Usiwape pesa watu wenye mikosi, utapoteza zaidi

Usiwape pesa watu wenye mikosi, utapoteza zaidi

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Hili jambo nimelifanyia utafiti wa kutosha.

Ni hivi: Kuna watu wamenajisiwa na majini, wachawi, mizimu au mapepo ili wasisitawi kwenye jambo lolote lile. Kielimu, kiuchumi, kisiasa na hata kijamii ukinajisiwa na wachawi huwezi kustawi. Utaishi kwa mateso mwanzo mpaka mwisho wa uhai.

Sasa watu wa namna hii usiwe mwepesi kuwapa msaada au kuwapa pesa. Kama kutakuwa na ulazima wa kuwasaidia basi hakikisha unaivunja ile nira yake isikuguse wewe. Hawa watu ukitaka kuwasomesha biashara yako inaweza kufa, kazi yako inaweza kuingia mchanga ili tu waendelee kuteseka.

Hata kwenye kuhonga kuwa makini, mwanamke mwingine ukimpa pesa yako tu lazima utapoteza zaidi.

Kuna watu ukiwasaidia ile wakigeuka tu unapata zaidi ila wengine ukiwasaidia ile wakigeuka tu subiri maumivu.
Cha msingi acha kutoa hovyo, hata walemavu si watu wa kuwapa hovyo. Wengine ulemavu wao ni laana za Mungu ili wateseke zaidi.

Amani ndani ya moyo wako ndio sauti ya Mungu inayompa mtu ruhusa ya kufanya au kutokufanya jambo.
 
Kuna muda mwingine unaweza kuta wewe ndio mwenye mikosi. Kuwa pale unapomsaidia mtu basi anaanguka zaidi na mikosi yako inashika hatamu kwako unaenda chini zaidi.

Linapokuja swala la kusaidia elewa lina Mungu ndani yake. Ukiona umefilisika sababu ya kusaidia basi elewa kulikuwa na walakini kwenye dhamira ya msaada wako au mali yako.
 
Ukweli mtupu huu

Hata wewe mwenyewe ukinajisika usiombe watu msaada ukawaingiza kwenye unajisi wako

Jisafishe uwalinde wote watakao kuwa na moyo wa kukusaidia
Huwa kuna sms inatumwa kuwa sasa umenajisika au unaetaka kumsaidia amenajisika?

Tusihalalishe uchoyo wetu kwa imani potofu.
Ukiwa na nia ya kusaidia wewe saidia tu, ukianza kuchunguza mikosi unaweza shindwa msadia hata baba yako mzazi kwa kigezo cha dhiki ya mtu ama mapitio yake.
 
Wewe kopa pesa kawagawie walemavu utabarikiwa zaidi. Si imeandikwa ukimpa maskini ni sawa umemkopesha Mungu
Usitoe sadaka kwa walemavu wanaojipanga road Hawa wengi wao pesa zao wanatumia kulewa na kununua wanawake sadaka itakayokubariki ni ile utakayotoa kanisani au kwenye taasisi ya kusaidia wenye mahitaji
 
Back
Top Bottom