Usiuze kwanza Subiri Mji Ukue hapo pakishachangamka patakulipa sana

Usiuze kwanza Subiri Mji Ukue hapo pakishachangamka patakulipa sana

Kama huna uwezo wa kuendeleza eneo fulani, wewe uza tu ili ukajenge maisha yako kwingine ukiwa na mtaji.
Imajini una eneo Kariakoo na hauna uwezo wa kujenga ghorofa la biashara halafu unapewa m 800, kwa nini usiuze na kujisogeza kule Gezaulole au Kibaha unapiga mjengo wa maana wa angalau 200m na zilizobaki unaenda kujenga simple apartment maeneo mengine ili kuendeleza mrija wa pesa ikizingatiwa kuwa pesa inategwa na si kutafutwa.
Haya ndio ninayoyaita malengo ila wengine hawana haya malengo mkuu, unakuta mtu mwingine yeye anataka auze atumie kwa matumizi mengine sio hayo uliyoyaeleza wewe na mbaya zaidi anauza kwa bei ya hasara sokoni kwamba amechelewa au anachelewa ngoja tu auze kumbe angejua angesubiri tu kwanza mambo yanabadirika na wakati unabadirika

Kuna sehemu fulani hua nikipita najifunza jambo ni good location and very potential area for doing good business, ngoja nikuelezee kidogo kuna mtu lile eneo ni kubwa sana alipolinunua nahisi lengo lilikua ajenge chuo hivi vyuo vya kawaida tu vya watu kujifunzia km college hivi ile biashara nahisi ikamtupa mkono haikwenda vizuri akaifunga akaona aanzishe eneo lilelile km kumbi ya sherehe watu wakiwa na sherehe zao wanakwenda pale anakodisha akaenda akaona eneo lile na ile biashara haimlipi vizuri km vile yeye anavyotaka, kumbuka eneo linazidi kuchangamka zaidi na watu wanazidi kuongezeka siku baada ya siku, washauri wakamweka chini wakamwambia hapa kwa jinsi palivyo fanya moja mbili tatu na utakachofanya kitakulipa zaidi na ndicho anachokifanya sasa na kila mtu akiangalia anasema sasa huyu huu ni wakati wake na amelenga kitu sahihi pale mwanzo alikua anatapatapa hajua apafanyie nini hapa angeingia mkenge wa kusema hapa hapaendelei na hapanipi faida ninayoitaka mapema angeshapauza kumbe ni haraka zake tu angesubiri km alivyofanya na kufuata ushauri mzuri kutoka kwa watu wenye ushauri mzuri km alivyofanya sasa anatengeneza kitu cha kumlipa miaka zaidi ya 100, hapo nahisi umenielewa namaanisha nini maana inabidi nikupe na mifano ili unielewe vizuri
 
Wakuu, katika kitu kuna Mzee wangu mmoja kila tukikaa anajutia ni kuuza eneo maeneo fulani ya Dar ambapo kipindi hicho palikua ni km Chaka la Simba tu. Enzi hizo kitambo sana akapaona sio kitu akauza akahama anakwambia leo hii akirudi kupaangalia pale alipouza anajuta ni mji pameshushwa ghorofa safi na zimepigwa apartment.

Another mistake, akanunua Shamba poli huko almost Ekari 10 au 15 kwa bei ya kawaida sana, pale aliponunua palikua Chaka tena yaan ni poli hakuna makazi ya watu wala nini kutoka nyumba mpaka kuifikia nyumba ni umbali sana huduma za kijamii hakuna barabara mbovu, akachoka akafanya mpango akauza sasa yule aliemuuzia eneo lilelile akafanya uwekezaji kwanza akajenga Zahanati, Kituo cha kufundishia Watoto yaan Nursery & Primary, kisha akajenga real estate yaan nyumba za kupangisha na fremu za kutosha za maduka, sasa hivi pamechangamka sio kawaida ukienda kupaangalia unajutia kupauza, hii pia anajuta laiti km angejua angesubiri kwanza pachangamke.

