Usomaji wa Maandiko ya kidini (Biblia)

Achana na hadithi zisizo na kichwa wala miguu.

Biblia ni sawa na Hekaya za Abunuwasi au riwaya za Alfu Lela ulela.

Unasoma huku unajipa matumaini uchwara na kusema unapata ufunuo kumbe ni Hallucinations tu.

Biblia ni hadithi hadithi zisizo na ufunuo wowote ule zaidi ya hallucinations zinazoitwa imani.

Amka wewe!!
 
Umefika hatua nzuri ya kujikomboa kifikra na kiakili.

Mungu na Shetani ni dhana za kutungwa hazipo katika uhalisia.

Ndio maana watu wanahangaika sana kuelezea na kuzizungumzia dhana hizi kwa vile hazipo na hazijawahi kuwepo kujiongelea zenyewe.
 
Neno la Mungu ni jipya kila siku tunahitaji upatanisho wa roho mtakatifu wakati wote kumbuka binadamu tunatenda dhambi hivyo ukifanya dhambi roho mtakatifu anaondoka yule adui ankuja kukuangamiza
Huyo Roho mtakatifu anashindwa vipi kukuzuia usifanye dhambi?

Yani huyo roho mtakatifu ni mjinga sana, Anakaa ndani yako badala akuwezeshe na akuzuie usitende dhambi anakuacha utende dhambi kisha aondoke!!

Halafu tena wewe uanze kumtafuta arudi kukaa ndani mwako for nothing ilhali hata uwezo wa kukufanya usitende dhambi hana..

Huyo Roho mtakatifu ni mjinga sana.
 
sawa mkuu, vipi abaout illuminates or freemasons , i think ni kama wameelezewa katika kitabu cha ufunuo, maana huwa na relate hicho chama na kilichopo now kinachonendesha dunia, kwa kujiita 666 na nembo zao.
 
Mkuu vitu usivyokua na ufahamu/hujavi-experience maishani mwako usivizungumzie kabisa hadharani... Kuna watu wanakuamini na kwa namna moja ama nyingine wanapotoka.

Ivi we unafikili watu ni wajinga kiasi hicho... Kuna level wamefikia katika upande wa pili wa Shilingi ambao wewe hujafika na inawezekana wewe umekwamia kwenye upande mwingine (elimu dunia(science)) ukaona umamaliza, mkuu nikuambie tu kua safari bado.

Kama una miaka chini ya 30 basi usifikie hitimisho kwa jambo lolote kwani kuna mengi ya kujifunza bado... , sayansi yenyewe ni inabadilika(dynamic) na elimu ya ulimwengu huu ni pana sana, (wahenga wanakwambia elimu haina mwisho).
Kuna vitu huwezi kuelewa /huwezi kupata taswira halisi bila kuviishi/kivi-experience... Ni kama vile mtoto anavyokanywa na kuadhibiwa na wazazi wake kwa level ya uelewa wake a naona anaonewa ananyanyaswa lakini akikua anaelewa nini wazazi wake walikikusudia juu yake.
 
Mkuu vitu usivyokua na ufahamu/hujavi-experience maishani mwako usivizungumzie kabisa hadharani... Kuna watu wanakuamini na kwa namna moja ama nyingine wanapotoka.
Ufahamu ni nini?

Umeshawahi ku experience vitu vya kwenye biblia zaidi ya hadithi hadithi tu zisizo na uthibitisho wala uhalisia wowote ule?
Watu wengi kuamini kitu fulani haina maana kwamba kitu hicho ni cha ukweli kama hakina uthibitisho.

Uwingi wa watu kuamini kitu fulani sio uthibitisho wa ukweli wa hicho kitu.
Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika.

Ukweli hauendani na imani, ukweli unaendana na uwepo wa uthibitisho
 
sawa mkuu, vipi abaout illuminates or freemasons , i think ni kama wameelezewa katika kitabu cha ufunuo, maana huwa na relate hicho chama na kilichopo now kinachonendesha dunia, kwa kujiita 666 na nembo zao.
Nimekuambia 666 ni mwili wako wewe mwenyewe ...afataye tamaa za mwili uzaa dhambi ambayo ndiyo chapa ya huyo mnyama. Dhambi ndiyo neno pekee duniani la kuchukua Tahadhari siyo habari ya freemasoni maana hao freemason wasingekuwa tatizo kama dhambi isingekuwepo
 
Maswali ni mengi sana ila majibu ni machache mnoooo.
 
Be blessed brother.
 

Nina uhakika wewe ni open minded person, kwa msingi huo huo wa kufikiri nje ya boksi, ukiwa katika huu ulimwengu unaonekana kwa kutumia milango mitano ya fahamu, jishughulishe katika kufahamu je? kuna ulimwenguni usioonekana na usiokua percieved na our 5sense organ.

