Usitafute pesa kwasababu ya mwanamke, iwe kwaajili maisha yako. Kilichomkuta huyu jamaa ni fundisho tosha!

Usitafute pesa kwasababu ya mwanamke, iwe kwaajili maisha yako. Kilichomkuta huyu jamaa ni fundisho tosha!

Peter alimpa fursa Lucy ya kuona upande mmoja tu wa Peter ambao ni ule wa fedha na huduma, akasahau mahitaji ya Lucy ya kihisia. Kwahiyo Lucy alijikuta akimfikiria Peter anafikiria upande wa huduma na fedha.

Boyfriend wa Chuo akaja kutatua tatizo la Peter la kihisia. Hisia ambazo ndo upande dhaifu zaidi wa mwanadamu haswa mwanamke. Kwa kawaida mwanamke ni mkweli sana haswa kwa vitendo linapokuja suala linalogusa hisia zao, hivyo kwa hapo walipofikia niseme tu Peter ameingia mtumbwi wa vibwengo.

Kumjali sana mwanamke ni kitu kizuri lakini ukivuka mipaka unakua huna jipya tena kwa mwanamke, na kawaida ya hawa wenzetu jinsia ya kike atahitaji zaidi pale utakapompa zaidi. Wanaridhika na vitu ambavyo hawana pekee.

Kuwajali sana ni kitu hatari mno, wanatakiwa wapewe hekaheka kidogo za kiakili ili wasikusahau, hawatakiwi kuona attention kutoka kwa mwanaume ni kitu rahisi sana kukipata, hawatakiwi kuwa na mwanaume anayetabirika, wanapenda kusumbuliwa akili. Na wanaume wengi wanaosumbua akili wanawake ndio wanaobakia kwenye kumbukumbu zao daima.

My take: Jali ila usipitilize.
Nadhani kila mwanamume amesikia✊
 
Back
Top Bottom