Usiuze kwanza Subiri Mji Ukue hapo pakishachangamka patakulipa sana

Hata ukisubiri uuze mwaka 2070 bado thamani ya eneo hilo itabaki sawa na ile uliyouza mwaka 1990. Niamini mimi Thamani ya pesa inaenda na wakati.
Akili kubwa sana...

Inaitwa inflation.........

Hata ukisubiri uuze siku unakufa bei zitaendelea kwenda juu tu maana hela inazidi kupungua thamani.

Cha muhimu usiuze bila sababu ya msingi; na ukiuza hakikisha kiasi cha hiyo hela unaiwekeza mahali fulani ambapo itaendelea kukuletea hela zingine.

Economics 101
 
Jipe moyo hivyo hivyo
 
Tatizo,shidaa
 
Hata ukisubiri uuze mwaka 2070 bado thamani ya eneo hilo itabaki sawa na ile uliyouza mwaka 1990. Niamini mimi Thamani ya pesa inaenda na wakati.
Tuliosoma uchumi tu ndo tutakuelewa
 
kimfaacho mtu chake tusipangiane
 
We kama huna eneo umeuza yote Kwa njaa usijipe moyo ardhi ni Mali kadri miaka inavyoendea endelea kujiandikia porojo kama hizo humu
Nasubiri kuona kama una hoja mbali na innuendos tu. Ukitoa hoja iliyosimikwa katika misingi ya Economics nitakujibu ila kwa sasa comment yangu hii hapo chini inakutosha.

Endelea kutoa povu mpaka uwe dehydrated!

 
Ardhi inaoanda thamani ndio ila shida ni baada ya musa mrefu
 

"Lile eneo ni faida ya milele..."

HOW ???????? Kivipi.

Apartment na Zahanati na shule na fremu hujengi wewe! Nini kujenga, huna hata hela ya kula.

Sasa faida ya milele inakuja kivipi hapo ?

Kwamba kukodisha mtu ajenge ma hospitali na shule na ma fremu ?

Nani atakubali aweke ma bilioni na mabilioni ya infrastructure yake kwenye ardhi yako wewe kwa ku renti eneo ??? Enhee, lease ikiisha majengo anakuachia ?

Hiyo faida ya milele unaipataje kwenye shamba poriiiiiii ????

Mfano iliotoa wa sehemu iliyobadilika, pamejengwa ma infrastructure, jamaa anajuta,, nani kajenga ????????
 
Ardhi inaoanda thamani ndio ila shida ni baada ya musa mrefu
Ndio maana nikasema ipe muda kwanza thamani yake ipande unaweza hata usiuze ukampa mtu apaendeleze kisha akawa anakulipa ila ardhi ni yako na miradi ni yake yaan yeye anakodisha ardhi yako tu sio unamuuzia moja kwa moja, hio watu wengi wanafanya hawauzi wanakodisha kwa muda
 
Sio la Baba yangu mkuu mimi katika kitu napenda kuongea na wazee zaidi maana kuna nondo nazipata zaidi kuliko kuongea na vijana wa ovyo ovyo kwa hio ninaposema mzee haina maana ni baba yangu usinitoe nje ya reli
Hiyo ni tafsiri yako binafsi, mimi nimejibu kadiri ya ulivyoandika na kwa tafsiri yangu.
 
Inshort ardhi sio uwekezaji mzuri coz return yake inachukua mda mrefu ambapo kimahesabu unakuta inaingiza kiasi kidogo sana per months huo ni mtizamo wangu wakuu
 
Usiuze bila malengo wengi wanauza ila hawana malengo ya baadae na mara nyingi wanauza kwa bei ya hasara sababu ya shida na mahangaiko ila sio kwamba wanapenda kuuza ndio nawaambia usiuzee, kule shamba watu wana mashamba ila hata wapate shida kiasi gani hawauzi wanakodisha kwa muda tu anaweza akakukoshia hata mwaka mzima au miaka miwili wewe unalitumia tu ila baada ya miaka miwili shamba linabakia kua lake, hii ni akili kubwa kuzidi hio uliyonayo, kuna watu wanaongea na wenye maeneo mengi ya mjini mtu kalipenda eneo anamuomba mwenye eneo ajenge labda fremu za kufanyia biashara wanaingia makubariani wanasaini jamaa anajenga kwenye ardhi yako ila ardhi inabaki kua yako na anakulipa, akili kubwa zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…