Usomaji wa Maandiko ya kidini (Biblia)

Unatubu nini wakati huna dhambi? Dhambi zako Yesu mwenyewe Yesu alishatubu kwa ajili yako pale Msalabana "Baba uwasamehe kwa maana hawajui walitendalo" sasa wewe unatubu nini wakati Yesu alishamaliza kila kitu pale Msalabana au Wewe ni Mkristu Jina?
Sasa na ile warumi 10:9 inamaana gani.. Ndio Yesu alisulubiwa.. Yes alizikiwa Yes alifufuka.. kuna process hapo kati ya mtu kuukubali huu ukweli Kwa kinywa chake na kuamini.. ndipo anazaliwa mara ya pili
 
Sasa na ile warumi 10:9 inamaana gani.. Ndio Yesu alisulubiwa.. Yes alizikiwa Yes alifufuka.. kuna process hapo kati ya mtu kuukubali huu ukweli Kwa kinywa chake na kuamini.. ndipo anazaliwa mara ya pili
Then i qualify for these favours right???
 
Jenga IMANI YAKO KWA KRISTO, atakuongoza. Ukiwa na mashaka na unaehitaji msaada wake, utaupataje?
Yesu aliipindua Torati ya Musa kwa maana Torati ya Musa inaongelea Sheria Ila Injili ya Yesu inazungumzia Uzima wa Milele na kusamehewa dhambi na Wokovu kwa hio wote tumeokolewa kwa kufa kwake Sisi tumepona amezitakasa dhambi zetu zote kuanzia alipokufa pale Msalabana hata sasa hakuna dhambi mpya tena kila utendalo sio dhambi kwa maana dhambi zote alishazifia pale Msalabana huna dhambi na hutendi dhambi km hufati Sheria za Musa yaan Torati Agano la Kale Torati IPO kwa ajili ya Wayahudi na Waisrael, Wewe unaefuata Injili ya Yesu hakuna kitu unatenda ukaambiwa ni dhambi maana huna dhambi na hutendi dhambi Ila km unafuata Torati ya Musa basi Wewe jua unatenda dhambi, cha kujiuliza Torati na Sheria za Musa ni nini?
 
Then i qualify for these favours right???
Ni ngumi mimi kukujibia hapa.. ili mtu azaliwe mara ya pili anahitaji kupokea mbegu sahihi(yaani neno sahihi)limpe kujuta then ndio akubali hayokwa kinywa chake kwamba kweli Yesu ni bwana tena mwokozi.. hapo ndio anakuwa amezaliwa mara ya pili kama umepita hapo.. then unazo
 
Na hapa ukapata muda ukasoma wagalatia friend utaelewa sheria fresh kabisa..
 
Sasa na ile warumi 10:9 inamaana gani.. Ndio Yesu alisulubiwa.. Yes alizikiwa Yes alifufuka.. kuna process hapo kati ya mtu kuukubali huu ukweli Kwa kinywa chake na kuamini.. ndipo anazaliwa mara ya pili
Ndio nakwambia Wewe unapozaliwa tu tayari Wewe ni kiumbe kipya Wewe ungali Mtoto ndie unaetakiwa umfunze Mzazi wako kuhusu Wokovu na sio Mzazi wako akufunze Wewe na kukutwisha masheria kibao ambayo Yesu alishayaondoa, process zote ulishazipitia kabla hujazaliwa tangu kutungwa kwa Mimba yako Yesu mwenyewe alishasema "waacheni watoto wadogo waje kwangu, kwa maana ufalme wa Mungu ni kwa ajili ya watu km hao"
 
Mathayo 5 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁷ Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
¹⁸ Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.


Naomba kuuliza.
Nikiua sasa hivi sihesabiwi dhambi?
 
