo basi, mtu toka Kenya hawezi kuja Tanzania leo na kuomba uraia pacha, sio rahisi.

Hivyo ieleweke wazi kwamba wewe Mtanzania ambaye hujawahi hata siku moja kuishi South Africa, huwezi kuondoka Tanzania leo hii kwenda bondeni ukaombe uraia ili uwe raia pacha. Vivyo hivyo mtu wa South Africa ambaye hajawahi kuishi Tanzania, hawezi kuja Tanzania leo ili apewe uraia wa Tanzania na kuwa raia pacha.

3. Nini hasa baadhi ya vigezo vya msingi vya kuwa raia pacha?
Inategemea nchi inaweka vigezo gani kwa raia wa nchi nyingine kuomba uraia pacha. Sharti kubwa la nchi nyingi ni kwamba usiwe na rekodi ya uhalifu (criminal record) ya nchi uliyotoka au nchi unayoishi na unaomba uraia, na uwe umeishi kwa muda fulani katika nchi unayoomba uraia ili uwe raia pacha.

Kama nilivyosema katika swali la kwanza, kigezo cha kawaida ni kuwa umeishi kihalali (sio kuzamia) katika nchi nyingine kwa zaidi ya miaka mitano. Sasa kuna nchi nyingine, ikiwa umeoa au kuoelewa na raia wa nchi hiyo basi unapata uraia wa nchi ya mume/mke wako na kuwa raia wa nchi hiyo, hivyo kuwa raia pacha. Sasa kuna baadhi ya nchi ziliona hili lilitumika vibaya, watu walioa au kuoelwa ili tu kupata uraia. Hivyo walibadilisha huu utaratibu na kusema lazima uishi katika ndoa, na kuthibitisha unaishi na mumeo/mkeo kwa angalau miaka 3 kabla ya kuomba uraia.

Kwa hiyo kila nchi inakuwa na vigezo vyake, na Tanzania tukiamua kuruhusu uraia pacha lazima tutaweka vigezo vyetu. Hatuwezi kutoa uraia kama sadaka ili watu wawe raia pacha.

4. Kuna watu wanakuwa na uraia pacha wa kununua?
Ndio, zipo nchi zinauza uraia. Kwa mfano, kuna nchi zinaweza kusema ukiingiza katika nchi hizo mtaji kuanzia Dola 250,000 basi una haki ya kupewa uraia. Kwa hivyo nchi kama hizo zitasemwa zinauza uraia. Tanzania hatulazimishwi na mtu yeyote kuuza uraia wa Tanzania, kwa hiyo tunaweza kuruhusu watu wa nje kuwa na uraia wa Tanzania bila kuwa na kigezo cha kununua uraia wa Tanzania

5. Je, Tanzania tunaweza kuwawekea Watanzania masharti ya kuwa na uraia pacha na nchi nyingine?
Sio rahisi, kwa sababu ni sawa na kusema tutaziwekea hizo nchi masharti ya wao kumpa Mtanzania uraia wa nchi hizo. Ila sasa, Tanzania tunaweza kuweka masharti kwa Watanzania walio na uraia pacha ili kulinda vitu kama usalama wa nchi yetu, nk

6. Je uraia pacha hauwezi kutuletea athari za usalama wa Tanzania?
Hii ni hoja potofu na imetumika vibaya na watu wengi. Ili mtu kusababisha athari za usalama wa nchi yetu sio lazima awe raia pacha. Na pia kama kuna maeneo ambayo tunaona uraia pacha unaweza kuhatarisha usalama wa Tanzania basi tutawawekea watu wenye uraia pacha masharti fulani ili kuzuia hilo. Kwa mfano, tunaweza kusema Mtanzania mwenye uraia pacha haruhusiwi kugombea nafasi za kisiasa kama ubunge na uraisi, au kutumika katika vyombo vya usalama kama JW, Polisi, na TISS.

