Usisite kumsaidia mtu anayeomba umnunulie chakula

Wakati mwingi namuomba mwenyezi Mungu anijalie moyo wa kutoa, kutoa kuna furaha sana, kuna hisia fulani inakujiaga wakati tayari umesha toa, ila kabla kuna karoho kanaweka ugumu hivi ila ukifanikiwa ukashindwa unajawa na furaha sana.
Hii ni kweli kabisa, nadhani shetani huwa anahusika hapo
 
Naunga mkono hoja. Mimi mtu aniambie tu ana njaa nitamnunulia chakula au nitampikia.

Chakula na paa la nyumba ni kitu cha mwisho binadamu anatakiwa kukosa.

Sijawahi kukosa chakula so i don’t know how it feels, ila nikiumwa njaa muda mrefu naishiwa nguvu 😅
 
Good
 
Mchana jua la utosi wakati naenda matembezi,,napita njia fulani ya vumbi,nikaona mtoto kalala barabaran,nikamuita akaitika akasimama,nkamuulza maswali yangu mwisho akasema ana njaa,

Nkamwambia twende nkakununilie chakula kule ni mazingira ya mbali kidogo na maduka, mtoto akagoma kabisa eti anaogopa,basi nkaishia tu kumwambia aende nyumbani,nisingeweza kumlazimisha mwisho niitwe mtekaji

Ingawa kalionesha kutamani.
Kama ulijiridhisha kuwa ana njaa ungempa tu hela.. sometime unatoa tu usitake kujua mengine.. hiyo ni sadaka hata kama ataenda ku abuse au kudanganya, nia yako ndio muhimu. Utajisikiaje ukipita pale kesho ukakuta msiba ukaambiwa kuna mtoto amefariki kwa njaa? Na ndio huyo.
 
Umeongea jambo la msingi sana kuwakumbuka wenzetu wenye shida.
Mara nyingi binadamu huwa tuna tabia ya kusahau pindi tunapobarikiwa ila kusema ukweli kuna watu wanapitia maisha magumu.
Wewe fikiria mtu umeajiriwa mahali unalipwa mshahara kila mwezi na bado hesabu zinagoma muda mwingine mambo hayaendi sasa vuta picha kwa mtu ambaye hana kazi au biashara ya kueleweka ugumu wake wa maisha utakuwaje na anatakiwa ale kila siku na kila mwezi alipie kodi ya chumba.
 
ni mtoto mdogo,, ndomana nikamwambia aende nyumbani,,na siwezi mpea 5000 au 10000 yote bwan 😂 ndoman nilimtaka twende dukani.
 
Umeongea jambo la msingi sana kuwakumbuka wenzetu wenye shida.
Mara nyingi binadamu huwa tuna tabia ya kusahau pindi tunapobarikiwa ila kusema ukweli kuna watu wanapitia maisha magumu.
Wewe fikiria mtu umeajiriwa mahali unalipwa mshahara kila mwezi na bado hesabu zinagoma muda mwingine mambo hayaendi sasa vuta picha kwa mtu ambaye hana kazi au biashara ya kueleweka ugumu wake wa maisha utakuwaje na anatakiwa ale kila siku na kila mwezi alipie kodi ya chumba.
Ni hatari sana mkuu
 
Mchana jua la utosi wakati naenda matembezi,,napita njia fulani ya vumbi,nikaona mtoto kalala barabaran,nikamuita akaitika akasimama,nkamuulza maswali yangu mwisho akasema ana njaa,

Nkamwambia twende nkakununilie chakula kule ni mazingira ya mbali kidogo na maduka, mtoto akagoma kabisa eti anaogopa,basi nkaishia tu kumwambia aende nyumbani,nisingeweza kumlazimisha mwisho niitwe mtekaji

Ingawa kalionesha kutamani.
Exactly. Unatoa msaada lakini pia angalia na usalama wako. Mifano hai ipo kwa waliotoa misaada kwa hawa ombaomba wa barabarani kumbe kile kidogo unachompa ndo "kiunganishi" na pesa yako nyingine yote uliyonayo mfukoni kwa siku hiyo - unakuwa umeibiwa kimazingara. Wengine walitoa msaada wa kumwonesha mgeni njia kumbe wanapumbazwa (unageuzwa zombie) unakwenda kufanya kama wanavyotaka wao n.k. n.k.
 
ni kweli kabisa,, huruma mda mwingine huponza mambo mabaya,,ingawa hatuombei ila usalama muhimu,,ukiangalia na yanayoendelea sasa,, uuuuweeeeh nkaondoka
 
Sio kumpa tu chakula na tumwombee pia kwa Mungu maana hali wanazopitia ni ngumu.

Mungu tupe roho ya UTU kwa watu wenye uhitaji.
 
Back
Top Bottom