Usomaji wa Maandiko ya kidini (Biblia)

Yah niko kwenye situation hiyo pia na hata kanisan kwasasa niwe mkwel naemda kwa manat sana ili tu watoto wasipate confusion

Ahsante sana
Nakuelewa sana. Imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa neno la Mungu. Kuna battle kubwa sana kwa wanaosoma bibilia ili wasisikie neno la Mungu ambalo ndio msaada kwa maisha ya sasa. Endelea kusoma, USIACHE.
 
Kuna tofauti ya kusoma Biblia na kusoma kitabu cha historia. Kusoma Biblia kunahitaji kutafakari, kusoma kitabu cha historia kunahitaji kuweka kumbukumbu (kama unavyosoma Biblia kwa sasa). Husomi kwa kutafakari, unasoma kwa kuweka kumbukumbu au kukariri. Ukisoma kwa kutafakari, utapata funzo (maana kwa maisha yako). Ukisoma kwa kutafakari, mfano, ukisoma juu ya huruma ya Mungu, utatafakari juu ya huruma yako mwenyewe, juu ya watu wanaokukosea na kuomba uwasamehe. Utatafakari pia juu ya wale unaowakosea na jinsi unavyotaka usamehewe. Halafu utajiuliza, kama nikiwakosea wengine huwa nataka nisamehewe, kwa nini wao wakinikosea sitaki kuwasamehe? Ukisoma kuhusu upendo wa Mungu, utatafakari kuhusu upendo wako mwenyewe ukoje. Upendo wa Mungu unataka uwapende wengine kama unavyotaka kutendewa wewe mwenyewe na ujaribu kuona 'tendency' yako ikoje? Mfano, upendo wako kwa mkeo unaendana na huo unaofundishwa kwenye Biblia? Kama siyo, then utaanza kuona maeneo yenye upungufu. Labda kwamba humpendi mkeo kutoka moyoni, ila ni upendo wa juujuu tu wa bora liende/wa kinafiki. Hivyo, ukisoma Biblia kwa kutafakari kila utakaposoma utakutana na ujumbe mpya unaotaka uboreshe maisha yako ili yaendane na maisha Biblia inayofundisha ya kuwa mtu mpya/mwema zaidi kuliko ulivyo sasa/kuweka utaratibu mpya wa maisha yako. Utapenda pia kuboresha mahusiano yako na watu wengine ambao ulikuwa umeshawaondoa kwenye orodha ya watu unaoweza kushirikiana nao/ambao ulikuwa umeshawatenga na unaamua kuwapokea tena kama simulizi la Mwana Mpotevu kwenye Injili ya Luka. Unaweza pia kutafakari kuhusu mambo unayowatendea wengine wenye shida kama simulizi la siku ya mwisho (Matayo 25:31-46).
 
unasoma kama kitabu cha hadithi, namshukuru Mungu mimi nikisoma naelewa na kamwe hilo neno nililosoma halitoki na huwa napata wasaa wa kuwasadia wengine
Actually zile ni hadith za kale in first place, mengine yanafuata baada ya hapo kama revelations na mafunzo toka kwenye hizo hadith
 
Sina uelewa mkubwa lakini naelewa, hasa kitabu cha Ufunuo wengi hawajui kuna mengi mule yameshatokea siyo mambo yajayo.

Mnyama 666 mpinga kristo alikuwa mtawala wa dola la Rumi.
Kusema kuyaelewa maandiko ya ufunuo bado sijayapata fresh.. ila kila kilichopo katika biblia hakijakosewa kule.. kuna vitabu kama unataka kuwa enlighted ni muhimu kuvisoma japo ni vigumu ila ukitia nia yanawezekana tu.. matendo.. wakorintho zote mbili.. efeso..wagalatia.. wakolosai.. nyaraka za petro na yohana.. zitakufanya uelewe mengi
 
Sina uelewa mkubwa lakini naelewa, hasa kitabu cha Ufunuo wengi hawajui kuna mengi mule yameshatokea siyo mambo yajayo.

