Usitake kumfunika boss wako, kilichomuondoa Makamba Wizara ya Mambo ya Nje

..uwezo hana anasingizia wasaidizi.

..tangu aingie ameteua na kutumbua Wakuu wa Usalama wanne.

..idadi sawa na wakuu wa usalama wakati wa Mwalimu Nyerere aliyeongoza miaka 24.
Magufuli alitumbua viongozi wangapi?, tena wakati mwingine kwa hisia zake tu zilizojaa unyonge.

Uwezo wake unaongea kwa vitendo wewe unayelalamika ukiwa shujaa wa nyuma ya keyboard huwezi ukaona wala ukathamini kinachofanyika.
 
imhotep ona siasa za kimaskini hapa. Ajabu na kweli hata wanakohimiza makamanda kukomaa, ni hivi hivi.

Bure kabisa!
Makamba ni mchafu tu na amejaa mawazo mabaya kwa serikali ya Samia. Wewe huwezi ukaona kwa sababu sio Rais na hujui malengo halisi aliyonayo moyoni mwake.
 
Mama nae ana wivu ameona makamba atamnyang'anya urais 2025 akaona amtulize kwanza na si ajabu akamtupa mbali kabisa hata akampa ubalozi wa Quba ili amtenganishe na siasa alimradi asipate UPINZANI wa urais 2025
Makamba analo tatizo la kujikweza na kutoheshimu mamlaka yanayokuwa juu yake.

Hulka yake ndio ile ambayo Polepole aliita siasa za kihuni, uhuni wenyewe ndio huo wa kuingilia kazi za watendaji wengine wa serikali.
 
Rais Nyusi alipoenda kumuaga Rais Hussein Mwinyi,ikulu Zanzibar.Walifika na kuondoka kwenye gari Moja pamoja na Januari.
Imekaaje hii kiitifaki?
Je ni kujikweza au Kawaida tu wanasave gharama za mafuta wakaamua kutembelea gari Moja!
Ana tabia ya kupandisha haiba yake akiwa mbele ya wakubwa, kumwandikia hotuba Mzee Kikwete awamu ya nne kulimdanganya akadhani anasubiri tu kuapishwa.
 
Makamba ni mchafu tu na amejaa mawazo mabaya kwa serikali ya Samia. Wewe huwezi ukaona kwa sababu sio Rais na hujui malengo halisi aliyonayo moyoni mwake.

Hakuna nilipomwongelea mtu ila nalipojikita ni kwenye hii dhana ya:

"Never to outshine your boss."

Boss kama hakusoma, hakusoma tu. Si aende shule kama anataka kutofunikwa?!

Au nasema uongo?

imhotep komaa kamanda.
 
Hakuna nilipomwongelea mtu ila nalipojikita ni kwenye hii dhana ya:

"Never to outshine your boss."

Boss kama hakusoma, hakusoma tu!

Au nasema uongo?

imhotep komaa kamanda.
Hakusoma lakini wasaidizi wake wote ni maprofesa na anaimalizia miradi yote aliyoirithi kutoka kwa hayati JPM.

Waliosoma sio ndio hao kina Mwigulu na Nape?. Akili matope ndio hizi sasa, zinababaika na elimu za madarasani.
 
Tulichogundua ni kuwa hamna hoja ya msingi katika kumtumbua January. Ni personalities na vita ya madaraka tu!

So endeleeni kuendesha nchi kwa personalities zenu. Siku TISS na Jeshi wakiwachoka na kuwalazimisha nchi ipate Katiba Mpya ndo mtaelewa kuwa mlikuwa wajinga!
 
Magufuli alitumbua viongozi wangapi?, tena wakati mwingine kwa hisia zake tu zilizojaa unyonge.

Uwezo wake unaongea kwa vitendo wewe unayelalamika ukiwa shujaa wa nyuma ya keyboard huwezi ukaona wala ukathamini kinachofanyika.

..hakuna Raisi wa Tanzania aliyeteua na kutumbua wakuu wa usalama wanne ktk awamu yake.

..kwa mwendo huu mpaka 2030 tutakuwa na wakuu wa usalama kumi na moja.

..ndio maana nasema mnalaumu watendaji wakati mnajua kiongozi Mkuu ndio hana uwezo.
 
