Usiwape pesa watu wenye mikosi, utapoteza zaidi

Kuna mshikaji alikua mlemavu wa miguu mchana kutwa anaomba ila ana mademu kitaa anaonga balaa
Ahahahaha
Kuna mshikaji alijifanya bubu anaomba msaada aende kwao kaachwa na gari
Watu wakachanga na kumpa kibunda, jioni wakamkuta bar na totozi pande zote anaongea vizuri tu
 
Kuhusu Wana wake hii nikweli Kuna wanawake ukihonga kupata mchongo nibaada ya mwezi mzima lakini wengine Leo una mpa 50 kesho unapika laki kadhaa
 
Kama unasema ukweli vile
 
acha imani za kishirikina hiyo ni law of nature/God.. kama kuna waganga wanatiumia ni kwa sababu wanajua ni sheria za Mungu
Unaongea na mimi au unaongea na Mengi au mleta mada, wapi nimesema naamini ushirikina?!
 
Utoaji ni jambo takatifu sana na linapaswa kufanywa kwa utakatifu. Ni kweli hela yako ikiangukia mikononi mwa mshirikina na akaifanyia uchawi kama huna kinga ya kimungu utapoteza. Suluhisho ni kuwa vizuri kiroho na kuombea kila unachofanya na kuepuka dhambi.
 
Hakuna kitu kama hicho hata siku moja, ndio nyie mnaamini mtu wa kwanza kuonana nae asubuhi akiwa mwanamke eti siku mbaya. Illusilions zisizo na maana kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…