7. Uraia pacha unakuwaje na manufaa za kiuchumi kwa Tanzania?
Hili ni swali la msingi sana. Jambo la kukumbuka ni kwamba unapokuwa wa nchi ya kigeni, kunakuwa na masharti yanayokuzua kufanya mambo fulani katika nchi nyingine. Kwa mfano, si rahisi kwa Mtanzania kutuma fedha za kigeni kwenda nchi nyingine, na ndivyo isivyo rahisi kwa mtu aiye Mtanzanaia katika nchi ya nje kutuma fedha za kigeni Tanzania. Sasa unapokuwa unaishi nchi ya kigeni na una uraia wa Tanzania, moja kwa moja unakuwa na kitu tunaita haki ya kutuma faida kwenye nchi yako (repatriation of profits) bila masharti magumu. Na kumbuka kwamba, kwa upande wa Tanzania, unakuwa na urahisi wa kuwekeza ukiwa na uhakika kwamba investments zako Tanzania ziko salama kwa kuwa unalindwa kwa haki za kuwa raia. Mtu kama Aliko wa Dangote huwezi kumlinganisha katika uhuru wa investments zake kama alionao MO kwa kuwa MO kama raia wa Tanzania ana wigo mwepesi na mpana zaidi wa kufanya biashara Tanzania kuliko Dangote.

Kwa hiyo Watanzania waliochukua uraia wa nje watajisikia huru zaidi kuhamisha mitaji yao kuja Tanzania wakijua kwamba wanahamishia mitaji Tanzania kama raia wa Tanzania bila kuhofu kubadilika kwa upepo wa kisiasa au hata kutaifishwa mali zao

Lakini zaidi, raia wa nje wenye uraia pacha na Tanzania wanakuwa na uhuru zaidi wa kuwekeza Tanzania ikiwa watakuwa na uraia wa Tanzania. Itakuwa rahisi sana na kutompa hofu yoyote Dangote kuhamishia mtaji mkubwa Tanzania akijua anafanya hivyo kama raia wa Tanzania

8. Vipi ikiwa nchi ya nje ambayo una uraia pacha nayo inataka uihujumu Tanzania, sio rahisi hilo kufanyika kama raia pacha?
Suala la nchi uliyonayo kukutaka uihujumu nchi yako ya kuzaliwa ni suala la uhalifu kama uhalifu mwinginme wowote wa kimataifa, na linaweza kufanywa na mtu yeyote hata asiye na uraia pacha. Nikiukana uraia uraia wa Tanzania na kuchukua tuseme uraia wa Burundi, kama Burundi watataka kunituma kuihujumu Tanzania sio lazima niwe raia pacha. Bado wanaweza kunituma kufanya hujuma hata bila kuwa na uraia pacha. Na kimsingi, ni rahisi mie kukataa kuja kuihujumu Tanzania nikiwa na uraia pacha kuliko kama niliukana uraia wa Tanzania kwa kushurutishwa ili nipate uraia wa Burundi. Kwa hiyo ni hoja poofu kuhusianisha uraia pacha na watu kuihujumu nchi yao ya kuzaliwa.

9. Je uraia pacha hauathiri uzalendo wako kwa nchi yako ya kuzaliwa?
Kwanza nini hasa maana ya mzalendo, na uzalendo au kutokuwa mzalendo kunathibitishwa na matendo gani? Je ndio tuseme mtu akiwa na uraia pacha na anaishi Tanzania atakuwa fisadi, mwizi, mhujumu uchumi, mvivu na mtoro kazini kuliko yule Mtanzania asie na uraia pacha? Hii pia ni hoja potofu inayotumiwa vibaya na watu wengi. Wengi watakubali kwamba Tanzania kwa sasa inapigika sana, watu wanafuja fedha za serikali na wanafisadi sana nchi hii. Sasa ndio tuseme watu wanaofanya haya ni raia pacha? Jambo moja la kuelewa ni kwamba, ni raisi kwa mtu asiye na uraia pacha kufanya ufisadi katika nchi yake kuliko yule aliye na uraia pacha.

10. Vipi raia pacha akifanya uhalifu na kukimbilia nchi nyingine aliko na uraia wa pili?
Dunia ya sasa ni kama kijiji. Unapofanya uhalifu wa aina yeyote ukiwa raia pacha, usidhani kwamba kukimbilia nchi nchingine kutakuokoa. Kumbuka katika masuala ya uhalifu kuna Interpol, polisi ya kimataifa, ambayo ni rahisi Tanzania kuitumia na wewe kukamatwa hata ukiwa umekimbilia nchi nyinge. Ukiiba gari Tanzania ukakimbilia USA ambako una uraia pacha, usidhani kwamba utapona. Na kumbuka kwamba, nchi nyingi zinaruhusu uchukue uraia wao kwa masharti ya kutokuwa na rekodi ya kihalifu (criminal record). Kwa hiyo sidhani kwamba utafanya ubakaji Tanzania ukimbilie USA na kuwa salama. USA watatengua uraia wako wa USA na utarudishwa Tanzania kwa nguvu (deportation) kwa sababu tayari umekiuka mashart ya kutokuwa na criminal record. Dunia ni kijiji siku hizi.

