Usiyoyajua kuhusu nguvu za mnyama simba

Usiyoyajua kuhusu nguvu za mnyama simba

SIMBA si mnyama mrefu kuliko wote. SIMBA sio mnyama mwenye kilo nyingi kuliko wote.

SIMBA sio mnyama mwenye akili nyingi kuliko wote. Na pia SIMBA sio mnyama mkubwa kuliko wote.

Lakini cha kushangaza, SIMBA ndie mfalme wa Msituni.

Ikiwa sifa zote hizo hana je, ni kipi kinachomfanya SIMBA awe ndoo Mfalme wa Msituni kwa wanyama wote.

Kinachomtofautisha SIMBA na wanyama wengine ni MTAZAMO wake.

SIMBA sio mrefu kama TWIGA.. SIMBA hana kilo nyingi kama KIBOKO.. SIMBA hana akili nyingi kama FISI au NYANI.. SIMBA sio mkubwa kama TEMBO.

Lakini ndie mfalme wa Msituni. MTAZAMO wake Chanya alionao unamfanya awe kiongozi kwa wanyama wengine.

SIMBA anapomuona TEMBO haangalii umbo lake, haangalii ukubwa wake, haangalii unene wake, haangalii nguvu zake, na wala haangalii urefu wake.

SIMBA anapoona TEMBO anaona fursa ya chakula kwake . Anaona hiki ni chakula nachoweza kula. Na kwa sababu hii ya mtazamo wake Chanya SIMBA akimuonsTEMBO anamvamia kwa lengo la kupata chakula.

Hivi_unaamini_kuwa

TEMBO na ukubwa wote ule na unene wake wote ule anapomuona SIMBA, anaona mlaji huyo ananiijia.

kinachomfanya TEMBO amuone SIMBA mlaji, ni Kwa sababu ya MTAZAMO HASI alionao, unaopelekea SIMBA na udogo wake wote ule amle TEMBO.

Hapa ni MTAZAMO HASI pekee ndio unaomuangusha TEMBO!!!

MTAZAMO wako ukiwa unayaona kama chakula kwako lazima utaweza kuyashinda( Mtazamo Chanya). Lakini kama unayaona ni makubwa na huyawezi, basi hautayaweza lazima ya kushinde tuu kwa sababu umeamini Katika Mtazamo hasi au Mtazamo Mgando.

***Wewe jinsi ulivyo ni MTAZAMO wako. Mafanikio yetu kwenye kitu chochote kwa asilimia kubwa yanategemea MTAZAMO wetu. Sio elimu, akili, sehemu tunakotokea wala rangi zetu, MTAZAMO ndio unabeba sehemu kubwa ya maisha yatu tuliyonayo na tunayoishi!!.

*** Unaonaje shida unazozipitia? Unazionaje changamoto unazozipitia? Unayaonaje magumu unayopitia?
Je,Unaona ni chakula kwako(utaweza kushinda) au unaona ni mlaji huyo( utashindwa)? MTAZAMO wako uko wapi?

*** Haijalishi una elimu kiasi gani, haijalishi una nguvu kiasi gani, haijalishi una akili kiasi gani, kinachokufanya uwe kiongozi mzuri ni MTAZAMO wako yaani Mtazamo chanya( Mtazamo wa ukuaji)

*** Ikiwa utasema hauna akili nyingi, SIMBA hana akili nyingi kama NYANI lakini anatawala Msituni. Kama unasema wewe ni mfupi, SIMBA sio mnyama mrefu Msituni lakini ndie kiongozi..

Hauna sababu ya kwa nini usiwe kiongozi, Hauna sababu za kwanini usiwe mshindi Katika maisha haya unayoyaishi. Tafuta sababu yoyote unayotafuta, lakini hakuna sababu itakayokufanya usiwe kiongozi au mshindi.

*** Acha vijisibabu badili MTAZAMO wako, Jenga tabia ya mtazamo chanya, Mtazamo wa uwezekano, mtazamo wa ukuaji, mtazamo wa ushindi Katika maisha yako....

