Kwa ninavyowaona wageni wakipata uraia wa Tanzania hamna maajabu watafanya. Yani Mhindi umpe uraia wa Tanzania akiwa katoka India unadhani atafanya nini, ataleta mapikipiki yao auze achukue hela arudishe kwao India. Ukimleta Mfaransa hivo hivo atafanya. Hawa wataondoa nafasi za wabongo wanao-import bidhaa za nje, watakuwa export houses za makampuni ya kwao
Wabongo walioko nje ni wachache na wana hela kidogo tu za kupandia ndege. Ukiwaambia watoe mitaji walete uku haiwezi fidia hela inayochotwa kwenye mzunguko wetu kwenda nje. Kwa mtazamo wa kiuchumi
Umeeleza mengi ambayo sikuyafahamu. Asante
Ni Kwa nini jambo la uraia pacha huwa linahusishwa sana na kuleta hela Tanzania, uwekezaji na mengineyo? Hebu niambieni, tangu lini mama/Baba mzazi akamkana mtoto wake aliyepotelea ng'ambo kisa tu ana makaratasi mfukoni yenye nchi nyingine? Na huu uraia pacha kwa wageni, hivi utakuwa unagawiwa kama njugu? Mbona watawala wetu wakoloni wa uingereze, Ujerumani, Australia, Ireland , Kenya, Rwanda na nchi nyingine zote zinazoruhusu uraia pacha haziweki kigezo cha uwekezaji kama sharti kuu la uraia pacha? Mbona hizo nchi ziko poa tu hata uwe na makaratasi mia? Ni nini sisi kama nchi Tanzania tunaweza kujifunza katika nchi hizo zilizo tutangulia kuukubari uraia pacha kabla yetu au ni mawazo fiunyu tu, uvivu wa kufikria na ntima nyongo isiyo na wivu? Kama ni issue ya uzalendo, nafikiri wa-diaspora ni wazalendo number 1 kuliko hata hao wanaopoinga kulipa Kodi ya Miamala kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Mwisho, haki ya mtu kuishi, kukaa au kwenda mahali popote pale duniani, ni haki ya msingi- fundamental right ambayo haitakiwi kuchanganywa (Breach) na mambo mengineyo kama ya usalama na uwekezaji, ili hali tu- save for- kama hawavunji sheria za nchi husika , haina maana kuwanyima kwa sababu tu ya ntima nyongo na wivu usio wa maana.
Kama watakuwa waharifu, sheria nyinginezo za criminal law perocedures zitachukua mkondo wake ikiwemo jela kama wakipatikana na hatia.
Sheria nyinginezo hazilali , uraia pacha ni fundamental rights za wanadamu na dunia inaelekea huko kwa sasa ...Amkeni enyi mawazo Mgando, ndondocha na wakaidi wa haki za raia, mko fofofo sana na dunia inakimbia mwendo kasi sana kwa haya mambo. Amkeni na Amkeni sana , fofofo za uraia pacha zinadumaza maendeleo yetu kama nchi...