Kwenye masuala ya uongozi kuna kanuni moja muhimu sana isemayo ' usitake kumfunika boss wako'.

Kwa kingereza wanasema 'never outshine your master', anayekuapisha daima ni mkubwa wako wa kazi hata kama nafsi yako inakuambia kwamba wewe unamzidi maarifa na kila kitu. Siku zote jifanye mjinga kwa mtu anayekupa mshahara na kukufanya ukaonekana na kuthaminika.

Hiyo kanuni imekuwa ngumu kwa Mheshimiwa January Makamba, ni mtu mwenye kujitutumua kila anapopata nafasi kiasi cha kusahau matendo yake yanaonekana vipi kwa wakubwa waliomuapisha pale ikulu.

Kuna lile suala la kutokuelewena kati ya mamlaka ya anga ya Tanzania TCAA na mamlaka ya Anga ya Kenya. Na mkurugenzi wa mamlaka ya Tanzania akawaandikia wale wa Kenya kuhusu umuhimu wa kufungua anga lao kwa biashara zetu kwa mujibu wa taratibu za anga za kimataifa.

Ni suala ambalo kwa namna yoyote ile barua iliyotoka upande wa Tanzania ilikuwa imetosha kuwakumbusha majirani juu ya kupunguza kiburi na dharau katika sekta zao, na kwa namna yoyote ile lisingeweza kuvuka siku tatu bila ya ufumbuzi kuwa umepatikana.

Na ilikwishatokea hivyo hivyo wakati wa awamu ya tano na mawaziri wa mambo ya nje wa Kenya na Tanzania wakaliachia limalizwe katika ngazi za wakurugenzi bila ya wao kulazimika kuingilia kati.

Safari hii katika awamu ya sita Mheshimiwa Makamba akaona ni sehemu ya 'kutokea', akaona ni nafasi ya kuchukulia ujiko kwa bosi wake. Akaamua kuingilia kati akimhusisha waziri wa mambo ya nje wa Kenya. Hakujua kwamba ameikera ofisi iliyomteua na kumwapisha kiasi cha mwenye ofisi kuwapigia simu wahusika akimshangaa waziri wa mambo ya nje kwa namna alivyoingilia suala lenye kutakiwa kumalizwa katika ngazi za chini.

Kingine kilichomkera SSH ni kuona kwamba hilo ni suala la wizara ya uchukuzi na mawasiliano na hapakuwa na haja ya wizara ya mambo ya nje kutumia nguvu kubwa kwenye utatuzi.

Tatizo la mheshimiwa ni kujiweka katika haiba ya urais akidhani anasubiri tu muda ufike aapishwe pale ikulu. Anaishi na tatizo hili akilini mwake na hajijui kuwa analo.

Wazungu wanasema ' never outshine your master'.
Hii inaitwa "KIMBELE MBELE"
 
Tatizo la mheshimiwa ni kujiweka katika haiba ya urais akidhani anasubiri tu muda ufike aapishwe pale ikulu. Anaishi na tatizo hili akilini mwake na hajijui kuwa analo.🪅
Lakini si kosa kuishi katika Imani hiyo, ila tu inakuwa kosa pale ambapo inashindwa kufuata utaratibu ama kutanguliza maslahi yako na ya nchi yanakuja baafaye
 
Hakusoma lakini wasaidizi wake wote ni maprofesa na anaimalizia miradi yote aliyoirithi kutoka kwa hayati JPM.

Waliosoma sio ndio hao kina Mwigulu na Nape?. Akili matope ndio hizi sasa, zinababaika na elimu za madarasani.

Akili matope zinaweza kuwa hizi zako za kutaka kulazimisha mambo.

Wapi nimemwongelea mtu ndugu?

GTGwRoUWIAkdhjh.jpeg

imhotep, kuna mkereketwa huku ikikupendeza mkumbushe hata kwetu tunahimizwa kukokamaa.

Ndiyo siasa za bongo hizo. Kusheheni wasomi si ndiyo akili yenyewe sasa?

Si ndiyo maana tunasema hii dhana ya kutomfunika bosi si ndiyo upumbafu wenyewe?

Lucas Mwashambwa kuna nduguyo wa kuelimishwa huku!
 