Kuna mwingine hapa amepanga kuuza nyumba kwa million zaidi ya 800, mimi naona mbali nimemwambia usiuze hilo eneo ni very potential hilo eneo ni zaidi ya hio pesa hio mwaka hauishi imeisha lile eneo ni faida ya milele, anafikiri atakufa kesho ooh watakaobakia watafaidi bora niuze tu nile hela zangu nijue moja hata nikifa hela zangu nimeshakula si nilijenga mwenyewe, mentality za kijinga sana pesa zikiisha akipita palepale alipouza akakuta aliemuuzia kashusha ghorofa la apartment kadhaa kaweka watu wanaishi anaanza kujilaumu ujinga kwanini aliuza kwanini hakusubiri.

Usiuze kwanza subiri mji uchangamke hapo hapo unapopadharau leo kesho patakulipa sana.
Kitu usichojua/ama umejitoa ufahamu,kwenye haya maisha hatuishi milele na Kila mtu ana "phase"yake ya kuenjoy maisha,.......mawaziri,mabalozi,wabunge wa enzi za Mkapa wengi ni wazee sana aam wameshatangulia mbele za haki,........hata kama walijenga masakinna Oysterbay,waliowaachia watauza tu Ili wagawane kwa minajiri ya urithi...........Sasa mtu kuuza chake akiwa hai kwa matumizi yake halali,unadhani ni makosa?
 
Kama wazee wote na wazaramo wote wangegoma kuuza ardhi zao hapa Dar es salaam, Je Dar es salaam ingekuwa na maendeleo na miundombinu iliyopo leo hii?

Je wazaramo wangeweza kujenga jiji la Dar es salaam liwe kama lilivyo leo?

Wazaramo wote wangeamua kutunza ardhi zao bila kuuza hata mita moja, Dar es salaam ya leo si ingekuwa kama Kigoma au Katavi.

Kama huwezi kujenga maghorofa, mahoteli, shule, hospitali kwenye hiyo ardhi yako, Sasa unaishikilia hiyo ardhi ya nini?

Wauzie wenye uwezo wa kujenga hayo maghorofa waendeleze mji. Maana wewe hata ukikaa na hiyo ardhi hadi mwaka 3000 huwezi kuleta mabadiliko yeyote zaidi ya kuishikilia tu.

Kwenye haya maisha kila mtu ana malengo na vipaumbele vyake.

Wewe unaweza kuona kipaumbele chako ni kutunza hiyo ardhi. Mwingine yeye wala hana hayo mawazo.

Acha watu wauze, maana hawana uwezo wa kujenga hayo maghorofa, mahoteli, shule, hospitali au viwanda.

Acha watu wauze, waponde mali kufa kwajaaaa!!

Sio kila mtu alizaliwa kuja kuwa tajiri.

Sio kila mtu alizaliwa kuja kufanya uwekezaji.
 
Mkuu kuna kitu bado hujanielewa ila ukiendelea kunisoma vizuri nadhani utaelewa nimelenga nini
 
