Usomaji wa Maandiko ya kidini (Biblia)

Usomaji wa Maandiko ya kidini (Biblia)

Nimeitikia wito baba mchungaji wangu,

Ivan,
Nimesoma comments, wengi wamekushauri vyema kabisa..!! Neno la Mungu wetu ni jipya kila iitwapo Leo, Neno la Mungu halizoeleki, halichuji, wala haliboi kabisa..!!

Unaiona tofauti sababu unalisoma Neno la Mungu kama unasoma hizi makala nyingine, huwa unasoma Neno mpaka unahisi 'mtetemo' flani hivi kwenye moyo wako..? Unaona kabisa hichi hasa ndiyo hasa ulitamani kukisikia kwa wakati huo..? Ama unasoma Neno kana kwamba unasoma Jibu la kilichokuwa kinakutatiza hasa kwenye maisha yako..?

Kama jibu lako ni Hapana, basi itafute hasa kuijua nguvu iliyopo kwenye Neno la Mungu, Biblia inasema Neno la Mungu ni Pumzi ya Mungu, maana yake siyo maneno tu Hapana, ila ni maneno yenye 'uhai' ndani yake..!!

Hivyo basi ili uielewe Biblia vizuri inakubidi ukae darasani kwa Roho Mtakatifu na umruhusu akufundishe vile apendavyo yeye mwenyewe. Muombe Roho wa Mungu akufundishe, kabla ya kuanza kusoma mruhusu Roho Mtakatifu akufundishe na kukuongoza,

Natumaini unafahamu Roho Mtakatifu ndiye msaidizi na muangalizi wetu tuliyeachiwa baada ya Bwana wetu Yesu kurudi Mbinguni, na Biblia inatusisitiza kabisa kuwa Roho Mtakatifu hutuombea kwa kuugua kusikotamkika..!! Hivyo jitahidi kabla hujaanza kusoma Biblia, Omba kwanza usaidizi wa Roho, ili kufahamu hasa hekima na ufunuo uliopo kwenye Neno..!!

1 Wakorintho 2 : 10-11
10 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. 11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila Roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.
Mungu hana muda wa kukuwekea wewe mafumbo, Mungu akuwekee mafumbo ili iweje?
 
Mungu hana muda wa kukuwekea wewe mafumbo, Mungu akuwekee mafumbo ili iweje?
😂 😂 😂
Mambo mengi ni myths tu halafu Waafrika ndio tunaumizwa sana na hizi dini hasa huu Ukristo. Angalia China, Japan, Korea hawana stress za kijinga zinazo sababishwa na hizi dini hasa ukristo.
 
😂 😂 😂
Mambo mengi ni myths tu halafu Waafrika ndio tunaumizwa sana na hizi dini hasa huu Ukristo. Angalia China, Japan, Korea hawana stress za kijinga zinazo sababishwa na hizi dini hasa ukristo.
Na hakuna anayelazimishwa mkuu, kila mtu aishi vile anavyoona yeye ni sawa, wengine tumemuona Mungu kwenye maisha yetu, wacha tuendelee kumuamini..!!
 
Na hakuna anayelazimishwa mkuu, kila mtu aishi vile anavyoona yeye ni sawa, wengine tumemuona Mungu kwenye maisha yetu, wacha tuendelee kumuamini..!!
Hakuna asiyemuamini Mungu, Sisi waafrika tumekuwa watumwa wa hizi dini hasa Ukristo. Inawezekana wewe umemuona Mungu kupitia dini lakini kumbuka kuna Wajinga wengi wamekuwa kama misukule. Wameshindwa hata kuwa na maamuzi na maisha yao
 