..hakuna Raisi wa Tanzania aliyeteua na kutumbua wakuu wa usalama wanne ktk awamu yake.

..kwa mwendo huu mpaka 2030 tutakuwa na wakuu wa usalama kumi na moja.

..ndio maana nasema mnalaumu watendaji wakati mnajua kiongozi Mkuu ndio hana uwezo.
Nchi inakwenda vizuri sana nyinyi manabii wa majanga mmeachiwa kazi ya kutabiri yasiyo mema. Hamuwezi kumsumbua Samia wala mfumo unaomlinda pale ikulu.
 
Akili matope zinaweza kuwa hizi zako za kutaka kulazimisha mambo.

Wapi nimemwongelea mtu ndugu?

View attachment 3050124

imhotep, kuna mkereketwa huku ikikupendeza mkumbushe hata kwetu tunahimizwa kukokamaa.

Ndiyo siasa za bongo hizo. Kusheheni wasomi si ndiyo akili yenyewe sasa?

Si ndiyo maana tunasema hii dhana ya kutomfunika bosi si ndiyo upumbafu wenyewe?

Lucas Mwashambwa kuna nduguyo wa kuelimishwa huku!
Pole sana mkuu, naona una maumivu fulani yanasumbua kichwa chako, jaribu panadol labda itakusaidia.
 
Kwenye masuala ya uongozi kuna kanuni moja muhimu sana isemayo ' usitake kumfunika boss wako'.

Kwa kingereza wanasema 'never outshine your master', anayekuapisha daima ni mkubwa wako wa kazi hata kama nafsi yako inakuambia kwamba wewe unamzidi maarifa na kila kitu. Siku zote jifanye mjinga kwa mtu anayekupa mshahara na kukufanya ukaonekana na kuthaminika.

Hiyo kanuni imekuwa ngumu kwa Mheshimiwa January Makamba, ni mtu mwenye kujitutumua kila anapopata nafasi kiasi cha kusahau matendo yake yanaonekana vipi kwa wakubwa waliomuapisha pale ikulu.

Kuna lile suala la kutokuelewena kati ya mamlaka ya anga ya Tanzania TCAA na mamlaka ya Anga ya Kenya. Na mkurugenzi wa mamlaka ya Tanzania akawaandikia wale wa Kenya kuhusu umuhimu wa kufungua anga lao kwa biashara zetu kwa mujibu wa taratibu za anga za kimataifa.

Ni suala ambalo kwa namna yoyote ile barua iliyotoka upande wa Tanzania ilikuwa imetosha kuwakumbusha majirani juu ya kupunguza kiburi na dharau katika sekta zao, na kwa namna yoyote ile lisingeweza kuvuka siku tatu bila ya ufumbuzi kuwa umepatikana.

Na ilikwishatokea hivyo hivyo wakati wa awamu ya tano na mawaziri wa mambo ya nje wa Kenya na Tanzania wakaliachia limalizwe katika ngazi za wakurugenzi bila ya wao kulazimika kuingilia kati.

Safari hii katika awamu ya sita Mheshimiwa Makamba akaona ni sehemu ya 'kutokea', akaona ni nafasi ya kuchukulia ujiko kwa bosi wake. Akaamua kuingilia kati akimhusisha waziri wa mambo ya nje wa Kenya. Hakujua kwamba ameikera ofisi iliyomteua na kumwapisha kiasi cha mwenye ofisi kuwapigia simu wahusika akimshangaa waziri wa mambo ya nje kwa namna alivyoingilia suala lenye kutakiwa kumalizwa katika ngazi za chini.

Kingine kilichomkera SSH ni kuona kwamba hilo ni suala la wizara ya uchukuzi na mawasiliano na hapakuwa na haja ya wizara ya mambo ya nje kutumia nguvu kubwa kwenye utatuzi.

Tatizo la mheshimiwa ni kujiweka katika haiba ya urais akidhani anasubiri tu muda ufike aapishwe pale ikulu. Anaishi na tatizo hili akilini mwake na hajijui kuwa analo.

Wazungu wanasema ' never outshine your master'.
Mkuu lile la nchi jirani lilikuwa la wote😂😂😂
 
Back
Top Bottom