Umeongea jambo jema sana ila mimi nilichokieleza ni future focus, ukisoma kwa umakini nilichokieleza nadhani utapata kunielewa ila ukisoma haraka haraka bila kua na subra ndio mawazo yako yanaishia hapo kua sio kila mtu amekuja duniani kua tajiri ila kaa chini jiulize je ni nani ambae hataki kua tajiri? Jibu utakalokuja nalo ni hakuna ambae hataki kua tajiri si ndio na ndio maana leo wewe ukiletewa pesa uuze kitu kitakachokunufaisha miaka 50 mbele wewe umeishia kufikiri miaka miwili mbele kwa hio utauza ili utumie miaka miwili mbele halafu basi bila kufikiri kwamba kuna miaka mingine mbele inafuatia ukiondoa hio miaka miwili unayoiona wewe, nilichomaanisha sio kwamba ukalie tu eneo na kuliangalia fanya jambo fanya jambo kwenye hilo eneo likuingizie kitu, kule shamba watu wanachukua maeneo wanalima wanapata mazao wanaingiza sokoni wanapata pesa miaka na miaka sio kwamba hizo pesa wanazopata zinakua za milele ila zinawasaidia kwa wakati but still bado wanakua wanamiliki eneo hawaliuzi sababu wamewekeza kwenye kilimo, huo ni mfano rahisi ukija huku mjini una eneo fikiria ufanye nini kwenye hilo eneo ambacho kitakuingizia faida sio kuacha tu eneo limekaa miaka nenda miaka rudi huna unachokifanya hizo sio akili, fanya kitu piganisha akili yako tafuta kitu cha kufanya usiwe na mawazo ya leo ndio mwisho kesho sitokuwepo tena nitakua nimeondoka ngoja nimalize nisiache chochote hizo sio akili na kuhusu suala la Wazaramo sio wote ambao wameuza maeneo yao wapo ambao wameyaendeleza maeneo yao na yanawalipa mpaka kesho, yupo Mzee mmoja namfahamu ni Mzaramo alikua mfanyakazi wa Bandari TPA yule Mzee ana eneo lake kubwa tu somewhere mwanzo kwa kuliangalia mtu yoyote hakufikiria km Mzee alikua na plan za baadae hakupauza pale leo hii kajenga real estate safi kabisa anakula vichwa kila mwisho wa Mwezi watu wanamlipa vizuri wanaishi na yeye anaishi angepauza na kusema hapa hakuna kitu hapanifai na kuhamia nje ya mji ingekuaje? Alisubiri wakati sahihi na wakati ukafika akafanya jambo
 
Umeongea jambo jema sana ila mimi nilichokieleza ni future focus, ukisoma kwa umakini nilichokieleza nadhani utapata kunielewa ila ukisoma haraka haraka bila kua na subra ndio mawazo yako yanaishia hapo kua sio kila mtu amekuja duniani kua tajiri ila kaa chini jiulize je ni nani ambae hataki kua tajiri?
Kuwa tajiri kila mtu anataka, lakini sio kila anayetaka kuwa tajiri ana uwezo wa kuwa tajiri.
Jibu utakalokuja nalo ni hakuna ambae hataki kua tajiri si ndio na ndio maana leo wewe ukiletewa pesa uuze kitu kitakachokunufaisha miaka 50 mbele wewe umeishia kufikiri miaka miwili mbele kwa hio utauza ili utumie miaka miwili mbele halafu basi bila kufikiri kwamba kuna miaka mingine mbele inafuatia ukiondoa hio miaka miwili unayoiona wewe, nilichomaanisha sio kwamba ukalie tu eneo na kuliangalia fanya jambo fanya jambo kwenye hilo eneo likuingizie kitu,
Kama huna uwezo wa kubadilisha hiyo ardhi ukajenga maghorofa, mahoteli, shule, hospitali, maduka n.k Hata ukae na hiyo ardhi kwa miaka 100 ni kazi bure kwako na haikusaidii chochote.

Afadhali uiuze uwaachie wenye uwezo wa kuiendeleza.

Waliokuja kujenga maghorofa kariakoo walikuja na mitaji mikubwa na walikuwa na uwezo, Sasa wazaramo wangegoma kuuza ardhi zao za kariakoo, Je wangeweza kuijenga kariakoo iwe kama ilivyo leo?

Wazaramo wangegoma kuuza ardhi zao hapa Dar, Je wangeweza kuijenga Dar es salaam iwe kama ilivyo leo?

Kuwa na ardhi na kuwa na uwezo wa kuitumia hiyo ardhi ni vitu viwili tofauti.