Naomba unieleweshe zaidi
 
Reactions: 511
Hata walimu wazuri wa mashuleni walifundishwa na walimu wa zaman hata wafanyakaz pia,,mimi mwakasege hua namwelewa sana.
Siku moja nilikatiza sehemu nikakuta mkutano wa Mwl Mwakasege, nikaona ngoja nimsikilize kidogo maana anasifiwa sana anajua NENO, akawa anafundisha tafsiri za ndoto Kibibilia........ NILICHOKA KABISA
Hakuwa na tofauti yoyote na mpiga ramli

Hakika IMANI haitaki kabisa matumizi sahihi ya AKILI
 
😁😁😁😁👍👍👍
 
Acheni pia ku'simplify' to the extent ya kufanya dini isiwe/ikose maana na waoni haiwasaidii kwa chochote. To make religion too simple to have any meaning in your life. Acheni kufanya hivyo pia.
Woga wako tu mkongwe!

Biblia ni mkusanyiko vitabu vinavyoelezea historia ya dini ya kikristo. Ukitaka kuijua dini ya Kikristo vyema unatakiwa kusoma biblia. Ukisoma biblia utaona wapi tumetokea kama Wakristo na wapi tunaelekea na nini tufanye na kipi tusifanye katika safari yetu ya Ukristo. Wala hauhitaji kutafakari sana ukiwa unaisoma, Mungu wetu anajua kabisa sisi watu wake ni wavivu kiasili ndo maana amenyoosha sana maelekezo yake kupitia manabii tofauti tofauti katika biblia.

Hii habari ya kutafakari sana kuisoma biblia ni porojo tu zilizoletwa na wapigaji, watu waliofanya dini kuwa vitega uchumi, wanataka kuaminisha watu kuwa biblia ni ngumu sana kuielewa mpaka ufundishwe kuisoma. Na kuna wakati mwingine ni hofu yao tu ya kupoteza waamini mara baada ya kuisoma biblia, maana ukiisoma vyema biblia mwanzo mpaka mwisho kuna “contradictions” nyingi sana zimejitokeza (mimi binafsi ninaamini kulingana na ukale wa Biblia, pia kwenye mchakato wa kuitafsiri hii kitu ilikuwa ni lazima itokee).

Labda kama unazungumzia kuichambua Biblia kama kazi ya fasihi. Hii ni kawaida kwa kazi zote za fasihi, sio kitu kikubwa sana. Kuchambua fasihi sio kitu kigeni, hata kitabu cha TAKADINI kimefanyiwa uchambuzi, unaamini kitabu cha TAKADINI kinahitaji tafakuri sana kukisoma?

NB: MIMI NI MKRISTO​
 
Na hapa ukapata muda ukasoma wagalatia friend utaelewa sheria fresh kabisa..
Soma : Wagalia 3 YOTE ili uelewe ninachokuambia kwamba Wewe huna dhambi Ila kukwambia Wewe una dhambi sijui Ukoo kufanya nini unatishwatishwa tu Ni ili wao wafanye biashara zao za Dini Ila Wewe mbele ya Yesu huna dhambi dhambi zako zote yeye alishazifia pale Msalabana na akatubu kwa ajili yako na dhambi zako pale Msalabana, km unafuata Yesu (Mkristu) Wewe huna dhambi Ila km unafuata Sheria na Torati ya Musa Wewe unachofanya hata kutembea bila viatu, kusuka, kuvaa nguo za kike, kutokuoga mara 3 kwa siku, kutokupiga mswaki, zote hizo ni dhambi

Wagalatia 3:1-29

1 Enyi Wagalatia, mmekuwa wajinga kweli! Ni nani aliyewaloga? Habari juu ya kusulubiwa kwake Yesu Kristo ilielezwa waziwazi mbele ya macho yenu.

2 Napenda kujua tu kitu kimoja kutoka kwenu: Je, mlipokea Roho wa Mungu kwa sababu ya kutimiza matakwa ya Sheria ama kwa sababu ya kuisikia na kuiamini Habari Njema?

