Usiyoyajua Kuhusu Samia UN: Kumbe alitaka kuhutubia Kiswahili! Baada ya Kiswahili kuwa Lugha ya Afrika, Rais Samia kukipaisha kuwa Lugha ya Dunia

Usiyoyajua Kuhusu Samia UN: Kumbe alitaka kuhutubia Kiswahili! Baada ya Kiswahili kuwa Lugha ya Afrika, Rais Samia kukipaisha kuwa Lugha ya Dunia

Paskali nikujibu hivi mama kapotoka sababu alizotoa ni za ajabu,eti alikosa mkalimani,hii ni aibu sana,wangekuchukua hata wewe tu,kuhusu john kukacha trip za majuu kuna mawili.

Betri kwenye moyo na lugha, kule UN unaweza kustukizwa tu kuwa rais wa USA anataka kuongea na wewe angeongea nini sasa
 
Pasikali.... kanyagia hapo hapoooo. nani anamteua mtu asiyefanana naye? asiyenia naye mamoja? wacha wakusakame watakuwa wa kwanza kukupa hongera by the way nimefurahia ripoti yako maana nimeelewa na kujifunza kitu.
 
Unapokuwa na msimamo chanya na UN ni bora ujitoe, ukiwa memba wa JF kisha unamsimamo chanya na JF ni bora ujitoe. UN si mali ya marekani ni mali ya nchi wanachama, unapoisusa huku ukiwa mwanachama maana yake nini! Jitoe.
Umeelewa hata nilichokiandika kweli?

Nimeongelea mtu kuwa na msimamo kwenye jambo lolote. Nani ameongelea UN na JPM?

Alikua natuma wawakilishi huko kwenye vikao vya UNGA, alitoa hotuba ya kiswahili AU na EA...nilichoshangaa ni mtu kusifiwa kwa nia ya kutaka kuongea kiswahili wakati alikua ana nafasi ya kuongea kiswahili.
 
Ukwli Hawezi kupaisha Lugha ya kiswahili, huu ni ujanja ujanja wa kutaka teuzi.

Mzembe aliyesahau kuwa na mkalimani huyo ndo anatka kukipaisha kiswahili?

Hahahahaha tuache sifa za kinafiki wana JF ni dhambi kusma uongo.
 
Mi nilidhan amehutubia kwa kiswahili kumbe ALITAKA KUHUTUBIA KWA KISWAHILI....bado kwakutaka kwake ( ila hakufanikiwa)bado watu wapuuz wanashangilia...[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]THIS KANTREE BWANA
 
Wanabodi,

Baada ya Rais Samia kuhutubia Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York nchini Marekani kwa kutumia lugha ya Kiingereza safi kilichonyooka, kuna wajinga fulani huku kwenye mitandao ya Kijamii, walimpongeza Rais Samia kwa kuhutubia kwa Kiingereza safi na huku wakimponda mtangulizi wake kuwa alikacha kukanyaga UN kwasababu ya lingua, kitu ambacho sii kweli.

Leo katika pita pita yangu, nikatembelea website ya UN, ndio nikakutana na hii kitu ambayo si wengi nyumbani tuliijua

Kumbe Rais Samia alitaka kuhutubia UN kwa kutumia lugha ya Kiswahili.... ila ...
Hii maana yake ni kuwa, sababu zilizomfanya mtangulizi wa Samia asikanyage UN kuhutubia, sio issues za lingua!. Mimi mwenyewe, kama mwandishi wa habari wa kujitegemea, nimehudhuria vikao vya Baraza Kuu la UN mara kibao nikiwa na Ben na JK, kuna viongozi kibao, wanahutubia UN kwa kutumia lugha zao, kitu kinachofanyika ni kwa ubalozi wa nchi husika hapo UN, kuarifu rasmi Secretariat, na kulipia gharama za mkalimani, Rais wa nchi husika, atahutubia kwa lugha yake, halafu kutakuwa na wakalimani wanne, ambao wataitafasiri hiyo hotuba kwa zile lugha 4 rasmi za UN. Hivyo hata kama ingekuwa ni kweli, Kiingereza cha kiongozi wa taifa lolote, hakijasimama kuhutubia UN kwa Kiingereza, angeweza kuhutubia kwa lugha nyingine yoyote, hivyo naomba kuwahakikishia wajinga hao, sababu za mtangulizi wa Samia kutohutubia UN, sio lugha!.