Sina muda wa audio.
Kosoa kwa maandishi kwa uelewa wako sio kwa mawazo ya wengine.
Nionyesha mstari unaosema alitengua torati.
Neno linasema ktk 1 YOHANA 3:4 'Kila atendaye dhambi afanya uasi,kwakua dhambi ni uasi.
Zingatia kabla ya Bwana Yesu kuja na kuiondoa dhambi,wanadam wote walikua ni wenye dhambi bila kujali umri wao so mtu anakua mwenye dhambi kwasababu amezaliwa ana dhambi sio kutenda.
Tazama WARUMI 5:12-14 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;
13 maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria;
14 walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, NAYO ILIWATAWALA HATA WAO WASIOFANYA DHAMBI IFANANAYO NA KOSA LA ADAMU, aliye mfano wake yeye atakayekuja.
Pia tunajua kua mshahara wa dhambi ni mauti (WARUMI 6:23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.)hivyo basi watoto wadogo wanakufa kwasabab ya dhambi! Dhambi inayowaua sio walioifanya maana kuna vichanga kuna vinavyokufa kabla ya kuzaliwa pia bali ni ile waliyoirithi kupitia Adamu na asili yake ya dhambi toka eden ambayo ipo ndani yao!
Lakini Mungu apewe sifa kwakumleta mwanawe mpendwa duniani kutukomboa na dhambi na ktk hali ya uasi.YOHANA 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Uzima unakujaje bila dhambi kuondolewa kutokana na YOHANA 3:16 hapo?
Dhambi na asili yake imeondolewa milele na Bwana Yesu WAEBRANIA 10:10 Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.
12 Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu;
14 Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.
17 Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa.
18 Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.

Cheki WARUMI 5:8-10 Basi Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, TULIPOKUWA TUNGALI WENYE DHAMBI.
9.Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.
10 Kwa maana ikiwa TULIPOKUWA ADUI TULIPATANISHWA NA MUNGU KWA MAUTI YA MWANA WAKE; zaidi sana BAADA YA KUPATANISHWA tutaokolewa katika uzima wake.
Yesu hakutufia tukiwa watakatifu wenye matendo mema bali tukiwa waasi na sio wakristo tu bali ulimwengu mzima!
Hatupatanishwi na Mungu kwa matendo mazuri ya kila siku.

Mtu aliezaliwa mara ya pili ni mwenye haki sio mdhambi tena.2 WAKORINTHO 5:21 Yeye[YESU] asiyejua dhambi ALIMFANYA KUWA DHAMBI KWA AJILI YETU, ILI SISI TUPATE KUWA HAKI YA MUNGU KATIKA YEYE[YESU].
1 WAKORINTHO 6:17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.
So kama umeokoka dhambi huna,coz kama ndani ya Mungu hakuna dhambi nami sina sababu tumekua kitu kimoja naye.
1 YOHANA 3:9-10 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.
10 Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.

uthibitisho mwingine ni 1 YOHANA 2:1-2 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
2 naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.
Hivyo jua kwamba ondoleo la dhambi huja kwa kuliamini jina la Yesu Kristo(MATENDO YA MITUME 10:43)
Kwa maana pia dhambi ni kutokumuamini Yesu(YOHANA 16:8-9)

Yani unamuamini Yesu ila kazi yake ya pale msalabani kumwaga damu yake kwa ajili ya ondoleo la dhambi ya ulimwengu huiamini! Na amesema yeye mwenyewe sehemu nyingi tu ila unachagua kujiita mwenye dhambi,dhaifu,usiefaa,usie kitu na kukiri ungamo kila jumapili kanisani ilhali umekua kiumbe kipya mwenye haki,utakatifu na ukombozi wa Mungu baba!
Kiukweli inashangaza mno wakristo waliokoka wanavyoshikilia dhambi ambayo ilishafutwa milele!

Ktk MATHAYO 5:17-48 Bwana Yesu anaelezea amekuja kuitimiliza yani kuitimiza na kuirekebisha sababu yeye ameleta neema na kweli.maana yake ni kua torati yote ya musa na manabii inatimia katika yeye.so ukiwa ndani yake basi torati yote na manabii inakamilika ndani yako.
Na ndio maana unaona kwanzia mstari ya 21 Bwana Yesu anazinukuu baadhi ya sheria za torati zilivyosema na yeye anaziongezea kua yote hayo ni upendo tu ndio amri kuu(kumpenda Mungu na jirani yako basi)
 
AHsante sana, niseme tu hii class au bideo hii ya huyu nwana nimeshawahi iona.
Ameelezaa yooooote hayo nakubaki na ninaelewa, but

swali langu ni hili, HOW DO YOU COME INTO ACQUIRING ALL THOSE SPOKEN STUFFS???
nimeshajua hizo ginosco, epigniss etc, HOW DO I THEY COME INTO ME?????.

