Usiuze kwanza Subiri Mji Ukue hapo pakishachangamka patakulipa sana

SIki zote zali huwa ni kwa mwebye pesa tu!!masikini ni ngumu!!yaani uache kuuza eneo lako leo usubiri baada ya miaka kadhaa mbelee huku matatizo ndio kila leo yanakua andama!!Hiyo wanaweza wenyenpesa zao
 
hadi kuuza maana yake kuna sababu/changamoto flani sasa wewe unaleta ushauri wa usiuze kwanza iyo changamoto anaitatua vipi

alafu wewe unaye ona mbali badala ya kulia lia usiuze usiuze, nunua wewe hayo maeneo ili badae yakiwa potential unufaike wewe mwona mbali
 
Umepiga kwenye kidonda kibichi, huyu ni wale hawana kitu mfukoni ila washauri wakuu wa wenye hela. Anataman vya watu, anavionea huruma vikiuzwa na hana uwezo kuvipata
 
Inategemea Hilo eneo liko wapi...


Hilo eneo la 5000 Kwa miaka ya 1980 kama ni vijijini unaweza kulinunua Sasa hivi Kwa chini ya milion ila kama ni mjini hata milion 50 inafika na inategemea ni miji gani
Emu fafanua tena kidogo, mfano eneo lililokua linauzwa shillings 5000 mwaka 1980 leo bei yake ni hio hio Shs.5,000?
 
Pale Tegeta Kwa Ndevu si uswekeni tu pale nyumba zimepangana kama uko Islamabad!

Nilidhani unazungumzia viwanja vya mbezi Beach au Masaki.



kwa ardhi sikukatalii. mwaka 1996 tuliendaga pale tegeta kwa ndevu marehem babu alikataa eneo kubwa tukasema porini. leo je? ardhi mzee haina ubaya. si unaona walioshika beach plot kigambon wengine wameshakufa
 
Ushauri Mzuri ikiwa MTU hana sababu ya msingi ya kuuza Eneo , kiwanja anabidi asiuze Ila pia ikiwa ana sababu zake auze.


Babu yangu alikuwa na eneo very potential aliuza 8K Ila kwa sasa hilo eneo limgekuepo ndo lingewatoa katika umasikini .


Kuna mambo huwa nayaona kwa watu .

Kukosa maono
Ubinafsi
Kukosa kushaurika.
 
Acha ujinga mleta Mada

Anaweza kuuza eneo lake Kwa milion 500 Kisha akaenda Kununua Bonds za serikali za miaka 25 zenye riba ya 15% yaani Kwa mwaka atakuwa anapewa milion 75 na Kwa mwezi anapewa milion 6.


Na miaka 25 ikifika anarudishiwa milion 500 yake kama ilivyo.


Sio lazima anunua bonds za serikali ya Tanzania tu anaweza kwenda hata hapo Kenya akanunua.


Acheni kuishi Kwa kuiga wazazi wenu walivyoishi miaka ya 80 kumiliki maviwanja hovyo wakati Kuna namna unaweza kula maisha vizuri tu Hadi unakufa na unawaachia watoto mamilion.


Sasa mtu una miaka 60 unaogopa kuuza kiwanja cha milion 500 una akili kweli wewe ? Maeneo kibao ya investment yamejaa. Si utembelee hata BOT hapo uone Bonds za miaka 25 zinafanyaje kazi.


Ukinunua za miaka 25 maturity yake utakuwa na miaka 85 na unarudishiwa milion 500 yako.

Na ukinunua bonds za milion 500 una uwezo wa kukopa Bank Hadi mkopo wa asilimia 60.

Sasa fursa zote hizo unaziacha kwasababu tu unaweza kumiliki kiwanja Ili ujenge mafrem uanze kukimbiza na watu kuwadai Kodi hahahaha elimu elimu elimu.
 
Watu wanauza majumba New York, Paris , Monaco , London


Ndio ije kuwa huko kwenu uswekeni Nyumba ziko unplanned kama uko Islamabad au Benghazi - Libya.
 
Watu wanauza majumba New York, Paris , Monaco , London


Ndio ije kuwa huko kwenu uswekeni Nyumba ziko unplanned kama uko Islamabad au Benghazi - Libya.
Hatuuzi wewe nenda ukauze cha kwenu, future itakuheshimisha
 
Hela zangu zote nikampe bank?
 
Watu ukiwaambia hawaelewi mkuu hawa watu kuwaelewesha ni kazi sana inabidi ushike fimbo kabisa bila hivyo hawaelewi kabisa
 
Emu fafanua tena kidogo, mfano eneo lililokua linauzwa shillings 5000 mwaka 1980 leo bei yake ni hio hio Shs.5,000?
5000 ya mwaka 1980 yaweza thaminishwa na 5m ya leo au zaidi, kama iliwekeza na kuzaa bila kuitumia na faida yake .
 
Watu hawauzi kwa kupenda, muda mwingine shida zinawakabili.
 
Hizo sasa ni tamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…