Pili naomba kuchukua fursa hii kuwatangazia trends za hotuba ijayao ya Rais Samia kwenye 77 UNGA, itatolewa kwa lugha ya Kiswahili. Kitendo hicho, sio tuu kitaipaisha sana lugha ya Kiswahili kimataifa, bali rais Mama Samia, ataacha legacy ya kukipaisha Kiswahili, kukiingiza UN na kukifanya Kiswahili kuwa ni moja ya lugha kuu za dunia.

Hongera sana in advance rais wetu Mama Samia, Chief Hangaya kutaka kuhutubia UN kwa Kiswahili. Ukisikia uzalendo wa kweli kwa nchi yako, sasa ndio huu, huwezi kuwa mzalendo, Mkuu wa machifu wa kiasili, halafu uendelee kuhutubia kwa lugha za watu, uzalendo wa kweli ni pamoja na kuuenzi utamaduni wako, na lugha ndio kielelezo cha kwanza cha utamaduni wa jamii.

Kwa sasa Kiswahi tayari ndio lugha ya Afrika, Mama Samia atakipaisha kuwa moja ya lugha kuu za dunia.

2025 Tusifanye Makosa!.

Paskali.
Upuuzi mtupu! Tuna wizara husika, tuna ubalozi UN, kikao Cha UNGA Kiko kwenye calendar ya UN kila mwaka; walishindwaje kufanya maandalizi husika kupata mkalimani?! Wacha kutetea ujinga,
 
Kuna vitu vingine ni ujinga wa hali ya juu. Eti atakipaisha Kiswahili, atakipaisha kwenda wapi? Yaani kama angetumia tu Kiswahili kuhutubia, basi tayari kingepaa.

Kichina kimetumika miaka mingapi kuhutubia UN? Kichina kimepaa kufika wapi? Hivi hapa Tanzania kwenye shule zetu, tumeanza kufundisha Kichina kwa sababu wachina wanakitumia kuhutubia UN?

Hoja za kijinga kabisa kufikiria unaweza kuifanya lugha ya nchi yako itumike na mataifa mengine kwa vile tu Rais wa nchi ametumia lugha hiyo kuhutubia UN au AU.

Mayala mpaka leo hii hajui vitu vilivyokuwa na mchango mkubwa kwa lugha fulani kutumika na mataifa mengi:

Ukoloni - mataifa yaliyoweza kuwa na makoloni (Uingereza, Ufaransa na Ubeligiji, Hispania, Ureno), biashara ya utumwa (nchi za Uarabuni), dini (Warumi, Waarabu).

Kwa sasa hakuna lugha yoyote itakayozizidi lugha za English, Spanish, French na Arab kwa kuongewa nabmataifa mengi Duniani. Kama unahitaji kuwa mfaidika mkubwa wa fursa za Dunia, hizo ndizo lugha za kujifunza. Hutaki acha. Mwenye akili huifuata Dunia. Wewe kaa usubirie Dunia ikufuate.

Mwalimu Nyerere, pamoja na uzalendo wake, aliwahi kunena, ni lazima tujitahidi kukifahamu Kiingereza maana ni Kiswahili cha Dunia.
Lipe makavu Hilo poyoyo, njaa inalitesa Sana na uchu wa uteuzi! Mayala, Njaa, Njala![emoji2][emoji2956]
 
Nimefurahishwa sana na hotuba kutoka kwa raisi wa taifa la Ghana. Ni hotuba iliyokuwa na muunganiko tofauti sana na hotuba ya mama yetu. Walioandika io hotuba bado sana.
Hakika wanaomsifia Hangaya nadhani hawakufuatilia vizuri UNGA!
Kuna VIONGOZI walitoa speech Matata Sana; kwa mfano Joe Biden, Nana Addo wa Ghana na HH wa Zambia!
 