Mnyama 666 mpinga kristo alikuwa mtawala wa dola la Rumi.
Kwamba 666 is already fullfiled sir and not something to come??
 
Sio shetani tu, hata Yesu. Ukimkiri kuwa mwokozi wa maisha yako atakuponya hata kama haujawahi kushika biblia.
Noted.
Kinachofanya kazi ni neno sio Biblia. Hapo ndipo tumeachana. Naongelea neno, wewe unaongelea biblia. Kama haulijui neno na kuliishi, biblia itakuwa hirizi tu kwako kama hirizi zingine.
 
Mkuu upo karibu kabisa na kuwa na fikra huru

Ukweli ni kwamba wahubiri makanisani wanahubiri Hadithi zile zile ambazo zina mtengeneza Mungu kuwa ni Mwema na Mtakatifu na haswa Agano Jipya

Trust me mkuu kuna hadithi na mistari mingi zaidi ya unayohubiriwa kila siku ambayo huwezi kamwe abadan kukuta inahubiriwa makanisani kwasababu ya utata wake

Hebu jitutumue ukasome kumbukumbu la torati yote...... unaweza kufika mahali ukadhania hausomi Bibilia unayoijua wewe

Zamani za kale baada ya vitabu kukusanywa na kuidhinishwa kama Bibilia ilikua ni MARUFUKU mtu baki kusoma Bibilia zaidi ya viongozi wa kanisa tu....... na baada ya kuruhusiwa ikatengenezwa dhana kwamba viongozi wa kiroho ndio wenye uwezo wa kutafsiri maandiko na kwamba eti ukisoma wewe hutaelewa na blah blah kibao

Makanisa mengi yanatengeneza kalenda ya masomo kwa mwaka ambayo ina mistari na visa vya Bibilia vile vile kiasi kwamba unaweza kudhani unaijua Bibilia yote

Hizi ni hekaya za kale tu ambazo hazina ukweli wowote
 
Kuna kitu umenifungua macho mkuu, barikiwa sana
 
UMenena vyema.ni kwel kabisa
 
Me sina hata majibu ya kukupa ila mwamba mmoja hivi huwa mafundisho yake ni ya kitofauti kabisa ngoja nikikumbuka jina lake ntalikupa upate mwanga
TOP Plus TV
Mchungaji : Pastor Ceasar Masisi
YouTube Channel : Saa Ya Neema Tv
Mawasiliano : 0753 999 989
 
Neno lipi unalizungumzia wewe mkongwe tofauti na neno la kwenye Biblia?
Naongelea neno la Mungu (single word)
Wewe unaongelea mkusanyiko wa maneno katika biblia.
Tofauti yake ni kwamba, mfano unaomba uponyaji, utatakiwa kusoma neno lililobeba ahadi ya uponyaji, hautakiwi kusoma biblia (mkusanyiko wa maneno). Ukisoma biblia ili upate uponyaji ni sawa na kupiga ramri maana huna hakika na unachokitaka.
 
Neno la Mungu Ni chakula cha roho...roho yako lazima uilishe chakula ambacho Ni neno la Mungu .,.the more you eat the hunger you get nkimaanisha Kadri unavyokuwa unasoma Neno unakua unazidi kutaka kusoma....biblia tunatakiwa tuisome mara Kwa Mara haijalish hata kama unaujua mstari umeukariri tunatakiwa tusome sababu Neno linatia uzima ndani yako.........ukitaka usiboreke close your mind isome kutoka ndani ya Moyo wako usisome akilini sababu faith ipoo moyoni akilin hamna faith.....the moment utakapoanza kuisoma kutoka moyoni utaanza kusikia Nguvu za Mungu ndani yako Na hutoboreka kamwe.
 
AHsante sana, niseme tu hii class au bideo hii ya huyu nwana nimeshawahi iona.
Ameelezaa yooooote hayo nakubaki na ninaelewa, but

swali langu ni hili, HOW DO YOU COME INTO ACQUIRING ALL THOSE SPOKEN STUFFS???
nimeshajua hizo ginosco, epigniss etc, HOW DO I THEY COME INTO ME?????.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…