Usiyoyajua kuhusu nguvu za mnyama simba

Usiyoyajua kuhusu nguvu za mnyama simba

SIMBA si mnyama mrefu kuliko wote. SIMBA sio mnyama mwenye kilo nyingi kuliko wote.

SIMBA sio mnyama mwenye akili nyingi kuliko wote. Na pia SIMBA sio mnyama mkubwa kuliko wote.

Lakini cha kushangaza, SIMBA ndie mfalme wa Msituni.

Ikiwa sifa zote hizo hana je, ni kipi kinachomfanya SIMBA awe ndoo Mfalme wa Msituni kwa wanyama wote.

Kinachomtofautisha SIMBA na wanyama wengine ni MTAZAMO wake.

SIMBA sio mrefu kama TWIGA.. SIMBA hana kilo nyingi kama KIBOKO.. SIMBA hana akili nyingi kama FISI au NYANI.. SIMBA sio mkubwa kama TEMBO.

Lakini ndie mfalme wa Msituni. MTAZAMO wake Chanya alionao unamfanya awe kiongozi kwa wanyama wengine.

SIMBA anapomuona TEMBO haangalii umbo lake, haangalii ukubwa wake, haangalii unene wake, haangalii nguvu zake, na wala haangalii urefu wake.

SIMBA anapoona TEMBO anaona fursa ya chakula kwake . Anaona hiki ni chakula nachoweza kula. Na kwa sababu hii ya mtazamo wake Chanya SIMBA akimuonsTEMBO anamvamia kwa lengo la kupata chakula.

Hivi_unaamini_kuwa

TEMBO na ukubwa wote ule na unene wake wote ule anapomuona SIMBA, anaona mlaji huyo ananiijia.

kinachomfanya TEMBO amuone SIMBA mlaji, ni Kwa sababu ya MTAZAMO HASI alionao, unaopelekea SIMBA na udogo wake wote ule amle TEMBO.

Hapa ni MTAZAMO HASI pekee ndio unaomuangusha TEMBO!!!

MTAZAMO wako ukiwa unayaona kama chakula kwako lazima utaweza kuyashinda( Mtazamo Chanya). Lakini kama unayaona ni makubwa na huyawezi, basi hautayaweza lazima ya kushinde tuu kwa sababu umeamini Katika Mtazamo hasi au Mtazamo Mgando.

***Wewe jinsi ulivyo ni MTAZAMO wako. Mafanikio yetu kwenye kitu chochote kwa asilimia kubwa yanategemea MTAZAMO wetu. Sio elimu, akili, sehemu tunakotokea wala rangi zetu, MTAZAMO ndio unabeba sehemu kubwa ya maisha yatu tuliyonayo na tunayoishi!!.

*** Unaonaje shida unazozipitia? Unazionaje changamoto unazozipitia? Unayaonaje magumu unayopitia?
Je,Unaona ni chakula kwako(utaweza kushinda) au unaona ni mlaji huyo( utashindwa)? MTAZAMO wako uko wapi?

*** Haijalishi una elimu kiasi gani, haijalishi una nguvu kiasi gani, haijalishi una akili kiasi gani, kinachokufanya uwe kiongozi mzuri ni MTAZAMO wako yaani Mtazamo chanya( Mtazamo wa ukuaji)

*** Ikiwa utasema hauna akili nyingi, SIMBA hana akili nyingi kama NYANI lakini anatawala Msituni. Kama unasema wewe ni mfupi, SIMBA sio mnyama mrefu Msituni lakini ndie kiongozi..

Hauna sababu ya kwa nini usiwe kiongozi, Hauna sababu za kwanini usiwe mshindi Katika maisha haya unayoyaishi. Tafuta sababu yoyote unayotafuta, lakini hakuna sababu itakayokufanya usiwe kiongozi au mshindi.

*** Acha vijisibabu badili MTAZAMO wako, Jenga tabia ya mtazamo chanya, Mtazamo wa uwezekano, mtazamo wa ukuaji, mtazamo wa ushindi Katika maisha yako....

