Usiruhusu mwanaume kuhamia kwenye nyumba yako uliyojenga kwa jasho lako

Usiruhusu mwanaume kuhamia kwenye nyumba yako uliyojenga kwa jasho lako

Kama wewe sio mario basi tulia waache wadada wachukue ushauri kwa faida yao.

Pilipili ya shamba haikuhusu hiyo
Hakuna Cha ushauri acha wivu
...wivu Ni kidonda ukishiriki utakonda.
Tena yawezekana kuna jiran yako anafaidi hapo kwako Sasa unataka kupasuka ukaona dawa kuja kuleta Hasira zako huku

Hayo Mambo ya watu hayatuhusu sisi'
 
Mimi sihitaji kujitambusha, Mwandiko pekee tu unanitambulisha. Sasa wewe unaandika kitu mpaka tunaulizia jinsia huoni kama una tatizo?
Na usipojitambulisha jinsia yako maana yake wewe ni bendera kufuata upepo [emoji3]
 
Acha utoto sasa kambi ya fisi

Nishakwambia njoo dm elewa basi .... wewe vipi? Kambi ya fisi hayaa mambo ya kikubwa sasa tunayoongea sasa hivi kuwa seriously
Gay wengi hukimbilia dm, if you're not a gay komaa hapa hapa utachumbiwa tu
 
Mwanamke Usiruhusu Mwanaume Kuhamia Nyumbani Kwako...

Ukiamua kuolewa usimruhusu ahamie kwako, hata kama unamiliki jumba la kifahari katika soko la juu halafu huyo jamaa anaishi katika nyumba ndogo ya kupanga, ni heri ujishushe daraja na utoke kwa jumba lako la kifahari na uhamie katika kijumba chake hicho muishi hapo hadi mnunue au mjenge nyumba yenu pamoja.

Kuna sababu tatu za kutomruhusu ahamie kwako …

1. Mwanamume anayehamia kwenye nyumba ya mwanamke hukimbia wajibu.

Kwa kawaida mwanaume anayejua wajibu wake huchukua hatua kabla ya kuoa.

Hutayarisha makao ya bibi-arusi wake kabla ya kumpata huyo bibi-arusi.

2. Ikiwa unaweza kumudu kumiliki nyumba halafu mwanaume unayeishi naye hawezi kumudu kumiliki nyumba basi yeye sio saizi yako.

Akihamia kwenye nyumba yako ipo siku mtaingia katika ligi ya kupigana juu ya nani anayedhibiti nyumba.

Hivyo achana naye mwache aende akapate mwanamke wa saizi yake.

3. Ikiwa mwanamume atahamia nyumbani kwako, matarajio yake makuu ni kulelewa na wewe, atakufanya uwe mtoaji wake kwa kila kitu. Muda si muda, hutamheshimu tena, yeye pia hata kupenda tena.

Katika dunia ya sasa wanawake hawawezi kujisalimisha kwa wanaume ambao hawatoi.

NB: ujumbe huu ni kwa wanawake wote ambao hawajaingia ktk ndoa, ila kwa wale waliopo ktk ndoa na wanaishi na hao wanaume majumbani kwao huu ujumbe hauwahusu, wakomae tu waume zao wazembe.
Kwetu, wanawake tunajengewa au tunapewa makazi kabla ya kuolewa.

Hatukubali kwenda kuishi kwa mume, mume ndiye anaeishi kwa mke na mume hamiliki samani yoyote ya ndani ya nyumba isipokuwa nguo zake. Bahati mbaya ikitokea kuachana ni mwanamme anaeondoka nyumbani.
 
Mwanamke Usiruhusu Mwanaume Kuhamia Nyumbani Kwako...

Ukiamua kuolewa usimruhusu ahamie kwako, hata kama unamiliki jumba la kifahari katika soko la juu halafu huyo jamaa anaishi katika nyumba ndogo ya kupanga, ni heri ujishushe daraja na utoke kwa jumba lako la kifahari na uhamie katika kijumba chake hicho muishi hapo hadi mnunue au mjenge nyumba yenu pamoja.

Kuna sababu tatu za kutomruhusu ahamie kwako …

1. Mwanamume anayehamia kwenye nyumba ya mwanamke hukimbia wajibu.

Kwa kawaida mwanaume anayejua wajibu wake huchukua hatua kabla ya kuoa.

Hutayarisha makao ya bibi-arusi wake kabla ya kumpata huyo bibi-arusi.

2. Ikiwa unaweza kumudu kumiliki nyumba halafu mwanaume unayeishi naye hawezi kumudu kumiliki nyumba basi yeye sio saizi yako.

Akihamia kwenye nyumba yako ipo siku mtaingia katika ligi ya kupigana juu ya nani anayedhibiti nyumba.

Hivyo achana naye mwache aende akapate mwanamke wa saizi yake.

3. Ikiwa mwanamume atahamia nyumbani kwako, matarajio yake makuu ni kulelewa na wewe, atakufanya uwe mtoaji wake kwa kila kitu. Muda si muda, hutamheshimu tena, yeye pia hata kupenda tena.

Katika dunia ya sasa wanawake hawawezi kujisalimisha kwa wanaume ambao hawatoi.

NB: ujumbe huu ni kwa wanawake wote ambao hawajaingia ktk ndoa, ila kwa wale waliopo ktk ndoa na wanaishi na hao wanaume majumbani kwao huu ujumbe hauwahusu, wakomae tu waume zao wazembe.

Ukiona mwanaume amehamia ujue tuu huyo sio mwanaume wa kiume. Ana hitilafu tayari
Mwanaume aliye sawa hufanyi hivyo
 
Wanawake wengine watakwambia
1. mie napenda mwanaume tuanze nae moja kutaftaeeee
2. mie sipendi mwanaume mwenye maendeleo sana ntanyanyasika
3. Mie napenda mwanaume msikivu na mwenye hofu ya mungu hata ka hana hela takula daga na hata lala njaa

mwanaume uwapo na nguvu tengeneza njia ya maisha yako ya baadaeee, kabla na baada ya kuwowa
 
Na kwanini umweleze kuwa una nyumba?[emoji1787][emoji1787][emoji1787]acha kiherehere ,we mwambie hapo umepanga,na Kodi ni kiasi kadhaa,mkubaliane kama mtamudu kuilipia pamoja,ikishindikana muhame hapo,mkapange nyumba mtakayoimudu kutokana na vipato vyenu,simple as that.
Maisha ya ndoa na udanganyifu ni maji na mafuta. Na kwa nini udanganye?

Mwanaume anayejielewa haswa ukishamwambia nyumba ni yako kwanza hatakubali kuja kuishi hapo(nasema anayejielewa).

Mume akija kugundua kuwa ulimdanganya hiyo ndoa itaingia doa kubwa. Usipende kudanganya hata kwa vitu visivyo na ulazima.
 
Siyo hivyo mkuu, nia ya uzi huu ni kuweka sawa uwajibikaji ktk ndoa, mwanamume akiwa kama kichwa lazima apambane kiume awe na nyumba au ashirikiane na mkewe wajinyime wapate hela ya Kujenga wakiwa ktk ndoa.

Kinachopingwa ktk huu uzi ni "mwanaume kuhamia kwenye nyumba ya mwanamke" hii haifai kabisa.
Basi na mwanamke kuhamia kwenye nyumba ya mwanamme hii haifai kabisa

Wanatakiwa wapamban wajenge hamsini kwa hamsini
Shieeet
 
Back
Top Bottom