Si kila mtu mwenye ardhi ana uwezo wa kuiendeleza hata kama mji uwe unakua kiasi gani. Ndio maana bora wauze wawape wenye uwezo wa kuiendeleza.
kule shamba watu wanachukua maeneo wanalima wanapata mazao wanaingiza sokoni wanapata pesa miaka na miaka sio kwamba hizo pesa wanazopata zinakua za milele ila zinawasaidia kwa wakati but still bado wanakua wanamiliki eneo hawaliuzi sababu wamewekeza kwenye kilimo, huo ni mfano rahisi ukija huku mjini una eneo fikiria ufanye nini kwenye hilo eneo ambacho kitakuingizia faida sio kuacha tu eneo limekaa miaka nenda miaka rudi huna unachokifanya hizo sio akili, fanya kitu piganisha akili yako tafuta kitu cha kufanya usiwe na mawazo ya leo ndio mwisho kesho sitokuwepo tena nitakua nimeondoka ngoja nimalize nisiache chochote hizo sio akili na kuhusu suala la Wazaramo sio wote ambao wameuza maeneo yao wapo ambao wameyaendeleza maeneo yao na yanawalipa mpaka kesho, yupo Mzee mmoja namfahamu ni Mzaramo alikua mfanyakazi wa Bandari TPA yule Mzee ana eneo lake kubwa tu somewhere mwanzo kwa kuliangalia mtu yoyote hakufikiria km Mzee alikua na plan za baadae hakupauza pale leo hii kajenga real estate safi kabisa anakula vichwa kila mwisho wa Mwezi watu wanamlipa vizuri wanaishi na yeye anaishi angepauza na kusema hapa hakuna kitu hapanifai na kuhamia nje ya mji ingekuaje? Alisubiri wakati sahihi na wakati ukafika akafanya jambo
Kama watu wangekuwa hawauzi ardhi zao, Ungepataje makazi ya kuishi?

Wazaramo wote wangegoma kuuza ardhi zao hapa Dar, Je wewe ungeweza hata kupata kiwanja Dar es salaam?

Tuchukulie mfano, kila mtu agome kuuza ardhi yake, Sasa makazi na viwanja vya kujenga vingepatikana vipi?
 
nadhani hii ni stori tu ya kusadikika, mtu uwe na milioni mianane ufe masikini? inamana alikula zote bila hata kuwekeza chochote? kama wabunge wanapiga mil 300 tu na hata wasiporejea wameshatoboa maisha iweje huyo wa 800 awe masikini, is it real?
 
Haya ndio ninayoyaita malengo ila wengine hawana haya malengo mkuu, unakuta mtu mwingine yeye anataka auze atumie kwa matumizi mengine sio hayo uliyoyaeleza wewe na mbaya zaidi anauza kwa bei ya hasara sokoni kwamba amechelewa au anachelewa ngoja tu auze kumbe angejua angesubiri tu kwanza mambo yanabadirika na wakati unabadirika

Kuna sehemu fulani hua nikipita najifunza jambo ni good location and very potential area for doing good business, ngoja nikuelezee kidogo kuna mtu lile eneo ni kubwa sana alipolinunua nahisi lengo lilikua ajenge chuo hivi vyuo vya kawaida tu vya watu kujifunzia km college hivi ile biashara nahisi ikamtupa mkono haikwenda vizuri akaifunga akaona aanzishe eneo lilelile km kumbi ya sherehe watu wakiwa na sherehe zao wanakwenda pale anakodisha akaenda akaona eneo lile na ile biashara haimlipi vizuri km vile yeye anavyotaka, kumbuka eneo linazidi kuchangamka zaidi na watu wanazidi kuongezeka siku baada ya siku, washauri wakamweka chini wakamwambia hapa kwa jinsi palivyo fanya moja mbili tatu na utakachofanya kitakulipa zaidi na ndicho anachokifanya sasa na kila mtu akiangalia anasema sasa huyu huu ni wakati wake na amelenga kitu sahihi pale mwanzo alikua anatapatapa hajua apafanyie nini hapa angeingia mkenge wa kusema hapa hapaendelei na hapanipi faida ninayoitaka mapema angeshapauza kumbe ni haraka zake tu angesubiri km alivyofanya na kufuata ushauri mzuri kutoka kwa watu wenye ushauri mzuri km alivyofanya sasa anatengeneza kitu cha kumlipa miaka zaidi ya 100, hapo nahisi umenielewa namaanisha nini maana inabidi nikupe na mifano ili unielewe vizuri
Uwe na eneo na uwe na huo uwezo wa kutakeover hizo biashara.
Pia hakikisha watoto wako umewasomesha na wanapata kazi za kueleweka.
Bila hivyo watagawana au utalazimika kuuza ili familia iende
 