Mtazamo Hasi, mtazamo Mgando,mtazamo wa haiwezekani, mtazamo wa kushindwa ndio unaotupoteza wengi wetu na sio kitu kingine. Wewe ni mshindi na kiongozi, kama ukiamua kubadili MTAZAMO wako.

kama_hujui MUNGU ameweka Uungu ndani yako. Wewe ni Mungu mdogo Kama unabisha Soma

*** Wewe umeumbwa na uwezo mkubwa ndani yako. MTAZAMO wako ulionao ndio unaomfanya MUNGU afanye mambo makubwa kwako. MUNGU anaweza kufanya makubwa na mambo ya ajabu mno kama tu utatumia nguvu iliyomo ndani yako, kama tu utabadili MTAZAMO wako kutoka katika mtazamo wa haiwezekani na kuwa Mtazamo wa Inawezekana.

Ebu soma msitari huu aliouandika Paulo kwa Waefeso hata Kama Hauna mpango wa kwenda Mbinguni..

** MUNGU atafanya makubwa kwako kwa kadiri ya MTAZAMO wako. MUNGU anaweza kufanya makubwa kwako zaidi ya unavyoomba au kuwaza ikiwa utaishi kwa mtazamo wa Inawezekana nasio haiwezekani katika maisha yako...
( MUNGU hafanyi kazi na watu wenye mashaka)

Badili MTAZAMO wako. Yaone matatizo yako kama chakula kinachokuimarisha na kukufanya uonekane mwenye nguvu zaidi. MUNGU ameweka nguvu ya ushindi na uongozi ndani yako.

HAKUNA LISILOWEZEKANA KAMA UKIAMINI. KUNA UWEZO MKUBWA NA WA AJABU NDANI YAKO.
Kuna kijana mmoja ni muathirika wa mitazamo hasi, basi akawa anatumia nguvu zake zote kuniingiza kwenye hilo kundi la mitazamo ya kushindwa.
 
Lol motivational speakers huwa burudani sana.

Anyway, kwa elimu zaidi, nguvu kubwa ya simba ni teamwork. Ndio maana wanaishi kama jamii (pride), la sivyo hawatoboi. Hata wale machalii wanaofukuzwa na baba zao kwenye prides, lazima wajikusanye ku-survive. Hata wanapowinda, ile ni formation na kila mmoja ana majukumu yake.
Wenyewe wanasema simba ni "social animals" zaidi ya kuwa predator (muwindaji mlangwa nyama).
 
Motivesheno spika bana amka uteseke dunia haiko hivyo
 
Mbali na mtazamo wake, Simba anaheshimika kama mfalme wa nyika kutokana na tabia zao za asili.Simba huishi katika familia (Pride) na huishi kwa kutaka heshima katika eneo lake.Tabia hizi ni za ufalme.Ukijumlisha na manyoya mengi aliyonayo shingoni humpa simba muonekano wa dume la mbegu.Tiger ni mkubwa na mwenye nguvu kuliko simba.Lakini haheshimiki sana kama simba kutokana na lifestyle yake yeye haishi katika familia na wala hahangaiki kulinda territory. Tiger tunaweza kumuita Warrior kutokana na lifestyle yake lakini sio Mfalme!
 
simba akiona tembo anaona nini[emoji16][emoji16][emoji16].

na hili neno mfalme wa nyika kapewa na binaadam,nina uhakika hata yeye hajichukulii kama mfalme wala nini.

simba hawindi mnyama aliemzidi kimo kama nyati,tembo,falu,twiga,hao wote anavamia na wenzie kama wafanyavyo fisi nk.
simba ni mwoga sana ndio sababu huporwa windo na fisi kadhaa tu.

sifa zote anazopewa simba zilimfaa chui,maana haogopi mpuuzi yeyote na anajiamini hata mbele za watu kadhaa.
Hajapewa Jina la Mfalme ila aina tu ya maisha yake hata kama yeye hajui ila automatically anaishi kifalme. Chuo hana Pride wala territory. Mfalme gani asiye na territory
 
Simba ni King na sababu za kuwa King ni chache lakini zinashabiana na wafalme watu. Kwanza Simba akitoa sauti lake tu basi hata mtaa wapili wanajuwa mfalme anatawala, ana nguvu na anamiliki ardhi kubwa kuliko yote shujaa haogopi mnyama yoyote na ana muonekano wa kifalme good body. Fisi ni mpinzani wa Simba kwa maana wanagombania chakula kimoja na Simba lakini fisi angekuwa na muonekano mzuri angeweza kuwa anajina ila wao kumtoa Simba kwenye chakula lazima wawe wengi. Simba anaamua nyama gani ale na zaidi ni mnyama anapumzika zaidi ya masaa 15 kimyaa kama wafalme wetu. Chui muoga hasa akimuona Simba ndio maana akipata windo anakimbia juu ya mti. Fisi anasubiri King amaliza mnyama ndio wanakuja group kufanya fujo ni kama panya road tu fisi pora pora tu lakini mwizi wa maana anapiga hesabu mzigo mzito ndio King Simba.
 