3 Je, mu wajinga kiasi hicho? Ninyi mlianza yote kwa msaada wa Roho je, mnataka sasa kumaliza kwa nguvu zenu wenyewe?

4 Je, mambo yale yote yaliyowapata ninyi yamekuwa bure tu? Haiwezekani!

5 Je, Mungu huwajalia Roho na kutenda miujiza kati yenu ati kwa sababu mnatimiza yanayotakiwa na sheria, ama kwa sababu mnasikia Habari Njema na kuiamini?

6 Chukueni kwa mfano habari za Abrahamu: yeye alimwamini Mungu, naye Mungu akamkubali kuwa mwadilifu.

7 Sasa basi jueni kwamba watu wenye kumwamini ndio walio watoto halisi wa Abrahamu.

8 Maandiko Matakatifu yalionyesha kabla kwamba Mungu atawakubali watu wa mataifa kuwa waadilifu kwa njia ya imani. Hivyo Maandiko Matakatifu yalitangulia kumtangazia Abrahamu Habari Njema: "Katika wewe mataifa yote yatabarikiwa."

9 Basi, wale walio na imani wanabarikiwa pamoja na Abrahamu aliyeamini.

10 Lakini wote wanaotegemea tu kutimiza yanayotakiwa na Sheria, wako chini ya laana. Maana, Maandiko Matakatifu yasema: "Yeyote asiyeshika na kutimiza yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Sheria, yuko chini ya laana."

11 Ni dhahiri kwamba Sheria haiwezi kumfanya mtu akubaliwe kuwa mwadilifu; maana Maandiko Matakatifu yasema: "Mwadilifu kwa imani ataishi."

12 Lakini Sheria haitegemei imani, ila Maandiko yasema: "Mwenye kutimiza yanayotakiwa na Sheria ataishi."

13 Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya Sheria kwa kujitwalia laana hiyo kwa ajili yetu; maana Maandiko yanasema: "Yeyote aliyetundikwa msalabani amelaaniwa."

14 Jambo hili lilifanyika kusudi ile baraka aliyopewa Abrahamu iwashukie watu wa mataifa mengine kwa njia ya Kristo, na ili kwa imani, tumpokee yule Roho ambaye Mungu alituahidia.

15 Ndugu, nitawapeni mfano kutoka maisha yetu ya kila siku. Fikirini juu ya mkataba kati ya watu wawili. Mkataba ukisha fanyika na kutiwa sahihi hapana mtu anayeuweka kando au kuuongezea kitu.

16 Basi, Abrahamu alipewa ahadi, yeye pamoja na mzawa wake. Maandiko hayasemi: "Na wazawa wake," yaani wengi, bali yasema, "Na mzawa wake," yaani mmoja, naye ndiye Kristo.

17 Ninachotaka kusema ni hiki: Mungu alifanya agano lake akalithibitisha; Sheria ambayo ilitokea miaka mia nne na thelathini baadaye, haiwezi kulitangua hilo agano wala kuibatilisha hiyo ahadi.

18 Maana, kama urithi ya Mungu inategemea Sheria, basi, haiwezi kutegemea tena ahadi ya Mungu. Kumbe, lakini Mungu alimkirimia Abrahamu kwa sababu aliahidi.

19 Ya nini basi, Sheria? Iliongezwa hapo ili kuonyesha uhalifu ni kitu gani, mpaka atakapokuja yule mzawa wa Abrahamu aliyepewa ile ahadi. Sheria ililetwa na malaika kwa mkono wa mpatanishi.

20 Ama hakika, mpatanishi hahitajiwi ikiwa jambo lenyewe lamhusu mtu mmoja; na Mungu ni mmoja.

21 Je, Sheria inapingana na ahadi za Mungu? Hata kidogo! Maana, kama kungalitolewa sheria ambayo ingeweza kuwapa watu uzima, basi, tungeweza kukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya Sheria.