Wanabodi,

Baada ya Rais Samia kuhutubia Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York nchini Marekani kwa kutumia lugha ya Kiingereza safi kilichonyooka, kuna wajinga fulani huku kwenye mitandao ya Kijamii, walimpongeza Rais Samia kwa kuhutubia kwa Kiingereza safi na huku wakimponda mtangulizi wake kuwa alikacha kukanyaga UN kwasababu ya lingua, kitu ambacho sii kweli.

Leo katika pita pita yangu, nikatembelea website ya UN, ndio nikakutana na hii kitu ambayo si wengi nyumbani tuliijua

Kumbe Rais Samia alitaka kuhutubia UN kwa kutumia lugha ya Kiswahili ila hii maana yake ni kuwa, sababu zilizomfanya mtangulizi wa Samia asikanyage UN kuhutubia, sio issues za lingua. Mimi mwenyewe, kama mwandishi wa habari wa kujitegemea, nimehudhuria vikao vya Baraza Kuu la UN mara kibao nikiwa na Ben na JK, kuna viongozi kibao, wanahutubia UN kwa kutumia lugha zao, kitu kinachofanyika ni kwa ubalozi wa nchi husika hapo UN, kuarifu rasmi Secretariat, na kulipia gharama za mkalimani, Rais wa nchi husika, atahutubia kwa lugha yake, halafu kutakuwa na wakalimani wanne, ambao wataitafasiri hiyo hotuba kwa zile lugha 4 rasmi za UN.

Hivyo hata kama ingekuwa ni kweli, Kiingereza cha kiongozi wa taifa lolote, hakijasimama kuhutubia UN kwa Kiingereza, angeweza kuhutubia kwa lugha nyingine yoyote, hivyo naomba kuwahakikishia wajinga hao, sababu za mtangulizi wa Samia kutohutubia UN, sio lugha.

Pili naomba kuchukua fursa hii kuwatangazia trends za hotuba ijayao ya Rais Samia kwenye 77 UNGA, itatolewa kwa lugha ya Kiswahili. Kitendo hicho, sio tuu kitaipaisha sana lugha ya Kiswahili kimataifa, bali rais Mama Samia, ataacha legacy ya kukipaisha Kiswahili, kukiingiza UN na kukifanya Kiswahili kuwa ni moja ya lugha kuu za dunia.

Hongera sana in advance rais wetu Mama Samia, Chief Hangaya kutaka kuhutubia UN kwa Kiswahili. Ukisikia uzalendo wa kweli kwa nchi yako, sasa ndio huu, huwezi kuwa mzalendo, Mkuu wa machifu wa kiasili, halafu uendelee kuhutubia kwa lugha za watu, uzalendo wa kweli ni pamoja na kuuenzi utamaduni wako, na lugha ndio kielelezo cha kwanza cha utamaduni wa jamii.

Kwa sasa Kiswahi tayari ndio lugha ya Afrika, Mama Samia atakipaisha kuwa moja ya lugha kuu za dunia.

2025 Tusifanye Makosa!.

Paskali.
Brother! Usipoteze nguvu na akil zako kuwajibu wapuuzi wa humu jf. Watz wengi ni mburula! Hayajui yanataka nini, wala hayajui yanakosa nini. Jikite kwenye masaala ya kuwaelimisha mambo ya msingi ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kupiga kura na kusisimamia kura zao zisiibiwe
 
Nilitaka niseme kitu ila nikakumbuka wewe ni mwanasheria, unamhukumu au kumsifia mtu kwa kukusudia. Hapo nikaishiwa cha kusema.

Lakini kuna Rais yeye hata hakukanyaga UNGA, katuma tu video iliyorekodiwa watu wakasikiliza ukumbini.

Kama Chief alikua na nia na alidhamiria kuhutubia kiswahili na hajatekeleza, tubirie siku akifanikisha hiyo adhma.

JPM alikua na mapungufu yake mengi tu, lakini ikifika jambo la kuonyesha msimamo wake alikua vizuri sana kwenye hilo eneo.

Bila kujali msimamo wake uko hasi au chanya ila alijitahidi kuhakikisha msimamo wake unajulikana bayana.