Mtazamo Hasi, mtazamo Mgando,mtazamo wa haiwezekani, mtazamo wa kushindwa ndio unaotupoteza wengi wetu na sio kitu kingine. Wewe ni mshindi na kiongozi, kama ukiamua kubadili MTAZAMO wako.


kama_hujui MUNGU ameweka Uungu ndani yako. Wewe ni Mungu mdogo Kama unabisha Soma

*** Wewe umeumbwa na uwezo mkubwa ndani yako. MTAZAMO wako ulionao ndio unaomfanya MUNGU afanye mambo makubwa kwako. MUNGU anaweza kufanya makubwa na mambo ya ajabu mno kama tu utatumia nguvu iliyomo ndani yako, kama tu utabadili MTAZAMO wako kutoka katika mtazamo wa haiwezekani na kuwa Mtazamo wa Inawezekana.

Ebu soma msitari huu aliouandika Paulo kwa Waefeso hata Kama Hauna mpango wa kwenda Mbinguni..

** MUNGU atafanya makubwa kwako kwa kadiri ya MTAZAMO wako. MUNGU anaweza kufanya makubwa kwako zaidi ya unavyoomba au kuwaza ikiwa utaishi kwa mtazamo wa Inawezekana nasio haiwezekani katika maisha yako...
( MUNGU hafanyi kazi na watu wenye mashaka)

Badili MTAZAMO wako. Yaone matatizo yako kama chakula kinachokuimarisha na kukufanya uonekane mwenye nguvu zaidi. MUNGU ameweka nguvu ya ushindi na uongozi ndani yako.

HAKUNA LISILOWEZEKANA KAMA UKIAMINI. KUNA UWEZO MKUBWA NA WA AJABU NDANI YAKO.
Chukua supu ya mbuzi uiweke kwenye gazeti...
 
Anaitwa honey badger..Yule ndy kiboko Yao sasa[emoji28]

Ukisikia deadliest animal ndy Yule,hakuna kiumbe yoyote anayemwogopa hata huyo Simba anamwona km kirikuu Tu..namkubali sn Yule mdudu..ni bad ass animal

Yote Kwa yote andiko ni zuri sn na linatia moyo Kwa waliokata tamaa

View attachment 2231426
Huyu mdudu anakula mpaka nyoka tena kwa kumtafuna mithili ya Binadamu akitafuna miwa.
 
simba akiona tembo anaona nini[emoji16][emoji16][emoji16].

na hili neno mfalme wa nyika kapewa na binaadam,nina uhakika hata yeye hajichukulii kama mfalme wala nini.

simba hawindi mnyama aliemzidi kimo kama nyati,tembo,falu,twiga,hao wote anavamia na wenzie kama wafanyavyo fisi nk.
simba ni mwoga sana ndio sababu huporwa windo na fisi kadhaa tu.

sifa zote anazopewa simba zilimfaa chui,maana haogopi mpuuzi yeyote na anajiamini hata mbele za watu kadhaa.
Simba sio mwoga aisee, katika Cats Simba na Tiger ni majasiri sana

Simba ananyang'anywa chakula na fisi kwasababu fisi anakuwa kero, anamsumbua simba akila

Chui na Cheater wanaweza kumwogopa fisi lakini simba hapana aisee.

Simba ni mnyama jasiri na mpambanaji sanaa ingawa ana mwili mdogo
 
Mfalme halisi wa pori ni chui.
Huyu mwamba hata simba akikaa vibaya analiwa
Yupo sharp, mkali na anapanda miti lakini sio jasiri na hajiamini hata kama Simba jike

Chui hawezi kumuattack simba ila simba anamuattack Chui

Na Chui ni mwepesi na ana spidi sana ya uwindaji
 
Yeah mfalme wa popote pale akikukuta gladiator amekaa vibaya anamvua bila nyavu..

Huyo ni Jaguar sio Chui, Jaguar anaishi kwenye misitu minene sio kwenye savanna au tambarare

Huyo Jaguar ni paka mkali sana kuliko hata hawa Chui waliopo kwny mbuga zetu
 
Ni mkatili mmoja huyo
Hakuna tofauti hapo
 
Huyo ni Jaguar sio Chui, Jaguar anaishi kwenye misitu minene sio kwenye savanna au tambarare

Huyo Jaguar ni paka mkali sana kuliko hata hawa Chui waliopo kwny mbuga zetu
Huyu paka anamla simba vizuri tu akijichanganua
 
Mfalme halisi wa pori ni chui.
Huyu mwamba hata simba akikaa vibaya analiwa
Chui 'anapapaswa' hata na mbwa mwitu!
Screenshot_20220521-090554_Google.jpg
Screenshot_20220521-090419_Google.jpg
 
Back
Top Bottom