Hajapewa Jina la Mfalme ila aina tu ya maisha yake hata kama yeye hajui ila automatically anaishi kifalme. Chuo hana Pride wala territory. Mfalme gani asiye na territory
mkuu wewe ndio hujui kitu chui ana territory ,pride aliyo nayo simba ni kwa simba wenzie sio wanyama wengine.

chui anaishi peke yake,na eneo husika akikatiza predator mwingine chui lazima apambane naye hakimbii.
 
Sasa Mfalme anaishi peke yake? Namkubali chui ila namkubali zaidi kama Warrior sio King.Mfalme lazima awe na pride na kingdom to protect na aheshimiwe na wenzake
 
Yeah mfalme wa popote pale akikukuta gladiator amekaa vibaya anamvua bila nyavu..

Huyo sio Mfalme sasa! Mfalme havui anasubiri aletewe mezani! Huyo labda tumwite Shujaa (Warrior) Lakini sio Mfalme! Mfalme anaishi maisha ya Kifalme! Analala muda wote ! Amezungukwa na malkia muda wote! Anapigana pale tu inapobidi
 
Hapo upo sahihi.
Simba dume hawindi..ni kulinda territory yake tu.
Japo ni mzuri sana kwenye kuwinda akiamua kuwinda hakosi.
 
SIMBA si mnyama mrefu kuliko wote. SIMBA sio mnyama mwenye kilo nyingi kuliko wote.

SIMBA sio mnyama mwenye akili nyingi kuliko wote. Na pia SIMBA sio mnyama mkubwa kuliko wote.

Lakini cha kushangaza, SIMBA ndie mfalme wa Msituni.

Ikiwa sifa zote hizo hana je, ni kipi kinachomfanya SIMBA awe ndoo Mfalme wa Msituni kwa wanyama wote.

Kinachomtofautisha SIMBA na wanyama wengine ni MTAZAMO wake.

SIMBA sio mrefu kama TWIGA.. SIMBA hana kilo nyingi kama KIBOKO.. SIMBA hana akili nyingi kama FISI au NYANI.. SIMBA sio mkubwa kama TEMBO.

Lakini ndie mfalme wa Msituni. MTAZAMO wake Chanya alionao unamfanya awe kiongozi kwa wanyama wengine.

SIMBA anapomuona TEMBO haangalii umbo lake, haangalii ukubwa wake, haangalii unene wake, haangalii nguvu zake, na wala haangalii urefu wake.

SIMBA anapoona TEMBO anaona fursa ya chakula kwake . Anaona hiki ni chakula nachoweza kula. Na kwa sababu hii ya mtazamo wake Chanya SIMBA akimuonsTEMBO anamvamia kwa lengo la kupata chakula.

Hivi_unaamini_kuwa

TEMBO na ukubwa wote ule na unene wake wote ule anapomuona SIMBA, anaona mlaji huyo ananiijia.

kinachomfanya TEMBO amuone SIMBA mlaji, ni Kwa sababu ya MTAZAMO HASI alionao, unaopelekea SIMBA na udogo wake wote ule amle TEMBO.

Hapa ni MTAZAMO HASI pekee ndio unaomuangusha TEMBO!!!

MTAZAMO wako ukiwa unayaona kama chakula kwako lazima utaweza kuyashinda( Mtazamo Chanya). Lakini kama unayaona ni makubwa na huyawezi, basi hautayaweza lazima ya kushinde tuu kwa sababu umeamini Katika Mtazamo hasi au Mtazamo Mgando.

***Wewe jinsi ulivyo ni MTAZAMO wako. Mafanikio yetu kwenye kitu chochote kwa asilimia kubwa yanategemea MTAZAMO wetu. Sio elimu, akili, sehemu tunakotokea wala rangi zetu, MTAZAMO ndio unabeba sehemu kubwa ya maisha yatu tuliyonayo na tunayoishi!!.

*** Unaonaje shida unazozipitia? Unazionaje changamoto unazozipitia? Unayaonaje magumu unayopitia?
Je,Unaona ni chakula kwako(utaweza kushinda) au unaona ni mlaji huyo( utashindwa)? MTAZAMO wako uko wapi?