Na kukiendelea ndio unakuta wanauza maana alienunua kafika dau kubwa zaidi mfano wewe unasema hili eneo langu nitaliuza kwa million 200 anakuja mtu anakwambia anataka hio eneo kwa million 500 hapo ndipo watu wanapoachia maeneo na ndipo maeneo unapoona yanaendelezwa sababu mtu kauza kwa faida maradufu sio kwa hasara, kuna Mzee mmoja walimfuata hawa watu wanaojenga minara ya simu wakamtaka awauzie eneo lake wajenge Mnara Mzee akawagomea akawaambia anawapa eneo wajenge Mnara ila yeye anachotaka wamlipe mpaka pale watakapouondoa huo Mnara wakaingia makubariano wakasaini Mnara ukajengwa Mzee akaanza kulipwa, akili kubwa pesa aliyolipwa ni zaidi ya ile ambayo angelipwa kwa mkupuo kuwaachia watu wa Mnara wajenge Mnara wao
Ok mkuu
 
Mwingine aliuza eneo usawa wa Barabara eneo alilouza hakujua kua ni eneo very potential na alimuuzia alikua na akili mingi tajiri mmoja hivi tena kamuuzia kwa bei ya hasara kabisa bonge moja la eneo, baada ya kununua akajenga Kituo cha Mafuta unaambiwa kile kituo kimeanza kupiga kazi tangu miaka ya 90 mpaka leo jamaa anaendelea kula faida, waliouza wakipita pale wanajilaumu tu kwanini waliuza eneo very potential km lile

Kujilaumu huja mwishoni huku mwanzoni hakuna kujilaumu.
Wanajilaumu nini? kwani walikuwa na uwezo wa kujenga kituo cha mafuta? kama uwezo wanao bado maeneo potential ni mingi sana. Hela yako tu hata pale Posta unamhamisha mtu. Kama huna uwezo huna sababu ya kuziba ziba fursa za watu kupiga ma Bilioni. Unatakiwa kwenda shamba kama ngiri.
 
Wengi wanaouza maeneo yao ni kwa sababu ya shida ya pesa kwa wakati huo imagine mtu anahitaji msaada wa million 3 tu lakini hakuna wa kumpa hizo pesa so anachofikilia ni kuuza tu mali yake 🙏 ni sawa na mtu anamiliki simu ya laki mbili alafu anaomba msaada wa elfu 70 ili aweze kufungua biashara ya genge ✍️
 
Haya mambo kwa waafrika bora uuze tu...
Mzee aliacha viwanja maeneo potential kweli, sasa kila nikisema tusiuze...nageuziwa kibao kwa kuwa nimeajiriwa...basi nawaza bora mwenyewe angeuza tu
 
Unajifanya mshauri mzuri hadi unamuita Mjinga.....hilo eneo ni lako? Wewe tafuta ya kwako ndio upangie matumizi.

Hata akiliacha miaka 10 akija mtu kununua bilion moja. Si utamwambia aache kwanza huk mbele atauza bilioni 1.2?

