Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
- Thread starter
-
- #61
Umejibiwa vizuri. Kataa wenzio ndio tunaondoka hivyoEti utaratibu wa raia pacha, nani kauweka,si binadamu tuu,tena kwa interests hasi.Achaneni na kusombwa na ideas fake zenye nia ovu,be pragmatic,that is deal with things sensibly and realistically in a way that is based on practice rather than theoretical considerations.
Freedom is coming tomorrow!!!!!Hili swala la uraia pacha huwa linapotea na kurudi kama homa ya vipindi.....
kamwe hamtofanikiwa
Kwa hiyo Tanzania tukiruhusu uraia pacha, wageni wataruhisiwa kununua/kumiliki ardhi ya Tz freely?Leteni maswali wana JF, bado nasubiri. Au thread imekalimilika na kufumba watu midomo?
Freedom is coming tomorrow!!!!!!Sasa ndio hoja unazofikiri zinaweza shawishi wengi kuunga mkono Uraia Pacha? Kwamba kwa vile vipo tulivyocopy na hili nalo tubebe tu?
Hatutaki! Hoja zako ni dhaifu, Dunia ina maelfu ya Sera na Itikadi, Kwanini usihoji kuwa hatukuchukua zote? Na kwanini iwe Uraia Pacha tu?
Hatutaki! Bakini na mkiitacho Usasa. Endeleeni kupiga poyoyo za hapa na pale kwa wakati huu. Muda bado.
Uraia pacha ndio huo unakuja, mtabaki madungaembe mnahangaika eeh!Hili la uraia pacha hatulitaki. Lilishindwa wakati wa kikwete na litashindwa hata sasa. Hatuhitaji raia mamluki wenye kuweza kua wazalendo kwa nchi nyingie au kuweza kutumiwa na adui wa nchi au kuweza kuisaliti nchi au kuihujumu uchumi wake. Hao wanaokupa uraia nao wana malengo yao.
Hawawezi kuwa wageni tena, watakuwa ni raia wa Tanzania waliopewa uraia kwa kuzingatia vigezo na masharti. Na wakiwa raia ndio watakuwa na haki sawa kama raia wengine, japo nimesema kunaweza kuwa na exceptions katika suala la nafasi za kisiasa, ingawa ukifanya hivyo inakuwa unapingana na Katiba.Kwa hiyo Tanzania tukiruhusu uraia pacha, wageni wataruhisiwa kununua/kumiliki ardhi ya Tz freely?
Ni Kwa nini jambo la uraia pacha huwa linahusishwa sana na kuleta hela Tanzania, uwekezaji na mengineyo? Hebu niambieni, tangu lini mama/Baba mzazi akamkana mtoto wake aliyepotelea ng'ambo kisa tu ana makaratasi mfukoni yenye nchi nyingine? Na huu uraia pacha kwa wageni, hivi utakuwa unagawiwa kama njugu? Mbona watawala wetu wakoloni wa uingereze, Ujerumani, Australia, Ireland , Kenya, Rwanda na nchi nyingine zote zinazoruhusu uraia pacha haziweki kigezo cha uwekezaji kama sharti kuu la uraia pacha? Mbona hizo nchi ziko poa tu hata uwe na makaratasi mia? Ni nini sisi kama nchi Tanzania tunaweza kujifunza katika nchi hizo zilizo tutangulia kuukubari uraia pacha kabla yetu au ni mawazo fiunyu tu, uvivu wa kufikria na ntima nyongo isiyo na wivu? Kama ni issue ya uzalendo, nafikiri wa-diaspora ni wazalendo number 1 kuliko hata hao wanaopoinga kulipa Kodi ya Miamala kwa ajili ya maendeleo ya nchi.Kwa ninavyowaona wageni wakipata uraia wa Tanzania hamna maajabu watafanya. Yani Mhindi umpe uraia wa Tanzania akiwa katoka India unadhani atafanya nini, ataleta mapikipiki yao auze achukue hela arudishe kwao India. Ukimleta Mfaransa hivo hivo atafanya. Hawa wataondoa nafasi za wabongo wanao-import bidhaa za nje, watakuwa export houses za makampuni ya kwao
Wabongo walioko nje ni wachache na wana hela kidogo tu za kupandia ndege. Ukiwaambia watoe mitaji walete uku haiwezi fidia hela inayochotwa kwenye mzunguko wetu kwenda nje. Kwa mtazamo wa kiuchumi
Umeeleza mengi ambayo sikuyafahamu. Asante
Hawawezi kuwa wageni tena, watakuwa ni raia wa Tanzania waliopewa uraia kwa kuzingatia vigezo na masharti. Na wakiwa raia ndio watakuwa na haki sawa kama raia wengine, japo nimesema kunaweza kuwa na exceptions katika suala la nafasi za kisiasa, ingawa ukifanya hivyo inakuwa unapingana na Katiba
Hili la uraia pacha hatulitaki. Lilishindwa wakati wa kikwete na litashindwa hata sasa. Hatuhitaji raia mamluki wenye kuweza kua wazalendo kwa nchi nyingie au kuweza kutumiwa na adui wa nchi au kuweza kuisaliti nchi au kuihujumu uchumi wake. Hao wanaokupa uraia nao wana malengo yao.