Well, ili uweze kukua katika knowledge ya Kimungu unahitaji machache yafuatayo:

1. Lazma uwe na mwalimu anayekulisha neno, ambaye unamsikiliza mafundisho na mafunuo yake. In the first place, Mungu anasema nawe kupitia kwa Mtumishi wake. Kadri unavyokuwa msikivu na mtiifu kwa Mtumishi wako ndivyo Mungu huanza kusema nawe pia. (1samuel 3:1-10) utaona Mungu anamuita nabii Samuel mara kadhaa lkn Samuel anasikia kwa sauti ya kuhani Eli ambaye alikuwa ni mlezi wake kiroho.

2. Lazma uwe na ratiba ya kusoma neno kwny biblia, sehemu kubwa ya neno la kwny biblia ni sauti ya Mungu mwenyewe kupitia kwa Roho Mtakatifu anazungumza kwa kupitia watumishi wake (2timoth 3:16) all scripture is given by the inspiration of God…

3. Kuwa na muda wako maalum wa kuomba, tafsiri ya maombi ni kuzungumza na Mungu. Na maombi ni dialogue sio monologue, maana yake unazungumza na Mungu anakujibu. Unaweza ht kutega alarm km ni usiku saa fulani pakiwa na utulivu unaamka na kuomba. Kupitia vipindi vya kuomba utaanza kupata maelekezo kuhusu mambo yanayo kuhusu, utapata suluhu la changamoto zako na pia majibu ya maswali yako. Unakuwa na jambo linakutatiza lkn ukiwa ktk kuomba unapata idea ya namna ya kulitatua, hivyo ndivyo Mungu anasema nawe(anakupa revelation).
Utaanza kupata uelewa mpana wa maandiko na kiu yako kusoma neno itaongezeka siku ht siku. Vitu ambavyo mwanzo ulivisoma ukaona km vya kawaida, this time vinakuwa revealed in an extraordinary way. Sometimes unarudia kusoma kitu ulichokwisha kisoma way back ila unapata another new revelation.

4. Pata muda wa kutafakari neno (meditation). Unaposoma neno kwa mara ya kwanza linaenda kwny mind yako. Meditation ni kitendo cha kulihamisha neno toka kwny ufahamu wako na kuliingiza rohoni mwako ambapo ndipo neno huwa roho na linapata uzima (manifestation). Meditation ndio humfanya mtu aweze kutenda kama ilivyo agizwa kwny neno, pia humfanya mtu kufanikiwa (prosperity) na kustawi (success).
Joshua 1:8.
 