*** Haijalishi una elimu kiasi gani, haijalishi una nguvu kiasi gani, haijalishi una akili kiasi gani, kinachokufanya uwe kiongozi mzuri ni MTAZAMO wako yaani Mtazamo chanya( Mtazamo wa ukuaji)

*** Ikiwa utasema hauna akili nyingi, SIMBA hana akili nyingi kama NYANI lakini anatawala Msituni. Kama unasema wewe ni mfupi, SIMBA sio mnyama mrefu Msituni lakini ndie kiongozi..

Hauna sababu ya kwa nini usiwe kiongozi, Hauna sababu za kwanini usiwe mshindi Katika maisha haya unayoyaishi. Tafuta sababu yoyote unayotafuta, lakini hakuna sababu itakayokufanya usiwe kiongozi au mshindi.

*** Acha vijisibabu badili MTAZAMO wako, Jenga tabia ya mtazamo chanya, Mtazamo wa uwezekano, mtazamo wa ukuaji, mtazamo wa ushindi Katika maisha yako....

Mtazamo Hasi, mtazamo Mgando,mtazamo wa haiwezekani, mtazamo wa kushindwa ndio unaotupoteza wengi wetu na sio kitu kingine. Wewe ni mshindi na kiongozi, kama ukiamua kubadili MTAZAMO wako.

kama_hujui MUNGU ameweka Uungu ndani yako. Wewe ni Mungu mdogo Kama unabisha Soma

*** Wewe umeumbwa na uwezo mkubwa ndani yako. MTAZAMO wako ulionao ndio unaomfanya MUNGU afanye mambo makubwa kwako. MUNGU anaweza kufanya makubwa na mambo ya ajabu mno kama tu utatumia nguvu iliyomo ndani yako, kama tu utabadili MTAZAMO wako kutoka katika mtazamo wa haiwezekani na kuwa Mtazamo wa Inawezekana.

Ebu soma msitari huu aliouandika Paulo kwa Waefeso hata Kama Hauna mpango wa kwenda Mbinguni..

** MUNGU atafanya makubwa kwako kwa kadiri ya MTAZAMO wako. MUNGU anaweza kufanya makubwa kwako zaidi ya unavyoomba au kuwaza ikiwa utaishi kwa mtazamo wa Inawezekana nasio haiwezekani katika maisha yako...
( MUNGU hafanyi kazi na watu wenye mashaka)

Badili MTAZAMO wako. Yaone matatizo yako kama chakula kinachokuimarisha na kukufanya uonekane mwenye nguvu zaidi. MUNGU ameweka nguvu ya ushindi na uongozi ndani yako.

HAKUNA LISILOWEZEKANA KAMA UKIAMINI. KUNA UWEZO MKUBWA NA WA AJABU NDANI YAKO.

Very wrong! Kinachombeba simba ni umoja nguvu na mwili wake ulivyo , Simba ni mnyama social sana, huishi kwa makundi na simba akibaki peke yake huwa anatafuta kundi au anakufa. Hakuna simba mmoja au wawili wanaweza muwinda tembo, sahau bali simba wengi ndo huwida tembo. Hii ndo tofauti iliyopo (ushirikiano) tofauti na wanyama wengine simba mmoja akishambuliwa huwa anapata msaada kwa wenzake. Simba hugawana majukumu hasa ya uwindaji wanajua muda mzuri wa kuwinda na muda mzuri wa kupumzika. Factor kubwa hapo ni social factor na ndo hii inambeba mwanadamu hata mbele ya hao simba, mwanadamu in large numbers and social corporation ameweza kuwa mfalme wa kila mnyama duniani.
 
mkuu wewe ndio hujui kitu chui ana territory ,pride aliyo nayo simba ni kwa simba wenzie sio wanyama wengine.

chui anaishi peke yake,na eneo husika akikatiza predator mwingine chui lazima apambane naye hakimbii.

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Chui hamna kitu mkuu, chui hana uwezo wa kupambana hata na fisi aliyeshiba . Chui ni mnyama mwenye aibu na muoga sana labda iwe vs wanyama wadogo kama mbwa au jackar . Chui dume aliyeshiba hafui dafu kwa simba jike ni anakimbia au kupanda mti .
 
Back
Top Bottom