Kingine hao diasprora wenyeywe kwa wenyewe hawapendani huko ughaibuni,hawana umoja kama wenzetu wa bara Asia.Mtz kumpa dili za pesa mtz mwenzake ni ngumu sanaUraia pacha kwa Tanzania naona Kama ujinga tu uraia pacha unawafaa wazungu,wahindi na waarabu na wachina kwa sababu wana faida kwenye zao kiuchumi na kibiashara wakiwa Nchi sio zao
Mfano mhindi wa Tanzania ndio importer mkubwa wa bidhaa za India kuleta Tanzania
Mwarabu pia ndie importer mkubwa wa bidhaa za Uarabuni Kama mafuta nk kuleta Tanzania
Mchina vivyo hivyo
Diaspora wa kwetu wa nini kikubwa wanacho import kwenye Nchi zao waliko watafute masoko huko?
Uraia pacha kwa watanzania hawana maana yeyote ninkujaza tu mipassport tu kwenye kabati
Diaspora wetu was kitanzania Ni choka mbaya
Mhindi,mwarabu na mchina diaspora yeye huwaza tu namna ya kuleta bidhaa toka nchini kwake kwenye country of origin kuuza aliko tofauti na midiaspora mitanzania .Ni kelele tu ohhh tunataka uraia pacha kwa kipi Cha maana walichonacho wanachosaidia Nchi?
Wenye mawazo yako ni wachache.Tanzania unakwepeka
Tukutane bungeni waambieni madalali wenu wa uraia pacha akiwemo huyo Mulamula Waziri wa Mambo ya nje Mwambieni anasubiriwa kwa hamu bungeni ndipo atajua miaka aliyokaa USA Haina maana kuwa anaijua TanzaniaUraia pacha ndio huo unakuja, mtabaki madungaembe mnahangaika eeh!
Mwelekeo mpya kwa uraia pacha
Balozi Mulamula alisema suala la diaspora kupiga kura linahitaji utaratibu na miundombinu, hasa kwa kutumia teknolojia kama zinavyofanya nchi nyingine zilizofanikiwa kwa kutumia mifumo ya kimtandao.www.mwananchi.co.tz
Hawa watu wanatoka vichakani huko wao wanapinga kila kitu Yani pamoja na elimu zinazotolewa especially kuhusu faida ya uraia pacha bado tu anaibuka anasema hataki uraia pacha, sasa muulize hata kuvuka mpaka wa nchi ya mguu tu pale tarakea au Namanga au Tunduma kama amewahi kuvuka tu ataanza maelezo mengi yasiyo na maana.Hulitaki wewe, na sisi tunalitaka. Kwa hiyo tufanyeje sasa?
Kama vyeti vyao vya kuzaliwa vinaonyesha wewe ndio baba, na wewe ni Mtanzania, basi haina tatizo, wao wanatambuliwa kuwa ni Watanzania hata kama wana passport za Mozambique kwa sasa. Unatakiwa kuwaombea passport za Tanzania ili uweze kuwaleta Tanzania na wataishi nawe bila Tatizo. Il a wakifika miaka 18 lazima wathibitishe uraia wao wa Tanzania na hiyo itabatilisha uraia wao wa Mozambique ambao huenda wanao.Binafs nina watoto wanne Mocambique, na wote wamezaliwa huko, na mama zao ni raia wahuko, inawezekana vipi kwa wao kuja kusoma Tanzania kama raia wa Tanzania?
Nb. Sijui sheria ya nchi yetu inasemaje, kwa mtu asie raia kupata haki ya kupata elimu kama raia wa kawaida.
Hivi wewe, kwa upeo wa akili yako, unafikiri wabunge wa CCM wanaweza kupinga muswada wa serikali? Unafikiri wamesahau kwa nini na kwa namna gani walifanywa kuwa wabunge?Tukutane bungeni waambieni madalali wenu wa uraia pacha akiwemo huyo Mulamula Waziri wa Mambo ya nje Mwambieni anasubiriwa kwa hamu bungeni ndipo atajua miaka aliyokaa USA Haina maana kuwa anaijua Tanzania
Mulamula peleka mswada Bungeni wa uraia pacha
Kwa hiyo hicho ndio kiwe kigezo cha kutoruhusu uraia pacha?Kingine hao diasprora wenyeywe kwa wenyewe hawapendani huko ughaibuni,hawana umoja kama wenzetu wa bara Asia.Mtz kumpa dili za pesa mtz mwenzake ni ngumu sana
Huo ni ubaguzi.Suala hili linapaswa kufikiriwa haswa kwakuwa umiliki wa ardhi unahitaji kuwa raia, hii imesaidia kutunza ardhi ya tanzania na kuifanya kuwa ya bei inayohimilika mpaka sasa, wakiruhusu tu uraia pacha watajaa raia wa nchi mbali mbali kwa njia ya upacha na kuhodhi ardhi ya tanzania.
Ikibidi kuruhusu basi iwe kwa watu wenye asili ya tanzania tu, yaani mtu mwenye mzazi mtanzania au kuzaliwa tanzania lasivyo wachina na wengineo kutoka watahodhi ardhi ambayo ni muhimu kwa vizazi vijavyo.
Hiyo ardhi ni benki ya akiba populaton inaongezeka wanakuwaq na eneo la kupanukia kuishio na kulimaHuo ni ubaguzi.
Watanzania mnang'ang;ania ardhi ambayo mnataka siku zote muione ikiwa mapori tu au mlime vishamba vya nusu eka na kuomba Mungu alete mvua kisha mnaishia kupata mazao afadhali hata ungenunua sokoni badala ya kupoteza nguvu na fadha kulima.