Neno linasema ktk 1 YOHANA 3:4 'Kila atendaye dhambi afanya uasi,kwakua dhambi ni uasi.
Zingatia kabla ya Bwana Yesu kuja na kuiondoa dhambi,wanadam wote walikua ni wenye dhambi bila kujali umri wao so mtu anakua mwenye dhambi kwasababu amezaliwa ana dhambi sio kutenda.
Tazama WARUMI 5:12-14 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;
13 maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria;
14 walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, NAYO ILIWATAWALA HATA WAO WASIOFANYA DHAMBI IFANANAYO NA KOSA LA ADAMU, aliye mfano wake yeye atakayekuja.
Pia tunajua kua mshahara wa dhambi ni mauti (WARUMI 6:23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.)hivyo basi watoto wadogo wanakufa kwasabab ya dhambi! Dhambi inayowaua sio walioifanya maana kuna vichanga kuna vinavyokufa kabla ya kuzaliwa pia bali ni ile waliyoirithi kupitia Adamu na asili yake ya dhambi toka eden ambayo ipo ndani yao!
Lakini Mungu apewe sifa kwakumleta mwanawe mpendwa duniani kutukomboa na dhambi na ktk hali ya uasi.YOHANA 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Uzima unakujaje bila dhambi kuondolewa kutokana na YOHANA 3:16 hapo?
Dhambi na asili yake imeondolewa milele na Bwana Yesu WAEBRANIA 10:10 Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.
12 Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu;
14 Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.
17 Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa.
18 Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.
Cheki WARUMI 5:8-10 Basi Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, TULIPOKUWA TUNGALI WENYE DHAMBI.
9.Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.
10 Kwa maana ikiwa TULIPOKUWA ADUI TULIPATANISHWA NA MUNGU KWA MAUTI YA MWANA WAKE; zaidi sana BAADA YA KUPATANISHWA tutaokolewa katika uzima wake.
Yesu hakutufia tukiwa watakatifu wenye matendo mema bali tukiwa waasi na sio wakristo tu bali ulimwengu mzima!
Hatupatanishwi na Mungu kwa matendo mazuri ya kila siku.
Mtu aliezaliwa mara ya pili ni mwenye haki sio mdhambi tena.2 WAKORINTHO 5:21 Yeye[YESU] asiyejua dhambi ALIMFANYA KUWA DHAMBI KWA AJILI YETU, ILI SISI TUPATE KUWA HAKI YA MUNGU KATIKA YEYE[YESU].
1 WAKORINTHO 6:17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.
So kama umeokoka dhambi huna,coz kama ndani ya Mungu hakuna dhambi nami sina sababu tumekua kitu kimoja naye.
1 YOHANA 3:9-10 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.
10 Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
uthibitisho mwingine ni 1 YOHANA 2:1-2 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
2 naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.
Hivyo jua kwamba ondoleo la dhambi huja kwa kuliamini jina la Yesu Kristo(MATENDO YA MITUME 10:43)
Kwa maana pia dhambi ni kutokumuamini Yesu(YOHANA 16:8-9)
Yani unamuamini Yesu ila kazi yake ya pale msalabani kumwaga damu yake kwa ajili ya ondoleo la dhambi ya ulimwengu huiamini! Na amesema yeye mwenyewe sehemu nyingi tu ila unachagua kujiita mwenye dhambi,dhaifu,usiefaa,usie kitu na kukiri ungamo kila jumapili kanisani ilhali umekua kiumbe kipya mwenye haki,utakatifu na ukombozi wa Mungu baba!
Kiukweli inashangaza mno wakristo waliokoka wanavyoshikilia dhambi ambayo ilishafutwa milele!
Ktk MATHAYO 5:17-48 Bwana Yesu anaelezea amekuja kuitimiliza yani kuitimiza na kuirekebisha sababu yeye ameleta neema na kweli.maana yake ni kua torati yote ya musa na manabii inatimia katika yeye.so ukiwa ndani yake basi torati yote na manabii inakamilika ndani yako.
Na ndio maana unaona kwanzia mstari ya 21 Bwana Yesu anazinukuu baadhi ya sheria za torati zilivyosema na yeye anaziongezea kua yote hayo ni upendo tu ndio amri kuu(kumpenda Mungu na jirani yako basi)