11. Je ukiwa uraia pacha, Tanzania inaweza kuutengua?
Inawezekana. Kama vile tu USA wanaweza kuutengua uraia wa Mtanzania kule USA kwa sababu ya makosa ya jinai, ndivyo Tanzania tunavyoweza kutengua uraia wa Tanzania wa Mchina ambaye anafanya makosa au uhalifu akiwa anaishi hapa Tanzania kama raia pacha

12. Je kuna Watanzania wenye uraia pacha kwa sasa?
Sio rahisi, hasa ikiwa waliupata uraia wa nchi nyingine ukubwani. Mara nyingi ili uwe raia wa nchi nyingine, lazima nchi hiyo ipeleke taarifa za ombi lako la uraia kwenye ubalozi wa nchi yako. Tanzania wanapopata ombi hilo basi wataubatilisha uraia wako wa Tanzania. Kuna nchi mtu unakuwa raia kwa kuzaliwa katika nchi hiyo. Ndio maana Tanzania kwa watu waliozaliwa nje, wenye birth certificate za nje, lazima uthibitishe uraia wako wa Tanzania ukifikisha miaka 18. Hiki ndicho tumesikia katika nyanja za siasa kwamba fulani sio faia wa Tanzania. Hii ni mara nyingi kwa wale waliozaliwa nje ya Tanzania.

Na suala la kuthibitisha uraia linakuja kwa kuwa kuna nchi zinakupa uraia ukizaliwa kwenye hizo nchi, hata kama wazazi wako sio raia. Kimsingi, watoto wanaozaliwa nje ya Tanzania wapo ambao ni kama wana uraia pacha ikiwa nchi walikozaliwa iliwapa uraia kwa msingi wa kuzaliwa huko. Ndio maana wakifikisha miaka 18 Tanzania inataka wathibitishe uraia wao wa Tanzania au waende nchi walikozaliwa ambako wanaweza kutambuliwa kama raia. Unaweza usithibitishe uraia, lakini huenda siku moja ukakwama pale itakapoonekama una birth certificate ya nje na hukuthibitisha uraia wako wa Tanzania ulipofika miaka 18. Ndio utasikia fulani hana sifa za kugombea ubunge kwa kuwa sio Mtanzania ingawa wazazi wake wote unakuta ni Watanzania.

13. Nini tofauti ya ukazi wa kudumu (permanent residency) na uraia pacha?
Ukazi wa kudumu ni kwamba wewe unakuwa mkazi wa nchi fulani, na unaruhusiwa kufanya kila kitu kama vile tu raia isipokuwa baadhi ya vitu hasa kugombea nafasi za kisiasa, kupiga kura na nchi nyinge huruhusiwi kumiliki ardhi.

Huruhusiwi kujihusisha na siasa. Huhitaji visa kuingia hiyo nchi, na unaruhusiwa hata kufanya kazi bila kibali cha kazi (work permit) na hata kufanya kazi serikalini. Na ukazi wa kudumu unaweza kuupoteza ikiwa hutaishi katika nchi ya ukazi wako wa kudumu kwa kipindi cha muda fulani. Kwa hiyo ukazi wa kudumu huwezi kabisa kuulinganisha na uraia pacha. Uraia pacha unakupa uhuru zaidi na hauna kikomo wala masharti ya kuendelea kukaa katika nchi muda wote.

14. Vipi kwa walioukana uraia wa Tanzania na sasa ni raia wa nchi nyingine, wanaweza kupata uraia pacha?
Hili ni jambo gumu kidogo, na litahitaji ufikirio maalum wa kibinadamu (special consideration on humanitarian grounds) wa serikali. Uraia pacha si kwa ajili ya raia wa Tanzania ambaye aliukana uraia wa Tanzania na sasa anaishi nje ya Tanzania kama raia wa nchi nyingine. Ikiwa Mtanzania alishaukana uraia wa Tanzania na sasa anaishi nje ya Tanzania, kimisingi, ili aweze kuwa raia pacha inabidi aombe uraia wa Tanzania upya kama mtu mwingine tu ambae sio raia wa Tanzania. Huenda kwanza arudi Tanzania, na labda aishi kwa kibali (residence/permanent permit) nchini kwa muda usiopungua miaka mitano, na ndio ataomba tena kuwa raia wa Tanzania na kumfanya awe raia pacha - ikiwa nchi ambayo ni raia wake kwa sasa inamruhusu kuwa raia pacha, na Tanzania itakubali kumpa tena uraia. Sasa ndio maana nimesema serikali inaweza kutoa ufikirio, kwa sababu kimsingi huyu mtu ni mzaliwa wa Tanzania, na hivyo wakasema hawa watarudishiwa uraia wa Tanzania kwa msingi wa kuzaliwa Tanzania ili wawe raia pacha na nchi ambayo wana uraia kwa sasa.

