Usisite kumsaidia mtu anayeomba umnunulie chakula

Usisite kumsaidia mtu anayeomba umnunulie chakula

Habari za kutwa wana JF

Natambua hali ya maisha ni ngumu kwa ujumla, matapeli ni wengi mno, wengine wanajifanya wagonjwa ili tu wapate msaada, nk...

Ikiwa Mwenyezi Mungu amekujalia unakula vizuri, unalala pazuri, unavaa vizuri wewe na familia yako, Mshukuru sana lakini usisite kuwasaidia wenye uhitaji.
Hakuna Mungu anayejalia watu kula vizuri, kulala vizuri wala kuvaa vizuri.

Binadamu tupo responsible kwa matendo yetu yote tunayo yafanya.

Binadamu tungekuwa na hulka ya kusaidiana, kuinuana na ku maintain Amani ya dunia tungepunguza matatizo mengi sana hapa duniani.

Lakini muda mwingi tunatumia kuchukiana, Kutengana na kuvuruga amani ya dunia ndio maana dunia imekuwa sehemu ngumu sana kuishi.
 
Mafundi hatuna Mambo mengi.Twatenda hakika🤣🤣🤣🤣
Ahahaha assume ndo saidia fundi katoka kwenye pilika la zege kapata chochote kitu alafu anakutana na dhahama kama hyo...
Hapo ndo utajuaa kweli kuna majaribu duniani
 
Habari za kutwa wana JF

Natambua hali ya maisha ni ngumu kwa ujumla, matapeli ni wengi mno, wengine wanajifanya wagonjwa ili tu wapate msaada, nk...
yeah umeshauri kweli mkuu, na tusipende kuwaza tu utapeli, just sio lazima utoe pesa umpe, angalia mkahawa karibu enda nae mnunulie tu, asee me hua siwezi muacha mtu akiomba chakula ale , hata kama ni kidogo apunguze njaa nampele namnunulia cha kutosha cas inaumiza sana njaa, hadi anajidharirisha kuomba ujue ameshindwa hajui afanye nini
 
yeah umeshauri kweli mkuu, na tusipende kuwaza tu utapeli, just sio lazima utoe pesa umpe, angalia mkahawa karibu enda nae mnunulie tu, asee me hua siwezi muacha mtu akiomba chakula ale , hata kama ni kidogo apunguze njaa nampele namnunulia cha kutosha cas inauziza sana njaa, hadi anajidharirisha kuomba ujue ameshindwa hajui afanye nini
Kabisa mkuu, ogopa kitu kinaitwa njaa
 
Lakini pia usisite kumsaidia mtu anayeazima fedha
huyu it depends, sio kila anaeazima ana sababu ya kueleweka, mwingine anaazima akale bata kidimbwi, au akahonge tu michepuko, au akafanyie nonsense issues, so inadepend, na maelezo yanyooke
 
Habari za kutwa wana JF

Natambua hali ya maisha ni ngumu kwa ujumla, matapeli ni wengi mno, wengine wanajifanya wagonjwa ili tu wapate msaada, nk...
Uko sahihi kwa 100% Mkuu. Majuzi nilitoka kula Mdudu ( Kitimoto ) mahala hapa Kampala na wakati naondoka nikamuona Jamaa Mmoja ambaye amekuwa na Changamoto ya Akili sasa japo nimeambiwa alikuwa ni Mhubiri mzuri tu pale Mtaani. Nilimkuta kalala huku Watu wakimpita hata hawamjali. Nilichofanya ( nikikumbuka Maisha niliyoyapitia kabla ya Mwenyezi Mungu kunifungulia tena Milango ya Baraka ) nilienda kuuliza Mdada jirani aliyekuwa anauza Bidhaa zake kuwa je, naweza Kumnunulia Chakula na Maji kisha akiamka akampa?

Kwanza alinishukuru na kusema ni Moyo wa Ajabu na Mungu azidi Kunibariki na akasema atampa hivyo nikatoa Hela ya Sahani mbili za Wali Nyama na Mboga za Majani pamoja na Maji makubwa apewe akiamka. Nakumbuka mida ya Jioni nikiwa Kwangu nilipokea Ujumbe kutoka Ofisi ninayoifanyia Kazi huku kuwa sasa Posho yangu ya Mwezi imeongezwa kutoka ile ya mwanzo jambo ambalo nilisema Asante Mwenyezi Mungu na nikawa nakumbuka ile Hisani niliyoitoa kwa yule Mwanadamu Mwenzangu mwenye Changamoto ya Akili.

Ukiona unatoa sana ila hufanikiwi kwa Kufunguliwa na Baraka jua unatoa kwa kutaka Sifa au Umaarufu ila ukitoa kwa Moyo kwa Kuguswa kutoka Moyoni mwako unajibiwa hapo hapo na Baraka za Mwenyezi Mungu. Na hakuna Silaha nyingine inayonifanya Mola azidi Kunibariki kama ya kupenda kuwazawadia Watoto Zawadi na imenilipa mno na kamwe huwa siiachi kwani hakuna Watu ambao wana Baraka za moja kwa moja na wanapendwa na Mwenyezi Mungu kama Watoto tena ukiweza wale Wachanga kabisa wazawadie kupitia Baba au Mama zao au wale Watoto ambao wana Umri kati ya mwaka Mmoja hadi Sita au Saba.
 
Uko sahihi kwa 100% Mkuu. Majuzi nilitoka kula Mdudu ( Kitimoto ) mahala hapa Kampala na wakati naondoka nikamuona Jamaa Mmoja ambaye amekuwa na Changamoto ...
Shukrani sana mkuu, Mwenyezi Mungu akubariki sana
 
Wakati mwingi namuomba mwenyezi Mungu anijalie moyo wa kutoa, kutoa kuna furaha sana, kuna hisia fulani inakujiaga wakati tayari umesha toa, ila kabla kuna karoho kanaweka ugumu hivi ila ukifanikiwa ukashindwa unajawa na furaha sana.
 
Back
Top Bottom