mkuu , kidogo unaweza nifafanulia 666 na zile events zitakazotokea mpka kunatokea kuuza na kutokuuza bila ya chapa ya mpinga kristo 666 na ujio wa yesu? mana huwa nachanganyikiwa sana.
666 ni mwili wako mwanadamu..... chapa kwenye paji la uso ni nia ovu moyoni na chapa kwenye mikono ni matendo maovu ambayo yote hayo yana tokana na huyo mnyama (mwili) yaani kuzifuata tamaa za mwili ....chapa ya mnyama maana yake ni DHAMBI👉 siyo mtu fulani au kiumbe fulani kijacho au kipitacho kwa sababu imeandikwa wenye chapa ya huyo mnyama ndiyo watakao ingia motoni na tunajua kuwa kitu pekee kinacho mpeleka mtu motoni ni dhambi ....kwenye ufunuo 666 pia maana yake ni moja na yale maandiko yanayo sema KAHABA mkuu ambaye wafalme wamezini naye huyo KAHABA ndiyo 666 (yaani mwili wako ) na (wafalme ni nafsi inayo utawala mwili) kahaba kulewa kwa maombi ya watakatifu ni wachamungu kuzishinda tamaa za mwili ambao ndiyo huyo kahaba .....hivyo hizo funuo mbili maana yake ni moja .....huyo kahaba na 666 maana yake ni moja tu kuzini na huyo kahaba ni kufuata tamaa za mwili kwa sababu nguvu ya dhambi ipo kwenye miili yetu.👉kuhusu kuuza wala kununua isipokuwa watakuwa na chapa ya mnyama) hapo nadhani umesha jua maana yake, kwa kuwa chapa ya mnyama ni DHAMBI hivyo maana yake ni kuwa kila kitu atendacho mwadadamu kitakua kiovu chenye kutawaliwa na dhambi itokanayo na tamaa za mwili ...sasa ikiwa huyo mnyama ni papa je waliokufa kabla ya kuwako papa wataingia peponi ? Je ikiwa huyo mnyama ni kiumbe kijacho je walio kufa kabla ya hicho kiumbe wataingia peponi wote ? Kwa vyovyote vile nilazima huyo mnyama yupo sikuzote za mwanadamu duniani....maana imeandikwa wenye chapa yake ndiyo watakao tupwa motoni je.. chapa ni nini kama siyo dhambi maana ni dhambi tu ndiyo itakayo mpeleka mtu motoni .
 
Ili uweze kusoma kitabu (biblia) na kuelewa au kupata ufahamu wa juu zaidi lazima uyajue yafuatayo:-

1.Majira saba za kanisa na manabii waliongoza majira hizo.

2.Hatua kumi za uumbaji.

3.Vizazi vinne vya kanisa toka kiuno cha Ibrahimu na walioongoza hivyo vizazi.

4.Nyota 12 zilikatika ufunuo 12:1.

Sababu kila kilichoandikwa katika biblia kiliandikwa kitimie maana Muumba anafanya kazi kwa majira au wakati.

Warumi 11:36
Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.

Zekaria 14:9
Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja.
HAYA NI MAFUNDISHO YA INJILI FEKI ZA MADHEHEBU YA DINI ...NENO DHEHEBU MAANA YAKE NI HEKATU LA SHETANI
 
Hata me niliposoma bandiko lake cha kwanza akanijia kichwani Uebert Angel maana nimetoka kumsikiliza muda mfupi na ninamsikiliza kila wakati.

Linapokuja suala la revelation, Uebert Angel ni next level aisee.
Uebert Angel aliyenaswa na camera za Aljazeera akifanya biashara ya magendo ya dhahabu kutoka Zimbabwe?
 
Jibu zuri kaka..
Na mimi nimesema hapo nikatoa mfano, leo i was about to read certain chapter in nee testament, lakin nikaboreka maana nikafikiri, mbona hiz bmhabar zote nishazisoma na kuzisikia, sasa nisome tena ili iweje????

Ndio maana naukiza, au kuna namna mpya ya kusoma napaswa kuifahamu?
Kaka yanayokukuta wewe kama yanayonikuta mimi ila kwangu naona ni zaidi.
Yani am not interested anymore kwenye habari za hizi dini.
Nakua napatwa na khofu labda mungu kaondoa imani juu yangu ndo maana niko hivi kama wao wasemavyo.

Yani nikisikiliza mashekhe na mapastor naona nikama mawazo yangu ni makubwa mbele ya wanachokinena, yani naona tu ni upigaji uliowekwa kwa misingi ya kumtisha na kumfubaza kiakili mwanadamu na sio kumjenga.

Naamini mungu yupo but nakua nakosa right connection kwangu na kwake maana uyu wa kwenye izi dini naona sio kabisa au yawezekana ndio ila sio kwa jinsi wanavyomnena.

VITU VINAVYO NIKATISHA TAMAA KWENYE HIZI DINI.