Maswali mengine yanakaribishwa japo nahisi vipengele nilivyoweka vinajitosheleza
Eti utaratibu wa raia pacha, nani kauweka,si binadamu tuu,tena kwa interests hasi.Achaneni na kusombwa na ideas fake zenye nia ovu,be pragmatic,that is deal with things sensibly and realistically in a way that is based on practice rather than theoretical considerations.
 
Kwa miaka kibao uzoefu uko wazi watanzania walioko nje hawasaidii viwanda vya Tanzania kuuza bidhaa za Tanzania kwenye nchi zao Kama wahindi na waarabu .kikubwa Ni kuangalia faida ya diaspora kwenye uchumi mkubwa wa movement of goods kwenda soko kule aliko sio vihela vidovidogo vya remmittance vya pesa za rambi rambi na michango ya harusi

Wahindi na waarabu tunao miaka nenda Rudi lakini wanachofanya Ni kutuletea tu bidhaa zao .Sisi soko lao la bidhaa zao tu kwa asilimia kubwa.miaka nenda Rudi.Mchina kaja ndio kabisa katufanya gulio la bidhaa zake.Ukimpa uraia pacha ana kipi kikubwa Nchi.? Wahindi,waarabu,wachina etc hutoa uraia pacha wakijua what will happen kwa viwanda vyao na bidhaa zao.
Mkuu Yehodaya acha hizo. Watanzania wa diaspora watasaidia viwanda vya Tanzania kuuza bidhaa za Tanzania kwenye nchi zao kwa msingi gani, kwa framework gani hasa? Yaani bado uko kwenye mfumo wa uzalendo wa kuwa na viwanda vya serikali kwa hiyo kwa uzalendo watangaze bidhaa za serikali?

Yaani wewe leo uende USA, utazipigia debe bidhaa za juice za Azam kwa kuwa tu ni za Tanzania? Kwa gharama ya nani? Na kwa nini uwalaumu hao Watanzania badala ya kumlaumu Azam kuwa ameshindwa kutumia Diaspora ku-promote bidhaa katika nchi wanazoishi?

Kwani Azam akisema nataka Watanzania mlioko nje muwe ma-agent wangu wa Azam Juice, na awaandalie mazingira ya kuwa agents, nani atakataa fursa kama hiyo?

Na labda pia usisahau chema chajiuza kibaya chajitembeza. Bidhaa za Tanzania zikiwa na viwango bora kuliko hizo za huko wanakoishi Diaspora, zitauzika tu. Lakini Azam akitengeneza juice ambazo baada ya wiki mbili ya shelf life unakuta juice imegawanyika unga chini maji juu, nani atanunua hizo juice huko majuu?

Na usisahau suala la kuwa na competitive advantages. Tanzania tunaweza kuwa na juice bora za machungwa kuliko zilizoko USA, lakini unajua cost za kuzalisha na machungwa kati ya Tanzania na USA? Unaweza kukuta hadi uifikishe orange juice ya Azam USA, itabidi uuze dola 5 kwa kopo la 500ml, wakati juice za USA zinauzwa dola moja kwa kopo la ml 500.

Kwa hiyo mambo sio rahisi kama unavyofikiria, na tusiwalaumu Diaspora kwa mambo ambayo yako nje ya uwezo wao. Jambo rahisi ni Diaspora kuleta capital Tanzania ili kuinua kiwango cha maisha ya Watanzania kwa kutengeneza nafasi za kazi nk. Hata Diaspora kuleta tu fedha za kujengea nyumba ni jambo kubwa sana, na ujue Diaspora ambaye amechukua uraia wa nje anaweza kusita hata kujenga nyumba moja tu Tanzania, wakati ana uwezo wa kujenga nyumba hata kumi akazipangisha. Kwa hiyo tunapoongelea Diaspora kuleta capital Tanzania, usifikirie mambo makubwa sana. Ni katika economies of scale, kwamba kile kidogo kidogo wanacholeta, kwa sababu wako wengi, kinaishia kuwa kikubwa sana.
 
