King Jody
JF-Expert Member
- Oct 8, 2022
- 1,834
- 3,456
Habari za kutwa wana JF
Natambua hali ya maisha ni ngumu kwa ujumla, matapeli ni wengi mno, wengine wanajifanya wagonjwa ili tu wapate msaada, nk,
Lakini ukikutana na mtu hakuombi pesa ila anakwambia ana njaa anaomba umnunulie chakula na ukimwangalia kwa jicho la kawaida anamaanisha anachokisema, usisite kumsaidia, kama unahisi ni tapeli mpeleke kwenye mgahawa mnunulie chakula then uendelee na mambo yako, usimpe pesa mkononi.
Njaa mbaya sana ndugu zangu, siyo kila mtu ana kazi, siyo kila mtu anatafuta kazi akapata kirahisi, maisha ni fumbo, tenda wema nenda zako.
Wengine wamesoma wana ma degree lakini milango bado haijafunguka,kazi zenyewe wanapeana kwa kufahamiana, hawaangalii vigezo, ni mwendo wa kujuana, wanaita connection.
Watu wanapitia magumu yasiyoelezeka hadi wanafikia hatua ya kujinyonga kwa sababu hawaoni thamani yao katika ulimwengu huu.
Ikiwa Mwenyezi Mungu amekujalia unakula vizuri, unalala pazuri, unavaa vizuri wewe na familia yako, Mshukuru sana lakini usisite kuwasaidia wenye uhitaji
Kwa leo ni hayo tu nimeona ni vyema kushare na nyie.
ASANTENI SANA