Usomaji wa Maandiko ya kidini (Biblia)

Enendeni huku mkijitafakari.

Mwana wa adamu atachoka kurudia maandiko matakatifu,
Naye hatochoka kurudia dhambi afanyayo kila siku.

Amin amin maandiko matakatifu hayana mwisho na hayakuwa na mwanzo,
Kwani siku zote yatokayo ndani mwake ni makumbusho na ni ufunguo,

Enyi mliokwisha kukalili yote basi nanyi mkayaaishi yote yaliyoandikwa, haijalishi ni Quran au Biblia.

Ameen 🙏
 
Acha porojo bhana!!!

Unauliza nimeandika nini kwakuwa umesoma andiko langu bila kutumia akili.

Mtu ameweza kutumia akili kuweka uzi JF useme anashindwa kutumia akili hiyohiyo kuisoma Biblia, acha dharau!
Kuandika huu uzi tu ametumia nguvu kubwa kuliko nguvu anayotakiwa kuitumia kuisoma Biblia.
 
Reactions: 511
Acha porojo bhana!!!
Mtu ameweza kutumia akili kuweka uzi JF useme anashindwa kutumia akili hiyohiyo kuisoma Biblia, acha dharau!
Kuandika huu uzi tu ametumia nguvu kubwa kuliko nguvu anayotakiwa kuitumia kuisoma Biblia.
Si ndivyo unavyotaka wewe? Sasa unaposema tusome Biblia bila kutafakari maana yake ni nini? Hebu eleza hapa. Nasubiri.
 
Si ndivyo unavyotaka wewe? Sasa unaposema tusome Biblia bila kutafakari maana yake ni nini? Hebu eleza hapa. Nasubiri.
Soma kama unavyosoma masimulizi/hadith zingine, unataka kutafakari nini sasa na kitu umekisoma zaidi ya mara 10?
 
Injiri❌
Injili✅
Kuferi❌
Kufeli✅
 
Kuna upotoshaji mkubwa sana humu ndani!
Watu wanataka tusome Biblia kama tunajiandaa na UE, tena huu sio upotoshaji tu ni roho mbaya kabisa.​
 
Reactions: 511
Kwa kawaida, Kila mwaka unatakiwa usome BIBLIA mwanzo Hadi ufunuo na kuimaliza,

Ukimaliza kuisoma, nunua mpya uanze kuisoma tena January Hadi December Mwanzo Hadi ufunuo umalize.

BIBLIA Si kitabu kama vitabu vingine,

BIBLIA ni Neno la Mungu, ni Pumzi ya Mungu, BIBLIA ni kuongea na Mungu na kuisikia sauti yake kupitia Neno lake. Hivyo huwezi kumuelewa Mungu siku moja au mwaka mmoja, ni lifetime process, ni milele na milele

Katika BIBLIA, unaweza kusoma mstari mmoja pekee na ukajikuta unapata mafunuo yanayoweza kujaa kwenye kitabu kizima.

Kusoma BIBLIA ni kuongea na Mungu kupitia Roho mtakatifu, hivyo ujisoma Kwa Roho, sahau kuchoka au kuizoea.


BIBLIA, Neno la Mungu ni chakula Cha Roho ambayo ndio wewe mwenyewe.
Sasa kusema kuwa umesoma na kuimaliza na hujisikii kusoma tena na tena, ni sawa na kusema kuwa nimekula vyakula vyote duniani na sijusikii kula tena kesho, Hilo Haiwezekani. Kula chakula Cha mwili na Roho ni suala la Kila siku,

Kumeditate, kutafakari neno la Mungu ni mchana na usiku 24/7.

Omba Mungu akupe kusoma Kwa Roho, kamwe hutotamani kuacha kusoma BIBLIA.

Mungu akubariki. Amen
 
Nimesoma full Biblia mara nne, sasa almost namalizia kuisoma kwa mara ya tano.

Japo kwa mara ya kwanza mpaka ya tatu nilikuwa sielewi, sasa ndivyo ninazidi kuielewa.

Bible ni ngumu sana kusoma, sometimes unasinzia unalala unaamka unaendelea kusoma tena.

Ayubu 22: 21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.
 
Inabidi upate ufahamu sahihi wa nini maana ya mwanadamu kua ndani ya Kristo na Kristo kua ndani ya mwanadamu(Kuokoka),ufahamu wa dhambi kwake,ufahamu wa haki nk(yaani mafundisho ya Kristo na kumfanania yeye maana ametuita tufanane nae)
Sikiliza hizi audio chache,ya 3 ina jibu la huo mstari hapo uliouandika.
Your browser is not able to play this audio.

Your browser is not able to play this audio.

Your browser is not able to play this audio.
 
Ili uweze kusoma kitabu (biblia) na kuelewa au kupata ufahamu wa juu zaidi lazima uyajue yafuatayo:-

1.Majira saba za kanisa na manabii waliongoza majira hizo.

2.Hatua kumi za uumbaji.

3.Vizazi vinne vya kanisa toka kiuno cha Ibrahimu na walioongoza hivyo vizazi.

4.Nyota 12 zilikatika ufunuo 12:1.

Sababu kila kilichoandikwa katika biblia kiliandikwa kitimie maana Muumba anafanya kazi kwa majira au wakati.

Warumi 11:36
Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.

Zekaria 14:9
Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja.
 
Carleen umeitwa huku, mama mchungaji wangu.
Nimeitikia wito baba mchungaji wangu,

Ivan,
Nimesoma comments, wengi wamekushauri vyema kabisa..!! Neno la Mungu wetu ni jipya kila iitwapo Leo, Neno la Mungu halizoeleki, halichuji, wala haliboi kabisa..!!

Unaiona tofauti sababu unalisoma Neno la Mungu kama unasoma hizi makala nyingine, huwa unasoma Neno mpaka unahisi 'mtetemo' flani hivi kwenye moyo wako..? Unaona kabisa hichi hasa ndiyo hasa ulitamani kukisikia kwa wakati huo..? Ama unasoma Neno kana kwamba unasoma Jibu la kilichokuwa kinakutatiza hasa kwenye maisha yako..?

Kama jibu lako ni Hapana, basi itafute hasa kuijua nguvu iliyopo kwenye Neno la Mungu, Biblia inasema Neno la Mungu ni Pumzi ya Mungu, maana yake siyo maneno tu Hapana, ila ni maneno yenye 'uhai' ndani yake..!!

Hivyo basi ili uielewe Biblia vizuri inakubidi ukae darasani kwa Roho Mtakatifu na umruhusu akufundishe vile apendavyo yeye mwenyewe. Muombe Roho wa Mungu akufundishe, kabla ya kuanza kusoma mruhusu Roho Mtakatifu akufundishe na kukuongoza,

Natumaini unafahamu Roho Mtakatifu ndiye msaidizi na muangalizi wetu tuliyeachiwa baada ya Bwana wetu Yesu kurudi Mbinguni, na Biblia inatusisitiza kabisa kuwa Roho Mtakatifu hutuombea kwa kuugua kusikotamkika..!! Hivyo jitahidi kabla hujaanza kusoma Biblia, Omba kwanza usaidizi wa Roho, ili kufahamu hasa hekima na ufunuo uliopo kwenye Neno..!!

1 Wakorintho 2 : 10-11
10 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. 11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila Roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…