Ikiwa Watanzania wazawa tu tena mpaka wamepewa hatamu serikalini, Wanauza Taifa kwa vipande vya fedha, Itakuwaje kwa mzaliwa wa UK aliyepewa haki yavkuitumikia Tz sambamba na UK yake moyoni?

Sisi nje waliopo nje wengi wamejiendea wenyewe, lakini wageni wengi toka nje WAMETUMWA(hata tudhaniao kuwa ni watalii) Wanakuja with missions, sisi tunawaza njaa zetu binafsi.

Tujenge uwezo kwanza, Uwezo was Kutuma watu nje, sio Uhuru wa kila ajisikiaye kwenda sense tu.
Wewe umesoma sana hadithi za Musiba, vitabu vya Kufa na Kupona, nk. Kwa nini uwe na mawazo negative sana? Kwani nchi ngapi zinaruhusu dual citizeship, na hayo unayosema yameshafanyika katika nchi ngapi unazoweza kuzitolea mfano?

Kwani pia Tanzania tumelala kiasi hicho hadi watu wawe wanajifanyia hujuma wanavyotaka?

Na uraia pacha hauna maana tunatuma watu nje, hiyo ni wrong perception.
 
Eti utaratibu wa raia pacha, nani kauweka,si binadamu tuu,tena kwa interests hasi.Achaneni na kusombwa na ideas fake zenye nia ovu,be pragmatic,that is deal with things sensibly and realistically in a way that is based on practice rather than theoretical considerations.
Inabidi usikilkize ushauri wako mwenyewe - be pragmatic.
 
Kwani nchi ni mali ya nani mpaka muwaombe uraia? Kama makaburi ya babu na bibi zako yako hapa, babu na bibi zako waliishi hapa kabla hata ya nchi kupata uhuru, kwa nini unabembeleza serikali ikupe haki yako ya kuishi hapa kama mzawa?
 
Mkuu Yehodaya acha hizo. Watanzania wa diaspora watasaidia viwanda vya Tanzania kuuza bidhaa za Tanzania kwenye nchi zao kwa msingi gani, kwa framework gani hasa? Yaani bado uko kwenye mfumo wa uzalendo wa kuwa na viwanda vya serikali kwa hiyo kwa uzalendo watangaze bidhaa za serikali?

Yaani wewe leo uende USA, utazipigia debe bidhaa za juice za Azam kwa kuwa tu ni za Tanzania? Kwa gharama ya nani? Na kwa nini uwalaumu hao Watanzania badala ya kumlaumu Azam kuwa ameshindwa kutumia Diaspora ku-promote bidhaa katika nchi wanazoishi?

Kwani Azam akisema nataka Watanzania mlioko nje muwe ma-agent wangu wa Azam Juice, na awaandalie mazingira ya kuwa agents, nani atakataa fursa kama hiyo?

Na labda pia usisahau chema chajiuza kibaya chajitembeza. Bidhaa za Tanzania zikiwa na viwango bora kuliko hizo za huko wanakoishi Diaspora, zitauzika tu. Lakini Azam akitengeneza juice ambazo baada ya wiki mbili ya shelf life unakuta juice imegawanyika unga chini maji juu, nani atanunua hizo juice huko majuu?

Na usisahau suala la kuwa na competitive advantages. Tanzania tunaweza kuwa na juice bora za machungwa kuliko zilizoko USA, lakini unajua cost za kuzalisha na machungwa kati ya Tanzania na USA? Unaweza kukuta hadi uifikishe orange juice ya Azam USA, itabidi uuze dola 5 kwa kopo la 500ml, wakati juice za USA zinauzwa dola moja kwa kopo la ml 500.

Kwa hiyo mambo sio rahisi kama unavyofikiria, na tusiwalaumu Diaspora kwa mambo ambayo yako nje ya uwezo wao. Jambo rahisi ni Diaspora kuleta capital Tanzania ili kuinua kiwango cha maisha ya Watanzania kwa kutengeneza nafasi za kazi nk. Hata Diaspora kuleta tu fedha za kujengea nyumba ni jambo kubwa sana, na ujue Diaspora ambaye amechukua uraia wa nje anaweza kusita hata kujenga nyumba moja tu Tanzania, wakati ana uwezo wa kujenga nyumba hata kumi akazipangisha. Kwa hiyo tunapoongelea Diaspora kuleta capital Tanzania, usifikirie mambo makubwa sana. Ni katika economies of scale, kwamba kile kidogo kidogo wanacholeta, kwa sababu wako wengi, kinaishia kuwa kikubwa sana.
Umeongea vitu vingi sana ohhh Azam aandae mazingira atafute Diaspora wawe agent wake.Mmmmmmm

Wahindi , waarabu na wachina walioko Tanzania hatuna mtu Wala kampuni yeyote huwatongoza kuwa wawe agents wao wa Nchi walikotoka !!!!