Huu mwili tulionao ni kama body tu ambayo imefungwa senser kuu 5(5sense organ) ili kutusaidia katika mazingira ya hapa duniani. Sasa fikilia vipi kungekua na senser zaidi ya tano kunauwezekano tungeweza ku-detect mambo mengine pengine kwa usalama wetu na afya ya Akili yetu isingeweza kuhimili hivyo ni hekima/busara tu imetumika.

Sasa fanya u-dig more deeper kuhusu sixth sense (jicho la tatu)) . Kwanini ni kwasababu huo ulimwengu upo!

Na unapokua unahitaji uthibitisho huku ukiwa katika ulimwengu ambao sense organ za mwili wako zipo adaptable na zina access only na physical world, hazina access ya ku-recieve/detect taarifa yoyote kutoka ulimwengu mwingine pasipo kua na connection yoyote ambayo kwa maumbile yetu hatujaumbiwa nayo.

We huoni unatupatia changamoto!!! chukulia mfano umekutana na kipofu wa kuzaliwa anakuomba umuelezee/umchanganulie tofauti iliyopo kati ya rangi ya blue na nyekundu utamueleza vipi hadi aelewe somo, ni Ngumu...! labda umponye kwanza apate kuona tena ndio mkae meza moja hapo mtaelewana.

Sikulazimishi uamini ila fanya udadisi(just for curiosity purpose).
 
😁
 
Jicho la tatu ni nini?

Unathibitishaje jicho la tatu lipo?

Wewe mwenyewe upo kwenye
huu huu ulimwengu ambao ni physical kwa sense organs 5,

Sasa unajuaje na unathibitishaje kwamba kuna ulimwengu usio onekana upo, ilihali wewe mwenyewe unadai ulimwengu huo hauwezi kuwa accessed kwa sense organs zetu.

Wewe umetumia nini ku access huo ulimwengu usio onekana?
 
Uebert Angel aliyenaswa na camera za Aljazeera akifanya biashara ya magendo ya dhahabu kutoka Zimbabwe?

Baada ya hiyo documentary waliyo tengeneza nini kimefatia? Ulijipa muda wa kusikiliza upande wa pili uliotuhumiwa? Ulisikiliza maelezo yaliyo tolewa na serikali ya Zimbabwe kuhusu hizo tuhuma?

Biblia inasema, β€œIt’s only a fool who judges a matter after hearing only one voice”
 
Unapotosha
 
HAYA NI MAFUNDISHO YA INJILI FEKI ZA MADHEHEBU YA DINI ...NENO DHEHEBU MAANA YAKE NI HEKATU LA SHETANI
Ili ujue ni kwamba Muumba hana DINI wala Dhehebu, ni mmoja tu na hagawanyiki.sio wa kabila, lugha wala jamaa maana wote tumetoka kwake.

Warumi 11:36
Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.

Ila dunia ilitengeneza mfumo kila kabila lilikuwa na Mungu wake, kila taifa lilikuwa na Mungu wake na kila jamaa ilikuwa na Mungu wake ndio mfumo uliokuwepo.

Ni ufinyu wa uelewa na ufahamu ndo mana unasema ivyo ungejua usiyoyaona ungeelewa.
 
Majibu yote yapo humo πŸ‘†πŸ‘†πŸ‘† moja wapo ni kiunganishi.
connection
Pia
labda umponye kwanza apate kuona tena ndio mkae meza moja hapo mtaelewana.
Kuto kuthibitika kwa haya mambo katika ilimwengu wa kimwili haimaanishi kwamba mambo hayo hayapo..! La! Mambo hayo yapo sema wewe binafsi hujataka kuyafahamu... na uwezo huo umepewa, kila mtu anao ila hatuutumii(hatuamini)

Narudia tena uwezo huo upo na kila mtu anao pasipokujali dini yake, anaendaga ibadani au hua haendi, shida inakuja ni mhusika hajataka kuutumia kwa kufuata kanuni.

Sasa kazi ni kwako kama unataka na wewe kufahamu,,, kwasababu nitakutofautishiaje rangi ya blue na nyekundu ilihali wewe ni kipofu tokea unazaliwa hujawahi ona chochote. Hutanielewa kamwe!. Na kwa kutumia kanuni/ufahamu wa elimu (sayansi) ndio utaona nimechanganyikiwa kabisa.

Sasa nakushauri usifikie hitimisho kwa jambo lolote ambalo Huna uzoefu nalo.
Elimu haina mwisho kila siku tunajifunza vitu vipya unaweza ukajifuza kitu kipya hata ukiwa na miaka 99.

Haya mambo ya imani ya hukulie kama changamoto mpya kwako mwaka huu... uipatie ufumbuzi, kwa lengo la kijifunza zaidi. kama una nia njia huwezi kukosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…