22 Lakini sivyo; Maandiko Matakatifu yamekwisha sema kwamba ulimwengu wote upo chini ya utawala wa dhambi; na hivyo, kwa kumwamini Yesu Kristo, wenye kuamini watimiziwe ile ahadi.

23 Kabla ya kujaliwa imani, Sheria ilitufanya wafungwa mpaka imani hiyo iliyokuwa inakuja ifunuliwe.

24 Basi, hiyo Sheria ilikuwa kama mlezi wetu mpaka alipokuja Kristo, ili kwa njia ya imani, tukubaliwe kuwa waadilifu.

25 Tangu kufika kwa hiyo imani, Sheria si mlezi wetu tena.

26 Kwa njia ya imani, ninyi nyote mmekuwa watoto wa Mungu katika kuungana na Kristo.

27 Ninyi nyote mliobatizwa mkaungana na Kristo ni kama vile mmemvaa Kristo.

28 Hivyo, hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na mtu huru, mwanamume na mwanamke. Nyote ni kitu kimoja katika kuungana na Kristo Yesu.

29 Ikiwa ninyi ni wa Kristo, basi ni wazawa wa Abrahamu, na mtapokea yale aliyoahidi Mungu.
 
Kwa hiyo, umeandika nini sasa? Kusema wewe ni Mkristo ina mchango/maana gani kuhusiana na swali alilouliza aliyeanzisha uzi huu? Kama ukisoma bila kutafakari ina maana unasoma bila kupata maana ya kile unachokisoma - yaani kusoma kama kasuku. Kusoma kwa kutafakari ni kusoma kwa kutumia akili/intelligent reading au reflection. Sasa wewe unasema tusome Biblia bila kutumia akili, siyo? Mimi siwezi kufanya hivyo na wala siwezi kumshauri mtu anahitaji ushauri namna hiyo. Kukosoma Biblia bila kutafakari ni kama kutafuta kitu mchangani huku umefumba macho. Kwa Kiingereza ningeweza kusema unintelligent reading of the Bible na hakuna kitu kibaya kama kufanya hivyo. Mungu amekupa rational facultities na inabidi tuzitumie na siyo kusoma blindly.
 
Kwa mujibu wa Sheria za Musa yaan Torati hapo umetenda dhambi

Km unasoma Bible niambie Yesu aliwaambia nini wale waliomletea yule Mwanamke aliefumwa akizini na Mwanaume mwingine?

Kwenye Yohana 8:2-11

Yohana 8:4-5

4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.

5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje?

Yohana 8:7

7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.

"..na km kuna mmoja kati yenu awaye hajawahi kutenda dhambi km hii na awe wa kwanza kumpiga mawe" sio hivyo? Kisheria huyo Mwanamke ilibidi apigwe Mawe mpaka afe Ila Yesu akasema hii sio dhambi ya kupigwa Mawe mpaka kufa maana wanaopiga Mawe nao wanatenda dhambi hio hio

Hapa namaanisha ukiwa wa Yesu Wewe tayari umemvaa Yesu yule Mwanamke alipelekwa kwa Yesu maana yake yule Mwanamke alikua wa Yesu na baada ya wale watu wote kuondoka

Yohana 8:10-11

10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?

11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena

Yesu akamwambia yule Mwanamke "..enenda zako Ila usitende dhambi tena" Wewe ukiwa wa Yesu huna dhambi yoyote ya kupigwa Mawe kwa mujibu wa Sheria za Musa na Torati kwa Yesu ni Wokovu na Uzima wa Milele tu (Wagalatia 3:10) sasa ni Yesu gani mwenye dhambi au Yesu gani anaetenda dhambi? Wagalatia 3:27 Hakuna awaye kwa Yesu mwenye dhambi wote walio kwa Yesu hawana dhambi

Sijui unanielewa ninaposema Wewe km ni wa Yesu basi hauna dhambi unanielewa vizuri sijui hapo?
 
Reactions: 511
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…