Diaspora ya watanzania iliyo nje Ni hopeless na malofa wa kutupwa

Ohh yaandaliwe mazingira Wahindi,waarabu wamekuwa matajiri toka kipindi Cha ukoloni na kipindi Cha Nyerere cha ujamaa wa kikomunisti wakiwa importers was bidhaa toka Nchi zao

Ndio maana nasema kumpa uraia pacha mtanzania wa country of origin Tanzania Ni ujinnga tu ana Nini Cha maana wengi malofa tu hata wakifiwa huko nje hulia michango ya kusafirisha tuchange tulioko Tanzania pia
 
Hili swala la uraia pacha huwa linapotea na kurudi kama homa ya vipindi.....
kamwe hamtofanikiwa
 
Wewe umesoma sana hadithi za Musiba, vitabu vya Kufa na Kupona, nk. Kwa nini uwe na mawazo negative sana? Kwani nchi ngapi zinaruhusu dual citizeship, na hayo unayosema yameshafanyika katika nchi ngapi unazoweza kuzitolea mfano?

Kwani pia Tanzania tumelala kiasi hicho hadi watu wawe wanajifanyia hujuma wanavyotaka?

Na uraia pacha hauna maana tunatuma watu nje, hiyo ni wrong perception.
Una safari ndefu ya kujifunza. Katika Maisha mengi udhaniayo kuwa rahisi ndiyo yabebayo Uzito, na yale uyaonayo kuwa magumu ndiyo yajaayo Viini Macho.

Uraia pacha ni Fursa, hasa kwenye Ujasusi was Kiuchumi. Ukichagua kutokuona hayo, ni hiyari yako.
 
Naomba unifafanulie namba 10 na 14 kuna sehemu umesema kama utafanya uhalifu nchi uliopewa uraia wanaweza kukunyanganya uraia wao. Suali langu sasa hawa wanakurudisha nchi gani wakati ushaukana uTanzania wako?Ikiwa mzaliwa wa Tanzania wamfanyie update tu ya uraia pacha kwasababu Tanzania ni mama kwake na mama hamkatai mwana. Kwanini aombe tena uraia wa Tanzania? Uraia wa kuzaliwa na wa kuomba upi una nguvu zaidi? Mfano baba Mzaramu mama Mmakonde mtoto akienda umamani hutambulika mtoto wao lakini kabila yake ipo palepale ya kizaramu. Sasa kwanini mzawa wa Tanzania asiwe mtanzania wakati hakiharibu ulaya au America atarudishwa Tanzania tu.
 
Hili swala la uraia pacha huwa linapotea na kurudi kama homa ya vipindi.....
kamwe hamtofanikiwa
Diaspora huwa wanadhani wao huko waliko wana akili sana waliobaki Tanzania Ni wajinga wajinga .Wapeleke mswada bungeni ndio watajua walioko Tanzania akili zimo au la.Tunawaangalia tu .They think we are stupid.
 
Una safari ndefu ya kujifunza. Katika Maisha mengi udhaniayo kuwa rahisi ndiyo yabebayo Uzito, na yale uyaonayo kuwa magumu ndiyo yajaayo Viini Macho.

Uraia pacha ni Fursa, hasa kwenye Ujasusi was Kiuchumi. Ukichagua kutokuona hayo, ni hiyari yako.
Yaani wewe katika kufikiri kwako na conspiracy theory zako, katika ncho zoote Africa zinazoruhusu uraia pacha hilo hawajaliona ila wewe tu ndio una busara ya kuliona? Angalia ramani hapa chini hadi sasa ni nchi ngapi Afrika zimebaki madungaembe ya uraia pacha kwa kuwa zina mawazo kama unayosema. Yaani hawa wote ni wajinga wa kuuza nchi zao ila sisi ndio tunajua.

Unajua, siku ikitokea Watanzania wote wakapoteza pua zao na kutokuwa na pua, na wewe peke yako ndio ukabaki na pua, basi wewe ndio utakaekuwa mwenye ulemavu wa pua. Fikiria hilo kwa makini.

1628326004345.png
 
  • Thanks
Reactions: CES
Back
Top Bottom