Usisome kozi ya clinical medicine (clinical officer) kabla ya kusoma thread hii

nice thread
 
Mkuu huu uzi umekaa kukatisha tamaa sanaa
Hpn sio kukatisha watu tamaa huu uzi kuwajuza watu alaf wao wachague kupanga ni kuchagua . ...NAJUA WATU HAWAWEZI ACHA KUSOMA HIYO KOZI WATAENDELEA LKN MM NIMETAKA WAJUE WAELEWE WANAPOKUJA KUNA NINI ... Kila siku watu wanasema waliimu wa arts hawana ajira lkn watu bado wanasoma
 
ni kweli lakini kwa yule ambaye bado anampango wa kusoma hiyo kozi akisoma huu uzi anapoteza mwelekeo...inawezekana wewe ni miongoni mwa watu kwenye kada ya Afya so unawashauri nini wale waliosoma may be wakaishia ngazi ya cheti(CA) au diploma na ambaye mazingira hayaruhusu kuendelea na masomo
 
Nadhani hujamuelewa mtoa mada, nacte guidebook inaruhusu hizo D, sasa vyuo vya private viko vingi, na vingine ni cheap kwahiyo wanapata nafasi ya kusoma huko.
 
Nadhani hujamuelewa mtoa mada, nacte guidebook inaruhusu hizo D, sasa vyuo vya private viko vingi, na vingine ni cheap kwahiyo wanapata nafasi ya kusoma huko.
Vyuo vya private vinadahili vzuri tu ata ukiwa na D kwasababu vinadahili wanafunzi wengi sana
 
Ndio maana kipindi kile madaktari wa Kenya walivyogoma (sikumbuki mwaka) Magufuli akamwambia Uhuru atampa madaktari kutoka Tanzania, WaKenya wakachekaa kwa dharau wakasema kama kuna madaktari Tanzania basi ni Waganga wakienyeji. Basically, kusema kiwango cha elimu yetu kikochini sana. Very poor quality of education kwamba kwenye soko la ajira duniani hatuwezi kucompete na mfumo huu. Ni waambie tu, CCM hawatakaa waboreshe kiwango cha elimu Tanzania kwasababu wao ndio wanafaidika kwa kuwa na wananchi wasio na elimu bora. Ni rahisi sana kumtawala mtu asiye na elimu.
 
Maelezo mengi ila hujatoa maoni yako kwamba unashauri asome kozi gani ngazi ya diploma tofauti na hiyo?
 
Kufeli Nako kupo wanadahiliwa 100 wanahitimu 35/ pia Kuna vifo.Kila mtu na ridhika yake🤣🤣🤣🤣🤣🪑🪑🪑💺💺💺🎶🎶🎶📌
 
Kila kitu ulichosema ni kwel umepita mulemule...ushauri bora kusoma diploma ya dental, radiology au orthopaedic
 
Umeongea ukweli ila hizo program ulizoweka hauwezi kufananisha na clinical medicine
 
Kwenye sekta ya afya wamezingua sana


Maana qualifications ni ndogo mno


Yaani wanazidiwa hata na walimu
 
Mkuu quality ya D ya 2015 kushuka chini......ni tofauti na quality ya D hzi za miaka hii....miaka hii ya one za saba kama njugu ukipata D sawa na hamna kitu
Sahihi, japo hata D ya miaka ya 2010 ilikuwa tough ziaidi
Inshort serikali inaharibu sana mfumo wa elimu Kwa kuingiza siasa
 
Unavyosema bro kama vile hao wanafunzi 4100 wanahitimu kweli.
Katika wanafunzi wanaodahiliwa nusu ya wanafunzi hufeli kuendelea kimasomo kwasababu kuu mbili eidha ada ama kufeli.
Asikudanganye mtu kuwa eti kisa umeenda jiandikisha CMT basi shwaa miaka mitatu umemaliza.
Na hiyo kujiunga bachelor ya MD lazima ufikie GPA ya 3.5.
Usidhani ni rahisi mwaka wa tatu ufikishe GPA ya 3.5,wengi huishia 2.5-3.0.
Wanaofikisha 3.5 kwenda juu huwa wachache sana.
Ndio maana hata serikali sababu moja wapo iliofanya kozi ya CMT kutokuwepo kwenye orodha ya kozi za kupewa mikopo ya vyuo vya kati kwasababu wanafunzi wa CMT wanaongoza kufeli kuliko kozi yeyote ile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…