• Story
Izi dini zina story za historia ya mungu na Dunia mpaka kufika leo, kwakweli mwanzo nilikua naamini mambo ya adam na eva, ghalika na n.k ila nilivyokua nimejikuta izo stories haziningii kichwani mwangu naona ni uzushi tuu, maana issue za nuhu kasimulia nuhu mwenyewe unamiinije kama hakuongeza chumvi,
story za sodom na gomora ilikua ni kijiji sio Dunia yawezekana ikiwa ni natural disaster kama inavyotokea ata hiki kipindi kama volkano na kwa miaka iyo waliona ni jambo kubwa kutokana na teknologia yao kua ndogo ndo maana wakalikuza kupita kiasi!

Kuna hadith nyingi za kiislam kwamba kuna mda mungu alituma ndege wamebeba mawe kuua maadui wa mtume yani zinakua haziningii kabisa, habari za maliamu kuona malaika ndo kabisaa, najiuliza kwani shetani hawezi kua mweupe, au mtu akikumbia utazaa mtoto wa mungu na atahimiza kusali ndo inajustfy kua uyo malaika hakua jini wala shetani!! Maana leo hakuna mtu anayemjua jini malaika na shetani katika maumbile, watu wanadefine ivo vitu kwa matendo, ukitokewa na mtu mweupe akakumbia piga goti shika maji uombe mungu unaamini ni malaika, ukitokewa na kitu cheusi kinaogopesha kinataka kukuua unajua ni shetani.

• Dini kutokea sehemu moja.
Dini zote kuu zimetokea eneo moja, wengine tumekuja kupokea, Huwezi sikia kulikua na mtume wala nabii mchina wala nini, wote ni Middle East. Story za kupokea jumbe za mungu na kuona malaika saivi naona kama ni hadidhi za Juma na Uledi, maana kichwani mwangu inakataa kuamini mtu atoke alikotoka aseme kuua ni dhambi mungu atakuchoma moto!! Sababu naamini hata bila huo ujumbe kwa akili za kawaida tu lazima huone kuua sio sawa, kuiba, kuchukua mpenzi wa mtu, kutukana mtu n.k sio mpaka mtu utishiwe moto.

Kunamda nawaza tuu ni vipi kama hao mitume walikua ni watu kwenye koo zao baada ya kuona vita ni vikubwa na manyanyaso wakaamua kusema wamepokea funuo kuhusu habari za mungu ili kufanya hao wafalme wauaji wasiendelee kuua watu hovyo! Au watu kuchukua wanawake zao kibabe ndo waka establish ndoa!! Maana kabla y Dini kila sehemu kulikua kunaendeshwa kwa akili za wafalme na kwa ubabe tuu bila kujal haki za kibinadamu.

Inshort sidhani kama niko sahihi na wala sijui kama nipo wrong ila izo story za watu wa uko Middle East kutumbia kuna shetani na mungu wanakinzana, asee zimekua ngumu kuningia now days nahisi nahitaji maombi labda kweli uyo shetani kaniingia.
 
Aisee Asante sana mleta mada,
Hili suala mimi nilishawahi kujiuliza miaka mingi iliyopita,
1. Kanisani nimehudhuria mwaka mzima na nimefundishwa mafundisho lukuki, lakini je yamenifaidia wapi? Nimeyatendea kazi mangapi? Mbona mahubiri ni yaleyale tu yakijibadili kidogo tu?
  • Utoaji
  • Nguvu ya maombi
  • Jinsi ya kukua kiroho
N.k
2. Ndipo nilikuja kupata majibu kuwa kumbe neno la Bwana linatafsiri zaidi ya 70, kuna nyakati nilikuwa nikipitia nyakati za shida chaajabu nikishika biblia tu kusoma nakutana na andiko ambalo limebeba majibu ya shida zangu, au neno hilo linanitia nguvu ya kusonga mbele. Lakini neno hilo siyo kwamba linakuwa geni kwangu hapana nilishalisoma siku nyingi tu na mara nyingi tu, lakini huwa linajifunua kwa namna ya pekee kulingana na nyakati

USIACHE KUSOMA NENO WALA KUACHA KUHUDHURIA IBADA
 
Back
Top Bottom