Binafsi napenda mtu mwenye maamuzi na kusimamia maamuzi yake ( shida yanapokua na matokeo hasi).

JPM alikuwa na msimamo gani kuhusu UN?
 
Wanabodi,

Baada ya Rais Samia kuhutubia Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York nchini Marekani kwa kutumia lugha ya Kiingereza safi kilichonyooka, kuna wajinga fulani huku kwenye mitandao ya Kijamii, walimpongeza Rais Samia kwa kuhutubia kwa Kiingereza safi na huku wakimponda mtangulizi wake kuwa alikacha kukanyaga UN kwasababu ya lingua, kitu ambacho sii kweli.

Leo katika pita pita yangu, nikatembelea website ya UN, ndio nikakutana na hii kitu ambayo si wengi nyumbani tuliijua

Kumbe Rais Samia alitaka kuhutubia UN kwa kutumia lugha ya Kiswahili ila hii maana yake ni kuwa, sababu zilizomfanya mtangulizi wa Samia asikanyage UN kuhutubia, sio issues za lingua. Mimi mwenyewe, kama mwandishi wa habari wa kujitegemea, nimehudhuria vikao vya Baraza Kuu la UN mara kibao nikiwa na Ben na JK, kuna viongozi kibao, wanahutubia UN kwa kutumia lugha zao, kitu kinachofanyika ni kwa ubalozi wa nchi husika hapo UN, kuarifu rasmi Secretariat, na kulipia gharama za mkalimani, Rais wa nchi husika, atahutubia kwa lugha yake, halafu kutakuwa na wakalimani wanne, ambao wataitafasiri hiyo hotuba kwa zile lugha 4 rasmi za UN.

Hivyo hata kama ingekuwa ni kweli, Kiingereza cha kiongozi wa taifa lolote, hakijasimama kuhutubia UN kwa Kiingereza, angeweza kuhutubia kwa lugha nyingine yoyote, hivyo naomba kuwahakikishia wajinga hao, sababu za mtangulizi wa Samia kutohutubia UN, sio lugha.

Pili naomba kuchukua fursa hii kuwatangazia trends za hotuba ijayao ya Rais Samia kwenye 77 UNGA, itatolewa kwa lugha ya Kiswahili. Kitendo hicho, sio tuu kitaipaisha sana lugha ya Kiswahili kimataifa, bali rais Mama Samia, ataacha legacy ya kukipaisha Kiswahili, kukiingiza UN na kukifanya Kiswahili kuwa ni moja ya lugha kuu za dunia.

Hongera sana in advance rais wetu Mama Samia, Chief Hangaya kutaka kuhutubia UN kwa Kiswahili. Ukisikia uzalendo wa kweli kwa nchi yako, sasa ndio huu, huwezi kuwa mzalendo, Mkuu wa machifu wa kiasili, halafu uendelee kuhutubia kwa lugha za watu, uzalendo wa kweli ni pamoja na kuuenzi utamaduni wako, na lugha ndio kielelezo cha kwanza cha utamaduni wa jamii.

Kwa sasa Kiswahi tayari ndio lugha ya Afrika, Mama Samia atakipaisha kuwa moja ya lugha kuu za dunia.

2025 Tusifanye Makosa!.

Paskali.

Safi sana Rais Samia Suluhu Hasan. Nashangaa wanaokiponda kiswahili bila kuwa na hoja maalum. Lisu na company yake waendelee tu na juhudi zao za kukiponda kiswahili, eti kwa vile yeye anakitawala kiingereza ndio iwe sababu yakufikiri kuwa huwezi kujenga hoja kwa kiswahili.

Atipasi Lisu angezunguka kwenye kampeni 2020 na kuhutubia watanzania kiingereza pengine angeshinda kwa kishindo.
 
Toka ugombee uwakilishi wa CCM pale Kawe umekuwa sio Pascal tena!
You are somebody else with empty brain, vuvuzela type of person!
Nimeumia sana kumkosa Pascal wa awali. RIP original Pascal, yule aliyemtwanga maswali Magu hadi akaishia kumwita "njaa" kwa utani kulegeza uzito wa maswali.
 
Back
Top Bottom