Yeye pengine alijibana bana na kuhustle sana akapanunua milioni 20. Leo anauz mil 800 wewe unamuita Mjinga?
Watanzania Umaskini ni Mbata hadi tunaingilia mali za watu. We utakuwa mchawi ukizeeeka
Watu wanauza nyumba masaki ,obay
Nyumba zenyewe kama walipewa bure

Cha mtu chake.....bwana
Mambo ya potential sijui nini huyu mleta mada zake

Ova
 
Haya mambo kwa waafrika bora uuze tu...
Mzee aliacha viwanja maeneo potential kweli, sasa kila nikisema tusiuze...nageuziwa kibao kwa kuwa nimeajiriwa...basi nawaza bora mwenyewe angeuza tu
Uzeni kila mtu afe na chake tu

Ova
 
Mali ya urithi, unaambia tusiuze sjui potential 😄

Ova
 
Kama mimi nilivyodharau kununua hisa za CRDB mwaka jana miezi kama hii zilikuwa 510 na nilikuwa na 5Million mkononi, leo hisa ziko shilingi 1000 mara mbili yake
 
Wakuu, katika kitu kuna Mzee wangu mmoja kila tukikaa anajutia ni kuuza eneo maeneo fulani ya Dar ambapo kipindi hicho palikua ni km Chaka la Simba tu. Enzi hizo kitambo sana akapaona sio kitu akauza akahama anakwambia leo hii akirudi kupaangalia pale alipouza anajuta ni mji pameshushwa ghorofa safi na zimepigwa apartment.

Another mistake, akanunua Shamba poli huko almost Ekari 10 au 15 kwa bei ya kawaida sana, pale aliponunua palikua Chaka tena yaan ni poli hakuna makazi ya watu wala nini kutoka nyumba mpaka kuifikia nyumba ni umbali sana huduma za kijamii hakuna barabara mbovu, akachoka akafanya mpango akauza sasa yule aliemuuzia eneo lilelile akafanya uwekezaji kwanza akajenga Zahanati, Kituo cha kufundishia Watoto yaan Nursery & Primary, kisha akajenga real estate yaan nyumba za kupangisha na fremu za kutosha za maduka, sasa hivi pamechangamka sio kawaida ukienda kupaangalia unajutia kupauza, hii pia anajuta laiti km angejua angesubiri kwanza pachangamke.

Kuna mwingine hapa amepanga kuuza nyumba kwa million zaidi ya 800, mimi naona mbali nimemwambia usiuze hilo eneo ni very potential hilo eneo ni zaidi ya hio pesa hio mwaka hauishi imeisha lile eneo ni faida ya milele, anafikiri atakufa kesho ooh watakaobakia watafaidi bora niuze tu nile hela zangu nijue moja hata nikifa hela zangu nimeshakula si nilijenga mwenyewe, mentality za kijinga sana pesa zikiisha akipita palepale alipouza akakuta aliemuuzia kashusha ghorofa la apartment kadhaa kaweka watu wanaishi anaanza kujilaumu ujinga kwanini aliuza kwanini hakusubiri.

Usiuze kwanza subiri mji uchangamke hapo hapo unapopadharau leo kesho patakulipa sana.
Ila unatakiwa uvumilivu mkubwa sana sio rahisi
 
Watu wanauza nyumba masaki ,obay
Nyumba zenyewe kama walipewa bure

Cha mtu chake.....bwana
Mambo ya potential sijui nini huyu mleta mada zake

Ova
Yaani mleta mada kakasirika kabisa utadhani Mali zake.
 
Yaani mleta mada kakasirika kabisa utadhani Mali zake.
Mali ikishakuwa ya wengi basi kuna shida
Hapo kuna mmoja utakuta anajifanya mjuaji,yeye anafaidika zaidi kuliko wengine
Na hapo utakuta kuna wenzao wana watoto,wanaona ah nkingoka wanangu hawatoambulia kitu
Ndomana sahvi kuna upepo umepamba moto, kila mtu anakufa na chake 😄
Mambo ya potential hyo hawaielewi

Ova
 
Back
Top Bottom